MKASA WA KWANZA - Sehemu ya 9.
Inaendelea.............
Kiukweli hatukuelewa kinachomfanya acheke ni kitu gani!,akaanza kusema "mbona mnahangaika sana wakati haya mambo ni madogo sana?,sikuwa na sababu ya mimi kuja huku lakini hakijaharibika kitu!".
Basi wakati huo mimi nkiwa nimelala kitandani chumbani kwangu,huyo mganga alifanya mambo yake na alipomaliza kufanya mbwembwe zake alisema humo ndani bado kuna mali za dada Ashura,ukiondoa hiyo mali yake lakini pia akatuambia kuna mali ambazo ziko kama nguo ambazo si zetu inapaswa zikachomwe moto,kumbe zile Pajama tulizonunua siku ile kwa ajili ya ndugu zake kuja zilikuwa tayari zina nembo yake,hivyo zilikuwa mali ya Ashura!.Yule Mganga aliamlisha zile nguo kama zipo zichomwe moto saa hiyohiyo,Kila mtu alitoa nguo zake,kwakuwa mimi sikuweza kuamka pale kitandani kwa wakati huo,dada yangu yule l niliyemfuata alifungua kabati akazitoa, Yule mganga na baba walielekea nje kwa ajili ya kuzichoma moto.
Baada ya lile zoezi mganga alisema anasubiri ikifika usiku wa saa 6 kuna dawa ataifanya ili ile mali iliyopo chumbani kule alipokuwa akilala Ashura iwe rahisi kuichukua,kwani bila hiyo dawa itakuwa ni vigumu kuitoa hiyo mali!,Mzee alimuuliza hiyo mali niya aina gan?,Yule mganga akasema anaona kitu kama mkufu lakini aelewi upo maeneo gani,mpaka afanye hiyo dawa ndiyo ingejulikana vizuri.Huo mkufu nikaukumbuka maana Ashura alipokuja alipenda sana kuuvaa lakini kuna kipindi sikuwahi kumuona nao tena.Baba alikuwa akilalamika sana ya kwamba anajuta kumfahamu huyo dada Ashura,ndipo Yule mganga akamuuliza"ulimtoa wapi?".
Baba akasema "Nilipokuwa kikazi huko mkoani Singida,nilikutana na rafiki yangu wa siku nyingi ambaye tumesoma naye,huyo rafiki yangu alikuwa akielewana na mama yake na Ashura,sasa rafiki yangu akaniambia kwamba Ashura alikuwa akimsumbua sana amtafutie kazi,sasa tulipo onana na huyo rafiki yangu akaniambia kuna binti mmoja anahitaji kazi,akaendelea kuniambia nimchukue akanisaidie kazi kwakuwa sikuwa na binti wa kazi,basi nikakubali na ndiyo kuja na Ashura hapa nyumbani!".
Baba akaendelea kusema "laiti ningefahamu kama Ashura alikuwa na tabia hizi za ushirikina nisingemchukua maana ameiharibu sana familia yangu".
Sasa kumbe haya yote yaliyokuwa yanaendelea hapo nyumbani,muda huo dada Ashura yupo akiyashuhudia!,hakuna aliyefahamu,hata huyo aliyejiita mganga hakuwa akijua.Ilipofika usiku wa saa 6 yule mganga alianza kupiga manyanga pale sebuleni akiwa yeye na wazazi wangu,wengine wote waliambiwa waende vyumbani!.Kumbuka yule mzee alisema hawezi nitibu kwanza mpaka hiyo mali iliyoko chumbani ipatikane na itolewe!,lakini alisistiza kwamba ile ilikuwa kazi ndogo sana na haikuwa na ugumu!.Mzee akaanza kufanya mambo huko sebuleni,wengine huku vyumbani tunasikia tu anatamka maneno yasiyoeleweka,akiwa anaendelea kufanya mbwembwe zake za uganga,ghafla akaanza kusema"Nakufaaaa........nakufaaaa......nakufaaa".
