Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Mkuu tunachohoji ni mikanganyiko katika kitabu cha biblia, jaribu kupitia hiyo mistari michache hapo juu yaani sehemu Moja anasema hivi sehemu ya pili anasema hivi.

Karibu.
 
Sijauona huo mkanganyiko unaousema, mtu umeamka unapumua na umeshiba vizuri unaanza kumjadili Mungu
Mkuu Daudi1,
Kwenye pasaka mungu anawaambia wana wa israeli wapake damu katika vizingiti ili apate kufahamu sehemu waliyomo. embu tuondee mihemko.

Alishindwa kutambua sehemu walizopo na wakati anadai yeye yuko kila mahali?
 
Swali langu ni kwamba Mungu/Allah alikosea kumuumba shetani au alimuumba makusudi ili atutese watu aliotuumba???

Zingatia Mungu/Allah anajua kila kitu au labda uniambie kuna vitu Mungu/Allah hajui kama Sisi binadamu akajikuta anaumba malaika baadae akabadilika bila matarajio ya Mungu/Allah akageuka na kuwa shetani???
 
Hivi kwanini Mungu/Allah aliumba watu ambao baadae anaenda kuwachoma Moto mukusudi?????, halafu Mungu/Allah kwanini mbaguzi sana anaumba watu wengine maalumu wa kwenda kula bata na mabikira peponi na wengine kawaumba kwa ajili ya kuwachoma Moto????
 
Kwanza shetani sio malaika !

ALLAH ametuhabarisha katika Quran juu ya asili ya Iblis.

Al-Kahf 18:50

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَٰٓئِكَةِ ٱسْجُدُوا۟ لِءَادَمَ فَسَجَدُوٓا۟ إِلَّآ إِبْلِيسَ كَانَ مِنَ ٱلْجِنِّ فَفَسَقَ عَنْ أَمْرِ رَبِّهِۦٓۗ أَفَتَتَّخِذُونَهُۥ وَذُرِّيَّتَهُۥٓ أَوْلِيَآءَ مِن دُونِى وَهُمْ لَكُمْ عَدُوٌّۢۚ بِئْسَ لِلظَّٰلِمِينَ بَدَلًا

English - Sahih International

And [mention] when We said to the angels, "Prostrate to Adam," and they prostrated, except for Iblees. He was of the jinn and departed from [i.e., disobeyed] the command of his Lord. Then will you take him and his descendants as allies other than Me while they are enemies to you? Wretched it is for the wrongdoers as an exchange.

Swahili -

Na tulipo waambia Malaika: Msujudieni Adam! Walimsjudia isipo kuwa Iblisi. Yeye alikuwa miongoni mwa majini, na akavunja amri ya Mola wake Mlezi. Je! Mnamshika yeye na dhuriya zake kuwa marafiki badala yangu, hali wao ni adui zenu? Ni ovu mno badala hii kwa wenye kudhulumu.
 
Mkuu Daudi1,
Kwenye pasaka mungu anawaambia wana wa israeli wapake damu katika vizingiti ili apate kufahamu sehemu waliyomo. embu tuondee mihemko.

Alishindwa kutambua sehemu walizopo na wakati anadai yeye yuko kila mahali?
Hilo ni agano la Kwanza la damu analofanya na wanawaizrael, ndio maana akasema watalikumbuka miaka yao yote, maana yake pia ambaye asingefanya Kama maagizo ya Mungu angekuwa nje ya agano, ukitaka kujua ni agano angalia namna walivyooelekezwa kula hiyo nyama ambayo damu yake ilifanyika kuwa agano. Hamna contradiction hapo
 
Weka Mbali Na Hayo Yote Mbona Mikanganyiko Inaonekana Iko Wazi Na Hajabadili Maandiko Au Wewe Ndo Utakuwa Una Njaa Huelewi.
 
Iblis ni miongoni mwa MAJINI na hakuwa Malaika kama wengi wanavyodhani! Malaika hawana sifa ya uasi, hawana matamanio na wala hawana watoto . Majini wana sifa kama za wanadamu tu, wanaasi,wana jinsia, wana matamanio, wana uzao n k
 
Sasa hizo shida anazileta mungu au binadamu ndo tunazileta kwa mikono yetu?
Kamleta Mungu/Allah maana kila kitu kinachotikea duniani basi ni Kwa amri yake,
Kwa kuwa Mungu/Allah hakupanga tundu lissu are kwa risasi na hakufa hata baada ya kupigwa risasi 38, ila kama Mungu/Allah akipanga ufe risasi moja Tu ilitosha,

Kwa hiyo tunaona mratibu mkuu wa kila tukio linalotoke duniani ni mipango ya Allah/Mungu
 
Iblis ni miongoni mwa MAJINI na hakuwa Malaika kama wengi wanavyodhani! Malaika hawana sifa ya uasi, hawana matamanio na wala hawana watoto . Majini wana sifa kama za wanadamu tu, wanaasi,wana jinsia, wana matamanio, wana uzao n k
Malaika wanaasi pia, unawafahamu Wanefili?
 
Asante mkuu,
Hilo ni agano la kwanza alilolifanya na wana wa izraeli! Agano hilo wanalikumbuka kwa namba gani mpaka sasa?

Mungu huyo anakataza uzinzi, na anasema mimi si mwanadamu hata nibadili neno langu wakati hapo hapo mungu huyo anazo sifa zote za kibinadamu.

Baadae tena mungu huyo huyo anamuagiza Hosea akajitwalie mke wa uzinzi, unamtetea vipi katika hilo.

Contradiction zipo nyingi.
Karibu mkuu.
 
Majini, ibilisi waliumbwa na Nani???
Au na yenyewe Yana sifa kama ya Mungu/Allah kuwa hayakuzaliwa wala kuumbwa ????
 
Mungu ana elimu na mambo yote yanayotokea ulimwenguni, Kila kitu kinachotokea kilishapangwa kiwe kabla ya kuumbwa kwa hii dunia .

Mungu ameumba mwanadamu kisha akambainishia njia zote, njema na ovu kisha akampa uhuru achague wapi anaelekea.
 
Tujadili Mikanganyiko Katika Biblia Kama Ilivyoletwa Na Mtoa Mada Ili Tupate Elimu Maana Mada Imehamia Kwenye Uwepo Wa Mungu Wa Mungu,kinachojadiliwa Hapa Ni Kitabu
 
Je Mungu/Allah anawaumba majini, shetani na ibilisi alikuwa hajui kuwa watakuja kumuasi????

Yaani nataka kujua kama uinjinia wa Mungu/Allah ulishindwa kujua kuwa kuwaumba mashetani,ibilisi na majini kuwa yatakuja kumuasi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…