Nawasalimu ndugu wana JF
Mimi ni mwajiriwa katika kampuni moja hivi hapa Tanzania. Nilikuwa na plan ya kufanya kazi kwa muda wa miaka mi 3 then niwe na maisha yangu. But nikajikuta mpaka sasa mwaka wa nne bado nipo job, inaniuma sana na sipendi.
Miminapenda sana kusafiri safiri yaani nisiwe mtu wa kutulia sehemu moja kwa muda mrefu. Sasa nina milioni 20, je naweza fanya bishara gani ili niachane na hii ajira?
Wazo langu nifungue kampuni ya biashara ya mazao ya Nafaka. Niwe nafuata mazao vijijini na kuuza mjini. Na soko langu la kwanza nimepanga iwe Tanga mjini. Ila sijui taratibu za kufuata mpaka uweze safirisha Nafaka.
Naombeni ushauri wenu pia kama kuna bisahara nyingine naomba mnishauri.
Natanguliza shukrani