Mifumo ya Uendeshaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, iangaliwe upya! Watanzania "tutachoka" vibaya sana ndani ya hii miaka 10 ya Mhe. Rais Magufuli

Mifumo ya Uendeshaji wa Serikali ya Awamu ya Tano, iangaliwe upya! Watanzania "tutachoka" vibaya sana ndani ya hii miaka 10 ya Mhe. Rais Magufuli

Umeongea vizuri sana.....

Lakini kwa kuongezea tu kwenye hoja yako ni kuwa ishu si kutekelezwa ama kutotekelezwa kwa mega development projects kama vile mradi wa umeme wa Stiglers Gorge, ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), ufufuaji Airline Charter ya nchi (ATCL) nk nk....

Na nadhani tuwaambie wote na serikali kwa ujumla kuwa, hakuna anayepinga nchi kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya maendeleo kama inavyotajwa....

Sisi wakosoaji (na nadhani ndiyo lengo na mantiki ya makala hii ya Fumadilu Kalimanzila), pamoja na nia njema ya miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na nchi yetu, lakini tunataka mambo yafuatayo mambo yafuatayo yaende sambamba na hayo;

å MOSI, kuwe na uwiano ulio sawa kati ya maendeleo ya vitu na wakati huo huo tukiwaangalia watu kwa kuhakikisha kuwa wana uwezo wa kuuza na kununua, wana uwezo wa kumudu kupata mahitaji yao muhimu ya kila siku nk. Wengine wanasema tuangalie maendeleo ya watu zaidi kuliko vitu....!!!

Ukichunguza sana utagundua kuwa popote palipo na mitafaruku na migongano ya kijamii, chanzo chake ni watu kuchoka kwa kushindwa kumudu kupata mahitaji yao ya kila siku....

Kwa lugha rahisi na ya kueleweka, ni kuwa, fedha kuwa mikononi mwa wachache hususani tabaka la watawala huku wananchi wanyonge walio mengi kwa zaidi ya 95% wakiachwa bila kitu....!!

å MBILI, tabaka la WATAWALA na WATOA MAAMUZI liache kuhodhi nguvu ya watu kutoa maoni yao, hisia zao.....

Kwa lugha rahisi kabisa, tuachilie demokrasia ishike mkondo wake sawasawa na katiba na sheria zetu zinavyotuongoza.....

å TATU, tuachilie mifumo ya kiutawala na kisheria ifanye kazi pasipo kuingilia....

Mwandishi wa makala tunayoijadili ameeleza vizuri sana kuhusu hili....

Kwamba, ilivyo sasa Binge, Mahakama na vyombo vingine vyote vinavyosimamia mwenendo wa kijamii kama polisi, TISS, ofisi ya CAG, msajili wa vyama vya siasa viko compromised na Executive (kwa maana ya Rais)

Bunge haliko huru kabisa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba. Vivyo hivyo mahakama ukiachilia mbali Jaji na Hakimu mmoja mmoja....

Executive hujiamulia tu mambo ikiwemo kupanga matumizi ya fedha za umma huku kazi hiyo kikatiba na kisheria ikiwa ni ya Binge la wananchi na hakuna wa kuuliza....!!

MWISHO, namalizia tena kwa kusema, hakuna mwenye ishu na miradi mikubwa ya maendeleo. Na in fact, hakuna asemaye ni mibaya haina faida kwa nchi na watu sasa na hususani miaka mingi ijayo....

The problem ni namna inavyotekelezwa kwa maamuzi ya mtu mmoja aitwaye Rais. Na yeyote anayejaribu kuhoji, anaweza kujikuta amepotea ama kufa kabisa.....

Ndipo hapo watu tunajiuliza, kulikoni? Kuna nia njema kweli kwenye hii miradi? Na je, ni miradi ya wananchi kweli au ni ya viongozi tu kupigia fedha za umma?

Na mara nyingi sana miradi inayoanzishwa kwa njia za ulaghai laghai siku zote huwa siyo sustainable na hata ukamilikaji huwa ni wa taabu sana....

Mfano halisi ni mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Kwa kuwa ulianzishwa kilaghai, ndo hivyo tena umeishia njiani....

