Miguel Gamond ni kocha aliyekuja kuvuruga maana halisi ya "kikosi kipana"

Miguel Gamond ni kocha aliyekuja kuvuruga maana halisi ya "kikosi kipana"

Malengo yapi hayo
Umeusoma mkataba wake?
Ndani yake yame ainishwa malengo aliyopangiwa.
BTW, Mimi nimepinga kupangiwa kikosi na sijasema hajatimiza malengo. Nikasema asipotimiza malengo kwa muda aliopangiwa ukifika afukuzwe tu Ila so kuvuruga sasa kwa kuingilia squad selection na program zake.
 
Kama nimekuelewa vizuri ni kwamba unawata mashabiki wenye maneno maneno waachane nayo na waachie uongozi na benchi la ufundi wafanye majukumu yao kama walivyokubaliana.
 
Toka nimeanza comment ya kwanza mpk mwisho hakuna aliesema MKUDE aingie kama sub...yani hapo kwa Mkude mimi namcheka mnoo siicheki Yanga namcheka yeye...hana impact,,kapotezwa mazima haongelewi...yani bora angeenda Ruvu shooting walai.. [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787] [emoji1787]
HUYO ANASUBIRI MKATABA WAKE UISHE.
 
Maoni ya David kampista
 
Attachments

  • DA09AEBD-1337-4EF2-A0CC-2D69F5B982C0.jpeg
    DA09AEBD-1337-4EF2-A0CC-2D69F5B982C0.jpeg
    270.4 KB · Views: 3
  • BE64696B-B3D4-4013-9E75-1A0F977C414A.jpeg
    BE64696B-B3D4-4013-9E75-1A0F977C414A.jpeg
    214.1 KB · Views: 3
Gamondi Anavyowapa mtihani mawinga:

Muktasari:
Lakini kwenye timu hiyo ni wazi mawinga (viungo wa pembeni) halisi wa timu hiyo kazi wanayo msimu huu chini ya kocha Miguel Gamondi kwani ameonekana hana kipaumbele kwenye upande huo.

Klabu ya Yanga imerejea mazoezini Avic Town, Kigamboni ikijiandaa na mechi zijazo ikiwemo ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar itakayopigwa Disemba 16.
Lakini kwenye timu hiyo ni wazi mawinga (viungo wa pembeni) halisi wa timu hiyo kazi wanayo msimu huu chini ya kocha Miguel Gamondi kwani ameonekana hana kipaumbele kwenye upande huo.
Tangu kutua Yanga na kuanza kazi rasmi mwanzoni mwa msimu huu, Gamondi ameonekana kuwa muumini sana wa viungo kuliko mawinga jambo linalowapa tabu mawinga wa timu hiyo kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi hicho na muda mwingi kusota benchi.

Mawinga asilia ndani ya Yanga ni watano, Jesus Moloko, Farid Mussa, Denis Nkane, Mahlatse Makudubela 'Skudu', na Maxi Nzengeli ambaye amebadilishiwa majukumu na kuwa kiungo mshambuliaji nyuma ya mshambuliaji.
Gamondi ni muumini wa mfumo wa 4-2-3-1, ambao mara nyingi umekuwa ukihusisha viungo watano na wakati mwingine ametumia mifumo ya 5-1-2-2, na 3-5-2, ambayo yote huwa na viungo wengi wa kati uwanjani.
Hali hiyo imemfanya Gamondi kumbadilishia majukumu yake halisi Maxi, na kumtumia kama kiungo mshambuliaji akicheza maeneo sawa na Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki ambao huwa wanabadilika wakiwa uwanjani wakati mpira ukichezwa.
Maxi amecheza mechi zote za Yanga kwenye Ligi Kuu na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu akitumika kwa dakika 1284.
Winga wa zamani Yanga, Saidi Maulid 'SMG' alisema ni jukumu la mawinga waliopo kwenye timu hiyo kupambana na kuhakikisha wanamshawishi kocha awapange.
"Kila kocha anataka kutumia wachezaji walio tayari, nadhani anaowapanga kwa sasa anaona ndio watamfaa hivyo mawinga wa Yanga waongeze juhudi na wakifanya vizuri mazoezini sidhani kama ataacha kuwapa nafasi kwenye mechi," alisema SMG.

