Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Migomo katika Vyuo Vikuu na serikali ya awamu ya Nne

Mkwawa Iringa nao waligoma jana wanasubili kufukuzwa.
 
washafukuzwa!!! poa sana...wanawasumbua wa private tu!!

Unajua sababu ama mkuu unaweka ushabiki bila kujua wamegoma kwa sababu gani? Ungekuwa umepitia kwenye vyuo vikuu vya Tanzania usingekuja na empty ended statement kama hiyo....pole sana

Ushi Wa Rombo
 
ata nisipotaka jua issue ni kwamba kila kitu kina taratibu zake za kufatilia mpk upate ushindi na mkija maofisini nyi ndo mtakuwa mnasumbua wananchi sana mana hamtofata taratibu za kazi...safi big up serikali!!!!fukuza wote hao ambao wamegoma rudisha wasiohusika...fukuzaaa!!!
 
ata nisipotaka jua issue ni kwamba kila kitu kina taratibu zake za kufatilia mpk upate ushindi na mkija maofisini nyi ndo mtakuwa mnasumbua wananchi sana mana hamtofata taratibu za kazi...safi big up serikali!!!!fukuza wote hao ambao wamegoma rudisha wasiohusika...fukuzaaa!!!

Nadhani hata uwezo wakutafakali issue huna wale wale, wasomi ni wakorofi!!!......serikali nayo ifuate taratibu si ubabe kama unavypendekeza....chuo kikuu ni sehemu wanapotoka intellectuals, kama wachukia wasomi maofisini basi una tatizo zaidi
 
serikali ina taratibu zake na pia izo taratibu kama zina kasoro huwezi kugoma ni kwamba unafata taratibu za kurekebisha izo policies mana point apa si kutumia nguvu iwe serikali au wanafunzi,ata mgomo una vibali na taratibu zake ingawa ni haki yako ona ata walimu walivofanikiwa na wazee wako njiani kufanikiwa wameamua kufata taratibu na iyo ndo point ambayo nataka nyi ma dent muelewe...rules,regulations and procedures!!!!!huu ni utawala wa haki na sheria kufatwa kama kila mtu akijiamulia ki vyake sidhani kama ata mi na we tungekuwa apa....
 
serikali ina taratibu zake na pia izo taratibu kama zina kasoro huwezi kugoma ni kwamba unafata taratibu za kurekebisha izo policies mana point apa si kutumia nguvu iwe serikali au wanafunzi,ata mgomo una vibali na taratibu zake ingawa ni haki yako ona ata walimu walivofanikiwa na wazee wako njiani kufanikiwa wameamua kufata taratibu na iyo ndo point ambayo nataka nyi ma dent muelewe...rules,regulations and procedures!!!!!huu ni utawala wa haki na sheria kufatwa kama kila mtu akijiamulia ki vyake sidhani kama ata mi na we tungekuwa apa....

Total confusion, am sorry sijakuelewa Kabisa!! nieleweshe taratibu ni utawala upi wa haki na sheria hufuatwa Tanzania? I in deep confusion na statement zako...Nimepitia vyuo vikuu vya Bongo, madai yetu yalikuwa haya tekelezwi bila Kunji hata vitu basic, haki ya mtu haiji kwa urahisi kama unavyoota, lazima ilazimishwe mifano unaijua.

Ushi
 
ata kama mlikuwa hamsikilizwi kuna njia nyingi za kusikilizwa sio izo za kitemi thats my point, leo watoto wa primary na secondary wanaona na wao watafanya ivo ivo ndo migomo haiishi vyuoni na ni utoto tuuu!! ombeni vibali vya maandamano ata kama kila wiki vyombo vya habari vipo sidhani kama mtakuwa ignored everytime....kaeni chini pangeni mbinu za amani na za kisasa za kuishinikiza serikali kijana!!
 
washafukuzwa!!! poa sana...wanawasumbua wa private tu!!

Are u sure? how many thse so called private students? Are daughters and sons of corrupt people in the land of Tanzania?

Watch out, I my self will take mods position to ban you here! Alaah!
 
