Mifumo ya kidunia ilishaamua mwanaume aishi kwa kukandamizwa na kufanyiwa ulaghai/ udanganyifu

Hiki kinachoendelea kitakuja kuwaweka sehemu mbaya sana watoto wa kike siku za baadae na watakosa kabisa utetezi sababu ya upumbavu wa kundi la wachache.

Unapokandamizwa au kuonewa ukapata nafasi ya kujitetea then tumia hiyo nafasi kumsaidia aliye kukandamiza ajue mapungufu yake na aweze jua jinsi ya kukusaidia usiumie.

Ujinga unaondelea kwa wanawake wa kisasa mnataka kushindana na wanaume as if walikuwapo miaka hiyo au walihusika. Binti kuzaliwa miaka ya 1980 au 1990 au 2000 visa vya kihistoria wewe vinakuhusu nini kutaka kujifanya shujaa wa jinsia utake kulipa kisasi? [emoji848]

Sasa nikwambie tu ufahamu, atakae komoka hapa ni mwanamke kwasababu haya mnayofanya kwa bahati mbaya sana yanatokea kizazi cha internet ambapo ushahidi upo wazi kabisa wa tabia na kauli za mwanamke anapofanikiwa au kuwezeshwa anakuwaje.

Unaweza kunipa ushahidi wa kukandamizwa mwanamke enzi za mababu zetu zaidi ya story za kuhadithiwa na mashangazi na mama zetu?[emoji848]

Ila mimi ukitaka nikuonyeshe kwa ushahidi wa video tabia mbaya za wanawake na kwann hawaruhusiwi hata kutoka nje ushahidi upo humo mitandaoni.

Unadhani uarabuni hadi wanakuwa watata kwa wanawake vile ilikuwaje?

Itakuja kufika kipindi hizi kauli zenu za madharau na jeuri na kutaka kujilinganisha na wanaume ndizo zitakuja tumika baadae kutunga sheria zitakazokataza wanawake kufanya kazi, kuongea mbele ya mwanaume, kutoruhusiwa kupiga kura yoyote, kutosikilizwa kwenye kesi au maushauri, kutokuwa na maamuzi yoyote sababu ya wanawake wapuuzi na wapumbavu wachache ambao walizaliwa nyakati za mabadiliko mkaleta utoto badala ya kutumia hiyo fursa kuprove kuwa mwanamke ni kiumbe anayejitambua na ni msaada mkubwa kwa mwanaume.
 
Teh teh teh 😂😂 yaani kutoka feminism mpaka malenisim...😂😂
 
Swala la decline birth rate lina mahusiano na women empowerment ?
Ndio, by 100%. Women empowerment imewafanya wanawake kujikita zaidi kwenye majukumu ya utafutaji mali na elimu hadi wakasahau wajibu wa kuwa mwanamke.

Tazama hapa Tanzania kwa wastani wanawake wasomi hawapati watoto zaidi ya 2 maximum. Ukikuta mwanamke ana watoto watatu au zaidi huyo alijitoa kimasomaso kuwa mrs mwaflani.

Sasa kama miaka ya 1970 kurudi nyuma wazazi walipata watoto kuanzia 7 hadi 12 kwa wastani.

Ina maana idadi ya watu itashuka sababu kila mtoto akizaa watoto wawili tu haitakuwa the same number kama wangezaa watoto 12 each.
 
Ukifanya tathimini ya machangudoa, single mothers, wezi, panya road, na wahuni, wengi wanatokea broken homes ambazo hakuna stable male figure wa kusimamia ubaba.
 
Hii point nzito sana
 
Good points
 
Una akili sana.
 
Aisee nipe namba yako ya M-pesa nikizawadie bando, umeongea point kishenzi.
 
Mh, ulikutwa na Nini mkuu? Pia uliwapa adhabu gani? ili namimi nimkomeshe atakayejileta.
 
Si ndo biblia inavyosema, mwanamke aliumbwa kwaajili ya mwanaume, na siyo kinyume chake.
 
Ila una uchungu mheshimiwa,navyojua mimi kuna nguvu kubwa Nyuma ya pazia kuhusu kampeni ya kulegeza wanaume kuwa duni kiuzazi ili dunia itawaliwe kiiluminat.
 