Mifumo na falsafa hizo za Gamondi imekuwa dozi chungu kwa mawinga Moloko, Nkane, Skudu na Farid ambao msimu uliopita walikuwa wakicheza mara kwa mara lakini sasa ni nadra sana kuwaona.
Katika takwimu ilizonazo Mwananchi, Yanga imecheza jumla ya mechi 16, za Ligi Kuu (9) na Ligi ya Mabingwa Afrika (7) ikiwa ni sawa na dakika 1620 lakini Skudu, Moloko, Nkane na Farid hakuna hata mmoja aliyecheza walau robo ya dakika hizo kwani Moloko ndiye amecheza nyingi kati yao akidumu uwanjani kwa dakika 323 tu.
Katika mechi tisa za ligi ilizocheza Yanga Moloko amecheza nne tu, akianza kikosini katika mechi ya kwanza dhidi ya KMC na kutolewa dakika ya 79, mchezo uliofuata dhidi ya JKT hakucheza baada ya hapo dhidi ya Namungo aliingia akitokea benchi na kucheza kwa dakika 23, ikafuata mechi na Ihefu aliyocheza dakika 68 tu huku akikosa nne mfululizo dhidi ya Geita, Azam, Singida na Simba na kuibukia kwa Coastal alipocheza kwa dakika 21 tu huku akiwa na pasi za mabao mbili.
Mechi za kimataifa kwa maana ya Ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga imecheza saba ikianza na Asas ugenini ambapo Moloko hakucheza lakini ile ya marudiano alicheza dakika 46, zikafuata mechi mbili na El Merrikh ya Sudan ambapo mchezo wa kwanza alicheza dakika moja tu na marudio akacheza dakika 76.
Nyota huyu ambaye alikuwa na uhakika kwenye kikosi cha Yanga msimu uliopita, msimu huu kwenye hatua ya makundi hadi sasa amecheza mechi moja tu dhidi ya CR Belouizdad akicheza kwa dakika tisa pekee.
Upande wa Farid Mussa ambaye msimu uliopita alikuwa na uhakika wa kucheza, mbele ya Gamondi mambo yamembadilikia kwani kwenye ligi hadi sasa amecheza mechi moja tu dhidi ya KMC alipoingia dakika 26 za mwisho huku kwenye zile saba za kimataifa akiwa hajacheza hata dakika moja licha ya kumudu pia kucheza kama beki wa kushoto .
Nkane ni kama vile hayupo kwenye mipango ya Gamondi kwani kwenye ligi hadi sasa amecheza michezo mitatu kati ya tisa ya Yanga. Aliingia dakika za jioni dhidi ya KMC dakika 11 za mwisho, ikafuata na JKT akacheza dakika 12 tu kisha ile na Geita Gold aliyocheza dakika 17 tu huku kwenye zile mechi saba za kimataifa akiambulia dakika 44 tu katika mechi ya marudiano dhidi ya Asas.
Kocha wa zamani wa Yanga, Kenny Mwaisabula alisema kila kocha ana falsafa zake na kinachofanyika sasa ni maamuzi ya Gamondi.
Mwaisabula alisema Nabi (Nasreddine) alikuwa ni muumini wa kuchezesha wachezaji wengi kwa maana ya kumpa nafasi kila mchezaji kuitumikia timu jambo ambalo lilikuwa faida kwa wachezaji wenyewe, Yanga na hata Taifa kwani wazawa wengi walipata muda wa kucheza.
"Kwa Gamondi mambo yamebadilika, ana watu wake wachache anaowaamini na mechi nyingi wanacheza wale wale na mfumo ni mmoja ambao hauwapi nafasi mawinga kwani anatumia zaidi viungo;
"Hii sio kwa mawinga tu kuna hata viungo waliopoteza nafasi kama Salumu Abubakar 'Sure Boy', ambaye kwa Nabi alikuwa mchezaji tegemeo, kiufupi yote hayo ni maamuzi ya Gamondi lakini binafsi sioni kama yana afya kwa timu katika siku zijazo."
Wakati huo huo upande wa Skudu aliyesajiliwa Yanga msimu huu akitokea Marumo Gallants ya Afrika Kusini, mambo yamekuwa magumu katika kikosi cha Gamondi kwani hadi sasa amecheza mechi tatu tu kati ya tisa ilizocheza Yanga kwenye ligi akianza dhidi ya Ihefu na kucheza kwa dakika 57, akacheza dakika 18 mbele ya Singida Bs na dakika moja tu dhidi ya Simba.
Kimataifa Skudu amecheza dakika 14 tu kwenye mechi ya marudiano dhidi ya Al Merrikh.
Kwenye mahojiano na Wanahabari baada ya mechi iliyopita kimataifa dhidi ya Medeama kumalizika, Gamondi aliulizwa swali kuhusu mabadiliko ya wachezaji kikosini na kujibu kwa ufupi tu; "Ni maamuzi yangu."
Mechi ijayo ya Yanga itacheza Desemba 16 uwanja wa Azam Complex dhidi ya Mtibwa Sugar iliyo nafasi ya mwisho kwenye ligi ikiwa na alama tano baada ya kucheza mechi 12, huku Yanga ikiwa nafasi ya pili na pointi 24 ilizovuna kwenye mechi tisa.

Chanzo : Mwananchi
 
Ki alipwaya mechi ya Al Ahly hapa akawa anashindwa hata kumtoa aingie nani? Waarabu wanafanya sub nne Yanga hawajui watamtoa nani wakati waliochoka walikuwepo wengi akawa anawaacha tu wapoteze muda mpaka tukafungwa na kusawazisha kwa nguvu...
Metacha huwa achezi mara kwa mara anakuja kupewa gemu na Waarabu kila mpira tunaoshambuliwa au kuokoa anaona kama moto...
Moloko, Mudadhiri,Mauya,Sure Boy wana mechi za kucheza sio hivi anavyofanya Gamondi...
Kikosi kitakachoanza leo inawezekana chose ndio kitaanza wiki ijayo na Medeana wakati ana Lundo la wachezaji pale...
 
