Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Tafiti zinaonyesha kwamba...
1. Dini ya Kikristo inaongoza Kwa kuzalisha Atheists wengi.

2. Asilimia kubwa ya Atheists wa Jamii Forum wana background ya Kikristo.

Hypothesis:- data zinaonyesha kwamba sababu kubwa ya atheists wengi kuwa na background ya dini ya Kikristo ni contradictions nyingi zilizojaa kwenye kitabu chao,.hali inayofanya wengi kushindwa kuelewa mafundisho yao.
Kila mtu huzaliwa Atheist hata wewe ulizaliwa Atheist mpaka pale ulipo aminishwa kwamba kuna invisible man beyond the sky anaitwa Mungu.

Wewe ungezaliwa kwenye ukristo ungepinga uislamu kwa vile ndivyo ulivyo aminishwa tangu utotoni mwako.

Vivyo hivyo, umezaliwa kwenye uislamu unapinga ukristo kwa vile siyo imani uliyo lelewa na kukuzwa nayo.

Mtoto akizaliwa na asiambiwe chochote kuhusu uwepo wa Mungu na akakuzwa hivyo hivyo. HAWEZI kuja kuaminishwa habari za uwepo wa Mungu ukubwani.
 
1. Maneno binafsi yanaweza kuwa na ukweli.

2. Maneno ya Jamii nzima yanaweza kuwa na uongo.

& Vice versa ni kweli

Hivyo basi kauli yako hapo juu haiingii akilini.
Hiyo inabaki kuwa ni opinion zako tu.
mungu wako kwenye Quran unavyodai ni mungu sahihi ni maneno yako tu hayawezi kuwa Yangu.

mungu huyo wako unayemtaja sikuwahi msikia sehemu yoyote zaidi ya stori za vijiweni hivyo kwangu ni upuuzi

Karibu tujadili mada iliyopo mkuu.
 
Mtoto akizaliwa na asiambiwe chochote kuhusu uwepo wa Mungu na akakuzwa hivyo hivyo. HAWEZI kuja kuaminishwa habari za uwepo wa Mungu ukubwani.
Kuzaliwa kwenye jamii Fulani na kufundishwa Imani za jamii hiyo,.hakumfungi mtu aamini Imani hiyo maisha yake yote.

Kumbuka kadri tunavyokua tunajifunza vitu na kuelewa reality ya vitu ilivyo,..vile vyote vya uongo tulivyofundishwa na jamii zetu tunaachana navyo baada ya kugundua ukweli ulivyo,..na vile vyote vya ukweli tulivyofundishwa na jamii zetu tunaendelea navyo baada ya kugundua ni ukweli wa mambo ulivyo.

Katika Dunia hii ya Sayansi na teknolojia ujinga ni maamuzi,.. A determined person can indeed shine away from adversity and the prevailing beliefs of their society. Hakuna kisingizio chochote...DUNIA SINIA CHAGUA UNACHOTAKA.
 
Kuzaliwa kwenye jamii Fulani na kufundishwa Imani za jamii hiyo,.hakumfungi mtu aamini Imani hiyo maisha yake yote. K

umbuka kadri tunavyokua tunajifunza vitu na kuelewa reality ya vitu ilivyo,..vile vyote vya uongo tulivyofundishwa na jamii zetu tunaachana navyo baada ya kugundua ukweli ulivyo,..na vile vyote vya ukweli tulivyofundishwa na jamii zetu tunaendelea navyo baada ya kugundua ni ukweli wa mambo ulivyo.
Katika Dunia hii ya Sayansi na teknolojia ujinga ni maamuzi,.. A determined person can indeed shine away from adversity and the prevailing beliefs of their society. Hakuna kisingizio chochote...DUNIA SINIA CHAGUA UNACHOTAKA.
Ndio maana imani na dini zimegundulika ni Uongo kupitia watu kujifunza na kuchunguza kwa kina ukweli wa mafundisho ya kidini.

Mafundisho ya kidini yamejaa Contradictions na stori za uongo uongo tu.

Watu sasa wanatafuta ukweli halisi sio kubaki na imani za kufikirika na kusadikika.

Imani ya uwepo wa Mungu ni uongo mtupu. Ni imani ya kurithishwa isiyo na ukweli wowote ule.
 
Hiyo inabaki kuwa ni opinion zako tu.
mungu wako kwenye Quran unavyodai ni mungu sahihi ni maneno yako tu hayawezi kuwa Yangu.

mungu huyo wako unayemtaja sikuwahi msikia sehemu yoyote zaidi ya stori za vijiweni hivyo kwangu ni upuuzi

Karibu tujadili mada iliyopo mkuu.
Upo sahihi kwamba Mungu ni upuuzi Kwa upande wako. Hiyo ni haki yako kuamini kile unachotaka.,

Peace.
 
Ndio maana imani na dini zimegundulika ni Uongo kupitia watu kujifunza na kuchunguza kwa kina ukweli wa mafundisho ya kidini.