Unajua huyo jamaa,asilinganishe utawala wa sheria wa nchi zilizoendelea na hapa Tanzania;kwa kufanya hivyo unapoze/unapotea kabisa(get lost or die).
Hapa Tz hiyo utawala wa sheria ndugu yangu ni kuongelea majukwaani na maandishi;kwa vitendo(practically) hakuna kitu kama hicho.
Mfano mzuri tu,serikali ya Uingereza ilitoa fedha ya kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki na hapa Tanzania hawa wastaafu ambao wanaandamana mpaka leo walitakiwa walipwe fedha yao tangu mwaka 1986 bila mjadala;na ndiyo maana wenzao wa Kenya na Uganda husikii vurugu zozote;kwasababu walishapatiwa chao.
Huo ni mfano mmojawapo mdogo tu,wakukuonyesha serikali ya TZ inavyocheza rafu makusudi.
Kuhusu wanafunzi na mgomo wa kuchangia elimu ya juu,bodi ya mikopo kwa elimu ya juu(HESLB)ilipoanzishwa rasmi wanfunzi walikuwa wanakopeshwa 100% ya gharama za elimu,na kigezo kilikuwa rahisi tu uweupata admission katika chuo husika.
Mwaka uliofuatia,wakaja na hadithi ngumu ambayo kwa mwanfunzi kuielewa ni tatizo ambalo ndiyo linaloendelee mpaka hivi sasa.
Hebu kwa hiyo mifano hai miwili ndugu yangu bado tu utaniambia serikali iko sahihi katika maamuzi yake?!
Ninachoona serikali ya Tanzania(TZ) laana wanazitafuta wenyewe na nafikiri ndiyo maana inakuwa kimeo karibia kwenye kila kitu katika hii sayari inayoitwa dunia.
Kwasababu huuwezi kuwanyanyasa watu kiasi hicho ili hali serikali inapoteza fedha nyingi katika mikataba mibovu,ubinafsi wa viongozi wake(ie.mafisadi),matumizi yasiyokuwa ya lazima(anasa) kwa kujilinganisha na nchi tajiri hapa duniani.
Hivyo basi,huwezi ni kuniambia serikali iko sahihi kwa mimi nilizaliwa hapa TZ na niko hapa hadi hivi sasa hunidanganyi lolote kwenye hiki kichwa cha mwendawazimu(dk.3 mbele dk.3 nyuma)
 
Unajua huyo jamaa,asilinganishe utawala wa sheria wa nchi zilizoendelea na hapa Tanzania;kwa kufanya hivyo unapoze/unapotea kabisa(get lost or die).
Hapa Tz hiyo utawala wa sheria ndugu yangu ni kuongelea majukwaani na maandishi;kwa vitendo(practically) hakuna kitu kama hicho.
Mfano mzuri tu,serikali ya Uingereza ilitoa fedha ya kuwalipa wastaafu wa iliyokuwa jumuiya ya Afrika mashariki na hapa Tanzania hawa wastaafu ambao wanaandamana mpaka leo walitakiwa walipwe fedha yao tangu mwaka 1986 bila mjadala;na ndiyo maana wenzao wa Kenya na Uganda husikii vurugu zozote;kwasababu walishapatiwa chao.
Huo ni mfano mmojawapo mdogo tu,wakukuonyesha serikali ya TZ inavyocheza rafu makusudi.
Kuhusu wanafunzi na mgomo wa kuchangia elimu ya juu,bodi ya mikopo kwa elimu ya juu(HESLB)ilipoanzishwa rasmi wanfunzi walikuwa wanakopeshwa 100% ya gharama za elimu,na kigezo kilikuwa rahisi tu uweupata admission katika chuo husika.
Mwaka uliofuatia,wakaja na hadithi ngumu ambayo kwa mwanfunzi kuielewa ni tatizo ambalo ndiyo linaloendelee mpaka hivi sasa.
Hebu kwa hiyo mifano hai miwili ndugu yangu bado tu utaniambia serikali iko sahihi katika maamuzi yake?!
Ninachoona serikali ya Tanzania(TZ) laana wanazitafuta wenyewe na nafikiri ndiyo maana inakuwa kimeo karibia kwenye kila kitu katika hii sayari inayoitwa dunia.
Kwasababu huuwezi kuwanyanyasa watu kiasi hicho ili hali serikali inapoteza fedha nyingi katika mikataba mibovu,ubinafsi wa viongozi wake(ie.mafisadi),matumizi yasiyokuwa ya lazima(anasa) kwa kujilinganisha na nchi tajiri hapa duniani.
Hivyo basi,huwezi ni kuniambia serikali iko sahihi kwa mimi nilizaliwa hapa TZ na niko hapa hadi hivi sasa hunidanganyi lolote kwenye hiki kichwa cha mwendawazimu(dk.3 mbele dk.3 nyuma)