Wabongo mnajuaga kukosoa. Haya ile mechi sio Aziz Ki tu aliyechoka, Maxi, Mzize, Pacome na mabeki wote walichoka uliona mabeki wanavyodondoka ovyo na kushindwa kupiga pasi. Haya niambie badala ya Pacome angeingia nani?
Nafasi ya Maxi achukue nani?
Nafasi ya Aziz Ki achukue nani?
Kule nyuma mabeki wangechukua nafasi wakina nani?

Al Ahly wana quality players, aliyekuwa benchi na aliyekuwa ndani hawapishani ubora na viwango uwezi kulinganisha na squad ya Yanga.
 
Ki alipwaya mechi ya Al Ahly hapa akawa anashindwa hata kumtoa aingie nani? Waarabu wanafanya sub nne Yanga hawajui watamtoa nani wakati waliochoka walikuwepo wengi akawa anawaacha tu wapoteze muda mpaka tukafungwa na kusawazisha kwa nguvu...
Metacha huwa achezi mara kwa mara anakuja kupewa gemu na Waarabu kila mpira tunaoshambuliwa au kuokoa anaona kama moto...
Moloko, Mudadhiri,Mauya,Sure Boy wana mechi za kucheza sio hivi anavyofanya Gamondi...
Kikosi kitakachoanza leo inawezekana chose ndio kitaanza wiki ijayo na Medeana wakati ana Lundo la wachezaji pale...
Unazungumzia lundo la wachezaji wenye ubora upi? Hilo lundo la wachezaji wameshindwa hata kuifunga Ihefu tu. Yanga ingekuwa na namba tisa mzuri, mechi zote mbili Yanga ingeshinda na kufikisha point 6. Na malalamiko yote kwa Gamond yasingekuwepo, ila kwasasa Gamond anabebeshwa lawama zisizomuhusu wakati tatizo la Yanga inajulikana hakuna straika, magoli yanafungwa na viungo ( max, Aziz Ki na Pacome) timu ina miliki mpira, timu inapiga counter attacks ila wakina Mzize, wanafanya counter ziwe hazina maana kwa kushindwa kufanya maamuzi sahihi kwa wakati.
 
Mkuu mpira hujui mpira wa ligi unafungwa na yeyote shida yenu ninyi wengine mmeanza kuangalia mpira ukubwani kwa sababu watu wengi wanauongelea na wewe unalazimika kuuzungumzia...angalia hata ligi za Ulaya ujifunze kitu Barca kafa mechi mbili za mwisho Chelsea kafungwa na Everton mimi nikiona mtu anazungumzia Timu kufungwa mechi kadhaa najua ana upungufu wa kutokujua mpira kabisaa..
 
Sasa kama unaamini kufungwa kwa timu, ni matokeo ya mpira kwanini umlalamikie kocha? Ungekuwa unajua mpira ungekaa kimya na ungeheshimu kazi aliyopewa kocha na sio kujifanya unajua zaidi ya kocha
 
Sasa kama unaamini kufungwa kwa timu, ni matokeo ya mpira kwanini umlalamikie kocha? Ungekuwa unajua mpira ungekaa kimya na ungeheshimu kazi aliyopewa kocha na sio kujifanya unajua zaidi ya kocha
Wewe mtu hakuna kitu unajua tunapozungumzia makosa ya kocha au viongozi wengine wowote ndio jukumu letu binadamu sio mawe kwamba wakae tu bila kukosoa hujui mpira bhana...Nchi zingine wanaandamana na mabango kocha atolewe ina maana washabiki hawajui mpira washabiki wa Ulaya walikataa Super Cup kwa mabango mpaka ikapelekea ifanyike Afrika tu maana huku mpo ninyi ambao hamjui kitu na hamna maamuzi kwenye vyama vya Mpira samahani kwa kukuambia ukweli maana hakuna tafsida ingine ya kutokujua kitu ningeitumia...yaani unalaumu Yanga kufungwa na Ihefu au nianze kulaumu Simba kufungwa mechi moja jua mimi pia ntakua sijui mpira kama wewe tunachozungumzia ni mfumo kwa baadhi ya Wachezaji upo sawa au haupo sawa siandiki tena baada ya hii wacha niendelee kuwasoma wanaojua mpira bhana...
 
Fatilia comments zangu, sijawahi kulaumu matokeo wala kocha. Ila nyie ndio mliomkosoa kocha, je kocha mnamkosoa kwa angle ipi kama sio kwa matokeo yanayopatikana? Aliyesema kuwa unayelaumu Yanga kufungwa hajui mpira ni nani kama sio tena wewe huyo huyo? Yaani unajifanya unang'ata na kupuliza.
 
Back
Top Bottom