Mikanganyiko katika Biblia ni kigezo kinachowapa watu uhalali wa kusema hakuna Mungu

😂😂😂 Kuna mtu anasemaga “imani ni shambulio la akili”

unajua nilichokuja kugundua ukiwa neutral kwenye hizi hekaya za kiarabu na kiyahudi utaishi kwa Amani.

Kuna rafiki yangu ni muislamu huwa kwenye mijadala yupo songea. Ni muislamu yule umuambii kitu.

sasa siku moja sehemu moja panaitwa mliyayoyo, tukawa yupo na jamaa wanabishana kuhusu Quran maeneo ya shambani. Mashamb ya mahindi.

Basi huyu rafiki yangu akaanza stori zake za uislamu, kuna jamaa akasema uislamu ni ushenzi tu, jamaa akakasirika akasema nitakuletea Quran sasahiv ubadilike chura!

Jamaa akasema leta, huwezi amini alienda kufata Quran Yule jamaa alivyofika akampa shika Halafu sema tena maneno yako uone.

Alishika ile Quran akachana vikaratasi vidogo vidogo ule ugomvi uliotokea pale😂😂.
Mpaka analia na maneno kibao sijui uamki, utakua chizi. Mpaka sasa yupo na anandelea kudundA.
Hivi vitu ukiendekeza utaumia sana.
Kweli kabisa, kuwa mfia dini ni kujiumiza akili tu maana utalazimika kukubaliana na Mambo mengine ambayo unaona wazi ni uongo. Mi nipo unguja kuna washkaji tupo nao kwenye kazi wanasema ukichana au kukojolea Quran unakuwa chizi, nikawaambia wanipe niikojolee hawajanipa hadi leo.
 
Katika vitu ambavyo huwa nasisitiza humu ndani ni kuwa, muwe mnasoma haya mambo sio mnajiandikia andikia, yaani mtu anakuja kubisha juu ya kitu ambacho kila anachoandika kuhusu hicho kitu anakosea. Wengi mpo hivyo humu ndani, maana yake mnakuja humu kupotezea watu muda.

Sasa tunakuuliza au tunakuomba utuambie nani ameandika Qur'an na alisoma Biblia ipi ? Sababu kipindi Mtume yupo hapakuwa na Biblia.

Njoo utuonyeshe hapa wapi Kuna mawazo ya kibinadamu ? Utakuta hujawahi hata kuisoma Qur'an zaidi ya kuisikia tu.

Unauliza tena ameandika nani na wewe unasema ni mawazo ya binadamu na una kiri muandishi wa Qur'an alisoma Biblia ? Tuambie wewe Sasa.
We jamaa inaonekana hata historia za dini hujui, yaani unasema kipindi cha mudi Biblia haikuwepo? Haupo serious wewe. Kwa hiyo Quran aliyoileta mudi imetangulia kuwepo kabla ya Biblia?
 
Wakuu habari zenu?binafsi nimekuwa nikifuatilia mijadala mingi sana kuhusu mikanganyiko(contradiction) katika vitabu vya dini.

Nimekuwa nikifatilia nyuzi nyingi za kiranga kuhusu kupinga uwepo wa mungu, tukitoa mihemko tukajenga hoja kwa mantiki (logical) character ya mungu mwenye nguvu zote, mwenye upendo wote na ajuaye yote hayupo na haiwezi kufit kwenye mizani ya mantiki.

Nimekuwa nikisoma Biblia na imekuwa ikijikanganya yenyewe na bado ikidai kwamba mungu huwa hakosei. Leo nitaonyesha baadhi ya mikanganyiko hiyo ambayo hata kiranga amekuwa akiiweka.hizi ni baadhi ya verse zenye mikanganyo👇

Mwanzo 1:3-5 BHN
Mungu akasema, “Mwanga uwe.” Mwanga ukawa. Mungu akauona mwanga kuwa ni mwema. Kisha Mungu akautenganisha mwanga na giza, mwanga akauita “Mchana” na giza akaliita “Usiku.” Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya kwanza.

Mwanzo 1:14 BHN
Mungu akasema, “Mianga na iweko angani, itenge mchana na usiku, ioneshe nyakati, majira, siku na miaka

Mwanzo 1:11-13 BHN
Kisha Mungu akasema, “Nchi na ioteshe mimea. Mimea izaayo mbegu, na miti izaayo matunda yenye mbegu.” Ikawa hivyo. Basi, nchi ikaotesha mimea izaayo mbegu kwa jinsi yake, na miti izaayo matunda yenye mbegu kwa jinsi yake. Mungu akaona kuwa ni vyema. Ikawa jioni, ikawa asubuhi; siku ya tatu.

