Migogoro mingi inayotokea maeneo ya kazi inatokana na wanandoa kutotimiza wajibu wao wa kupeana tendo la ndoa

Migogoro mingi inayotokea maeneo ya kazi inatokana na wanandoa kutotimiza wajibu wao wa kupeana tendo la ndoa

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Nikiwaambia 'banduaneni' kila wakati kama nifanyavyo ili muwe na Furaha na Wachangamfu muda wote mnaniona Muhuni
.......................................................................................................................................................................................................................................................

Iringa. Tatizo la wanandoa kushindwa kupeana tendo la ndoa limetajwa kuleta madhara kazini kutokana na wafanyakazi wengi kwenda kazini wakiwa na hasira na chuki zinazotokana na kutoridhishwa kimwili.

Mkuu wa dawati la jinsia mkoani Iringa, Elizabeth Swai amesema migogoro mingi inayotokea maeneo ya kazi inatokana na wanandoa kutotimiza wajibu wao wa kupeana tendo la ndoa.

Swai ameyasema hayo leo Jumapili Juni 16, 2024 mjini Iringa alipokuwa akifungua semina kwa watumishi na wanafunzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa.

Amesema tatizo hilo linawakumba hasa wanawake na huwafanya wengi wao kwenda kazini wakiwa na chuki inayotokana na kutotimiziwa haja ya tendo la ndoa.

"Mtu asipotimiziwa kwa kutokupewa inaleta madhara hata kazini hasa wanawake wanakuwa na hasira sana," amesema Swai.

Aidha, ametoa rai kwa wanandoa wajitahidi kuwajibika katika kupeana tendo la ndoa kwa sababu linapunguza kwa kiwango kikubwa migogoro ndani ya ndoa inayochangia matukio ya kujeruhiana na hata vifo.

Amesema kwa mwanaume akiwa na uhitaji na mwanamke akimnyima tendo la ndoa akili huwa zinaruka, hali inayosababisha achukue sheria mkononi kwa kufanya vitendo vya ukatili kwa mwenza wake.

"Mjitahidi sana kuwajibika kwa kupeana, msinyimane, kwa sababu linapunguza sana migogoro ndani ya ndoa. Mwanaume akiwa na uhitaji wa mwanamke halafu umnyime, akili huwa zinawaruka na kujikuta wanafanya ukatili,” amesema Swai.

Chanzo: mwananchi_official

Na mnaambiwa pia kuwa Wanaume na Wanawake wapenda Ngono / Mbanduano sana ndiyo wenye Akili / Werevu.
 
Inategemea pia na aina ya vyakula unavyokula,muhimu sn hii kitu,na kwa maisha ya kule wengi hawali vzr ilawanavita sigara na pombe so unakuta mama hatimiziwi vzr,but ili uwe na nguvu lazima ule vyakula vya protini iliupate nguvu
 
Mwanamke anaweza kutoa kabisa kwenye reli, we jamaa unahitaji therapy kwa yaliokukuta
 
Back
Top Bottom