Saint Anne
JF-Expert Member
- Aug 19, 2018
- 76,039
- 230,142
Watu na macrush wetu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Hahahah watu na macrush wenu
Mbona story zipo nzuri tatizo unapata notification za tag
Halafu uko kwingine kuna arosto sana utazivumilia
Nimeshakutag kama tatuWatu na macrush wetu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wametukatili, ilikuwa leo jioni tuwataje hao macrush.. ndiyo basi tena[emoji134]
Nitag,nitaona
Mimi hapa ni mgumu mno kuikubali story na kuisoma hadi mwisho.
Yaani hadi stori inivutie basi iwe imeenda shule sana.
Nipo hapa kusoma comments...Nimeshakutag kama tatu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mwenyewe nilikuwa nataka kumtaja wangu leo
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]Nipo hapa kusoma comments...
Story niishaanza kuisoma...[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
We soma tu
Haya matukio ya nyungu uliyafanya lini? Hii episode inanijulisha kuna baadhi ya episodes zingine sijasoma 😢MKASA WA PILI -Sehemu ya 46.
Inaendelea.............
Lile vumbi lilipotulia niliwaona wale wachawi wakiwa wameganda juu ya anga kama mwewe nikazidi kuwasogelea pale walipokuwa,wakati huo sikuwa na uwezo wa kupaa angani,kama nilivyosema hapo awali mimi sikuwa mchawi bali nilikuwa mshirikina!.
Sasa labda hapa nieleze vizuri,kuna tofauti kati ya kuwa mchawi na kuwa mshirikina!,mchawi anaweza kuwa navyo vyote viwili yaani ushirikina na uchawi ila mshirikina anaweza kuwa anafanya ushirikina na asiwe mchawi.
Kwa mfano- Kama wewe unatumia dawa ili mambo yako ya kimaisha au biashara yasonge mbele huo ni ushirikina lakini si Uchawi!.
Sasa kwa wakati huo mimi sikuwa mchawi ndiyo maana uwezo kama kupaa na kuning'inia angani sikuwa nao ila nilikuwa na uwezo mwingine tu mkubwa wa kuweza kupambana na wachawi wa kiwango cha kawaida ila wale mangunguli nilikuwa siwawezi,sasa utofauti wa mchawi wa kawaida na yule konkodi ulikuwa ni katika vitendo.Mchawi ngunguli mara nyingi hawakuwa na maneno mengi bali vitendo na vitendo vyao vilikuwa vinatisha,kwa wakati ule endapo ningekutana na ngunguli na ikajulikana nimevamia anga lake nilikuwa ninakwenda na maji,ila kwasababu hawa walikuwa wachawi wa kawaida tu ndiyo maana tulisumbuana.
Mpaka muda huo nilikuwa nina hasira sana yaani nilikuwa nimekasirika mpaka macho yalikuwa mekundu kama damu,ndipo sasa nilinyoosha ile pembe kuelekea juu walipokuwa wamening'inia wale wachawi,uwezo wa ile pembe iliwashusha chini kwa spidi kali kama umeme,kwakuwa walikuwa umbali mrefu kwenda juu,walipofika chini walivunjika viuno na hawakuweza tena kusimama,niliwasogelea na kuanza kuwasemesha pale "Nyie ndiyo mliyoniaharibia mipango yangu?".
Wakati huo nilikuwa ninaongea mpaka natetemeka kwa hasira maana nilifahamu kwamba,Malikia asingenielewa maana uwezo wote alikuwa amenipatia na aliniambia kabisa nisije nikarudia kosa nililokuwa nimelifanya Bungu,sasa kwasababu nilikuwa nimeikosa ile kafara niliyokuwa nimeitega pale barabarani kulikosababishwa na wale wachawi,nilidhamiria niwakarabati wale wachawi mpaka wanitambue.
Niliwauliza "Nyinyi ni akina nani na mnatoka wapi?".
Niliendelea kuwauliza kwa jazba niliyokuwa kuwa nayo,wale kina mama walikuwa watu wazima,kiumri nadhani walikuwa wakipelekana na marehemu mama yangu,sikuwa na huruma hata chembe wakati huo,niliendelea kuwahoji lakini walionekana kuwa na viburi,kwakuwa hawakuweza kunyanyuka niliona niwakaushe palepale kama nyama iliyokaushwa,kuna dawa niliwamwagia iwaozeshe ili hata kama kuna wenzao wangetaka kuja kuwachukua kwa ajili ya kuwala nyama washindwe kutokana na harufu kali!.
Hivi ndugu zangu umewahi kupita mahali iwe porini au kando ya barabara au mazingira yeyote yale ukakutana na harufu kali inayoumiza mapua na kila ukiangalia labda kuna mzoga wowote wa mnyama aliyekufa hayo maeneo humuoni?,bila shaka baadhi yetu hiyo hali tumewahi kukutana nayo,sasa ukikutana na hiyo hali ya harufu kali na ukitazama kila pembe ya eneo ulilosimama usione mzoga,tambua kabisa wachawi unakuta wamefanya kama nilichokuwa nimekifanya kwa wale wachawi.