Mwanzo 2:4-9 BHN
Hivyo ndivyo mbingu na dunia zilivyoumbwa. Siku ile Mwenyezi-Mungu alipoziumba mbingu na dunia, Hapakuwa na mimea juu ya nchi wala miti haikuwa imechipua kwani Mwenyezi-Mungu hakuwa ameinyeshea nchi mvua, wala hapakuwa na mtu wa kuilima. Hata hivyo, maji yalitoka ardhini yakainywesha ardhi yote. Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai. Kisha Mwenyezi-Mungu akapanda bustani huko Edeni,

Mwanzo 1:26-27 BHN
Kisha Mungu akasema, “Tumfanye mtu kwa mfano wetu, kwa sura yetu; atawale samaki wa baharini, ndege wa angani, wanyama wa kufugwa, dunia yote na viumbe vyote vitambaavyo.” Basi, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake; naam, kwa mfano wake Mungu alimuumba. Aliwaumba mwanamume na mwanamke. Hapa mungu aliumba mwanamume na mwamke.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

(Mbele kidogo mungu anaumba mwanaume)utaona jinsi gani anavyosahau kurekodi matukio katika mtiririko ulio sahihi.

Mwanzo 2:7 BHN
Basi, Mwenyezi-Mungu akamfanya mwanamume kwa mavumbi ya udongo, akampulizia puani pumzi ya uhai, na huyo mwanamume akawa kiumbe hai.

Mwanzo 6:6 BHN
Mwenyezi-Mungu alisikitika sana kwa kumuumba binadamu duniani. Mwenyezi-Mungu alihuzunika sana moyoni mwake

Hesabu 23:19 BHN
Mungu si mtu, aseme uongo, wala si binadamu, abadili nia yake! Je, ataahidi kitu na asikifanye, au kusema kitu asikitimize?

Kutoka 12:13 BHN
Basi, ile damu itakuwa ishara yenu ya kuonesha nyumba mtakamokuwa. Nami nitakapoiona hiyo damu, nitawapita nyinyi, na hamtapatwa na dhara lolote wakati nitakapoipiga nchi ya Misri.

Mithali 15:3 SRUV
Macho ya BWANA yako kila mahali; Yakimchunguza mbaya na mwema.

( kwenye kutoka mungu wa kiyahudi anatoa maagizo wapake damu kwenye vizingiti vya milango ili asije kujichanganya, lakini mungu huyo huyo anajinasibu katika mithali macho yake yapo kila mahali)

Kutoka 20:14 BHN
“Usizini.

HOSEA 1:2
2 Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha Hosea, Bwana alimwambia Hosea, Enenda ukatwae mke wa uzinzi, na watoto wa uzinzi; kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana.

Karibuni tujadili bila kashfa tujadiliane, hizi ni baadhi ya mikanganyiko iliyopo katika biblia.

Kwanini mungu mkamilifu kitabu chake kiwe na mikanganyiko kiasi hiki?

Mungu anasifa zote za binadamu anasahau, anabadili mawazo yake, ana hasira, Ana wivu, katili, na tabia zingine nyingi za kibinadamu.
Kama unafikiri kuna mikanganyiko ktk Biblia, na ukafikiri kuwa Quran Iko poa, basi nenda ukajionee na kusikia jinsi Quran ilivyokuwa na mikanganyiko kibao. Uchambuzi huo utafanywa na Mwl.Francis Ndacha ktk Mdahalo wake na Dr. SULE tarehe 16 na 17 December 2023 pale ukumbi wa PTA SABA SABA DAR ES SALAAM

View: https://www.youtube.com/live/MjV6HoXEAIs?si=LA4NBzAi2a2F6QMn
 
Kweli kabisa, kuwa mfia dini ni kujiumiza akili tu maana utalazimika kukubaliana na Mambo mengine ambayo unaona wazi ni uongo. Mi nipo unguja kuna washkaji tupo nao kwenye kazi wanasema ukichana au kukojolea Quran unakuwa chizi, nikawaambia wanipe niikojolee hawajanipa hadi leo.
Vitabu vyote viliandikwa ku control jamii zao kwa kutumia vitisho.

