Mifumo ya Uendeshaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, iangaliwe upya! Watanzania "tutachoka" vibaya sana ndani ya hii miaka 10 ya Mhe. Rais Magufuli

Iko hivi ili uendelee lzm uweke uwiano Wa maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu.Cuba Ina maendeleo ya watu kuliko maendeleo ya vitu.Nchi za scandinavia zinamaendeleo ya watu na vitu.Ethiopia,North Korea zina maendeleo ya vitu kuliko watu.
 
Iko hivi ili uendelee lzm uweke uwiano Wa maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu.Cuba Ina maendeleo ya watu kuliko maendeleo ya vitu.Nchi za scandinavia zinamaendeleo ya watu na vitu.Ethiopia,North Korea zina maendeleo ya vitu kuliko watu.

Nakubaliana na wewe na ndiyo hoja yangu....

Nisome vizuri hapo juu nimelieleza hili kwa kirefu sana....

Kwahiyo, tunakubaliana 100% kwenye hili
 
Hao wataalamu wanaoatakiwa kushauri hayo hawapo? au wamebaki kuimba sifa kukwepa kurudishwa jalalani
 
Fumadilu Kalimanzila na Kitaturu:
Asanteni kwa bandiko zuri na la kufungia mwaka ( kwangu Mimi)! Mmejadili kwa hekima na busara bila kutumia lugha ya maudhi ambayo ingewavuta wale wenye Noah nyeusi jirani yenu!
Ni sahihi sana wanasiasa wanaposimama majukwaani kunadi juu ya kukua kwa uchumi Basi wawe na uhakika wa kauli na tafiti zao kwani kiuhalisia Hali ni tofauti mno mtaani!
Pia hebu Hawa wapambe nuksi waambiwe ukweli kuwa hawamsaidii rais Bali wanajirahisishia wao kuishi vizuri! Kitendo Cha kuiweka mfukoni bunge, nec, mahakama na ofisi ya dpp na cag sio afya kwa ustawi wa taifa kenye kujinadi kuilinda amani! Ni wakati sasa, rais anapoitafakari xmass atafakari juu ya Uhuru wa mihimili mingine kutenda kwa mujibu wa katiba kwani vyote vinajenga nchi moja!
 
Kama
Kama hujui kitu usishupaze shingo! Ruhusu akili yako kujifunza vitu usivyovijua!

Na Elimu yako ya shule ya kata ukishatupiwa li nguo za kijani ukavaa basi unaona wewe ni mjuaji!

Halmashauri za Mji,Manispaa ni Serikali zilizokamilika,kuna Baraza la Madiwani ( ambalo kazi yake ni kama Bunge),Mkurugenzi kama Mtendaji Mkuu wa Halmashauri na Wakuu wake wa Idara na Baraza la Madiwani wanaweza kubuni miradi kwa ajili ya Wananchi.

Hivyo wanaweza kukopa kwa ajili ya miradi ambayo ni "income generating" na hivyo kuleta tija ikipangwa na kusimamiwa vizuri!

Miradi kama Stendi za Mabasi, Majosho, Masoko ,Minada, Machinjio,Vyoo vya Kisasa n.k ni aina ya miradi inayobuniwa na kusimamiwa na Halmashauri chini ya Wakurugenzi na kuharakisha maendeleo ya maeneo husika badala ya kusubiri kila kitu mpaka Rais aseme au atoe fedha!

Kwanza Rais anatoa fedha wapi?! Fedha ni za wa Watanzania wote na hata Rais kwa mujibu wa sheria anapangiwa matumizi yake ambayo yanaidhinishwa na Bunge!

Acheni ujinga utawala wa sheria lazima ufuatwe ( Rule of Law should prevail)!
 
MTAJI NI AKILI YAKO........ACHA UJINGA.......
 
Hao Hao wajukuu tutawanunua toka China?Babu zao wanakomolewa ili wao wake wafaidike?Hiyo ni kanuni gani ya maisha?
Hivi maendeleo hufanyika kwa ajili ya watu waliopo au wajao?Ndiyo Sera ya Dr.JPJM au chama chake?
 


Huu mchezo hauhitaji hasira [emoji3][emoji3]

Kwa hiyo umeleta uzi ukitarajia watu wote tukuunge mkono?

Hataki kupokea mawazo tofauti tofauti?

Je kwa kufanya hivyo unazani utakuwa unatutendea haki wote?

Hili ni jukwaa huru kwa majadiliano, jifunze kustahamili na kuwa tayari kupata mawazo tofauti na mbadala.

Usikasirike maana mwisho wake huwa ni kutenda dhambi!

Though umeshafanya inakubidi ufanye toba!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo miradi huwa ni rasmi?

Je huwa inafanyiwa visibility study kabla ya utekezaji ili kuona kama itakuwa na tija?

Je wataalam walosomea Projects management wapo?

Je huwa wanafahamu ku identify risks in advance na namna ya kuzi manage?

Je nidhamu ya matumizi ya umma ya Halmashauri nyingi uzoefu ukoje?