Who knows, kwamba, miradi kama ya SGR na Bwawa la uzalishaji umeme la Stiglers Gorge haitakuja kukumbwa na dhahama kama ulivyoikumba Bandari ya Bagamoyo??

Are we sure kuwa aliyeanzisha projects hizi Bwana Pombe Magufuli atakuwepo kesho au keshokutwa?

Anaweza kufa ama asiwe Rais tena in just a near future. Na akiondoka kwa namna yoyote ile, maana yake atakuwa ameondoka na SGR yake kama Kikwete alivyoondoka Bandari ya Bagamoyo!!

Tuache mifumo itende kazi yake. Maamuzi ya mtu mmoja tu katika nchi bila kuwa CHECKED and BALANCED ni janga kwa taifa....

Ndivyo ilivyo katika TZ yetu leo
Iko hivi ili uendelee lzm uweke uwiano Wa maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu.Cuba Ina maendeleo ya watu kuliko maendeleo ya vitu.Nchi za scandinavia zinamaendeleo ya watu na vitu.Ethiopia,North Korea zina maendeleo ya vitu kuliko watu.
 
Iko hivi ili uendelee lzm uweke uwiano Wa maendeleo ya watu na maendeleo ya vitu.Cuba Ina maendeleo ya watu kuliko maendeleo ya vitu.Nchi za scandinavia zinamaendeleo ya watu na vitu.Ethiopia,North Korea zina maendeleo ya vitu kuliko watu.

Nakubaliana na wewe na ndiyo hoja yangu....

Nisome vizuri hapo juu nimelieleza hili kwa kirefu sana....

Kwahiyo, tunakubaliana 100% kwenye hili
 
Hao wataalamu wanaoatakiwa kushauri hayo hawapo? au wamebaki kuimba sifa kukwepa kurudishwa jalalani
 
Fumadilu Kalimanzila na Kitaturu:
Asanteni kwa bandiko zuri na la kufungia mwaka ( kwangu Mimi)! Mmejadili kwa hekima na busara bila kutumia lugha ya maudhi ambayo ingewavuta wale wenye Noah nyeusi jirani yenu!
Ni sahihi sana wanasiasa wanaposimama majukwaani kunadi juu ya kukua kwa uchumi Basi wawe na uhakika wa kauli na tafiti zao kwani kiuhalisia Hali ni tofauti mno mtaani!
Pia hebu Hawa wapambe nuksi waambiwe ukweli kuwa hawamsaidii rais Bali wanajirahisishia wao kuishi vizuri! Kitendo Cha kuiweka mfukoni bunge, nec, mahakama na ofisi ya dpp na cag sio afya kwa ustawi wa taifa kenye kujinadi kuilinda amani! Ni wakati sasa, rais anapoitafakari xmass atafakari juu ya Uhuru wa mihimili mingine kutenda kwa mujibu wa katiba kwani vyote vinajenga nchi moja!
 
Kama
Hilo la Wakurugenzi wa Halmashauri kukopa hapana aisee?!

Hata mimi binafsi siliungi mkono!

Tena sikuwahi kuwaza kama kitu cha namna hiyo kinaweza kufanyika kwenye Halmashauri zetu nchini.

Wao waimarishe ukusanyi wa mapato, wabuni vyanzo vya mapato visivyoumiza watu.

Ruzuku na OCs wanazipewa wachanganye pamoja kisha watekeleze miradi ya maendeleo kwa ufanisi mkubwa


Sent using Jamii Forums mobile app
Kama hujui kitu usishupaze shingo! Ruhusu akili yako kujifunza vitu usivyovijua!

Na Elimu yako ya shule ya kata ukishatupiwa li nguo za kijani ukavaa basi unaona wewe ni mjuaji!

Halmashauri za Mji,Manispaa ni Serikali zilizokamilika,kuna Baraza la Madiwani ( ambalo kazi yake ni kama Bunge),Mkurugenzi kama Mtendaji Mkuu wa Halmashauri na Wakuu wake wa Idara na Baraza la Madiwani wanaweza kubuni miradi kwa ajili ya Wananchi.

Hivyo wanaweza kukopa kwa ajili ya miradi ambayo ni "income generating" na hivyo kuleta tija ikipangwa na kusimamiwa vizuri!

