Tatizo la Yanga ni kujisahaulisha kwamba timu ilikua ikibebwa na Mayele, yule mwamba mara zote alikua akiibeba Yanga mabegani mwake. Na mara nyingi alipokosekana mayele timu ili-struggle kupata matokeo hivyo jukumu la kuamua mechi lilibakia kwa Feisal feitoto, kwa lugha nyepesi mayele alikuwa akificha madhaifu ya wachezaji wenzie. Now that he's gone, hiyo mnayoita rotation hata ikifanyika itakua ni bure tu kwakuwa Yanga haina kikosi kipana bali imejaza wachezaji wengi ambao ni average.
Ukitaka uelewe nini namaanisha angalia margin ya magoli ambayo yanga ilikuwa ikifunga kipindi cha mayele, karibia kila mechi yanga inashinda goli 1 au 2 na mfungaji mayele itokee sana afunge mtu mwengine.
Kwa sasa kidogo wanajitahidi kugawanya magoli akina Azizi ki, Nzengeli,Pacome wanajaribu kufunga funga magoli. Sasa ukisema uwatoe hao wanao kufungia magoli aingie sureboy na mauya mnataka timu ishuke daraja ?.