Kipindi nimeamaliza fom4 mzee aliniachia ninsaidie kusimamia gest yake , siku moja wekeend jumapil majira ya saa sita usiku akaja jamaa anataka room yuko na manzi,nikampa room moja iliyokuwa imebaki, nikafunga zangu mlango wa upande wa gest niakahamia upande wa pili kiangalia video,ilikuwa nimebak na jamaammoja anaitwa Bonge tunacheki mieleka, basi ndani ya nusu saa tukasikia kelele upande wa gest,ikabidi nitoke nikaangalie in kuna nini, kufika nikakuta jamaa niliyempa chumba muda sio mrefu dem wake amepandisha mashetani na amekaa kwenye korido anaongea kimasai, kelele nyumba nzima,jamaa yangu bonge ikabidi amshike sikio aanze kumsomea dua, yale majini yakasema yanataka maziwa ya mtindi, muda hapo unaenda saa saba usiku, ilibidi tutoke na mshikaji tukaenda kwenye kiosk cha wapenba flan hivi tukaeagongea tukaomba watusaidie, tukachukua maziwa ya jelo ya mgando ya tanga fresh. tuliporud bonge akapiga tena dua demu akanyweshwa maziwa ya mtindi, akatulia,i akaanza kuongea kiswahili safi,na alikuwa mzigua, ila wakati alikuwa amepandisha alikuwa angea kimasai na kiswahil cha kimasai,baada ya hapo,jamaa aliondoka na mtu wake hata hawakulala tena