Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

Out of topic,
Soma kichwa cha uzi anzisha uzi wako kuhusu Quran nitakuja Kuchangia mkuu.

Halafu utuonyeshe mungu huyo asiyekuwa na mikanganyiko.
Sawa watakuja kuanzisha wanaojua kuandika.mimi siwezi.
 
Sasa kama huyo Mungu muweza na mwenye nguvu tulieaminishwa kuwa ana nguvu kumbe nae anafanya makosa kama ya kibinadamu, yaani Neno lake alilotuaminisha ni takatifu kumbe limejawa uongo na mikanganyiko, tunawezaje kuthibitisha au kuamini hata uwepo wake sio Uongo?

Ni sawa na kulazimisha maji kupanda mlima, ndivyo hivyo kulazimisha Mungu wa biblia/quran kuwepo wakati hawana vithibitisho.

Biblia/quran sio kithibitisho cha uwepo wa huyo Mungu maana hivyo vitabu havina logic wala ushahidi wa stories zake, pia huwezi kumthibitisha Mungu kupitia hizo ngonjera zake za uongo za vitabu vya dini.

Kuna wale wanaosingizia masuala ya Uumbaji, nipende tu kuwaambia ukweli mchungu, Mungu hausiki na uumbaji wa dunia wala kiumbe chochote dunian wala nje ya dunia, maana kiuhalisia Mungu nae ni kiumbe, je inawezekana kiumbe kuumba kiumbe mwingine?

Someni vizuri hizo ngonjera za vitabu vya dini zenu mtagundua kuwa kumbe hata binadamu akiwa na nguvu ktk jamii yake nae ni Mungu, kiumbe cha kiroho chochote ni Mungu, hata huyo Mungu wa Mbinguni nae ni kiumbe maana anaishi ktk ulimwengu, na sifa kuu ya kiumbe ni kuishi au kuwa covered/kupatikana/existence ktk ulimwengu wa Mwili au Roho.

Haiwezekani muumbaji aishi ktk kitu/ulimwengu aliouumba yeye mwenyewe je kabla hajazifanya hizo mbingu alikuwa wapi? Someni vizuri na mzielewe hizo stories zenu za uongo mtayajua madhaifu mengi ya huyo mnaemuita Mungu.

Narudia tena wanaopinga uwepo wa Mungu wako sahihi na wanaolazimisha uwepo wa Mungu wako sahihi pia maana hata sisi binadamu ni waungu kwa baadhi ya viumbe dhaifu hivyo tunavitawala, na wanaopinga uwepo wa Mungu wako sahihi maana huyo Mungu tulieaminishwa hayuko na wala hatowai kuwepo zaidi ya ngonjera za vitisho.
Kwani basi ukiuliza wanaojiona wanajua dunia au mbingu ni nini? Viko wapi? Kuna mwenye maelezo? Atakujibu tu alivyosikia kwa watu au kusoma,
Wanasema hakuna jipya chini ya jua. Vyote tunavyoviona vilikuwepo. Basi na hayo maandiko ni utapeli unaondelea. Wasiojua kuchagua mbivu na mbichi wataamini hivyo. Tatizo lao,wanatakaga kuaminisha na wengine uwepo wa huyo Mungu,mara msipomuamini atawafanya hivi na vile,msipomtumikia itakuwa hampati hiki na kile.
 
Mkuu mjinga,
Ni hivi nikiwasha feni nikaweka karatasi mbele yake itapepea Nina feel upepo, upepo unaweza kupimwa.
Upepo ukiwa mkali utaona outcome majani yana ruka light object vina move.

Thibitisha mungu kwa namna yoyote ile?
Umeona sasa kumbe unaamini upepo UPO KWA KUHISI KUWA KUNA UPEPO.ila haujawahi kuuona.ila mungu anasema kaumba dunia unabisha.kisa haonekani
 
Umeona sasa kumbe unaamini upepo UPO KWA KUHISI KUWA KUNA UPEPO.ila haujawahi kuuona.ila mungu anasema kaumba dunia unabisha.kisa haonekani
unaweza kunionyesha nilipoandika nina amini upepo upo?
 
Rhetorical questions! Ni maswali yasiyohitaji majibu ila yanamfanya msikilizaji afikiri zaidi. Mungu kuwauliza wapagani sio kwamba hajui majibu yake ila anawauliza ili wapate kutafakari zaidi.
Wapagani ni watu gani? Hivi huyo mungu wenu aliyeumba watu kwenye makundi tofauti,hamuoni ana shida? Sasa kama tumeumbwa katika yeye, je,unawezaje dhibitisha hayupo kwenye hilo kundi la wapagani? Wahalifu?........
 
Kama Mungu huyo yupo Nita muuliza maswali mengi sana anipe majibu ya kueleweka.