Mnadiscuss hizi mada kwa hasira sana, mna watoto wa kiume na wakike? Kama hamna mna mpango huo au ninyi ni pro-choice?

Pro-life sote tunatakiwa kuadvocate jamii yenye usawa and harmony huku kila mmoja kwa jinsia yake akiyafahamu majukumu yake vyema.

Vijana bwana mna mihemko tele na hasira za kujaa, y’all chill!
 
Sasa kutafuta furaha kukataa ndoa ?!
Maana yake una enda kinyume na matakwa ya Mwenyezi Mungu aliye kuumba. Sijui kama ume elewa. Unaweza vipi tafuta furaha kwa kukataa ndoa ebu nijibu hapo ?!
Hilo swali wanatakiwa waulizwe wanaume ambao ndio wanaongoza kampeni ya kataa ndoa, mnachotakiwa mjue ni kwamba lolote ambalo wanawake wanalifanya leo hii ni matokeo ya tabia za wanaume, sasa kama waoaji hakuna wanaume wengi hawataki kuoa unataka wanawake wafanyeje mkuu
 
Ndio nilichokiandika ndicho nilichokimaanisha wala sijakosea mkuu, ukiwasikiliza wanawake wanataka haki itendeke yani haki sawa kwa wote, ukiwasikiliza wanaume hawataki haki sawa wao wanataka mwanamke aendelee kukandamizwa ndio wapate furaha
 
Mkuu yupo sawa. Tupo affected sana na wamagharibi. Ni kama tunafata nyayo zao kwa kuchelewa. Yaani wakimalizana na stage fulani baada ya miaka na sisi tunaanza kuipitia kwa kujifunza bila kujali iliwaumiza au la. Sisi tunaiga tu.
Globalization
 
Hili tayari wanaume tumeng'amua kitambo sana, ndio maana kuna kampeni ya KATAA NDOA NI UTAPELI hii wameanzisha wanaume.
Mkuu ndio maana niliuliza kama unajua kusoma alama za nyakati, na sijui hata kama unauona uhalisia wa wapi tulipo kama jamii na wapi tunaelekea, usichokijua ni kwamba wanaume wameanzisha kampeni ya kataa ndoa si kwamba eti ni kweli hawataki ndoa

Bali lengo lao ni kuwakomoa wanawake ili wabadili tabia zao waanze kujirudi na kuwa wife material, sababu wanajua toka enzi jamii imemfanya mwanamke awe desperate na ndoa, hivyo wanaume wanaamini wakijifanya kususia ndoa basi wanawake watafanya kila namna wabadili tabia zao ili wapate ndoa

Sasa unfortunately wanawake wa aina hiyo walikuwepo zamani hawa wa sasa ukisusa hawabembelezi kwahiyo baada ya kuona kwamba wanaume wamesusa ndoa, nao ndio wanatafuta sasa namna ya kuwa na furaha bila ndoa kwahiyo ni kama wameenda kinyume na matarajio ya wanaume wengi, yani badala ya wanawake kuwabembeleza wanaume matokeo yake nao wameamua kususa
 
Hiyo 50/50 mnayo ipigania ndiyo ime fikisha huko, kwa ufupi waliyo ileta hiyo 50/50 hawaja tatua taitizo bali wame weka moto juu ya moto, tatizo juu la tatizo.
 
Mkuu unataka wanawake wawasaidie mara ngapi kujua hayo mapungufu yenu ya tangu enzi na enzi, kwani siyo ninyi mnaoambiwa kila siku muache kunyanyasa wanawake ila ndio kwanza mnajibu kwa jeuri kwamba wanaume kufanya hivyo ni sawa sababu ni viongozi, sikiliza mkuu hakuna kiumbe atakubali umnyanyase kwa sababu yoyote ile (hata kama unamhudumia) hata mifugo yako tu yenyewe ukiinyanyasa eti kisa unaihudumia ipo siku tu itachoka na itakugeuka sembuse mwanamke ambaye ni kiumbe mwenye utashi kama wewe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…