Ilibidi hata waliyokuwa pale sebuleni wakimbie kuelekea chumbani,mimi nikiwa chumbani nilisikia tu vishindo vya miguu ya watu wakikimbia,kumbe alikuwa mama na baba wakitoka nduki!,kiukweli sikufahamu ni nini lakini nilijua tu tayari yalikuwa yamewafika!,nikawa nacheka lakini kwa maumivu maana mgongo ulikuwa ukiuma sana.Kiukweli nadhani baada ya lile tukio siku ile bafuni nilishajikatia tamaa na nikasema liwalo na liwe,hivyo sikuwa nikiogopa tena!.Nilianza kusikia sauti ya kike pale sebuleni ikisema "Mnakimbia nini?,nyie si majasiri?,mbona mnakimbia?".
Ile sautu ikasisitiza ya kwamba "nawaomba mje hapa sebuleni mara moja!".
Nadhani ile hali iliwapatia wazazi wangu shida ila ilibidi watoke waende hawakuwa na namna!,Baada ya kurudi sebuleni nilisikia ile sauti ikisema "Huyu kaja hapa kuwadanganya na nyie mnadanganyika si ndiyo?,hakuna anayeniweza kwa taarifa yenu,labda niwaulize aliyewapa mamlaka ya kuchoma nguo zangu ni nani?".
Ile sauti niliyoisikia ikawa inasema "hii nyumba hapa ni kwangu,hakuna wa kunitoa hapa wala kunifukuza hapa, haya yote yanawapata kwasababu mmeanza kuwa wakaidi,sasa adhabu yenu ataibeba huyu mjinga,tangu mchana nipo hapa nawaona tu mnavyohangaika"
Yaani adhabu iliyokuwa itupate pale ndani ilibidi ibebwe na yule mganga,dada zangu nao wakiwa huko vyumbani walikuwa kimya wakisikiliza sauti toka sebuleni!,Ndugu zangu kama huwajawahi kukutwa usiombe yakukute maana inaweza onekana kama mchezo wa kuigiza lakini ni ukweli na hakika,namshukuru Mungu siku hizi mimi namtumikia Mungu hivyo mambo ya kishetani tena kama hayo huwa yananipita kushoto maana sina muhuri wa Ibilisi.Basi baada ya kuwa ameongea kwa msisitizo alianza kutamka pale laana.
Akawa anasema "Wewe mzee kwa kuwa nilikuheshimu na haya ndiyo uliyoyafanya ukiwa na dhumuni la kutaka kuniua adhabu yako haiko mbali".
Mzee wangu nilisikia akijitetea kwamba "haya yote nayafanya kwasababu ya mwanangu anaumwa"
Ile sauti ikamjibu ikasema "huyo anaumwa na hamuwezi kumponya na mpaka nipende mimi,hicho kilichomlaza hapo kitandani ni kiherehere chake mwenyewe".
Alipomaliza na baba akahamia kwa mama akaanza kusema "Na wewe nimekuwa nikikuonya lakini hukunisikia,kwanza ulinitelekeza njiani,ulidhani sitorudi,haya sasa nipo kwako niue".
Muda ulizidi kuyoyoma na ndipo sauti toka sebuleni niliskia ikisema " Wewe mjinga chukua kila kilicho cha kwako na unifuate".
Baada ya hapo kulitokea ukimya wa ajabu,ndipo baba aliwaita mama mdogo na dada zangu waende sebuleni,ndipo aliwaambia huyo aliyekuwa akiongea alikuwa ni Ashura,baba akawaambia ya kwamba waache kujihusisha na mambo hayo na yeye angejua la kufanya!.
Yule mganga alimfuata Ashura na mizigo yake aliyokuja nayo, haikujulikana alipelekwa wapi maana waliondoka hapo ndani huku mageti yakiwa yamefungwa na hakuna aliyefahamu nje walitokaje,ilikuwa kama sinema lakini ilikuwa halisi kabisa.Basi tulikaa na ile hali hapo nyumbani huku mimi mgongo ukiwa unanisumbua,sikuweza kutoka kitandani ila fahamu zilirejea na nilikuwa naelewa sasa lipi ni lipi ila kuamka kitandani ndiyo ilikuwa shughuli.Baada ya siku tatu baba aliaga akasema kuna sehemu anaenda na atarudi kesho au kesho kutwa na hakutaka kusema anaelekea wapi!.
Itaendelea......................