Splendid! dont waste time to discuss about that so called ''Arsenal '' he is living here in DSM he knows excatly the situation of TZ., his dormanted mind and corrupts ideas comes because isone of EPA fisadi or Richmonder!
 
Mods kwani ile thread ya kwanza imeenda wapi?? maana sasa mathread yanajaa tu kwa issue ile ile..
 
Date::11/14/2008
Wadau waponda wanafunzi kutimuliwa Chuo Kikuu

Leon Bahati na Mussa Mkama
Mwananchi

WADAU wa masuala ya elimu nchini wamepinga vikali hatua ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kukifunga chuo hicho wakisema, hatua hiyo haikuzingatia masuala muhimu ya msingi kitaaluma na haitasaidia kupunguza matatizo bali itachochea zaidi tatizo na kusababisha madhara zaidi kwa watoto wa masikini.

Mwenyekiti wa Taifa wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Mrema alisema kuwa, serikali ingepaswa kuwasikiliza na kwamba kuwasimamisha masomo ni kutumia ubabe uliopindukia.

"Hatua iliyochukuliwa ni sawa na kutumia rungu kuua nzi. Kama tuliweza kuwa na uvumilivu na mafisadi wa EPA (Akaunti ya Madeni ya Nje) tangu mwaka 2005, imeshindikana nini kuwa na 'dialogue' (mazungumzo) na wanafunzi hawa?" alihoji Mrema.

Alikosoa vigezo vinavyotumiwa na Bodi ya Mikopo katika utoaji wa mikopo, akitoa mfano wa sula la walemavu kupewa mikopo ya asilimia 100 bila kujali wametoka katika familia zinazojiweza au la.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Kitivo cha Sheria, Dk Sengodo Mvungi amesema sera ya uchangiaji elimu ya juu ilitungwa na Benki ya Dunia na sera hiyo ni kwa ajili ya nchi tajiri na si masikini kama Tanzania.

Alisema mgomo wa wanafunzi hao ni wa haki na utaendelea kuwa wa haki. Aidha alisema katika wanafunzi 18,000 walio nao ni wanafunzi 6,000 tu ndio waliosajiliwa kuendelea na masomo, kwa hiyo wanafunzi 12,000 hawajasajiliwa kutokana na kutolipa ada je wataingiaje madarasani.

Waziri anatoa amri ya kuwataka wanafunzi wote kuingia madarasani kuachana na mgomo, wataingiaje wakati hawajasajiliwa.

"Tuna wanafunzi 12,000 ambao hawajasajiliwa kutokana na kutolipa ada, hao wataingiaje madarasani wakati hawatambuliki, ni lazima wagome ili wapewe mikopo waingie madarasani," alisema Mvungi.

Alisema wapo wanafunzi wa mwaka wa kwanza hadi wa nne ambao hawajaonyeshwa matokeo yao ya mtihani kwa sababu hawajalipa ada sasa wanaambiwa waingie madarasani wakafanye nini ilihali serikali haijawapa mikopo hiyo.

"Tuna wanafunzi wengi wa mwaka wa kwanza hadi wa nne hatujawaonyesha matokeo yao ya mitihani kutokana na kutolipa ada wapo tu chuoni kama kivuli, bodi bado inawasumbua inawapa mikopo kwa ubaguzi, hakuna mtoto wa tajiri ambaye hajapewa mkopo," alisema Dk Mvungi.

Nacho Chama cha Wananchi (CUF) kililaani hatua iliyochukuliwa dhidi ya wanafunzi hao na kudai kuwa njia ya mazungumzo ilikuwa mwafaka.