Hizo quran zinachanwa kibao, biblia ndio usiseme.
Ila utofauti ni wakristo huwa hawa react kama waislamu
 
jibu la kwamba alikuja kufanya nini,rejea maana ya neno Immanuel,yaani Mungu pamoja nasi.
lengo la ujio wake ni kuja kuufunulia ulimwengu,Mungu ni nini,ana hulka na haiba gani.
ndio maana hata,sheria za sabato ni kama alikuja kuzifafanua na kuwaelewesha zaidi watu,ili wajue Mungu sio mgumu wa sheria namna hiyo,ila ni wa upendo na ushawishi.

leo hii kwa upendo tulioonyeshwa na Mungu kupitia Yesu,tunaiona thamani yetu kwake,kuliko kuishia kusoma maagizo tu na kujichukulia ni kama mifugo mbele yake ambao tunatakiwa kutii kwa lazima anachotuagiza,lakini Yesu anakuja kutujuza kumbe Mungu anatushawishi.
Because you brought it up lets talk about it first...

Immanuel halina uhusiano wowote na Yesu mkuu..Ila walijaribu kulihusianisha na hapo ndo muda mwingi walifeli...

Isaya au Yeshayahu alikuwa akilitumia neno hilo akimaanisha kuwapoza moyo watu na mpaka leo linatumika na wayahudi kutiana Faraja na kuambizana kuwa Mungu yu pamoja na Taifa teule....

Na neno Yimanuel (Immanuel kwenye Biblia limeandikwa zaidi ya mara moja)
Isaya 8:8, isaya 8:10, isaya 7:14
Isaya 8:8
Yeshayahu 8:8

וְעָבָ֥ר אֶל־יְהוּדָ֖ה שָׁטָ֑ף יַֽעֲבֹ֧ר עַד־צַוָּאר֛ יַגִּ֖יעַ וּפָרַ֥שׂ כְּנָפָֽיו׃ עִמָּנוּאֵֽל

Inatamkwa hivi:-

Ve'avar el-Yehudah, shataf; ya'avor ad-tsavar, yagiya u'faras knafav. Yimmanuel."

Swahili
"naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli."
Tugeukie Isaya 8:10 (Yeshayahu 8:10)

עֻצּוֹת נָאוּ וְתֻפָּר, דַּבְּרוּ דְבָרִים וְלֹא יָקוּם, כִּי עִמָּנוּאֵל
Inatamkwa hivi:

"Utzot na'u vetupar, dabru devarim velo yakum, ki Yimmanuel."

tafsiri yake wameischezea kidogo jina Immanuel walifanikiwa kuliondoa...na wakaweka Mungu Pamoja nasi..

Tafsiri..

Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.

Sasa naamia kwenye Fungu lenu Pendwa Wakristo na Waislamu linalowapa uhalali wa kusema Bikra alichukua Mimba...na hapa nitajitahidi nikuchambulie vizuri..

Isaya 7:14 (Yeshayahu 7:14)

לָכֵן יִתֵּן אֲדֹנָי הוּא לָכֶם אוֹת הִנֵּה הָעַלְמָה הָרָה וְיֹלֶדֶת בֵּן וְקָרָאת שְׁמוֹ עִמָּנוּאֵל׃

Inatamkwa hivi..

"Laken yiten Adonai hu lakhem ot; hineh ha'alma harah ve'yoledet ben ve'karat shemo Yimmanuel."

Uchambuzi wa Fungu....

Sasa Maneno niliyoyawekea Alama nyekundu ndo kwenu yamewatatiza lakini fair enogh ni kwamba mmedanganywa kwenye neno Halima,AU Ha'alima kuwa linamaanisha Bikira...
Well enough nenda kwa Myahudi yoyote au Muebrania yeyeto au Mtu yoyote anayejua kiebrania muulize Halima ,Ha'alima inamaanisha nini..
Haina maana ya Bikra...Bikra kiebrania huitwa "בְתוּלָה" (betulah)...
na Halima humaanisha msichana au Binti mdogo au Kijakazi na halina uhusiano wowote na BIKIRA KWA KIEBRANIA...

NEno hilo hutumika mara nyingi sana wasichana wanapomaliza "Bat Mitzvah" Na halimaanishi Kuwa ni bikra ...

