Wewe unaipinga dini, kwa nini unaifanya dini bado iwe dira yako? Kwa nini unaiga inachofanya dini wakati wewe unataka kutoka kwenye dunia ya dini?
Kwa nini unaicopy dini kwamba dini inapinga wasioamini, na wewe ambaye huamini unapinga dini?
Huoni mpaka hapo unakuwa bado unaifanya dini ikupangie maisha yako, badala ya kujitungia mfumo mwingine wa maisha?
Watu wengine tuliotoka kwenye dini hatusumbuliwi na waamini dini. Tunawaachia uhuru wao kwenye imani, ingawa tukija kwenye facts tuna wa set straight.
Kuhusu swali lako, wachawi, waganga wa jadi, kupiga ramli zote hizo ni imani tu, na as long as hawamdhuru mtu, waachiwe tu watimize imani zao, na hivyo ndivyo mtu asiyeamini dini kama mimi anatimiza uhuru wa kuamini wa kila mtu.
Watu wa dini wana haki ya kusema kwamba dini zao haziruhusu mambo hayo, and that is OK. There is nothing special in that. Ila, wewe ukianza kuwaonea gele watu wa dini kwa nini wanaweka mipango yao hivyo, wewe ndiye unawapa u special.
Wewe unaweza kuanzisha jamii yako ya wasioamini, ikasema kwamba waganga wa kienyeji ni watu muhimu katika research za madawa ya asili, hatuwabagui. Tutawa upgrade wafanye mambo kileo na kisayansi zaidi. Umeondoa ubspecial wa watu wa dini hapo. Waganga wa kienyeji kibao watasema hebu tumsikilize huyu mtu hatubagui kama dini zinavyotubagua.