"Kwa jinsi nilivyokuwa nawasikiliza wanafunzi hao kupitia kwenye televisheni, walionyesha wazi kuwa serikali ingeweka wazi mfumo wa mazungumzo, wasingeendelea kugoma," alisema Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Alfred Lwakatare.

Chama cha NCCR-Mageuzi kilitoa msimamo kuwa serikali ikiamua inaweza kuwapatia wanafunzi mikopo ya asilimia 100 na kwamba, picha inayoonekana kwa sasa ni suala la elimu ya juu kutotiliwa mkazo kama ilivyo masuala mengine hasa yanayohusu maslahi ya viongozi serikalini.

"Hivi leo serikali ingeamua, badala ya kununua magari ya bei mbaya kwa viongozi kama vile mashangingi na kununua mazuri ya kawaida ya bei ya chini, tungeshindwa kuwakopesha vizuri wanafunzi hawa?" Alihoji Mkuu wa Idara ya Organaizesheni, Kampeni na Uchaguzi ya NCCR, Faustine Sungura.

Alikosoa pendekezo lililotolewa hivi karibuni na CCM la wilaya zote nchini kufanywa majimbo, akidai kuwa mpango huo haufai kwa sababu utaongeza matumizi ya kuendesha serikali pasipo sababu ya msingi.

Hata hivyo, Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Propaganda cha CCM, Hiza Tambwe alikuwa na maelezo tofauti na vyama hivyo vya upinzani kwa maelezo kuwa walichofanya wanafunzi hao ni kinyume na mikataba waliyoingia na Bodi ya Mikopo.

"Kama mtu alijaza na kusaini fomu ya bodi ya kupatiwa asilimia 60, akapewa na kwenda chuoni, akasoma mwaka wa kwanza, halafu mwaka wa pili akaanza kugoma na kusema fedha hazitoshi, hii naona siyo sahihi," alisema Tambwe.

Alifafanua kuwa kama ni kugoma walitakiwa kuanza kugomea kusaini mikataba ile hivyo walipaswa watambue haki zao kulingana na mkataba.

Tambwe alielezea kusikitishwa na kitendo cha wanafunzi waliokuwa kwenye mgomo kuwalazimisha wenzao ambao hawakuwa wanaunga mkono hoja hiyo. Alielezea kitendo hicho ni kinyume cha haki za binadamu na kinapaswa kukemewa vikali.

Kuhusu suala la mizozo na mivutano mbalimbali ambayo ilitafsiriwa na wapinzani kama alama za nyakati za nchi kuelekea katika wakati wa kutotawalika, Tambwe alisema kuwa ni propaganda za wapinzani.

"Haijawahi kutokea wapinzani kuunga mkono utawala uliopo madarakani. Hivyo katika hili hakuna jipya," alisema Tambwe akiisifu CCM kuwa imetoa uwanja mpana wa demokrasia nchini, jambo ambalo linawapa fursa wapinzani kuropoka lolote wanalofikiria ni la kukiponda chama tawala.

Alielezea mizozo iliyojitokeza kuwa inatokana na serikali ya awamu ya pili kutoa nafasi kwa kila mtu kueleza madukuduku yake na kwamba kila jambo linashughulikiwa kwa kuzingatia taratibu.

Aliponda shutuma hizo kwa maelezo kuwa, wanachotaka wapinzani ni serikali kushughulikia mambo kwa papara jambo ambalo linaweza kuwa hatari kwa taifa.
 
Hawa wasomi wetu kweli kazi bado ipo maana hawa ndio kesho na kesho kutwatunatarajia wawe na nafasi katika jamii yetu (serikali na makampuni binafsi). Mwanzo wamwaka wao wa masomo wanaenda huko kwenye bodi wanasign mkataba kwambawatalipa hiyo 40% baada ya miezi mitatu wanagoma kwamba hawawezi na hii wanafanya miaka nenda miaka rudi (tunaasume wanaogoma ni pamoja nawale wanaondelea). Sasa kama mwaka jana waliweza kulipa hiyo 40% wakamaliza mwaka mwaka huu kinawashinda nini? Na utashangaa baada ya miezi kadhaa wakirudishwa kwa masharti kwamba walipe hiyo hela only a small percentage of them ndo hawatalipa au wakifukuzwa kabisa hutoshangaa kuwakuta wengo wao wakienda private universities kwa gharama kubwa zaidi. Sasa kwanini viongozi wo wasiwashauri wenye uwezo walipe na wao washughulikie wale tu wasiojiweza?