Imani ya uwepo wa Mungu ni uongo mtupu. Ni imani ya kurithishwa isiyo na ukweli wowote ule.
Upo sahihi,....cha ajabu ni kwamba:-
1. Wengine kwenye kuchunguza kwao wamegundua kwamba everything in this world is intelligently designed ndiyo maana wakaamini kwamba Kuna INTELLIGENT DESIGNER wa mifumo mbalimbali tunayoiona kwenye Dunia hii.

2. Wengine (ukiwemo wewe) kwenye kuchunguza kwao wamegundua kwamba there's no intelligent design,.. so Hakuna Intelligent DESIGNER,na mifumo yote hii tunayoiona imetokea tu accidentally.

Kwa mantiki hiyo makundi yote hayo mawili yanatokana na uchunguzi na kudadisi,..hivyo basi haina haja ya wewe kupambana kuonyesha kwamba upo sahihi sana kuliko wengine.,.. atleast ungeamua kuwa humble maana kwenye ulimwengu tunajua 0.0000% ya ukweli wa mambo ulivyo. Tunajua mambo machache sana kuhusu ulimwengu.
 
Exactly.

Hatuwezi kujua, tusicho kijua ila tuna punguza tusivyo vijua kwa kujifunza kadiri muda unavyokwenda.

Ishu ipo kwa hawa wafia dini wanao kaza mafuvu na wanao lazimisha imani zao za dini zina ukweli wote na majibu yote.

Hawa tuta deal nao Sawasawa hadi waelewe kwamba Atheists pia tupo sahihi...😅

Kama wewe ulivyo weza kutambua hivi.
 
Wewe Kisai kila siku nakwambia hivi

Unachojua ni Quran tu.

Si zaidi ya hapo.
Nilikwambia mje na zile hoja zenu za Kisayansi na Logic, uone kama hujaukimbia huu uzi, lakini mpaka muda huu unalalama.

Wewe leta hoja zako unazo ona ni sahihi kwenye Sayansi na kwingine, uone kama tunajua yaliyomo kwenye Qur'an pekee au vipi ?
 
Sasa kilichokufanya kujibu ni nini wakati hoja ni mikanganyiko iliyopo katika biblia?

Huoni unakosa utulivu wakusoma hoja na kuendekeza stori zako za kale za kiarabu mkuu?

Jikite katika hoja
Unaweza kuendelea na huyo unayeita ni mungu wako ukamuweka tukaja kujadili.

Karibu sana.
Angalia nilipo anzia humu kisha uje na haya uliyo yaandika.
 
Kutojua ulimwengu upo hivi ulivyo haimanishi niamini majibu ya uongo, na yanajidhihirisha ni ya uongo sababu ya contradiction zake, Na mola mwenye upendo mwingi lakini huyohuyo anasimamía uwepo wa maovu ,na si tu kusimamia vilevile yeye mwenyewe anaua.Ni dhahiri mungu huyo hayupo ila tu yupo kwenye vichwa vya wale walioamua kuwa mateka wa akili na hisia.
Safi kabisa, unapo kanusha jambo inamaanisha ya kuwa una ujuzi ukweli juu ya jambo hilo. Kinyume chake ni kuwa una shida katika akili yako.

Suala la Mungu ni suala maalumu, ambalo akili iliyo salama hailipingi hili, haiwezi kulilinganisha na mambo mengine ambayo uongo wake uko wazi.

Mfano haijawahi kuwa hoja eti kugongana kwa maandiko au kutokueleweka kwa maandiko ni sababu ya kutokuwepo kwa Mungu, sababu Kuna njia nyingi sana zinazo thibitisha uwepo wa Mungu, na si maandiko tu.

Bado hujawa na hoja ya kubatilisha uwepo wa Mungu zaidi ya maneno matupu na ujanja wa kucheza na maneno.
 
Mkuu,
Binafsi dhana nzima ya ukombozi kwenye mantiki huwezi kumueleza mtu akakuelewa.
Yaani alikuja kutukomboa katika dhambi, wakati kuna sehemu anatuma malaika waende kuua watu, nguvu za kugawanya bahari, kutembea juu ya maji , kurudisha sikio lililokatwa na kufufua zipo.

Ila akamleta mtoto wake afe kwa ajili ya ukombozi!
Mkuu DR Mambo Jambo embu weka neno hapa😂
🤣🤣🤣
Yaani Hilo tatizo kubwa sana mkuu...

Yaani Alikosewa yeye hakutoa Msamaha, akamtoa mwanae wa pekee ili afe awe kafara kwa ajili yake yeye mwenyewe ili ajiconvice yeye mwenyewe kutupa msamaha kwa ajili ya makosa yetu...

Kwanini aingesema tu nimewasamehe kuliko kujiconvince yeye mwenyewe na kutoa kafara kwa ajili yake?
 