Na kuhusu Masihi kazi alizofanya hazikutabiriwa, zilizotabiriwa hakuzifanya kmhata kidogo...
So anajidesqulify kuwa masihi...
Labda wewe ulinganishe kazi alizotabiriwa kwenye agano la kale na jipya
 
Nasubiri akujibu mkuu.
 
Katika vitu ambavyo huwa nasisitiza humu ndani ni kuwa, muwe mnasoma haya mambo sio mnajiandikia andikia, yaani mtu anakuja kubisha juu ya kitu ambacho kila anachoandika kuhusu hicho kitu anakosea. Wengi mpo hivyo humu ndani, maana yake mnakuja humu kupotezea watu muda.

Sasa tunakuuliza au tunakuomba utuambie nani ameandika Qur'an na alisoma Biblia ipi ? Sababu kipindi Mtume yupo hapakuwa na Biblia.

Njoo utuonyeshe hapa wapi Kuna mawazo ya kibinadamu ? Utakuta hujawahi hata kuisoma Qur'an zaidi ya kuisikia tu.

Unauliza tena ameandika nani na wewe unasema ni mawazo ya binadamu na una kiri muandishi wa Qur'an alisoma Biblia ? Tuambie wewe Sasa.
Mkuu Kisai!
I apreciate Utetezi wako..
Ila unaposema Kipindi Mtume yupo hapakuwepo na Bible unatumia Kigezo gani?

Lets see...

Mtume anakadiriwa kuzaliwa 15 Rabiul awali..Mwaka wa 570......
Au 8th June 570 siku ya Ijumaa
Biblia agano la kale mpaka Malaki Lilikuwepo na walikuwa wakizisoma Moja moja waliita vyuo...Magombo na mengine..
Kwa mfano chuo cha Nabii isaya ...
Chuo cha Daniel..

Miaka ya 80 AD mpaka 200 AD vitabu vya agano jipya Viliandikwa..

Na vilikuwa Unified Na canonisation na Baadhi council mbalimbali kuanza na Council of Naecea mwka 325 AD, council of Rome mwaka 382, Council of synod au Regional Synod mwaka 393, council of Carthage Mwka 397...
Na hapa ndo vikapatikana vitabu mbalimbalu sura mbalimbali za kweny biblia zenye uhalali wa kusomwa....

So Mtume alipozaliwa alikuta Vitabu hivyo Vikisomwa kote Duniani kwenye ukristo...
Na fair enough ni kwamba hata makka kipindi cha mtume kulikuwa na Wakristo na wayahudi (Alkitab)...

Quran iliandikwa kutoka katika Qiraa mbalimbali na iliunganishwa na kuwa Qiraa moja katika khulafa ya Uthman mwaka 653 mpaka 656...
Na ndo inayotumika mpaka leo...

So kulikuwa na Mapadre na wasomi wa biblia wakati huo including Waraqa ibn Nawfal...
Aliyemwambia Muhamed kuwa Yeye ni choosen one...

Japo Mtume Alikuwa na mijadala mingi sana na Wayahudi na wakristo...
 
We jamaa inaonekana hata historia za dini hujui, yaani unasema kipindi cha mudi Biblia haikuwepo? Haupo serious wewe. Kwa hiyo Quran aliyoileta mudi imetangulia kuwepo kabla ya Biblia?
Huwa hatutaki stori, wewe leta ushahidi ya kuwa kipindi cha Mtume Biblia ilikuwepo.

Hili swali hakuna anaye weza kulijibu. Nasubiri majibu hapa.
 
Mkuu Kisai!
I apreciate Utetezi wako..
Ila unaposema Kipindi Mtume yupo hapakuwepo na Bible unatumia Kigezo gani?

Lets see...

Mtume anakadiriwa kuzaliwa 15 Rabiul awali..Mwaka wa 570......
Au 8th June 570 siku ya Ijumaa
Biblia agano la kale mpaka Malaki Lilikuwepo na walikuwa wakizisoma Moja moja waliita vyuo...Magombo na mengine..
Kwa mfano chuo cha Nabii isaya ...
Chuo cha Daniel..

Miaka ya 80 AD mpaka 200 AD vitabu vya agano jipya Viliandikwa..

Na vilikuwa Unified Na canonisation na Baadhi council mbalimbali kuanza na Council of Naecea mwka 325 AD, council of Rome mwaka 382, Council of synod au Regional Synod mwaka 393, council of Carthage Mwka 397...
Na hapa ndo vikapatikana vitabu mbalimbalu sura mbalimbali za kweny biblia zenye uhalali wa kusomwa....