Harafu huku kugoma kwa mkumbo na makundi kutasaidia nini? Wakati UD wanagoma sua walikuwa wanaendelea tu kama kawaida (lwa mda huo walikuwa wanaweza kulipa 40%) baada ya UD kufukuzwa nao wanawapa support kwa kugoma sasa jiulize tunatengeneza watu wa aina gani hapo baadae? Wengine watasema umoja ni nguvu, sawa hilo nakubali lakini je kama hawa ndo wasomi wetu si tungetemea wawe na strategy nzuri zaidi zenye maslahi kwa wote yaani wao, serikali na Tanzania kwa ujumla. Suala kwamba mwaka 47 walikuwa hawapati kitu mpaka wagome sio sababu kwamba na mwaka 2008 nao wagome kila wakipata tatizo, au wagome kwa mikataba waliosign kama watu wazima kwamba watalipa kiasi fulani. Serikali ngewapeleka mahakamani kwa kukiuka mkataba ili miaka ya mbele aidha wgome mwanzo wa mwaka solution ipatikane au watafute njia m-badala ya kutatua matatizo yao. Kuna wagonjwa huko wanachangia madawa bila mikopo sasa hawa wasomi tulitarajia wawe wanakuja na solutions sio kuipatu wanamkumbuka Nyerere.......
 
Students abroad in Tanzania out of class from strikes



Jenna Stark

Issue date: 11/14/08 Section: Campus News


Seven students in the Brown in Tanzania program are sweating out a strike this week after students protesting financial aid policies forced the University of Dar es Salaam, the program's host school, to close indefinitely.

More than 10,000 students have been ordered to leave the major Tanzanian university after many defied government demands to stop their three-day boycott of classes, according to the Citizen, a Tanzanian newspaper.

Foreign students will be allowed to remain on campus, Associate Director of International Programs Ned Quigley said.

Of the students currently enrolled in the "Brown in Tanzania" program, he said, six are from universities other than Brown.

"We are monitoring the situation, and we expect that the students will receive a full semester of academic credit," Quigley said.

Students are demanding that the government drop a cost-sharing policy that requires some students to pay some fees out of pocket. Protesters want government loans to cover 100 percent of tuition and accommodations, the Citizen reported.

On Tuesday, Tanzania's Minister for Education and Vocational Training Jumanne Maghembe said that given the country's current economic climate, it would be impossible to comply with the students' demands, according to the newspaper.

Heavily armed anti-riot police have been patrolling the main campus of the university to prevent protestors from destroying property.

"We hope that the strike will come to a quick close and all students will come back to classes," Quigley said, adding that the Office of International Programs does not feel that the students' safety is in "jeopardy."

No students from the Brown in Tanzania program could be reached before press time.
 
Kuhusu suala la uwezo wa serikali, ukisoma bandiko la masanja hapo juu ameleza kinaganaga. Ni kweli kuwa serikali ina fedha lakini tukumbuke pia kuwa kuna matatizo mengi ambayo utatuzi wake unahitaji zaidi ya hizo fedha ambazo serikali inazo. tatizo ni kuwa wanafunzi wengi wanachukulia mikopo hii kama misaada-wana malengo ya kutorudisha fedha hizo. ndio maana utawaona wanahusisha masuala ya ufisadi na wao kuomba mikopo. Hoja kwamba "mbona mafisadi wanaiba fedha" unapoiingiza kwenye madai kama haya, unajionyesha kuwa na wewe una lengo la kufisadi pia.
Kuhusu suala la kubadili sera; linahusisha mchakato ambao unawahusisha watu na taasisi kadhaa zinazohusika na sera hiyo. katika hili, si suala la Maghembe au hata Pinda kukaa na kuamua kuwa kuanzia sasa tunaondoa means testing kwenye sera ya mikopo ya elimu ya juu. Inabidi wadau wakae, kukiwa na hoja za msingi kuhusiana na ubaya wa hicho kinachopingwa na wanafunzi na hoja hizo zitapimwa na iwapo itakubaliwa kwua hoja zao ni za msingi, hapo ndipo mchakato wa kuibadili sera hiyo utakapoanza, si waziri kukaa peke yake na kuamua kwa sababu si yeye aliyeiweka sera hiyo peke yake