Mkuu ,
Itabidi uanzishe uzi utuelezee hii dhana nzima ya ukombozi inakuwaje kuwaje😂

Mimi elimu yangu ndogo kwenye mambo Kama haya huenda wewe ukatuelezea maana kwenye akili yangu sikuwahi kuelewa.

Babu yangu ni mchungaji niliwahi kumuuliza jibu la mwisho akasema naona roho chafu ndani yako😂
 
Wakuu habari zenu?binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi sana kuhusu mikanganyiko(contradiction) katika vitabu vya dini.

Nimekuwa nikifatilia nyuzi nyingi za kiranga kuhusu kupinga uwepo wa mungu, tukitoa mihemko tukajenga hoja kwa mantiki (logical) character ya mungu mwenye nguvu zote, mwenye upendo wote na ajuaye yote hayupo na haiwezi kufit kwenye mizani ya mantiki.

Nimekuwa nikisoma Biblia na imekuwa ikijikanganya yenyewe na bado ikidai kwamba mungu huwa hakosei. Leo nitaonyesha baadhi ya mikanganyiko hiyo ambayo hata kiranga amekuwa akiiweka.hizi ni baadhi ya verse zenye mikanganyo[emoji116]

Mwanzo 1:3-5 BHN
Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.

Mwanzo 1:14 BHN
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka

Mwanzo 1:11-13 BHN
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.

Mwanzo 2:4-9 BHN
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni,

Mwanzo 1:26-27 BHN
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Hapa mungu aliumba mwanamume na mwamke.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

(Mbele kidogo mungu anaumba mwanaume)utaona jinsi gani anavyosahau kurekodi matukio katika mtiririko ulio sahihi.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

Mwanzo 6:6 BHN
Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake

Hesabu 23:19 BHN
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?

Kutoka 12:13 BHN
Basi, ile damu itakuwa ishara yenu ya kuonesha nyumba mtakamokuwa. Nami nitakapoiona hiyo damu, nitawapita nyinyi, na hamtapatwa na dhara lolote wakati nitakapoipiga nchi ya Misri.

Mithali 15:3 SRUV
Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.

( kwenye kutoka mungu wa kiyahudi anatoa maagizo wapake damu kwenye vizingiti vya milango ili asije kujichanganya, lakini mungu huyo huyo anajinasibu katika mithali macho yake yapo kila mahali)

Kutoka 20:14 BHN
“Usizini.

HOSEA 1:2
2 Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Karibuni tujadili bila kashfa tujadiliane, hizi ni baadhi ya mikanganyiko iliyopo katika biblia.

Kwanini mungu mkamilifu kitabu chake kiwe na mikanganyiko kiasi hiki?

Mungu anasifa zote za binadamu anasahau, anabadili mawazo yake, ana hasira, Ana wivu, katili, na tabia zingine nyingi za kibinadamu.
Kusoma biblia kama vile usomavyo vitabu vingine vya tunzi au novel ni kwamba unaingia chaka la tope nzito mazima.
Kitabu kinasomwa katikati ya mistari ambapo na karibu kitabu chote ni ufunuo uliofungwa kwa mihuri(code) ambapo mwenye uwezo wa kufungua hizi code ni manabii tuu kwa msaada wa Mungu kwa kila wakati husika.
Kitabu kimevamiwa na makanjanja ambao maandiko yanawaita vipofu na kwamba kipofu akimuongoza kipofu mwenzie wote wanatumbukia shimoni.
Ndicho kitu tunachoshuhudia hata leo hii.
Mmfano kitabu cha mwanzo sura ya kwanza ni uumbaji katika roho yaani wazo la mungu likiisha kutamkwa ndipo sura ya pili ni madhihirisho ya lile wazo lililotamkwa katika mwili(physical).
Mtu wa juu juu ni lazima uchanganyikiwe kuhusu kuumbwa kwa mtu katika sura na mfano wa Mungu na kule kufanywa kwa mtu katika mwili wa kufinyangwa udongoni katika sura ya pili ya kitabu cha mwanzo.
Sii watu wote wenye miili ya flesh lakini binadamu wote wana miili ya flesh (nyama na damu).

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huna tofauti na poyoyo wa mliyayoyo!

Karibu tujadili mada.
 
Mkuu ,
Itabidi uanzishe uzi utuelezee hii dhana nzima ya ukombozi inakuwaje kuwaje😂

Mimi elimu yangu ndogo kwenye mambo Kama haya huenda wewe ukatuelezea maana kwenye akili yangu sikuwahi kuelewa.

Babu yangu ni mchungaji niliwahi kumuuliza jibu la mwisho akasema naona roho chafu ndani yako😂
Hakuna Ukombozi wa kafara ya Mtu mkuu Hiyo ni changa la macho...
BIblia yenyew inasema kila mtu atabeba msalaba wake mwenyewe sasa iweje tu aambiwa kuna mtu akitubebea..
Watu wanashindwa kuamka kwenye ulimwengu huu
 
Back
Top Bottom