Miradi kama Stendi za Mabasi, Majosho, Masoko ,Minada, Machinjio,Vyoo vya Kisasa n.k ni aina ya miradi inayobuniwa na kusimamiwa na Halmashauri chini ya Wakurugenzi na kuharakisha maendeleo ya maeneo husika badala ya kusubiri kila kitu mpaka Rais aseme au atoe fedha!

Kwanza Rais anatoa fedha wapi?! Fedha ni za wa Watanzania wote na hata Rais kwa mujibu wa sheria anapangiwa matumizi yake ambayo yanaidhinishwa na Bunge!

Acheni ujinga utawala wa sheria lazima ufuatwe ( Rule of Law should prevail)!
 
Naandika waraka huu mfupi nikitambua kuwa kuna watu leo katika Nchi hii hawataki kusikia mawazo mbadala wala kukosolewa kwa mwenendo wa Serikali ya Awamu ya Tano.

Mhe.Rais Magufuli chukua muda sikiliza pia mawazo mbadala kutoka kwa watu ambao hawakusifii tu!

Mhe.Rais Mstaafu Benjamin Mkapa amekiri katika kitabu chake cha My Life, My Purpose kuwa kuna "wahuni" walimpotosha!

Lakini kumbuka alikuwa bingwa wa kuita wenye mawazo tofauti na yeye Wavivu wa kufikiri, leo yako wapi?!

Mhe.Rais Kikwete amelifanyia Taifa hili mambo mengi pia mazuri tena kwa unyenyekevu na uungwana wa hali ya juu!

Wakati wake kuna wapambe nuksi walikuwa hawawezi kumuita Mhe.Kikwete bila kuanza na neno "Dakta" tena kwa mbwembwe kweli! leo neno "Dakta" wamelisahau kabisa!

Hata wewe Mhe.Rais wetu Dr. Magufuli umezungukwa na wachumia tumbo wengi kweli ambao hawakwambii ukweli!

Wanajitahidi sana kutaja majina yako yote manne tena kwa mbwembwe ila wengine tunajua tu ni unafiki wa kutengenezea Ugali.

Kama unadhani nasema uongo Mhe.Rais Magufuli naomba uniwie radhi lakini nakuhakikishia tukiwa hai hapo utakapo kabidhi kijiti cha Urais pengine ukawa Rais Mstaafu utakayebezwa kuliko wenzako wote!

Na hata hawa wachumia tumbo uliowapa nafasi wanashindana kukutaja muda wote kwa majina manner(4) ya " Dokta John Pombe Joseph Magufuli" watapungua sana ama hutawasikia kabisa, na hata huko Chato hutawaona kabisa!

Ninatoa ushauri huu nikiamini kuwa viongozi tunapowachagua ni katika dhana ya kuwatanguliza mbele ili muongoze njia lakini si kwamba nyie mnajua kila kitu na mna hatimiliki ya kuhodhi mawazo na ubunifu wa kila jambo !

Mhe.Rais Dr.Magufuli hebu jaribu kuangalia kwamba Mfumo wako wa Utawala umeziua Halmashauri za miji,majiji na manispaa! ( ugatuzi wa madaraka haupo) ,kila kitu ni wewe tu ndo mpaka uamue!

Hii si sawa Tanzania ni Nchi kubwa! na Wananchi wanapaswa kujiamulia mambo yao kwa upana! Mwl.Nyerere alisisitiza sana umuhimu wa Serikali za Mitaa zenye Nguvu!

Hivi karibuni umepiga marufuku Wakurugenzi wasikope wasubiri Serikali iwape pesa za kujiendesha, hii si sawa unachelewesha maendeleo!

Pendekezo langu kwako ni kuwa rejesha Wizara ya TAMISEMI chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu ,maana hata Waziri Mkuu kwa sasa ni sawa tu na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum!

Kingine Mhe.Rais Dr.Magufuli tambua kuwa popote Duniani Serikali ndiye mchezeshaji Mkuu wa Uchumi katika Nchi husika!

Leo wewe mifumo yako ya uendeshaji wa Nchi inaua sekta binafsi ( Private sector) na hata Ma- Guru wa sekta Binafsi wanaondoka nayo ( refer Mzee Mengi na Ali Mufuruki).These Guys knew the truth na perhaps wamemezwa na Depression tu!

