Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

kwanini unasema MUNGU HAYUPO?
 
Ni hivi ALLAH alimchagua Muhammad kuwa ni mtume.Muhammad asili yake ni Uarabu na lugha aliyokuwa akiiongea ni kiarabu hivyo kama ALLAH angeiteremsha Quran kea lugha ya kilatini ama kingereza au kiswahili basi wale baba zenu waliowatangulia katika kukufuru wangedai mbona Quran imeteremshwa kwa lugha ya kigeni ili hali sisi ni waarabu au huyu Muhammad amejifunza lini lugha ya kigeni ilihali amekulia kati yetu....kuondoa hili ALLAH akaamua kuiteremsha kwa lugha fasaha ya kiarabu na hili halikuwazuia wale wasiokuwa waarabu wasijifunze Quran. Maana toka zamani walikuwapo watu waliozungumza lugha zaidi ya moja.
 
Naku uliza hivi 👇

Allah huyo kwa nini Aumbe binadamu wa lugha tofauti tofauti kisha ashushe Quran kwa lugha ya kiarabu tu?
 
Naku uliza hivi 👇

Allah huyo kwa nini Aumbe binadamu wa lugha tofauti tofauti kisha ashushe Quran kwa lugha ya kiarabu tu?
Quran haijaacha kitu katika kujibi hoja zenu ..

ALLAH anaelezea sababu za kuumba wanadamu tofauti tofauti na lugha tofauti....

Ar-Rum 30:22

وَمِنْ ءَايَٰتِهِۦ خَلْقُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضِ وَٱخْتِلَٰفُ أَلْسِنَتِكُمْ وَأَلْوَٰنِكُمْۚ إِنَّ فِى ذَٰلِكَ لَءَايَٰتٍ لِّلْعَٰلِمِينَ

English -

And of His signs is the creation of the heavens and the earth and the diversity of your languages and your colors. Indeed in that are signs for those of knowledge.

Swahili

Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi.
 
kwanini unasema MUNGU HAYUPO?
Kwa sababu dhana ya uwepo wa Mungu mwema, mwenye huruma, upendo, mkamilifu, mwenye kujua yote na muweza wa vyote kwenye dunia iliyo jaa uovu, ukatili, uasi na mabaya Hai make sense na haina mantiki.

Dunia imejaa uovu, ukatili, maasi, mabaya na shida za kila aina

Mungu mwema na mwenye upendo, Alishindwaje kuumba dunia isiyo na uovu?

Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu wasio na uwezo wa kutenda mabaya?

Dunia iliyoumbwa na Mungu Mkamilifu, inakuwaje na uovu, dhambi, ukatili na maasi?
 
Sio hivyo tu, ALLAH pia anatuarifu kuwa katika uumbaji wake wa wanyama na watu pia ametutofautisha rangi ukiacha na makabila na lugha zetu ..Hizi ni ishara zake ila hakuna anayetambua haya ila yule aliyepewa Elimu .

Fatir 35:28

وَمِنَ ٱلنَّاسِ وَٱلدَّوَآبِّ وَٱلْأَنْعَٰمِ مُخْتَلِفٌ أَلْوَٰنُهُۥ كَذَٰلِكَۗ إِنَّمَا يَخْشَى ٱللَّهَ مِنْ عِبَادِهِ ٱلْعُلَمَٰٓؤُا۟ۗ إِنَّ ٱللَّهَ عَزِيزٌ غَفُورٌ

English -

And among people and moving creatures and grazing livestock are various colors similarly. Only those fear Allāh, from among His servants, who have knowledge. Indeed, Allāh is Exalted in Might and Forgiving.

Swahili -

Na katika watu, na wanyama, na mifugo, pia rangi zao zinakhitalifiana. Kwa hakika wanao mcha Mwenyezi Mungu miongoni mwa waja wake ni wanazuoni. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye nguvu, Mwenye kusamehe.
 
Naku uliza hivi 👇

Allah huyo kwa nini Aumbe binadamu wa lugha tofauti tofauti kisha ashushe Quran kwa lugha ya kiarabu tu?
ALLAH anapambanua tena nini manufaa ya kutuumba wanadamu tukiwa na rangi,lugha na makabila tofauti....

Al-Hujurat 49:13

يَٰٓأَيُّهَا ٱلنَّاسُ إِنَّا خَلَقْنَٰكُم مِّن ذَكَرٍ وَأُنثَىٰ وَجَعَلْنَٰكُمْ شُعُوبًا وَقَبَآئِلَ لِتَعَارَفُوٓا۟ۚ إِنَّ أَكْرَمَكُمْ عِندَ ٱللَّهِ أَتْقَىٰكُمْۚ إِنَّ ٱللَّهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ

English -

O mankind, indeed We have created you from male and female and made you peoples and tribes that you may know one another. Indeed, the most noble of you in the sight of Allāh is the most righteous[1] of you. Indeed, Allāh is Knowing and Aware.

Swahili -

Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari.
 
ALLAH hakushindwa kutuumba wanadamu wote tukawa ni weusi tupu, ama weupe tupu au wa njano tu....ila anatuarifu kuwa lengo la kututofautiaha makabila ,lugha n k ni kwa manufaa yetu wenyewe wanadamu ili tupate kutambuana sisi kwa sisi. Na hakuna mbora kati yetu sisi isipokuwa yule anayemcha zaidi Mola.

Mweupe sio bora kuliko mweusi wala mweusi sio bora kuliko mweupe isipokuwa tu kwa yule anayemcha zaidi Mola wake. Uchamungu ndio kipimo cha ubora mbele ya Mungu.
 
Mimi naomba kuuliza hivi Mungu/ Allah anajua kila kitu???

