Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Iblis ni miongoni mwa MAJINI na hakuwa Malaika kama wengi wanavyodhani! Malaika hawana sifa ya uasi, hawana matamanio na wala hawana watoto . Majini wana sifa kama za wanadamu tu, wanaasi,wana jinsia, wana matamanio, wana uzao n k
Ibilisi aliumbwa na Nani????

Aliyemuumba alikuwa Hana uwezo wa kujua kuwa atamuasi?????

Sasa kama Mungu/Allah anakosea kwanini amchome binadamu Moto Kwa makosa yake yeye????

Kama Mungu/Allah aliumba malaika ambao hawana uwezo wa kumuasi Mungu/Allah alishindwa nini Kwa binadamu?????
 
MKuu Daudi!
Natamani niende one to one na tuanze kujadili contradiction moja baada ya Nyingine tutaanza agano la kale tutamalizia agano jipya kama hutojali...

Ili nijifunze zaidi maana ut seems uko vizuri...
Nasubiri comfirmation yako

ASANTE..!

Ni mimi
Dr Mambo Jambo Habari Hi
 
Malaika wanaasi pia, unawafahamu Wanefili?

Mwanzo 17:1-8 BHN​

Wakati Abramu alipokuwa na umri wa miaka tisini na tisa, Mwenyezi-Mungu alimtokea, akamwambia, “Mimi ni Mungu mwenye nguvu.



Waamuzi 1:19 SRUVDC​

BWANA alikuwa pamoja na Yuda; naye akawafukuza watu waliokaa katika nchi yenye milima; asiweze kuwafukuza hao waliokaa katika hilo bonde, kwa kuwa wao walikuwa na magari ya chuma.
 
unaweza ukajisaidia mbele za watu?
 
Problem of evil 🤣🤣
 
Hilo agano si ndio pasaka yenyewe sasa, waliagizwa kula mikate isiyotiwa chachu, hata Yesu alifanya pasaka na wanafunzi wake.

Hosea anaagizwa kwenda kuoa mwanamke kahaba, sio kwamba Hosea ni mzinzi la hasha, Soma mistari ya chini, alikuwa anazungungumza juu ya jamii ile iliyokuwa imemuasi Mungu, Hosea alitakiwa apeleke ujumbe wa laana, na ukiwa. "Kwa maana nchi hii imejaa inafanya uzinzi mwingi kwa Kumwacha BWANA"

Ukisoma mistari ya chini unaona Mungu anampa Hosea majina ya watoto wanaozaliwa na maana ya hayo majina, lakini Mungu anamwambia katika wana waizrael litasalia kabila la Yuda tu wengine watakutana na hasira ya Mungu.

Soma sura ya pili Hosea anachowaambia wanawe, hicho ndicho Mungu alikikusudia kwa nchi ile
 
swali ni Kwanini unakataza uzinzi Halafu unatoa Amri ya mtu kwenda kufanya uzinzi?
Halafu bado unasema wewe ni mungu ujuaye yote?
Kipindi anasema acha uzinzi hakufikiria kwamba atakuja kumwambia Hosea akafanye uzinzi? Alishindwa kufikiria hilo?
 
Tujadili Mikanganyiko Katika Biblia Kama Ilivyoletwa Na Mtoa Mada Ili Tupate Elimu Maana Mada Imehamia Kwenye Uwepo Wa Mungu Wa Mungu,kinachojadiliwa Hapa Ni Kitabu
Kabla ya kujadili vitabu lazma tumjue mwenye vitabu vyake yupo au hayupo.
 
Nashukuru Mkuu, ila nasikitika kuwa naingia kwenye majukumu pengine mpaka jioni Kama hautajal, Mimi pia napenda kujifunza, napenda sana kusoma na kuijadili Bibilia maana mnapojadili mambo ya Mungu Kuna wengine wanapona. Ubarikiwe sana
 
Mwanadamu ni kiumbe mbishi sana hata kama MUNGU angetuumba sote tuwe waarabu bado mngekuja na hoja ya kusema kwanini Mungu katuumba sote ni waarabu kwa nini asingetutofautisha.
Mungu huyo Aliumbaje binadamu wabishi sana?

Mungu huyo, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao mtii siku zote?
Mungu muweza wa vyote, Alishindwaje kuumba binadamu wema tu watakao fuata maagizo yake siku zote?
 
