Mkuu, familia inahitaji kiongozi kuliko mtawala.
Kiongozi anawapenda anaowaongoza, yupo pale kuwahudumia na anawasikiliza na kuzifahamu hisia zao. Maamuzi yake ya mwisho yanazingatia ushauri wa anaowaongoza.
Tofauti na Mtawala yeye ni top na haitaji mjadala, sauti yake haiojiwi hata kama kilichotoka ni ugoro, ni mshauri wa yeye mwenyewe.
Watawala katika familia ni sehemu ya chanzo cha kuibuka wapigania haki za wanawake.
Kiongozi na nyumba ndogo ni tabu sababu muda wote analazimika kuwa karibu na mke wake, mambo ni mengi ya kutatua, miradi ya maendeleo, shule watoto, marejesho. Kila siku kuna jambo la kujadili na mke.
Mtawala na nyumba ndogo ni rahisi sana sababu yeye anatoa maelekezo anaondoka na ole wake mtu asiyafate. Anapoenda hakuna wa kumhoji anafanya nini na atarudi lini.
Huo ni mfano mmoja tu wa utofauti wao