Leo kuna vitu kama "Force Account" ,NHC,TBA na Suma JKT ndio Contractors wanaofanya kazi za Serikali!

Mhe.Rais watu wako watapata fedha kutoka wapi na kwa kazi zipi?

Rais Barack Obama alivyoingia madarakani nchini Marekani wakati wa recession alichofanya ni kuingiza fedha mitaani kupitia kufufua miradi mikubwa ya ujenzi na kupunguza budget za Vita ya Afghanistan na Iraq.

Wachumia tumbo waliokuzunguka wanakudanganya Mhe.Rais wetu,hawakuambii ukweli!

Uendeshaji wako wa Nchi unawafukarisha Watanzania wengi!

Mhe.Rais Dr.Magufuli kuhusu uchapaji kazi wako sijawahi kuwa na mashaka nawe hata kidogo.Wewe ni mchapakazi kweli kweli na kwa hili vizazi vingi katika Taifa hili vitakukumbuka Mzee.

Ila kwenye eneo la uzalishaji ( productivity) nina mashaka sana na taarifa tunazopewa na Serikali yako!

Umenunua Ndege, Unajenga Reli,Unajenga Stiglers Gorge na Structures kibao zingine na unasema kwa fedha za Ndani!

Fedha za Ndani zipi? Mbona Deni la Taifa tunaambiwa ulikuta ni Trillion 29 na leo limepanda hadi Trillion 52!

Kwanini Deni hilo lipande kama kuna uzalishaji na uwekezaji wa maana?!

Maana kuongezeka kwa uzalishaji na uwekezaji ndo kuongezeka kwa mapato (Kodi) ya Serikali ambayo tungesema ndiyo unatumia kujenga hiyo miundombinu!

Kuongezeka kwa Deni la Taifa ni kielelezo cha kutokuwepo kwa ongezeko katika uzalishaji na uwekezaji na matokeo yake ndo ukosefu wa ajira tunaouona katika kipindi chako!

Sekta binafsi imekufa na haiwezi kuajiri na pia Serikali yako haiajiri japo kuna matamko eti Rais kasema waajiriwe elfu 40!

Mhe.Rais hutakiwi wewe useme watu waajiriwe kanuni za uchumi uzungumza zenyewe!

Automatically waajiriwa huuitajika pale uchumi unapo- perform!

Mhe.Rais Dr.Magufuli niwie radhi nirudie kauli ya yule Mtanzania pale Igunga!

Mhe.Rais ACHIA HELA! Serikali yako imeua Liquidity katika Mabenki! Rudisha fedha kwenye commercial banks toka BOT ili watu wakopeshwe wafanye kazi!

Watu wenye nguvu sasa wameamua kukaa vijiweni wanapiga soga,wana bet n.k hakuna mitaji!

Naomba kwa leo niishie hapa Mhe.Rais.

Mhe.Rais Dr.Magufuli nakutakia wewe pamoja na Mama yetu mpendwa Mama Janet Magufuli heri ya Christmas na Mwaka Mpya 2020.
MTAJI NI AKILI YAKO........ACHA UJINGA.......
 
Hao
Fumadilu Kalimanzila,

Wewe huoni hizi Mega projects zinazoendelea, unafikiri duniani kuna nchi haikopi? USA mwenyewe ana madeni sembuse TZ

Kwasasa tunajenga nchi waambie wawe wavumilivu, wajukuu zao watafaidi sana na waendelee kuchagua CCM na JPM 2020 maana nchi inajengwa na jemedari JPM kwa manufaa ya baadaye na ikiwezekana hata wafanye kazi bila mishahara..

Hao wafanya biashara ni wapiga dili na huko benki walikuwa wapiga dili na wezi CHADEMA sasa jemedari JPM ananyoosha njia wezi wote chali na sasa amerudisha weledi na utiifu kila mahala, heko JPM.

Tuwe wazelendo tumuunge mkono jembe letu JPM, maana watu wa hivi wanapatikana mara moja kama kakakuona.. Ni neema kwa watanzania kumpata JPM tumlinde na tumuongezee ulinzi ikiwezekana mabeberu wasije kumdhuru...
Hao wajukuu tutawanunua toka China?Babu zao wanakomolewa ili wao wake wafaidike?Hiyo ni kanuni gani ya maisha?
Hivi maendeleo hufanyika kwa ajili ya watu waliopo au wajao?Ndiyo Sera ya Dr.JPJM au chama chake?
 