So Mtume alipozaliwa alikuta Vitabu hivyo Vikisomwa kote Duniani kwenye ukristo...
Na fair enough ni kwamba hata makka kipindi cha mtume kulikuwa na Wakristo na wayahudi (Alkitab)...

Quran iliandikwa kutoka katika Qiraa mbalimbali na iliunganishwa na kuwa Qiraa moja katika khulafa ya Uthman mwaka 653 mpaka 656...
Na ndo inayotumika mpaka leo...

So kulikuwa na Mapadre na wasomi wa biblia wakati huo including Waraqa ibn Nawfal...
Aliyemwambia Muhamed kuwa Yeye ni choosen one...

Japo Mtume Alikuwa na mijadala mingi sana na Wayahudi na wakristo...
Swali langu ni Biblia hii mnayoitumia, ila ukisoma Historia mabaki ya vitabu vya kale yalikuwepo, kama Taurati ilikuwa pweke.

Nataka ushahidi wa hii Biblia kwamba ilikuwepo kipindi cha Mtume.

Qur'aan ya mwisho iliandikwa ikajumuisha viraa vyote kumi, baada ya shauri toka kwa swahaba Hudhaifa. Kwahiyo naona unaandika Historia kinyume nyume.
 
Mtume anakadiriwa kuzaliwa 15 Rabiul awali..Mwaka wa 570......
Au 8th June 570 siku ya Ijumaa
Biblia agano la kale mpaka Malaki Lilikuwepo na walikuwa wakizisoma Moja moja waliita vyuo...Magombo na mengine..
Kwa mfano chuo cha Nabii isaya ...
Chuo cha Daniel..
Kingine vitabu hivyo unavyo viongelea vilikuwa bado vikijulikana kwa majina yake ya asili. Rejea katazi la Mtume kwa swahaba Umar kama sikosei au Abuu Bakr, alipokuw ameshika kipande Cha Taurati. Hoja yangu ya msingi, nataka ulete ushahidi ya kuwa Biblia ilikuwepo kipindi cha Mtume, nikisema Biblia najua unanielewa vizuri.

Hii tarehe pia uliyo iandika si ya kweli, wewe habari za Uislamu huwa unazisoma toka kwenye vitabu gani ?

Maana naona kuna makosa kadhaa. Mtume alizaliwa tarehe 8, kama alivyo hakikisha Sheikh al-Albaaniy.
 
Because you brought it up lets talk about it first...

Immanuel halina uhusiano wowote na Yesu mkuu..Ila walijaribu kulihusianisha na hapo ndo muda mwingi walifeli...
nani na nani walijaribu kulihusianisha?
walifeli vibaya ukilinganisha na nani waliofanikiwa kuendana na wasifu wa jina husika?
Isaya au Yeshayahu alikuwa akilitumia neno hilo akimaanisha kuwapoza moyo watu na mpaka leo linatumika na wayahudi kutiana Faraja na kuambizana kuwa Mungu yu pamoja na Taifa teule....
lipi tatizo la hilo??kuna haki miliki ya jina hilo au maana ya jina husika kwa mtu yoyote?
Na neno Yimanuel (Immanuel kwenye Biblia limeandikwa zaidi ya mara moja)
Isaya 8:8, isaya 8:10, isaya 7:14
Isaya 8:8
Yeshayahu 8:8
hakuna sehem nimeandika kwamba limeandikwa mara moja.
וְעָבָ֥ר אֶל־יְהוּדָ֖ה שָׁטָ֑ף יַֽעֲבֹ֧ר עַד־צַוָּאר֛ יַגִּ֖יעַ וּפָרַ֥שׂ כְּנָפָֽיו׃ עִמָּנוּאֵֽל

Inatamkwa hivi:-

Ve'avar el-Yehudah, shataf; ya'avor ad-tsavar, yagiya u'faras knafav. Yimmanuel."

Swahili
"naye atapita, atapita kwa kasi na kuingia Yuda; atafurika na kupita katikati, atafika hata shingoni; na kule kuyanyosha mabawa yake kutaujaza upana wa nchi yako, Ee Imanueli."
Tugeukie Isaya 8:10 (Yeshayahu 8:10)

עֻצּוֹת נָאוּ וְתֻפָּר, דַּבְּרוּ דְבָרִים וְלֹא יָקוּם, כִּי עִמָּנוּאֵל
Inatamkwa hivi:

"Utzot na'u vetupar, dabru devarim velo yakum, ki Yimmanuel."

tafsiri yake wameischezea kidogo jina Immanuel walifanikiwa kuliondoa...na wakaweka Mungu Pamoja nasi..
unatakiwa useme ni akina nani hao,unaowashutumu kila wakati.achana na stori za"unaambiwa"
Tafsiri..

