Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Huyo roho wa mungu anafanyaje makosa ya kiuandishi? Na kwanini mungu awe na hasira ili hali hiyo ni weakness ya mental judgement.
 
Hapo tusingekuwa binadamu BALI NI MALAIKA SASA.
 
Hapo tusingekuwa binadamu BALI NI MALAIKA SASA.
Kwa mujibu wa Biblia hata shetani alikuwa Malaika na akaweza kufanya uasi na uovu,

Sasa utasemaje kwamba malaika ni wakamilifu hawawezi kufanya uovu?
 
Kwa mujibu wa Biblia hata shetani alikuwa Malaika na akaweza kufanya uasi na uovu,

Sasa utasemaje kwamba malaika ni wakamilifu hawawezi kufanya uovu?
Shetani hakuwahi kuwa malaika.yeye aliumbwa na moto na malaika waliumbwa kwa nuru.ni vitu viwili tofauti
 
Pamoja na hayo uliyosema, sasa kwanini kitabu kinachomwelezea mungu mwenyewe na ambacho kakiandika yeye mwenyewe kupitia watu kinajikontradict?kwanini aruhusu jambo hilo? Vilevile huyo mungu akili na uwezo wake havichunguziki kwa ukubwa wake, sasa kwanini awe na wivu na hasira vitu vinavyoashiria imperfection?
 
Kwanini wafanye uovu na kwanini kuna uovu? Ilishindikanaje mungu kuumba watu wasiofanya uovu?
Kwahiyo mkuu ulitaka uumbwe kama Malaika maana Malaika ndio hawafanyi uovu

Binadamu amewwkewa njia mbili njia ya mema na njia ya uovu na amepewa nafsi na akili ya kuchagua atakacho

Na amewwkewa moto na pepo pia amepewa nafsi na akili Ili achague anakotaka kuenda
 
Napinga uwepo wa imani na dini cause zinatuletea majanga na uharibifu mwingi, mfano vita vya kidini, degrade human thinking capacity. In short mambo ya imani na dini should perish from this world.
 
Mkuu,
Jadili hoja acha kelele Kama chizi aliyeona jalala jipya!
Karibu tujadili kwa staha.
 
Shetani hakuwahi kuwa malaika.yeye aliumbwa na moto
Kwa hiyo Mungu aliumba shetani?

Unaona sasa Mungu huyo alivyo mkatili? 😆

Yani Mungu anaumba Shetani wa kuleta uovu duniani halafu anataka tutende mema..!!

Niki kwambia kwamba, Maandiko ya kidini ni Hadithi za kutungwa ndio kama hivi sasa.

na malaika waliumbwa kwa nuru.ni vitu viwili tofauti
 
Kuwa na mental disorder na kutibiwa kisaikolojia haithibitishi mungu yupo.
 
Unakubaliana nami mungu Perfect hayupo?
Siwezi kubaliana na wewe, hiyo Ni imani yako, na nami nina imani yangu, na imani yangu inanihakikishia kuwa Mungu yupo na nimeona akinitendea mambo mengi hivyo Nina ujasiri wa kusema Mungu yupo, sijui kuhusu imani yako
 
Siwezi kubaliana na wewe, hiyo Ni imani yako, na nami nina imani yangu, na imani yangu inanihakikishia kuwa Mungu yupo na nimeona akinitendea mambo mengi hivyo Nina ujasiri wa kusema Mungu yupo, sijui kuhusu imani yako
Hujajibu swali mpaka sasa,
Unakubaliana nami mungu perfect hayupo?
 
Napinga uwepo wa imani na dini cause zinatuletea majanga na uharibifu mwingi, mfano vita vya kidini, degrade human thinking capacity. In short mambo ya imani na dini should perish from this world.
Hapo sasa kuna nuance kubwa kati ya kupinga uwepo wa dini/imani na kusema dini/imani zinapotosha ukweli.

Ukisema unapinga uwepo wa dini na imani, ni kama unataka kupiga marufuku imani/dini.

Dini ukiipiga marufuku, ndiyo unaipaisha umuhimu wake. Watu watakuita mpinga dini uliyetabiriwa, watasema huo ni utabiri unatimia. Matokeo yake utazidisha wafuasi wa hiyo dini.

Dini inapingwa kwa kuonesha isivyo kwenye ukweli, kuachiwa iwe huru, lakini kuelimisha watu kuhusu ukweli. Elimu ndiyo itawaongoza watu kujua mapungufu ya dini.

Kimsingi, uhuru wa kuabudu kwa dini/imani yoyote ni upande mmoja wa shilingi ambayo kwa upande mwingine ina uhuru wa kutoamini. Hata kwenye katiba nyingi na Universal Declaration if Human Rights, uhuru wa kuabudu unajumuishwa na uhuru wa kutoabudu.

Kwa hivyo, ukiruhusu dini zipigwe marufuku, kwa sababu zinalemaza uwezo wa watu kufikiri, kimsingi utakuwa pia umefungua mlango wa watu wasioamini kulazimishwa waamini, uhuru wa kuamini na kutoamini ni uhuru mmoja huo huo, kifalsafa, huwezi ku promote kuzipiga marufuku dini bila ya wewe usiyeamini kuhatarisha uhuru wako wa kutoamini dini.

Kwa falsafa hii, mimi napenda sana watu wawe na uhuru wa kuamini mpaka wao wenyewe wagundue kuwa imani hizi ni kamba tu. Na hata wasipogundua, ni sawa tu, ni haki zao za kikatiba na za kibinadamu.

Sitaki kumuondoa mtu kwenye imani yake kwa lazima, kwa sababu tu mimi nafikiri dini zinalemaza watu, au hata kama kweli dini zinalemaza watu, wakiamua kulemaa, ni haki yao.

After all, watu wana haki ya kuchagua maisha ya kulemaa akili, kama hicho ndicho kitu muhimu kwao.

Unajua kuwa kuna watu wanapenda uongo mtamu, kuliko ukweli mchungu.

Sasa, watu kama hao, wakichagua kuamini uongo mtamu wa dini, wewe ukawalazimisha waondoke kwenye uongo mtamu ukawapa ukweli mchungu kinyume na wanavyotaka wao, utakuwa umewakosea, umewaingikia kwenye uhuru wao.
 
Kama imechakachuliwa, huyo roho mtakatifu tunaeambiwa ndo alikuwa anawaongoza waandishi alikuwa anafanya kazi gani?
 
Adam ,Musa, ibrahimu, yakobo, walimwona mungu unasemaje mungu haonekani kwa macho ya mwili? Contradiction zipo nyingi tu ila we ndo huzioni maana unasoma biblia kishabiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…