Binafsi naheshimu Sana kazi yoyote halali inayomuingizia mtu kipato !
From no where mtu anakuja anamdharau boda boda ? Kuna watu wananyonga Tai kila siku mahofisini huko take home ni 450,000 kwa mwezi, wanaishi kwa mawazo wananuka madeni !!
Mimi nachoamini Ni nidhamu ya hela na malengo,,,, usijaribu kutumia ziadi ya kipato chako, mfano kwa siku unaingiza 30k alafu matumizi yako yanazidi hapo lazima ukwame!
Kuna wakurugenzi wanalipwa milions na kujikadiria posho lakini nao wanalalamika hela haiwatoshi ! Hao boda tunaowadharau wapo waliojenga, na wanaendesha families zao pia kusomesha kwa hicho hicho kipato tunachokidharau,,, !
Kuna jamaa yangu mmoja anapark maeneo ya sokoni, huwa wastani kila siku analaza 15k-25k(InAtegemea na siku),,, hapo familia imekula na mafuta kaweka,,, ! Ila hio boda ni yake ,,, anarelax hana presha ya kazi Wala sijui madeni , anaishi kwa Aman na familia yake,,,, !