Kama

Kama hujui kitu usishupaze shingo! Ruhusu akili yako kujifunza vitu usivyovijua!

Na Elimu yako ya shule ya kata ukishatupiwa li nguo za kijani ukavaa basi unaona wewe ni mjuaji!

Halmashauri za Mji,Manispaa ni Serikali zilizokamilika,kuna Baraza la Madiwani ( ambalo kazi yake ni kama Bunge),Mkurugenzi kama Mtendaji Mkuu wa Halmashauri na Wakuu wake wa Idara na Baraza la Madiwani wanaweza kubuni miradi kwa ajili ya Wananchi.

Hivyo wanaweza kukopa kwa ajili ya miradi ambayo ni "income generating" na hivyo kuleta tija ikipangwa na kusimamiwa vizuri!

Miradi kama Stendi za Mabasi, Majosho, Masoko ,Minada, Machinjio,Vyoo vya Kisasa n.k ni aina ya miradi inayobuniwa na kusimamiwa na Halmashauri chini ya Wakurugenzi na kuharakisha maendeleo ya maeneo husika badala ya kusubiri kila kitu mpaka Rais aseme au atoe fedha!

Kwanza Rais anatoa fedha wapi?! Fedha ni za wa Watanzania wote na hata Rais kwa mujibu wa sheria anapangiwa matumizi yake ambayo yanaidhinishwa na Bunge!

Acheni ujinga utawala wa sheria lazima ufuatwe ( Rule of Law should prevail)!


Huu mchezo hauhitaji hasira [emoji3][emoji3]

Kwa hiyo umeleta uzi ukitarajia watu wote tukuunge mkono?

Hataki kupokea mawazo tofauti tofauti?

Je kwa kufanya hivyo unazani utakuwa unatutendea haki wote?

Hili ni jukwaa huru kwa majadiliano, jifunze kustahamili na kuwa tayari kupata mawazo tofauti na mbadala.

Usikasirike maana mwisho wake huwa ni kutenda dhambi!

Though umeshafanya inakubidi ufanye toba!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo miradi huwa ni rasmi?

Je huwa inafanyiwa visibility study kabla ya utekezaji ili kuona kama itakuwa na tija?

Je wataalam walosomea Projects management wapo?

Je huwa wanafahamu ku identify risks in advance na namna ya kuzi manage?

Je nidhamu ya matumizi ya umma ya Halmashauri nyingi uzoefu ukoje?

Hayo ni maswali machache ya kujiuliza kwanza.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Usishangae fedha ya mkopo ilokusudiwa kwaajili ya miradi fulani isitumike ilivyokusudia badala yake watu inatumika kulipana posho na misreallocations chungu nzima!

Mikono inagharama kubwa kupitia riba kwa hiyo ni maamuzi ambayo yanapaswa kuwa magumu kufanyika .

Sasa mwerevu akiona mtu anaona swala la kukopa kuwa jepesi na rahisi tunaanza kujiuliza kwanini?






Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilizani ungenitaka kujustify hoja yangu badala yake mwenzangu naona unapanic [emoji14][emoji14]

Inabidi uwe na kifua!


Sent using Jamii Forums mobile app

OK sorry,kama nime - over react ! Unajua tatizo linalochosha kwa Watanzania wengi ni kwamba Watanzania wengi ni myopic lakini wanajifanya wajuaji sana!
Nchi zote zilizopiga hatua kubwa zinaendeshwa kwa mifumo imara na si "Watu" imara!
 
Hiyo miradi huwa ni rasmi?

Je huwa inafanyiwa visibility study kabla ya utekezaji ili kuona kama itakuwa na tija?

Je wataalam walosomea Projects management wapo?

Je huwa wanafahamu ku identify risks in advance na namna ya kuzi manage?

Je nidhamu ya matumizi ya umma ya Halmashauri nyingi uzoefu ukoje?

Hayo ni maswali machache ya kujiuliza kwanza.


Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe kojoa ukalale, nadhani naongea na " MTU" kumbe " Chicken "!
Halmashauri zina Wakurugenzi tena wasomi hadi ngazi ya PhD! Wakuu wa Idara wasomi kabisa! Wachumi, Ma - Engineers,Wanasheria, Internal Auditors!
Kila Sekta iko Katika Halmashauri husika ndo maana zinaitwa " SERIKALI ZA MITAA"!
Halafu na wewe unaweza ukakuta una ka- degree kutoka mojawapo ya Vyuo vikuu hivi vya Kata hapa Nchini!
Elimu ya Tanzania Aibu sana kwani inazalisha misukule badala ya wasomi!
 
samurai,
Ni sawa ila utambue tu kuwa Shibe yako ni ya muda mfupi tu! Tukiwa hai miaka 10 si mingi utakosa mahali pa kuficha uso na tumbo lako! Sisi tunaongelea mifumo mibovu ya uendeshaji wa mifumo!

Kama kuna miujiza inafanywa na Serikali ya Awamu ya 5,mbona hujibu hoja ya kupaa kwa Deni la Taifa kutoka trillioni 29 hadi trillioni 52 ndani ya miaka 4!

Hakuna Uchumi unaokua hapo ni uzuzu wako tu ndo unakudanganya! Leo Ajiri hakuna na walioajiriwa na Serikali wanasaga meno hakuna nyongeza ya Mishahara ndani ya miaka 4!

Na hata ukitaka kujiajiri mazingira ni magumu mno, Mabenki yamechoka na hayana pesa! Nenda Benki yoyote kati ya tarehe 15 na 19 kila mwezi uone huo Uchumi unavyokuwa kwa kasi!

Tarehe hizo Ma - Teller wa Bank wanapiga miayo tu!

Nenda Kariakoo uone Wananchi walivyochoka!
Ni masikitiko sana yaani tija inayotokana na sekta binafsi hakuna yaani serikali kwa sasa inategemea mikopo na sekta ya madini,na utalii yaani sekta ghafi ila sio zile za wananchi matokeo yake hali ni mbaya biashara zinajikongoja.Chonde chonde mlio karibu na mkuu mwambieni ukweli msimpambe mnaumiza watanzania wasio na ajira za serikali kwa ajili ya kuchumia matumbo yenu,Mungu anawaona
Leo hii mtu akiomba kazi au kibarua huko mitaani hata pesa ya kula haitoshi
 
Hiyo miradi haiwezi kujengwa huku ukiheshimu utendaji wa mifumo?
mbaya zaidi eti karne hii serikali imekuwa mfanyabiashara,ajabu sana wakati tayari historia imeshaonesha mfumo huo ulikufa,kwa nn serikali isibaki kuwa regulator tuu?
 
Wewe kojoa ukalale, nadhani naongea na " MTU" kumbe " Chicken "!
Halmashauri zina Wakurugenzi tena wasomi hadi ngazi ya PhD! Wakuu wa Idara wasomi kabisa! Wachumi, Ma - Engineers,Wanasheria, Internal Auditors!
Kila Sekta iko Katika Halmashauri husika ndo maana zinaitwa " SERIKALI ZA MITAA"!
Halafu na wewe unaweza ukakuta una ka- degree kutoka mojawapo ya Vyuo vikuu hivi vya Kata hapa Nchini!
Elimu ya Tanzania Aibu sana kwani inazalisha misukule badala ya wasomi!


Tena?! [emoji14][emoji14][emoji14]

Yamekuwa hayo?!

Kwani kuwa msomi peke yake inatosha kuwa mambo yataenda kwa kadri inavyotakiwa?

Vipi kuhusu swala la uadilifu?

Kwani mambo mengi yalikwama yamekwama sababu ya ukosefu wa elimu wa wahusika?

Utendaji wenye kuleta tija unahitaji zaidi ya kuwa na elimu kutosha.





Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uzoefu na historia umekuwa ukionesha performance ya Halmashauri nyingi haikuwa ya kuridhisha kwa miaka mingi [emoji108][emoji108]

Ikafika mahala hata zile zenye kupata hati safi ni kwamba pengine kwa kuwa walikuwa smati kwenye .......lakini swali la kujiuliza Je hizo Halmashauri zilizopata hati safi Je akija auditor mwingine huru akawakagua mwishoni atatoka na taarifa ile ile ya hati safi au la?