Namaanisha anajua kabla hajatuumba, anajua maisha yetu yote hapa duniani yapo/yatakuwa vipi na siku ya kufa anaijua na tutakufa vipi anajua??????
 
Quran haijaacha kitu katika kujibi hoja zenu ..

ALLAH anaelezea sababu za kuumba wanadamu tofauti tofauti na lugha tofauti....
Sasa kwanini ashushe Quran kwa lugha moja tu?

Wakati anajua aliumba wanadamu kwa lugha tofauti tofauti?
 
ALLAH hakushindwa kutuumba wanadamu wote tukawa ni weusi tupu, ama weupe tupu au wa njano tu....ila anatuarifu kuwa lengo la kututofautiaha makabila ,lugha n k ni kwa manufaa yetu wenyewe wanadamu ili tupate kutambuana sisi kwa sisi.
Tutapataje kutambuana sisi kwa sisi ilhali tuko na lugha tofauti, utamaduni tofauti na imani tofauti?

Allah huyo kama alitaka tutambuane sisi kwa sisi, Alishindwaje kutuumba wote tuwe waarabu?


Na hakuna mbora kati yetu sisi isipokuwa yule anayemcha zaidi Mola.

Mweupe sio bora kuliko mweusi wala mweusi sio bora kuliko mweupe isipokuwa tu kwa yule anayemcha zaidi Mola wake. Uchamungu ndio kipimo cha ubora mbele ya Mungu.
 
Shibe inayopatikana kwa shida sanaaaa au kwa wepesi sanaaaa, au njaa kali sanaa au shibe inayokosa kazi huleta matokeo kama haya tunayoyaona kwa mleta mada.

Aidha ulikua umevimbiwa
Au njaa imekukamata vya kutosha
Au michongo yako imekwama sana
Au michongo yako ni rahis sana

NDIO MAANA UKAANDIKA KITU KAMA HIKI
 
Tutapaje kutambuana sisi kwa sisi ilhali tuko na lugha tofauti, utamaduni tofauti na imani tofauti?

Allah huyo kama alitaka tutambuane sisi kwa sisi, Alishindwaje kutuumba wote tuwe waarabu?
Alishindwaje kutuumba sote waarabu...tayari unampangia Mungu afanye nini!? Unasahau kuwa Mungu hapangiwi afanye nini ila anatenda mambo kwa matakwa yake.


ALLAH anakujibu tena kupitia Quran

Hud 11:118

وَلَوْ شَآءَ رَبُّكَ لَجَعَلَ ٱلنَّاسَ أُمَّةً وَٰحِدَةًۖ وَلَا يَزَالُونَ مُخْتَلِفِينَ

English -

And if your Lord had willed, He could have made mankind one community; but they will not cease to differ,

Swahili -

Na Mola wako Mlezi angeli penda ange wafanya watu wote wakawa umma mmoja. Lakini hawaachi kukhitalifiana,


Quran 10:99-100
Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?

Na hawezi mtu kuamini ila kwa idhini ya Mwenyezi Mungu. Naye hujaalia adhabu iwafike wasio tumia akili zao."
 
Sasa hizo shida anazileta mungu au binadamu ndo tunazileta kwa mikono yetu?
 
Allah huyo, Anashushaje Quran kwa lugha moja tu ya kiarabu?

Allah huyo, Hakujua kwamba Duniani kuna watu wa lugha mbalimbali?

Allah huyo, Alishindwaje kushusha Quran hiyo kwa watu wote duniani wa lugha zote akaeleweka na watu wote kwa wakati mmoja?
Swali Lako Majibu Yapo QUR'AN 12:2 "Hakika Tumeiteresha Qur'an Kwa Kiarabu Ili Mpate Mazingatio" Biblia Iliyoandikwa Kwa Kila Lugha Wakristo Hawaijui Na Hakuna Hata Mmoja Duniani Aliyeikariri Yote Au Hata Agano La Kale Pekee Lakini Quran Iliyoshushwa Kwa Kiarabu Mpaka Watoto Wa Miaka 10 Wamekariri Yote Tena Waswahili Kabisa Wa Buza Hawana Uarabu Hata Wa Kusingizia,simamisha Muislamu Yoyote Mwambie Akusomee Quran Ataisoma Hata Waislamu Wa Kinyakyusa.Hayo Ndo Mazingatio.Tunaisoma Kama Alivyoisoma Mtume Na Tunaifuata Na Haipingiki Waislamu Ndo Wanaongoza Kwa Tabia Njema Wewe Mwenyewe Shahidi. Kushushwa Kwa Lugha Moja Ndo Kunafanya Mwafrika,mzungu Na Mchina Wakati Wa Ibada Wote Wanaelewana
 
Tutapataje kutambuana sisi kwa sisi ilhali tuko na lugha tofauti, utamaduni tofauti na imani tofauti?

Allah huyo kama alitaka tutambuane sisi kwa sisi, Alishindwaje kutuumba wote tuwe waarabu?
Mwanadamu ni kiumbe mbishi sana hata kama MUNGU angetuumba sote tuwe waarabu bado mngekuja na hoja ya kusema kwanini Mungu katuumba sote ni waarabu kwa nini asingetutofautisha. Ni sawa na watu wa Mussa walipokuwa wakiteremshiwa chakula kutoka mbinguni cha Manna na salwa....walipokuwa wakila na kushiba wakaanza kuhoji kwanini kila siku tunakula manna na salwa tu...kwanini Mungu asituache tukaenda kulima mazao mbalimbali huko mashambani!? Matokeo yake Mungu alisitisha ile ofa aliyokuwa akiwapa ya kula chakula bure pasi na kukitolea jasho na wakaachwa wakasulubike huko mashambani.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…