Coaster2015
JF-Expert Member
- Aug 21, 2018
- 2,607
- 2,730
Binti Kiziwi,Kama upo karibu na Juice bar yeyote take a glass nitalipa! Very well said.
Hakuna justification ya mtu kupigwa na kuburutwa namna hii, ukipigwa unakuwa umedhalilishwa na kutolewa utu, binadamu anatakiwa kupewa adhabu zitakazotunza ubinadamu wake hata kama yeye mwenyewe ni “mbaya”kiasi gani. Halafu kumpiga mwanamke ambaye hawezi hata kukurushia ngumi moja nao ni ugonjwa wa akili. Kama kuna chochote Nack alichofanya chochote kwa jamaa yake hili la kupigwa kalifit kama justification. Uliza sababu utaambiwa sijui usaliti, sijui ma nini nini, swali huyo kaka hajawahi msaliti mkewe? Au hajawahi mfanyia chochote kibaya! Is he malaika Gabriel or something like that, Holly! No no no! Mbona ye hakupigwa hivyo? What’s your point men! To me binadamu yeyote hatakiwi kupigwa leave alone a woman!
Sipati picha mangenita angekuwa katika ubora wake wa U Turn angeandika nini mbaya wake anapokaangwa hehe!
cc Zurie,
Maelezo yenu yana hoja, na ninaona jinsi ambavyo mnajaribu kuonesha hisia zenu juu ya kitendo cha kupigwa mdada,
Mimi nilitamani sana kuona mnaanza kwa kukiri kwamba inawezekana mdada alitenda kosa lililopelekea kupigwa kwake, unajua inaudhi sana mwanamke anapokuwa ametenda kosa zaidi ya mara moja unamwambia hasikii, huyo jamaa naamini naye hakupenda kumpiga mkewe tena mbele ya watoto wake, ndio maana utaona walitoana ndani, inawezekana jamaa alikuwa ameamua kutoka nje akapunge upepo hasira zake ziishe, lakini picha inatuonesha mwanamke ndie aliyekuja kwa nyuma, na inawezekana kabisa alikuwa akimfuata mumewe nje kwa matusi, inawezekana, angekuwa na adabu, angebaki ndani ya nyumba, mjifunze tu kuwa na adabu na heshima na usikivu na Utii, hakuna mwanaume anaeweza kupiga mke wake bila sababu ya msingi, hata namna mnavyo comment, mnaniacha hoi.