Mambo ni mengi!


Sent using Jamii Forums mobile app
 
samurai,
Hio miradi hata ikijakamilika japo atujui uhakika wa kukamilika kwake itamsaidia vipi mtu aliyepigika maana itakuwa ni mapambo kama hakuna purchasing power uwezo Wa watu kuitumia.Mfano ATC nauli mwanza dar si chini ya laki tano kwenda na kurudi hali fastjet ilikuwa laki na nusu,kwann zisiende tupu,hio sgr usidhani nauli itakuwa buku si chini ya laki au zaidi kwa purchasing power nani atamudu ili irudishe Pesa?
mashaka yangu hata ikikamilika serikali ijayo haiwez kubali kufanya marktime ya kuipa ruzuku wakati haina tija attaipiga chini ijifie hakuna maana kutoa ruzuku na kulipa madeni ya miradi isiyo na tija kwa watu na uchumi
Imagine serikali inadiriki kujenga daraja la kukatiza bahari na maziwa ilhali hadi sasa miaka 5 imefika hakuna barabara za kuunganisha mkoa wa kigoma na kagera,kigoma na katavi,kigoma na mpanda,mbeya tabora,ruvuma na morogoro,usafiri dar bado ni tatizo kubwa sasa hayo madaraja ni ya kazi gani?
 
Halafu wenye takataka kichwani humu wanakalia kuimba sifa!!
Inachofanya serkali ni uharamia dhidi ya jamii. Maelfu tayari wako vijiweni kwa jina la Machinga, na kama haitoshi bado secta binafsi inayoweza kukomboa watu nayo inatazamwa kwa jicho la husuda na watawala ambao wanapaswa kuisaidia ili iajiri zaidi.
Nafikiri kuna kitu si sawa kichwani kwa watawala hawa wa awamu ya tano japo tunajua CCM ni ile ile tangu kale!!!
ukipita mitaani unaumia na kupata na hali ya mambo ,sekta binafsi ndio ingekomboa maelfu ya vijana lakini ndio hivyo wanadanga kwenye uchuuzi
 
Kama

Kama hujui kitu usishupaze shingo! Ruhusu akili yako kujifunza vitu usivyovijua!

Na Elimu yako ya shule ya kata ukishatupiwa li nguo za kijani ukavaa basi unaona wewe ni mjuaji!

Halmashauri za Mji,Manispaa ni Serikali zilizokamilika,kuna Baraza la Madiwani ( ambalo kazi yake ni kama Bunge),Mkurugenzi kama Mtendaji Mkuu wa Halmashauri na Wakuu wake wa Idara na Baraza la Madiwani wanaweza kubuni miradi kwa ajili ya Wananchi.

Hivyo wanaweza kukopa kwa ajili ya miradi ambayo ni "income generating" na hivyo kuleta tija ikipangwa na kusimamiwa vizuri!

Miradi kama Stendi za Mabasi, Majosho, Masoko ,Minada, Machinjio,Vyoo vya Kisasa n.k ni aina ya miradi inayobuniwa na kusimamiwa na Halmashauri chini ya Wakurugenzi na kuharakisha maendeleo ya maeneo husika badala ya kusubiri kila kitu mpaka Rais aseme au atoe fedha!

Kwanza Rais anatoa fedha wapi?! Fedha ni za wa Watanzania wote na hata Rais kwa mujibu wa sheria anapangiwa matumizi yake ambayo yanaidhinishwa na Bunge!

Acheni ujinga utawala wa sheria lazima ufuatwe ( Rule of Law should prevail)!
Hii dhana imepitwa na wakati ni mulemule tu serikali kufanya biashara kwa mwamvuli wa kuongeza mapato ya halmashauri
Jambo la muhimu na wajibu wa serikali ni kuweka mazingira wezeshi tu ili kuwe na ushindani fair unaowapa fursa sekta binafsi kubuni miradi na biashara serikali ikusanye kodi sio sijui kujenga masoko na kupangisha au kutoza ushuru..Nina orodha ya miradi iliyobuniwa na hao serikali na imekufa wakati imezika pesa nyingi za wananchi
 
Back
Top Bottom