Zemanda
JF-Expert Member
- Jan 10, 2021
- 8,323
- 18,051
Hiki kinachoendelea kitakuja kuwaweka sehemu mbaya sana watoto wa kike siku za baadae na watakosa kabisa utetezi sababu ya upumbavu wa kundi la wachache.Mimi naona dunia imemsikiliza mwanaume kwa muda mrefu imefika pahala acha sasa imsikilize na mwanamke kwa sababu mfumo dume umemkandamiza mwanamke vya kutosha, wake walipokuwa wanavumilia kukandamizwa miaka yote hiyo ilionekana sawa sasa wameamka baada ya kuchoka na kukataa kukandamizwa wanaume mnaanza kulalamika na mnaona kama mnaonewa, wanawake wamechoka kulalamika wameamua kujibu mapigo kwahiyo tulieni tu dawa iwaingie mpaka pale siku mtakapoongea nao lugha moja
Unapokandamizwa au kuonewa ukapata nafasi ya kujitetea then tumia hiyo nafasi kumsaidia aliye kukandamiza ajue mapungufu yake na aweze jua jinsi ya kukusaidia usiumie.
Ujinga unaondelea kwa wanawake wa kisasa mnataka kushindana na wanaume as if walikuwapo miaka hiyo au walihusika. Binti kuzaliwa miaka ya 1980 au 1990 au 2000 visa vya kihistoria wewe vinakuhusu nini kutaka kujifanya shujaa wa jinsia utake kulipa kisasi? [emoji848]
Sasa nikwambie tu ufahamu, atakae komoka hapa ni mwanamke kwasababu haya mnayofanya kwa bahati mbaya sana yanatokea kizazi cha internet ambapo ushahidi upo wazi kabisa wa tabia na kauli za mwanamke anapofanikiwa au kuwezeshwa anakuwaje.
Unaweza kunipa ushahidi wa kukandamizwa mwanamke enzi za mababu zetu zaidi ya story za kuhadithiwa na mashangazi na mama zetu?[emoji848]
Ila mimi ukitaka nikuonyeshe kwa ushahidi wa video tabia mbaya za wanawake na kwann hawaruhusiwi hata kutoka nje ushahidi upo humo mitandaoni.
Unadhani uarabuni hadi wanakuwa watata kwa wanawake vile ilikuwaje?
Itakuja kufika kipindi hizi kauli zenu za madharau na jeuri na kutaka kujilinganisha na wanaume ndizo zitakuja tumika baadae kutunga sheria zitakazokataza wanawake kufanya kazi, kuongea mbele ya mwanaume, kutoruhusiwa kupiga kura yoyote, kutosikilizwa kwenye kesi au maushauri, kutokuwa na maamuzi yoyote sababu ya wanawake wapuuzi na wapumbavu wachache ambao walizaliwa nyakati za mabadiliko mkaleta utoto badala ya kutumia hiyo fursa kuprove kuwa mwanamke ni kiumbe anayejitambua na ni msaada mkubwa kwa mwanaume.