Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
washafukuzwa!!! poa sana...wanawasumbua wa private tu!!
ata nisipotaka jua issue ni kwamba kila kitu kina taratibu zake za kufatilia mpk upate ushindi na mkija maofisini nyi ndo mtakuwa mnasumbua wananchi sana mana hamtofata taratibu za kazi...safi big up serikali!!!!fukuza wote hao ambao wamegoma rudisha wasiohusika...fukuzaaa!!!
serikali ina taratibu zake na pia izo taratibu kama zina kasoro huwezi kugoma ni kwamba unafata taratibu za kurekebisha izo policies mana point apa si kutumia nguvu iwe serikali au wanafunzi,ata mgomo una vibali na taratibu zake ingawa ni haki yako ona ata walimu walivofanikiwa na wazee wako njiani kufanikiwa wameamua kufata taratibu na iyo ndo point ambayo nataka nyi ma dent muelewe...rules,regulations and procedures!!!!!huu ni utawala wa haki na sheria kufatwa kama kila mtu akijiamulia ki vyake sidhani kama ata mi na we tungekuwa apa....
washafukuzwa!!! poa sana...wanawasumbua wa private tu!!
Unajua huyo jamaa,asilinganishe utawala wa sheria wa nchi zilizoendelea na hapa Tanzania;kwa kufanya hivyo unapoze/unapotea kabisa(get lost or die).
Hapa Tz hiyo utawala wa sheria ndugu yangu ni kuongelea majukwaani na maandishi;kwa vitendo(practically) hakuna kitu kama hicho.
Mfano mzuri tu,serikali ya Uingereza ilitoa fedha ya kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki na hapa Tanzania hawa wastaafu ambao wanaandamana mpaka leo walitakiwa walipwe fedha yao tangu mwaka 1986 bila mjadala;na ndiyo maana wenzao wa Kenya na Uganda husikii vurugu zozote;kwasababu walishapatiwa chao.
Huo ni mfano mmojawapo mdogo tu,wakukuonyesha serikali ya TZ inavyocheza rafu makusudi.
Kuhusu wanafunzi na mgomo wa kuchangia elimu ya juu,bodi ya mikopo kwa elimu ya juu(HESLB)ilipoanzishwa rasmi wanfunzi walikuwa wanakopeshwa 100% ya gharama za elimu,na kigezo kilikuwa rahisi tu uweupata admission katika chuo husika.
Mwaka uliofuatia,wakaja na hadithi ngumu ambayo kwa mwanfunzi kuielewa ni tatizo ambalo ndiyo linaloendelee mpaka hivi sasa.
Hebu kwa hiyo mifano hai miwili ndugu yangu bado tu utaniambia serikali iko sahihi katika maamuzi yake?!
Ninachoona serikali ya Tanzania(TZ) laana wanazitafuta wenyewe na nafikiri ndiyo maana inakuwa kimeo karibia kwenye kila kitu katika hii sayari inayoitwa dunia.
Kwasababu huuwezi kuwanyanyasa watu kiasi hicho ili hali serikali inapoteza fedha nyingi katika mikataba mibovu,ubinafsi wa viongozi wake(ie.mafisadi),matumizi yasiyokuwa ya lazima(anasa) kwa kujilinganisha na nchi tajiri hapa duniani.
Hivyo basi,huwezi ni kuniambia serikali iko sahihi kwa mimi nilizaliwa hapa TZ na niko hapa hadi hivi sasa hunidanganyi lolote kwenye hiki kichwa cha mwendawazimu(dk.3 mbele dk.3 nyuma)
Chuo cha SUA kimefungwa!!
Kuhusu suala la uwezo wa serikali, ukisoma bandiko la masanja hapo juu ameleza kinaganaga. Ni kweli kuwa serikali ina fedha lakini tukumbuke pia kuwa kuna matatizo mengi ambayo utatuzi wake unahitaji zaidi ya hizo fedha ambazo serikali inazo. tatizo ni kuwa wanafunzi wengi wanachukulia mikopo hii kama misaada-wana malengo ya kutorudisha fedha hizo. ndio maana utawaona wanahusisha masuala ya ufisadi na wao kuomba mikopo. Hoja kwamba "mbona mafisadi wanaiba fedha" unapoiingiza kwenye madai kama haya, unajionyesha kuwa na wewe una lengo la kufisadi pia.
Kuhusu suala la kubadili sera; linahusisha mchakato ambao unawahusisha watu na taasisi kadhaa zinazohusika na sera hiyo. katika hili, si suala la Maghembe au hata Pinda kukaa na kuamua kuwa kuanzia sasa tunaondoa means testing kwenye sera ya mikopo ya elimu ya juu. Inabidi wadau wakae, kukiwa na hoja za msingi kuhusiana na ubaya wa hicho kinachopingwa na wanafunzi na hoja hizo zitapimwa na iwapo itakubaliwa kwua hoja zao ni za msingi, hapo ndipo mchakato wa kuibadili sera hiyo utakapoanza, si waziri kukaa peke yake na kuamua kwa sababu si yeye aliyeiweka sera hiyo peke yake