Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 58,636
- 220,438
DK. MIGUNA MIGUNA WA KENYA AMVAA JPM KUKAMATWA KWA TITO MAGOTI.
Mwanasiasa na Mwanasheria machachari nchini Kenya, Dk. Miguna Miguna amemtaka Rais wa Tanzania, Dk. John Magufuli kumwachilia huru Ofisa wa Kitengo cha Elimu kwa Umma wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu Tanzania (LHRC), Tito Magoti.
Dk. Miguna ambaye amewahi kuidhinisha kiapo cha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kuwa ni 'Rais wa Wananchi' Januari 2018, jambo lilisababisha kutimuliwa kwake nchini Kenya na kupelekwa nchini Canada ambako alidaiwa kuwa ni raia wa nchi hiyo amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kuwa Rais Magufuli anapaswa kutambua kuwa suala la kuwakatisha tamaa, kuwaogopesha na kujaribu kuwanyamazisha wakosoaji, wapinzani na wanaharakati za haki za binadamu nchini humo dhidi ya serikali yake halitafanikiwa.
Dk. Miguna ameita vitendo hivyo vya serikali dhidi ya wakosoaji, wapinzani na wanaharakati wa haki za binadamu nchini Tanzania ni dalili ya udhaifu mkubwa wa serikali hiyo.
Tito Magoti, ambaye ni mwanasheria anayehudumu LHRC alikamatwa siku nne zilizopita na watu wasiojulikana eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam, jambo ambalo lilizua taharuki kuwa ametekwa lakini baadae jeshi la polisi kanda maalum Dar es Salaam lilijitokeza hadharani na kukiri kumshikilia mwanaharakati Magoti, ingawa halikutaja moja kwa moja makosa yake wala kituo ambacho kinamshikilia.
Makundi mbalimbali ya wanaharakati wa haki za binadamu Tanzania na kimataifa yamelaani kitendo cha Tito Magoti kukamatwa kinyume na taratibu kitendo kinachotafsiriwa kama utekaji kutokana utata unaoligubika tukio hilo.
Wanaharakati hao pamoja na taasisi mbalimbali nchini Tanzania na zile za kimataifa zimekuwa zikishinikiza kuachiliwa huru ama kufikishwa mahakamani endapo Ofisa huyo wa LHRC kuna makosa anatuhumiwa nayo.
Jana Desemba 22, 2019 Kamanda wa polisi kanda maalum Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alinukuliwa na vyombo vya habari kuwa leo (Desemba 23, 2019) atatoa taarifa ya kina kuhusu kushikiliwa kwa Tito Magoti.
#JusticeForTitoMagoti