Ni wapi basi fedha hizo zimetumika ili wanafunzi hao wakiona waridhike kuwa serikali yetu ipo kwa maendeleo ya wote?
 
Ni vigumu mno kuona kama wasomi hawa wanagomea jambo la halali.Tafsiri rahisi kabisa ya kuwapa tunaweza kuwaita Wahuni kama waziri wa Elimu anavyotaka tuamini!
Lakini tukizingatia uhalisia wanachodai ni sahihi kabisa.
Kwanza kimsingi wankubaliana na sera ya uchangiaji wa huduma za jamii.Ndo maana hawajataka serikali iwasomeshe bure badala yake wanataka wapewe 100% ya mkopo ambapo watarudisha wote baadae!Hapo utaona kuwa hakuna wanachochangia!Lazima tuangalia uhalisia badala ya kuwabwatukia bila sababu ya msingi!Kwa wanaosoma sheria pale ada ni milioni moja na nusu kwa wale walioingia mwaka huu.Hii ina maana kwamba atakae pata 80% atajilipia mwenyewe sh 300,000,atakaepata 60%atalipa sh 600,000 na anepata 40% atalipa 900,000!Huyu anaelipa hivi alipokuwa anasoma Secondary alionekana masikini akashushiwa ada hadi sh 20,000 leo hii anaambiwa sera ya kuchangia elimu haikwepeki!
Anapoona wezi wa EPA wanabembelezwa kurudisha fedha,anapoona mbuga zetu zinauzwa kwa weupe,anapoona migodi yetu inaliwa na wamarekani na wacanada,anapoona viongozi wake wanapalilia uozo na uovu kuzalisha Taifa la wezi,na anapofikiria hali ya kijijini kwao kigoma,mtwara na Sumbawanga kwanini asigome? 'WIZI MTUPU!!!?
 
Na ieleweke kwamba hawajagoma from nowhere! Walianza kujadili kwa kutumia diplomasia.Viongozi wa TAHLISO wanaotoka vyuo binafsi wakawa wameshikishwa bahasha!Wanasema YES! Hii ikasababisha vyuo vya umma kujitoa na kuunda umoja wao na kudai haki zao.Migomo ina yoendelea imeridhiwa na mabunge ya vyuo vyote husika.Haiwezekani wote hawa wakawa hawana akili. Bodi ya mikopo inasema inatoa mkopo kutokana na hali ya mtu.Lakini watoto wa vigogo wanaofahamika wanapata 100% na wale wa vijijini wanapata B na C
Chukua mafano huu ambao ni kweli umetokea.

1.Wapo mapacha ambao wamepata grade tofauti.Mmoja 80% na mwingine 60%.Kama mikopo inatolewa kutokana na uwezo wakifamilia hii inakuwaje.

2.Yupo mwingine ambao kiumri amesonga kidogo.Alipokwenda kufuatilia mkopo baada ya kuona amebabaishwa sana jibu alilopewa huko bodi ni ULIKUWA WAPI SIKU ZOTE UNAKUJA SHULE LEO! Hii ni kauli ya kumpa mtu aliyefuata huduma!

Ingekuwa afadhali basi kama mtu unajua umepata mkopo toka ukiwa huko kwenu lakini sivyo!Unafika chuoni na kukaa kama wiki tatu then unapata taarifa kuwa umepata mkopo B au C na unatakiwa ulipe ada ili usajiliwe!
 
Mpaka sasa UDSM,DUCE,MUCE na SUA-Mazimbu wapo nyumbani for the same issue!Usisahau UCLAS wao toka Sept wapo nyumbani!
Bila kufikiri,ni rahisi kuwaita hawa wahuni!
 
Back
Top Bottom