Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

Migogoro ya kimahusiano: Janga kwa Wanawake Tanzania

ShesRise_1

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2025
Posts
22,235
Reaction score
51,111
Angalizo msomaji wangu bandiko ni refu kidogo
Naomba uwe mvumikivu katika usomaji wako
Karibu sana kwenye mada 😊

Hello Great Thinkers 🫡

Katika pita pita zangu huko IG nimekuta kuna dada mmoja amepost kuhusu vifo vinavyotokana na migogoro ya kimahusiano hapa Tanzania 🇹🇿

Nimekuwa shocked baada ya kuona takwimu zinaogopesha na kushangaza
Ikanisukuma niende kwenye mtandao ku search na nione hali ilivyo kwa kujihakikishia mimi tomaso nimeshtushwa
Sikujua hali ni mbaya kwa ukubwa huu!

Nimepigwa butwaa
Hali inatisha

Chanzo cha takwimu (LHRC Tanzania)

Niweke sawa hapa
Hizi takwimu ni kati ya mwaka 2019_2023

Hebu tuangalie hizi takwimu za mauaji yanayohusisha wenza wa kimapenzi Tanzania

2019: LHRC ilirekodi wanawake 12 waliouawa na waume/wenza wao ambapo 8 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2020: LHRC ilirekodi wanawake 32 waliouawa na waume/wenza wao, ambapo 23 ya matukio hayo yalihusishwa na wivu
Hii ilikuwa zaidi ya mara mbili ya matukio yaliyorekodiwa mwaka 2019

2021: LHRC ilirekodi jumla ya matukio 35 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika hao, 31 walikuwa wanawake na 4 wanaume, huku wanawake wakiwa takribani 89% ya waathirika
Pia, 72% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2022: Kulikuwa na matukio 33 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi
Kati ya waathirika, 31 walikuwa wanawake na 2 wanaume, wanawake wakiwa takribani 94% ya waathirika. 52% ya matukio hayo yalihusishwa na wivu

2023: LHRC ilirekodi matukio 50 ya mauaji yaliyohusisha wenza wa kimapenzi, ikiwa ni ongezeko la matukio 17 ukilinganisha na mwaka 2022
Kati ya waathirika hao, 45 walikuwa wanawake na 5 wanaume, wanawake wakiwa 90% ya waathirika. Takribani 46% ya matukio yalihusishwa na wivu.

Mjumuisho 2019–2023: Jumla ya matukio 162 ya mauaji yaliyorekodiwa katika takwimu hizi. Kati ya waathirika waliotajwa, wanawake ni 151

Mjadala👇

Sitaki kusema hakuna wanawake wanaofanya ukatili
Tumeona wapo na siwezi kufumbia macho hili hata kidogo

Wanawake wenzangu JF hakuna haja ya kukatisha maisha ya mtu kwa sababu tu ya mapenzi au migogoro mbalimbali
Ukiona mzigo ni mkubwa, tafuta msaada
Usimue mtu
Huna haja ya kuua, hilo sio jukumu lako

Kwa sababu hata usipomuua, kwa nature ya mwanadamu kila mtu lazima atakufa siku yake

Nina hakika wanaofanya mauaji huishia kwenye majuto ya milele

Tuje kwa wanaume ambao ni tishio...

Enyi wanaume, acheni kuua wanawake
Hawa ni mama zenu, dada zenu, wadogo zenu
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine kwa sababu tu amesalitiwa, amevunjwa moyo au amekataliwa

Ukihisi umefika sehemu huwezi kujidhibiti, tafuta msaada
Tafuta hata wataalamu wa saikolojia
Kama umechanganyikiwa na hujui ufanye nini, ongea uponeeee

Acha kubeba uchungu peke yako. Tafuta mtu wa kuongea naye
Kama unaogopa jambo lako kutangazwa, tafuta hata mtu asiyekujua, funguka na zungumza

Usiue Please
Hakuna mwenye haki ya kuua mwingine

Kama unaona hakuna future kwenye mahusiano, jikatae mapema na muachane kwa amani

Niseme hili👇
Wanaume, mkubali mkatae, mna udhaifu ambao mnatakiwa kuushinda
Kujifunza kustahimili maumivu rejection usaliti na kuvunjika moyo ni sehemu ya kukomaa

Chukulieni mfano hata hapa jukwaani
Watu wanaoongoza kuwakalia kooni wengine ni wanaume nyie hapo🫵
Nasikia wengine wanapita mpaka PM wakisambaza picha za wanawake ambao hawana hata uhakika nao
Kitu ambacho ni nadra kwa wanawake kufanya

Kuweni wakomavu
Jifunzeni kustahimili

Mbona wanawake wanahangaika na maisha?
Unakuta mama kaachiwa watoto, anakomaa na haui mtu
Amedhulumiwa anatulia

Anamfumania mume wake kitandani, tena na house girl kwenye kitanda chake mwenyewe lakini mama anapiga moyo konde

Mnazalisha nje huko, wanawake wanapiga moyo konde

Enyi wanaume, nyie mna roho za barafu?
Wanawake wana roho za chuma?

Sitetei yeyote
Sitetei mwanamke msaliti wala mwanaume msaliti

Lakini ukiona umeshindwa kabisa kuendelea na mahusiano, achaneni kwa amani

Tatizo ni nini mpaka hali imefika hivi?

Karibu tujadili kwa pamoja
Na kuelemishana 🙏🙏

ShesRise_1 ✋️
 
Ombeeni mahusiano yenu
IMG-20261007-WA0346.jpg
 
Nikiangalia chanzo kikuu hapo naona ni wivu wa mapenzi.

Huu wivu wa mapenzi unasababishwa na nini?

Kwa mtasamo wangu naona sababu ni usaliti, kutokuwa waaminifu kwenye mahusiano kunakofanywa na wanawake.

Kama wanawake wangetulia njia kuu, naamini kwa kiasi kikubwa wangepunguza tatizo la mauaji kwao.

Sasa inaonekana kama vile wanaume ndio wenye mapenzi ya dhati kwa wanawake wao, au kama wanawake huamua kuchepuka ili kulipa kisasi kwa wanaume wao, never know.
 
Back
Top Bottom