Fanyeni shauri pamoja, nalo litabatilika; Semeni neno, lakini halitasimama; Kwa maana Mungu yu pamoja nasi.

Sasa naamia kwenye Fungu lenu Pendwa Wakristo na Waislamu linalowapa uhalali wa kusema Bikra alichukua Mimba...na hapa nitajitahidi nikuchambulie vizuri..

Isaya 7:14 (Yeshayahu 7:14)

לָכֵן יִתֵּן אֲדֹנָי הוּא לָכֶם אוֹת הִנֵּה הָעַלְמָה הָרָה וְיֹלֶדֶת בֵּן וְקָרָאת שְׁמוֹ עִמָּנוּאֵל׃

Inatamkwa hivi..

"Laken yiten Adonai hu lakhem ot; hineh ha'alma harah ve'yoledet ben ve'karat shemo Yimmanuel."

Uchambuzi wa Fungu....

Sasa Maneno niliyoyawekea Alama nyekundu ndo kwenu yamewatatiza lakini fair enogh ni kwamba mmedanganywa kwenye neno Halima,AU Ha'alima kuwa linamaanisha Bikira...
Well enough nenda kwa Myahudi yoyote au Muebrania yeyeto au Mtu yoyote anayejua kiebrania muulize Halima ,Ha'alima inamaanisha nini..
Haina maana ya Bikra...Bikra kiebrania huitwa "בְתוּלָה" (betulah)...
na Halima humaanisha msichana au Binti mdogo au Kijakazi na halina uhusiano wowote na BIKIRA KWA KIEBRANIA...

NEno hilo hutumika mara nyingi sana wasichana wanapomaliza "Bat Mitzvah" Na halimaanishi Kuwa ni bikra ...
kwa maana moja ama nyingine hukubaliani kabisa na ubikira wa maria,kwa kupitia maandiko haya haya ambayo unadai ni ya kutunga tu.

embu elezea uma bikra ya malia iliondolewa lini na nani alikuwa mhusika wa zoezi hilo.

Na kuhusu Masihi kazi alizofanya hazikutabiriwa, zilizotabiriwa hakuzifanya kmhata kidogo...
So anajidesqulify kuwa masihi...
Labda wewe ulinganishe kazi alizotabiriwa kwenye agano la kale na jipya
wayahudi ambao hata hivyo nao sio halisi bado wanamsubiri masihi wao mpaka leo.
sio tatizo maana pia wana Mungu wao wa kwenye mfuko wa shati,wanayedhani anawapenda wao peke yao.
 
Swali langu ni Biblia hii mnayoitumia, ila ukisoma Historia mabaki ya vitabu vya kale yalikuwepo, kama Taurati ilikuwa pweke.

Nataka ushahidi wa hii Biblia kwamba ilikuwepo kipindi cha Mtume.

Qur'aan ya mwisho iliandikwa ikajumuisha viraa vyote kumi, baada ya shauri toka kwa swahaba Hudhaifa. Kwahiyo naona unaandika Historia kinyume nyume.
Nimekupa ushahidi mkuu Au unataka ushahidi gani?
Nimekupa ushahidi wa Kihistoria...Kuhusu Vikao vya kuipanga Biblia katika Mtiriko ilivyo leo...

Na vikao hivyo ndo vilizuka kupatikana Manuscript za biblia mwaka 300-600....

Sasa nifatilie haoa chini hizi ndo manuscript za zaman sana kuliko zote ....

Mpaka sasa kuna Manuscript za Miaka ya 300 mpaka 600 AD za Biblia..
KUNA...
Codex Sinaiticus hii Ni 4th century Manuscript (Ni ya mwaka 301-400)
Codex Vaticanus hii pia ni ya 4th Century...
Codex Alexandrinus hii ni 5th centrury
Codex Ephraemi Rescriptus: This 5th-century manuscript

Hizo ni mfano tu zipo za Zamani zaidi ya hizoo..
Na Baadhi zipo mpaka leo unaweza ukaenda Museum na utazikuta..