Mungu ana elimu na mambo yote yanayotokea ulimwenguni, Kila kitu kinachotokea kilishapangwa kiwe kabla ya kuumbwa kwa hii dunia .

Mungu ameumba mwanadamu kisha akambainishia njia zote, njema na ovu kisha akampa uhuru achague wapi anaelekea.
Kama Mungu/Allah kaweka njia zake binadamu anakwepa vipi?????

Kama Mungu/Allah anajua kila kitu hata kabla ya kuumbwa ulimwengu na kila kinachotokea alishakipanga sasa kosa la binadamu ni nini????

Unailaumu vipi Israel kuuwa wapalestina wakati ni mipango ya Mungu/Allah toka zamani????

Kama Mungu/Allah amepanga kila kitu na anajua kila kitu hata kitakachotokea baada ya kiama, maana yake kuna binadamu Mungu/Allah aliowaumba na anajua kabisa kuwa baada ya kifo chao wataenda motoni, yaani anajua kabisa binadamu huyu akizaliwa ataitwa majanga na katika maisha yake duniani yatakuwa ya dhambi na akifa nitamchoma Moto,

Kwa hiyo tunaona kabisa Mungu/Allah kaumba watu ambao watakwenda motoni na anawajua Kwa majina mpaka idadi na kuna watu Mungu/Allah kawaumba kwa ajili ya kwenda peponi anawajua Kwa majina na idadi,
Kwa hiyo ukiona binadamu anafanya dhambi Siyo kapenda Ila Mungu/Allah ndiyo kapanga iwe hivyo, ndiyo maana unaweza kwenda Kwa kahaba ukamlipa 100k halafu pesa hiyo hiyo ikaenda kumuokoa mwanae na kifo baada ya mtoto kuumwa na pesa hiyo ikatumika kumpeleka hospital na kulipia matibabu ya mtoto
 
Achana na Kiranga Komo,katika imani simama wewe kama wewe
 
swali ni Kwanini unakataza uzinzi Halafu unatoa Amri ya mtu kwenda kufanya uzinzi?
Halafu bado unasema wewe ni mungu ujuaye yote?
Kipindi anasema acha uzinzi hakufikiria kwamba atakuja kumwambia Hosea akafanye uzinzi? Alishindwa kufikiria hilo?
Mkuu samani hiyo logic ya kawaida sana, madawa ya kulevya yanakatazwa na ukikutwa nayo unajua nini kitakupata, lakini yanatumika hospital katika kutibu, hoja yangu Ni hii, jamii ya wana waizrael walimwasi Mungu na kuiasi hiyo amri ya kutozini, ndipo Mungu anamtuma Hosea kupeleka ujumbe kwa njia hiyo hiyo
 
Nashukuru Mkuu, ila nasikitika kuwa naingia kwenye majukumu pengine mpaka jioni Kama hautajal, Mimi pia napenda kujifunza, napenda sana kusoma na kuijadili Bibilia maana mnapojadili mambo ya Mungu Kuna wengine wanapona. Ubarikiwe sana
Asante kwa confirmation mimi pia nipo kwenye majukumu..
Nafikiri Muda wa Kaisari ukiisha kwenye saa kumi itakuwa vizuri
 
Ninachoomba ni kujikita katika sifa za ominiscent(mwenye kujua yote) omipresence(aliyeko kila mahali) .

Mkuu ukishaanza kutolea Mifano ya madawa unamleta katika mizani ya binadamu na yeye anasema si binadamu lakini sifa zote za binadamu anazo.

Tujikite katika sifa zake mungu ajuaye yote. Huoni Kama anajikanganya mwenyewe?

Pointi ni kwanini mjuzi wa yote Anabadilisha maneno?
 
Nae utasema MUNGU alipanga ajisaidie mbele za watu?
Kiufupi binadamu tumepewa akili,u tashi,tamaa n.k.
Tunayoyafanya mama au mabaya ni matokeo YA KUTUMIA AKILI ZETU VIZURI AU VIBAYA.
Ukisema hivi unataka kuniambia kuwa Mungu/Allah Hana uwezo wa kujua kuwa kiumbe wake aliyemuumba atakunya hadharani????

Halafu hata hiyo ya wewe kuona aibu kuisaidia hadharani ni Kwa kuwa Mungu/Allah kakufanya hivyo au kakupangia hivyo mbona Kwa mbuzi amezeza sasa kwako angeshindwa nini?????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…