Hamna hoteli ya maana pale mjini. Siku moja nimetoka mji wa kitalii Arusha tukaenda Musoma kikazi. Tukampigia jamaa yetu wa hapo Musoma atupe jina la hoteli nzuri akatupa (ingawa sikumbuki jina) Tulipofika tukashuka na mabegi yetu tukiwa na uhakika wa hoteli tuliyopewa na mwenyeji wetu. Tukaombwa tuoneshwe vyumba ili kila mtu achague, kuingia chumba cha kwanza, cha pili nikarudi nikatoka nje na begi langu dereva akanifata ananiambia vipi mbona umetoka nikwamwambia siwezi kulala hoteli ya hovyo kiasi hiki, nikamwambie twende tukazunguke huko mitaani tutafute hoteli ya maana (tena nilimuambia mbele ya yule mtu wa reception) Tukawasha gari tukaondoka, tukazunguka sana, sana, tukazunguka vichochoro vyote hoteli ni za hovyo sana hapo Musoma mpaka giza linaingia nikamwambia dereva ile hoteli tuliacha mwanzo ndio ina unafuu, hizi hazifai kabisa. Ikabidi turudi pale pa mwanzo kwa aibu jinsi nilivyotoa maneno ya dharau mwanzo mimi nikajificha kwenye gari dereva akashuka na begi langu akajifanya ni yeye anachukua hapo (akidanganya mimi ameshaniacha kwenye hoteli nyingine kwa hiyo ni yeye amerudi hapo). Akapewa kile chumba nilikataa akaweka begi tukaingia mtaani huko kula bata usiku saa nne nikarudi nikaingia kulala hata hawakunikumbuka. Pachafu sana.