Mika Mwamba ndiye Producer mwenye uwezo mkubwa wa kutengeneza beats kali kuwahi kutokea kwenye historia ya Bongofleva

Nichangie kidogo hapo maana pia nimezaliwa kitambo na naujua muziki wa enzi hizo japo mie sio msanii
Ila msanii wa zamani anaposema muziki wa zamani ulikuwa haulipi kivile ana maana kwamba kipato cha msanii kilitegemea mauzo ya kanda na malipo ya show kitu ambacho baadhi ya wasanii hawakufanikiwa kupata show nyingi zaidi walitegemea mauzo ya kanda ambapo pia distributes ndio walipiga faida kuzidi wasanii hivyo maisha ya wasanii wengi yakabaki kuwa ya kawaida tofauti na wasanii wa sasa ambapo kuna YouTube ndo inawalipa sana kiasi kwamba msanii akijibrand kwenye social media akapata mashabiki wengi basi ana uhakika wa kupiga pesa mingi mtandaoni ambayo haina udalali wala magumashi ya wahindi kama kipindi kile.
Ndio maana sa hivi msanii kumiliki gari kali ni jambo la kawaida.
 
Ni raha tu (remix) - P Funk
Nini mnataka mazee - P Funk
Sauti ya gharama - P Funk
Bush Party - Bonny Luv
 
Fikiria ya Mez B - P Funk
 
P anaficha mambo mengi, siwezi shangaa ni Bizman kapiga pale kinanda
Sio kweli kwamba huwa anaficha. Kwenye interviews zake amekuwa akitaja watu wote aliokuwa anawatumia kwenye production. Hata kwenye baadhi ya nyimbo zenyewe walikuwa wakitajwa, mfano Akwelina katajwa Ludigo, Jirushe katajwa Marijani n.k

Kuwa producer haimaanishi ufanye kila kitu, kazi kubwa ya producer ni kuleta concept nzima ya kazi. Producer mzuri ni yule anayehakikisha anatoa nyimbo bora kwa kutafuta watu mahiri watakaofanikisha kazi na sio lazima kila kitu afanye yeye.
 
Fikiria ya Mez B - P Funk
Ahsante mkuu. Kimawazo nafikiri nilichanganya, nilikuwa ninawaza ile ngoma ya D Knob na Mez B - ni kama mti usio na mizizi, upepo upepooo, ni kama ardhi juu ya maji, Mpenzi usiniache. Hiyo aliipika Mikka
 
Nini mnataka ni beat ya P, edit hapo!
 
Mmmmh, hapana. Hakuna producer nchi hii mwenye/aliyekuwa na uwezo wa kutengeneza mdundo kumzidi majani.
 
Basu huyu mwamba alikuwa noma
 
True man
 
Naomba kuweka kumbukumbu sawa,Ay Raha Tu original version ilikuwa ni kazi ya Bongo Records.Kwanza hiyo Beat ilibidi Eluka aifanyie kazi,baadaye akapewa A.Y.
 
Naungana na wewe.Maproducer wakubwa kama Quincy Jones,wqo hata chombo cha Muziki hawajui kupiga,lakini wana sikio na jicho la muziki.Wanajua chombo kipi kipigwe,ala ipi ipigwe vipi.Na ni mtu gani anafaa kwa kazi hiyo,wao kazi yao ni ku organise na kusimamia kazi mpaka inakamilika.
Hata P Didy.Hajui chombo hata kimoja lakini ni mmojawapo wa maproducer wenye mafanikio makubwa
Hata P Funk alishawahi kusema,kuna tofauti ya Producer na beat maker.Producer ni zaodo ya beat maker.
 
Miikka Aleksanteri Kari ndiye GOAT wangu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…