Comment yangu moja umeijibu mara mbili, na unaniletea cases tofauti kujustify upigaji, basi ngoja nikukubalie mwanamke anapigwa, na tena anapigwa sana, mwanamke ndiye mtu pekee hukosea duniani, hivyo kumpiga ni haki kabisa. You happy now!? [emoji3]
Ujue nimewasoma na kuwasoma tena, imebidi nianze kutafakari upya, hivi kupiga kwenu ninini? Kwanini mnaamini sana katika kupiga? Je ni kukomoa, kurekebisha au kumaliza hasira? Ama ni matatizo ya akili na hamjijui? Maana kila mtu anajimwambafy kuwa ni lazima kupiga na hamna namna!
Naendelea kusimama hapa, siafiki mtu kupigwa no matter aina ya kosa alilokosea, kupiga ni uonevu, unyanyasaji na udhalilishaji, na mwisho sifikirii kama kuna matokeo chanya juu ya upigaji. Nitaendela kusimama hapa hapa.
Africa tunapigana sana na hakuna chenye kinabadilika au kuleta unafuu, watoto majumbani wanapigwa, shuleni wanapigwa, wanawake wanapigwa, watu wanapigana ovyo mitaani, nini shida katika akili yetu? Note: sio kwamba race zingine hazipigani, lakini utaona reaction ya watu juu ya upigaji ndiyo inayotutofautisha sisi wa bara giza na wale. Huku ukireact kupinga upigaji you will be called names, Je ni kweli upigaji unasaidia kitu!?Hebu wapigaji mtuambie hapa.