Hayo ni maswali machache ya kujiuliza kwanza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usishangae fedha ya mkopo ilokusudiwa kwaajili ya miradi fulani isitumike ilivyokusudia badala yake watu inatumika kulipana posho na misreallocations chungu nzima!

Mikono inagharama kubwa kupitia riba kwa hiyo ni maamuzi ambayo yanapaswa kuwa magumu kufanyika .

Sasa mwerevu akiona mtu anaona swala la kukopa kuwa jepesi na rahisi tunaanza kujiuliza kwanini?






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilizani ungenitaka kujustify hoja yangu badala yake mwenzangu naona unapanic [emoji14][emoji14]

Inabidi uwe na kifua!


Sent using Jamii Forums mobile app

OK sorry,kama nime - over react ! Unajua tatizo linalochosha kwa Watanzania wengi ni kwamba Watanzania wengi ni myopic lakini wanajifanya wajuaji sana!
Nchi zote zilizopiga hatua kubwa zinaendeshwa kwa mifumo imara na si "Watu" imara!
 
Wewe kojoa ukalale, nadhani naongea na " MTU" kumbe " Chicken "!
Halmashauri zina Wakurugenzi tena wasomi hadi ngazi ya PhD! Wakuu wa Idara wasomi kabisa! Wachumi, Ma - Engineers,Wanasheria, Internal Auditors!
Kila Sekta iko Katika Halmashauri husika ndo maana zinaitwa " SERIKALI ZA MITAA"!
Halafu na wewe unaweza ukakuta una ka- degree kutoka mojawapo ya Vyuo vikuu hivi vya Kata hapa Nchini!
Elimu ya Tanzania Aibu sana kwani inazalisha misukule badala ya wasomi!
 
Ni masikitiko sana yaani tija inayotokana na sekta binafsi hakuna yaani serikali kwa sasa inategemea mikopo na sekta ya madini,na utalii yaani sekta ghafi ila sio zile za wananchi matokeo yake hali ni mbaya biashara zinajikongoja.Chonde chonde mlio karibu na mkuu mwambieni ukweli msimpambe mnaumiza watanzania wasio na ajira za serikali kwa ajili ya kuchumia matumbo yenu,Mungu anawaona
Leo hii mtu akiomba kazi au kibarua huko mitaani hata pesa ya kula haitoshi
 
Hiyo miradi haiwezi kujengwa huku ukiheshimu utendaji wa mifumo?
mbaya zaidi eti karne hii serikali imekuwa mfanyabiashara,ajabu sana wakati tayari historia imeshaonesha mfumo huo ulikufa,kwa nn serikali isibaki kuwa regulator tuu?
 


Tena?! [emoji14][emoji14][emoji14]

Yamekuwa hayo?!

Kwani kuwa msomi peke yake inatosha kuwa mambo yataenda kwa kadri inavyotakiwa?

Vipi kuhusu swala la uadilifu?

Kwani mambo mengi yalikwama yamekwama sababu ya ukosefu wa elimu wa wahusika?

Utendaji wenye kuleta tija unahitaji zaidi ya kuwa na elimu kutosha.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzoefu na historia umekuwa ukionesha performance ya Halmashauri nyingi haikuwa ya kuridhisha kwa miaka mingi [emoji108][emoji108]

Ikafika mahala hata zile zenye kupata hati safi ni kwamba pengine kwa kuwa walikuwa smati kwenye .......lakini swali la kujiuliza Je hizo Halmashauri zilizopata hati safi Je akija auditor mwingine huru akawakagua mwishoni atatoka na taarifa ile ile ya hati safi au la?

Mambo ni mengi!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
mashaka yangu hata ikikamilika serikali ijayo haiwez kubali kufanya marktime ya kuipa ruzuku wakati haina tija attaipiga chini ijifie hakuna maana kutoa ruzuku na kulipa madeni ya miradi isiyo na tija kwa watu na uchumi
Imagine serikali inadiriki kujenga daraja la kukatiza bahari na maziwa ilhali hadi sasa miaka 5 imefika hakuna barabara za kuunganisha mkoa wa kigoma na kagera,kigoma na katavi,kigoma na mpanda,mbeya tabora,ruvuma na morogoro,usafiri dar bado ni tatizo kubwa sasa hayo madaraja ni ya kazi gani?
 
ukipita mitaani unaumia na kupata na hali ya mambo ,sekta binafsi ndio ingekomboa maelfu ya vijana lakini ndio hivyo wanadanga kwenye uchuuzi
 
Hii dhana imepitwa na wakati ni mulemule tu serikali kufanya biashara kwa mwamvuli wa kuongeza mapato ya halmashauri
Jambo la muhimu na wajibu wa serikali ni kuweka mazingira wezeshi tu ili kuwe na ushindani fair unaowapa fursa sekta binafsi kubuni miradi na biashara serikali ikusanye kodi sio sijui kujenga masoko na kupangisha au kutoza ushuru..Nina orodha ya miradi iliyobuniwa na hao serikali na imekufa wakati imezika pesa nyingi za wananchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…