Wasalaam!
Kwenye haratakati za hapa na pale nilishawahi kukutana na Mikasa kadhaa ya lodge/gest nilizowahi kulala !
1.. Dsm,,, nilienda lodge moja nzuri tu yenye hadhi,, kufika reception mhudumu akanipatia chumba, nikasain na kulipa! Nikakumbuka Sina Kinga nikarudi kuuliza Kama wanauza,,, kalikuwa kadada hivi, Yan kalishangaa vile Kama nimeulizia kitu Cha ajabu Sana, akasema Hana nikarudi room, nikampigia mgeni wangu aje Nazo! Ajabu pale room ukutani kulikuwa na Sheria zao, mojawapo inasema mteja haruhusiwi kuingia au kutumia kilevi akiwa mle,,, mm nilikuwa na take away zangu nmeingia Nazo, kwa jeuri nilivyoondoka niliziacha chupa! Mpk leo najiuliza ile ni lodge au hostel ? Mmiliki Ni mchungaji ? Yule mhudumu alikuwa mtawa ? Ajabu Sana !
2..mahenge-ulanga, miaka flan kabla daraja la kilombero halijatengenezwa , nilipata safari ya huko , nilifika usiku Sana, (enzi za Moro best/alsaedy,,,now sijui Ni bus gani zinaenda huko), nikapanda boda inipeleke lodge/Gest, tulienda sehemu Kama mbili nafasi zimejaa, tunapata moja,, Bei ilikuwa 5000, dah kitanda Kama kaburi,, Yani Ni zege limetengenezwa godoro linawekwa juu unaambiwa karibu ! Nilikaa Kama siku 4, asbh nilihama kutafuta lodge nyingine !
3,, Babati,,, nilikuwa nasafiri, nikafika jion, sikuwa na uharaka wa kuunga safari,, nikaona nipumzike na kuyasoma mazingira,,, lodge moja hivi nilishukia, Yule mhudumu wakati ananisainisha, nikamtania kidogo,, ! Nikaenda room, nikaoga nikatoka kwenda kula na kupata kinywaji , wakati narudi kulala yule mhudumu wkt ananipa funguo, naona anacheka cheka, ! Aft 4/3 mins akaja kugonga anauliza mbona Niko alone ? Nikihitaji kampani nimuambie , nikajibu sAwa,,, ! Dem akijirahisisha Sana napoteza mzuka !
4,,shinyanga,, ! Mda mwingine shughuli zangu zinanilazimu kusafiri safiri hasa wilayani anghalabu,,,siku nimefika usiku kwa uchovu wa safari nikatafuta sehemu ya kupumzika, napewa room, nakuta ndoo mbili za zimejaa maji na kopo,,, !! Aloo, nakumbuka sikuoga, asbh nilinawa uso kwa maji nilokuwa nayo ya kunywa,,, nikaondoka zangu !!
Visa Ni vingi,,, nilishawahi kuibiwa bag Lina doc kadhaa, Ni ile unafika unalipa siku kadhaa, then unavyotoka asbh unamuachia mhudumu funguo ili afanye usafi,,, narudi nimeibiwa baadhi ya vitu,,, mhudumu ooh Kama uliingiza mwanamke akakuibia,,,na kwel sikua nimeingiza mwanamke,,, nilileta shida, hadi boss wake akaja, ananitisha ananipeleka police, Mara nasumbua wateja, nikamwambia tangulia nikukute huko, nakuapia hii nyumba utaigeuza Banda la kuku,,, mikwara kibao, akaanza kushuka, tukayajenga kiume,,, nikatumiwa doc nyingine nikaenda kuziprint,,,!