Sasa Narudi kwenye Viraa...

Mkuu Uthumani ibn Affan khalifa wa tatu ndiye aliye amua kuandika Quran kutoka katika vyanzo mbalimbali na aliynda kamati ya watu wanne Wenye Akili na waliohifadhi Quran katika Umma wote..

Kamati hiyo haikuwa na Hudhaifa peke yake..
Alikuwepo Zayd Ibn Thabit,ubay Ibn Ka'b na Abdallah Ibn Masudi..

Japo hawakumita Ally Ibn abi twalib wakati yeye Ndio Mtume alisema ndiye mlango wa elimu....

Mkuu
اتق الله أمام الناس ولا تكذب

Maana ulichosema hakina Uhalisia wowote..
Qiraa zilizokuwa zinafahamika Ni 7 wewe Kumi umezitoa wapi?

Qiraa hizo ni kama zifuatavyo..
  • Qiraa ya Hafs
  • Qiraa ya Warsh
  • Qiraa ya Nafi'
  • Qiraa ya Qalun
  • Qiraa ya al-Duri
  • Qiraa ya al-Kisa'i
  • Qiraa ya al-Susi
Lakini Qiraa Iliyopita na kuwa Standard Quranic Version ambayo tunayo mpake leo ni Qiraa ya Hafs..

Historia imeandikwa vizuri kabisa..
Na hicho ndo kisa cha Watu kumvamia Uthman na Kumuua..

Na ndo Sababu ya Ally kuanzisha vita na Muawiya Japo Bi Aisha naye aliingilia (Vita ya Jamal)..
Japo unawza ukaambiwa katika historia ilikuwa ni vita ya Kisiasa ila naku Assure ilikuwa na kidini zaidi..
 
nani na nani walijaribu kulihusianisha?
walifeli vibaya ukilinganisha na nani waliofanikiwa kuendana na wasifu wa jina husika?
Tatizo mkuu unasahau mapema Sana..
Sio wewe uliyeniambia jina la Emanuel ukiquote Isaya 7:14...😅😅
unatakiwa useme ni akina nani hao,unaowashutumu kila wakati.achana na stori za"unaambiwa"
Obvious ni wakristo wote na walijaribu Kuiweka Story ya Isaya mpaka kwa Mathayo..
Kitu ambayo nakiitaga the fail prophecy..
Ukitaka nikueleweshe nitakuelewesha zaidi..
kwa maana moja ama nyingine hukubaliani kabisa na ubikira wa maria,kwa kupitia maandiko haya haya ambayo unadai ni ya kutunga tu.

embu elezea uma bikra ya malia iliondolewa lini na nani alikuwa mhusika wa zoezi hilo.
kwanza kabisa mkuu Ni Maria sio Malia..
Pili hakuna Mahali nimesema hakuwa Bikra Ila Focusing ya Kuhusisha Bikra Yake na Maandiko Ya Isya its Manipulation of the text..
Kwa sababu haikuandikwa hivyo...

So yeye anaweza akawa bikra ia kuhusisha na Isaya 7:14 na kubadili Neno Ha'alima kusema ni bikra ili liendane na imani yao hilo ndo kosa..

wayahudi ambao hata hivyo nao sio halisi bado wanamsubiri masihi wao mpaka leo.
sio tatizo maana pia wana Mungu wao wa kwenye mfuko wa shati,wanayedhani anawapenda wao peke yao.
Hakuna aliye Mwema kati yenu Wote wayahudi,Wakristo mnaoamini Utatu, na waislamu..
Wote mko sawa tu baba yenu mmoja 😅😅
 
Naku uliza hivi 👇

Allah huyo Hakujua kwamba duniani kuna watu wa lugha mbalimbali ashushe Quran hiyo kwa watu wote duniani wa lugha zote?

Kwani Duniani lugha ni kiarabu tu?

Allah huyo, Hakujua kwamba kuna wajerumani, waingereza, waswahili, wafaransa, wafilipino, wahindi n.k

Yani Allah huyo Aumbe watu wa lugha tofauti tofauti kisha ashushe neno lake kwa lugha moja tu?

Hivi huyo Allah ana jielewa kweli?
Majibu yako yote yapo kwenye hii video. Usisumbue watu kwa ufinyu wako wa fikra
 
Attachments

  • 1688626173366.mp4
    7.7 MB
Back
Top Bottom