Ana umbaje dunia yenye shida halafu yeye anakula bata huko mbinguni?
🤣🤣

Alishindwaje kuumba dunia yenye bata kama anazo kula yeye huko?😅
Ayaa bhana
 
Mungu si Binadamu.wala hafanani na binadamu,wala malaika.yupoje anajua yeye.uwezo wetu wa kujua umeishia hapa

Nimekuuliza ni Mungu yupi unayemzungumzia wewe ili niwe specific

Binadamu wametengeneza miungu wengi sana
Naweza kumrejea Zeus kumbe wewe unamaanisha Yesu au Allah
 
Thibitisha kauli Yako, ukishindwa ichunge.
Nimsapoti. Adhibitishe kauli gani? Kwani Allah si ndo mungu?
Hivi hata ukianzia hapa tu,hamuoni kwamba mpo tu kwenye meri inayozama!!! Iweje watu mmezaliwa sehemu moja,mazingira ya pamoja,tena wengine familia moja. Af, mtu aje eri mi naamin Mungu. Mwingine hapana, ni Allah. Af kwenye kujibu mungu au allah,unapewa majibu sawa. Huo utofauti unatokaga wapi?
 
Kama Mungu huyo yupo Nita muuliza maswali mengi sana anipe majibu ya kueleweka.

Ana umbaje dunia yenye shida halafu yeye anakula bata huko mbinguni?
🤣🤣

Alishindwaje kuumba dunia yenye bata kama anazo kula yeye huko?😅
Mkuu,hao bata anakula basi? Ukiuliza utaambiwa tunaishi nae,hata hapa ulipo yupo. Hapo ni kwa kila mtu:
-kama kila mtu yupo na mungu,watu wanaosadikika kuwa bilioni ngapi hao,kila mtu ana mungu wake. Kwa nini tuaminishwe kuwa ni mmoja?
-Hilo lipo wazi wakienda kugegedana lodge na madangulo,mungu yupo. Mungu gani wanaenda kuchungulia watu watapofanya yao?
- huko baa,mungu wanae. Hata walevi sawa tu.
-wanaofanya uhalifu,anaenda nao,haoni tabu,kazi kuunga tera tuuuu.
-waendao kwa waganga,anao wanaongozana.
Mganga hapo hapo,ina maana yupo nae.
-wanakoua,yupo tuuu. Sasa hapa utajiuliza. Kuna mungu awasindikizae watakaouwa,na awasindikizae watakaouliwa.
Hao mungu ni wangapi?

Sasa kwa maovu ya viumbe wao au wake hayo,kama ni mmoja hamuoni udhaifu wake?/wao kama kila mtu ana wa kwake?
Kama na yeye anavumilia misukosuko kama tunayopitia,wa nini sasa!

Mungu wa mchongo aise
 
Nafikiri ungejikita katika mada mkuu.

Tumeweka mistari yenye mikanganyiko Hapo juu.
Unaweza ukaondoa contradiction hizo

Karibu sana.
Sijatoka kwenye mada, kama unakusudia hiyo mistari ya kwenye Biblia wenye Biblia yao watakuja kujibu.
 
Nimekuuliza ni Mungu yupi unayemzungumzia wewe ili niwe specific

Binadamu wametengeneza miungu wengi sana
Naweza kumrejea Zeus kumbe wewe unamaanisha Yesu au Allah
Mimi nipo UPANDE WA ALLAH.
 
Mungu hayupo kwa sababu mabaya yapo. Angekuwepo yasingekuwepo, pili kutojua kwanini ulimwengu upo hivi haithibitishi mungu yupo, kukimbilia jibu la kwamba mungu ndo katengeneza ulimwengu hivi ulivyo ni kutafuta psychological relief juu ya maswali yanayohitaji majibu yasiyokuwa na ukakasi.
Kusema atheism ni ugonjwa, nionyeshe mtu alielazwa hospital akipatiwa dozi ya atheism.
Mola ndio ameruhusu yote hayo yatokee.

Kadhalika hii sio hoja bali ni kioja, yaani kwa vipi uwepo wa mabaya ndio uthibitisho wa kuwa Mungu hayupo ? Hivi umekifikiria ulicho kiandika ?

Wewe umejuaje kama angekuwepo (kama unavyo dai) mabaya yadingekuwepo ? Yaani kipi kinakujulisha ya kuwa kutokuwepo kwa Mungu ni kuwepo kwa mabaya ?

Sasa tuambie wewe imekuwaje ulimwengu ukawa hivi ulivyo ? Kisha uthibitishe ukweli wa hoja yako.

Nani alikwambia mgonjwa ni mpaka alazwe hospitali ?
 
Wewe umejuaje kwanza! Kama anakupenda kwa nini asikupe hayo maarifa ya kumjua?
Kuna MIPAKA.wakati baba yako anakwenda kuoga uwa anakuita kumuangalia?
Ndivyo mungu kaweka mipaka ya kumjua.
 
Back
Top Bottom