Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Miji inayoongoza kwa vumbi Tanzania. Shati jeupe usiende nalo

Morogoro ili haribu raba yangu nyeupe [emoji28][emoji28]nka rudi nayo ime fubaa utazani ili pakwa rangi nyekundu
 
Karatu msimu wa Mvua Kuna kuwa na tope la Hatari sana, Unashindwa kunyanyua mguu kutoka chini, Haswa hayo maeneo ya CCM , uwanja Mboe Hadi kupandisha Maeneo ya Jublate Mnyenye, NMB, Kwa Lekashu, Kadtuli Hadi Peter Ombay , Crater Rim, upande police na TRA shuka mitaa ya NBC kote ni tope ama Vumbi
Kuna tope la Moshi nalo kiboko[emoji28][emoji28][emoji28]
 
Acha kutaja vijijini huko,kwa jinsi hiyo hakuna kijiji nchi hii kisicho na vumbi,ukiondoa vile vya mikoa ya pwani ambako ardhi yake ni ya kichanga,hapa tunazungumzia urban,Dodoma kwa sasa pako vizuri sana ukilinganisha na miaka 20 iliyopita...
Mkuu huyo dada sijui watu wa Dodoma walimkosea nini yaani yeye sikuzote huwa yupo negative tu kuhusu Dodoma.Kuna thread moja aliwahi kusema eti watu wa Dodoma ni wafupi,wamefubaa alafu weusi tiii nikamuuliza mbona huku Dar warangi,wasandawe na wanyambwa(wengine huwaita wagogo wa manyoni) wanasifika kwa uzuri na weupee wao(wa asili sio wa kujichubua) akakimbia😀😀.
Sasa leo tena thread inahusu miji yeye anakuja kutaja vijiji vilivyo wilaya za Bahi na Chamwino huko😀😀
 
Dodoma kunapausha sana yaani huku napaka Vaseline, Glycerin,lotion Ndo natoka na Bado kukatika miguu Ndo usiseme besti ..Kuna Hali ya hewa mbaya mnooo
Poleni nilikaa siku 2 ngozi ikabadilika na hapo natoka nje kwa masaa tu, nikajiuliza vip wakazi wa huku wana hali gani? Huko vijijini si watoto watakuwa wamepauka sana na kuumwa homa ya baridi? No siwezi ishi dom.
 
Mbele ya Lengijave, panaitwa Oldonyosambu, huko watu washarudi mavumbini kabla ya hata ya kufa. Kuna vumbi narudia tena KUNA VUMBI. Robo tatu ya vumbi la dunia liko huko. Kuna wakati unatembea ukijiangalia chini ujioni yaani unatembea lakini miguu yako huioni imezama kwa vumbi.
🤣🤣 Kuna wakati nilipata tenda ya ujenzi ya shule fulani mitaa hiyo sehemu inaitwa Engikaret... lile vumbi lilikuwa sio poa. Ila bahati nzuri vumbi la huko sio jekundu. Karatu kuna poda nyekundu kama jezi ya Simba.
 
Kinachoshangaza mkoa wa kigoma kuna viongozi wakubwa wametokea kule hivi wameshindwa kuupigania ule mkoa zile barabara zikapigwa lami? Imagine kuna vipande vipande kama mkate wa ajemi hapa na hapa lami kidogo vumbi la kwenda inakera sana
[emoji1787]
 
Hii ni miji kumi inayoongoza kwa vumbi nyakati za kiangazi nchini Tanzania. Ukienda huko achana na habari ya nguo nyeupe. Pendelea rangi nyeusi, brown au kijivu.

1. KARATU
2. KASULU
3. KIBONDO
4. BOMANG'OMBE, Hai
5. SONGEA
6. TUNDUMA
7. ORKESMET, Simanjiro.
8. DODOMA
9. MERERANI
10. MTO WA MBU
Mbinga
 
Back
Top Bottom