Umeongea vizuri sana.....
Lakini kwa kuongezea tu kwenye hoja yako ni kuwa ishu si kutekelezwa ama kutotekelezwa kwa mega development projects kama vile mradi wa umeme wa Stiglers Gorge, ujenzi wa Reli ya kisasa (SGR), ufufuaji Airline Charter ya nchi (ATCL) nk nk....
Na nadhani tuwaambie wote na serikali kwa ujumla kuwa, hakuna anayepinga nchi kuwekeza kwenye miradi mikubwa ya maendeleo kama inavyotajwa....
Sisi wakosoaji (na nadhani ndiyo lengo na mantiki ya makala hii ya Fumadilu Kalimanzila), pamoja na nia njema ya miradi mikubwa ya maendeleo inayotekelezwa na nchi yetu, lakini tunataka mambo yafuatayo mambo yafuatayo yaende sambamba na hayo;
å MOSI, kuwe na uwiano ulio sawa kati ya maendeleo ya vitu na wakati huo huo tukiwaangalia watu kwa kuhakikisha kuwa wana uwezo wa kuuza na kununua, wana uwezo wa kumudu kupata mahitaji yao muhimu ya kila siku nk. Wengine wanasema tuangalie maendeleo ya watu zaidi kuliko vitu....!!!
Ukichunguza sana utagundua kuwa popote palipo na mitafaruku na migongano ya kijamii, chanzo chake ni watu kuchoka kwa kushindwa kumudu kupata mahitaji yao ya kila siku....
Kwa lugha rahisi na ya kueleweka, ni kuwa, fedha kuwa mikononi mwa wachache hususani tabaka la watawala huku wananchi wanyonge walio mengi kwa zaidi ya 95% wakiachwa bila kitu....!!
å MBILI, tabaka la WATAWALA na WATOA MAAMUZI liache kuhodhi nguvu ya watu kutoa maoni yao, hisia zao.....
Kwa lugha rahisi kabisa, tuachilie demokrasia ishike mkondo wake sawasawa na katiba na sheria zetu zinavyotuongoza.....
å TATU, tuachilie mifumo ya kiutawala na kisheria ifanye kazi pasipo kuingilia....
Mwandishi wa makala tunayoijadili ameeleza vizuri sana kuhusu hili....
Kwamba, ilivyo sasa Binge, Mahakama na vyombo vingine vyote vinavyosimamia mwenendo wa kijamii kama polisi, TISS, ofisi ya CAG, msajili wa vyama vya siasa viko compromised na Executive (kwa maana ya Rais)
Bunge haliko huru kabisa kutekeleza wajibu wake wa kikatiba. Vivyo hivyo mahakama ukiachilia mbali Jaji na Hakimu mmoja mmoja....
Executive hujiamulia tu mambo ikiwemo kupanga matumizi ya fedha za umma huku kazi hiyo kikatiba na kisheria ikiwa ni ya Binge la wananchi na hakuna wa kuuliza....!!
MWISHO, namalizia tena kwa kusema, hakuna mwenye ishu na miradi mikubwa ya maendeleo. Na in fact, hakuna asemaye ni mibaya haina faida kwa nchi na watu sasa na hususani miaka mingi ijayo....
The problem ni namna inavyotekelezwa kwa maamuzi ya mtu mmoja aitwaye Rais. Na yeyote anayejaribu kuhoji, anaweza kujikuta amepotea ama kufa kabisa.....
Ndipo hapo watu tunajiuliza, kulikoni? Kuna nia njema kweli kwenye hii miradi? Na je, ni miradi ya wananchi kweli au ni ya viongozi tu kupigia fedha za umma?
Na mara nyingi sana miradi inayoanzishwa kwa njia za ulaghai laghai siku zote huwa siyo sustainable na hata ukamilikaji huwa ni wa taabu sana....
Mfano halisi ni mradi wa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo. Kwa kuwa ulianzishwa kilaghai, ndo hivyo tena umeishia njiani....
Who knows, kwamba, miradi kama ya SGR na Bwawa la uzalishaji umeme la Stiglers Gorge haitakuja kukumbwa na dhahama kama ulivyoikumba Bandari ya Bagamoyo??
Are we sure kuwa aliyeanzisha projects hizi Bwana Pombe Magufuli atakuwepo kesho au keshokutwa?
Anaweza kufa ama asiwe Rais tena in just a near future. Na akiondoka kwa namna yoyote ile, maana yake atakuwa ameondoka na SGR yake kama Kikwete alivyoondoka Bandari ya Bagamoyo!!
Tuache mifumo itende kazi yake. Maamuzi ya mtu mmoja tu katika nchi bila kuwa CHECKED and BALANCED ni janga kwa taifa....
Ndivyo ilivyo katika TZ yetu leo