Muda huo nilikuwa nina hasira sana na nilijiona kila mara nilikuwa nina bahati mbaya kwa Malikia,baada ya kuwaua wale wachawi na kuwaozesha,niliondoka zangu eneo la tukio kuelekea nyumbani,niliukamata mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na ile irizi kisha nikatamka ya kwamba inapaswa niwe nyumbani kwangu kwenye chumba cha siri,kilikuwa ni kitendo kufumba na kufumbua nikawa mle ndani ya nyumba,niliweka zana za kazi mahali ambapo huwa zinakaa siku zote,safari hii kibuyu kilirudi bila hata tone la damu,baada ya kuhakikisha kila kitu kimekaa mahali pake nikakifunga kile chumba nikaelekea zangu chumbani kupumzika.Nilipotoka huko Mulowo ilikuwa saa 10 jioni na kafara ya mwisho wa mwezi huo niliyokuwa nimeagizwa kuitekeleza ikawa imeshindikana,wakati huo mke wangu alikuwa hajarudi nyumbani.Sasa nilipokuwa nimepitiwa na usingizi,nilishitushwa na mlio wa simu,kuangalia vizuri kumbe alikuwa yule mwanamke ambaye ni mke wa bosi wake wa zamani dereva wangu aliyenifata pale nyumbani kwangu wakiwa na Scolastica kwa ajili ya kutaka mkopo.Baada ya kuopokea ile simu alianza kuniambia "Kumbe ulikuwa unatuzunguka ili utulale mimi na Scola?".
Muda huo alikuwa akiongea kwa jazba sana.
Nilimuuliza "Unasemaje mama mbona sikuelewi?".
Akaniambia "Kwanza acha kuniita mama,mimi si mama yako,pili ambacho huelewi ni nini,wewe siumetembea na Scola wewe!".
Akaendelea kuniambia "Mimi nilikwambia kabisa Scola anakupenda,wewe ukadai unanipenda mimi na nilitaka tu umuonyeshe kwamba una girlfriend ili asiendelee kukusumbua,kumbe nilipokupa namba yake wewe ulimtongoza na ukashiriki naye wakati unafahamu kabisa mimi na wewe ni wapenzi,sasa siku Scola akijua huoni kama utahatarisha urafiki wetu?".
Nilimwambia "Hawezi kujua kitu mama labda wewe tu uamue kumwambia".
Aliniambia "Mimi siwezi kumwambia ila naomba uhusiano wetu uwe mwisho,sitaki tena kuendelea na wewe".
Nilijaribu kumkumbushia ile hela niliyompatia ili kama anaweza kunirudishia basi anirudishie,hapo mwanzo sikuwaga kabisa na wazo na ile hela maana niliamua kuwapatia tu,nilitaka iwe kama chambo ya kuwapata wote wawili na kuwashughulikia,sikuwahi kuwaambia kama niliamua tu kuwapa.Sasa hii yote nilitumia tu kama fimbo kwa ile kauli yake ya kuanzia leo mimi na wewe iwe baasi!.
Aliniambia "Nilikuambia tangu mwanzo kwamba nipatie muda nitakurudishia pesa yako maana kila kitu nilikueleza".
Yule mwanamke baada ya kusikia nakumbushia ile hela alianza kuzungumza kama kapunguza jazba akidhani kwamba nitalegeza kamba.
Nilimuuliza "Utanilipa lini maana muda nao unazidi kusonga na mimi nina shida nayo".
Aliniambia kwa dharau "Kwani hata hivyo nisipokupa utanifanya nini,je ulikuwa na mashahidi walishuhudia umenipa pesa?,hata hivyo si umeshanitumia!,kwani ulinitumia bure?".
Nilimwambia "Lakini hayo hayakuwa makubaliano yetu".
Akaendelea kuniambia "Kwahiyo kama hayakuwa makubaliano mimi nifanyeje,hiyo hela mimi sina wewe fanya unalotaka".
Nilimwambia"Ok haina shida".
Toka nilipotoka Mbeya na kishindwa kutoa kafara sababu ya wale wachawi,yeye alikuwa ni kiumbe mwingine aliyepigilia msumari kwenye kidonda cha hasira nilizokuwa nazo wakati huo.
Nilikuwa najisema "Wewe utanitambua vizuri mimi ni nani mbwa wewe".
Niliapa ndani ya siku chache ningemshughulikia kikamilifu,sasa kwakuwa wakati huo hakuwa kwenye mipango yangu nilimuweka kwanza kiporo!.Ilipofika mida ya saa 12 jioni mke wangu alirudi akiwa na binti mmoja ambaye nilikuwa simfahamu.
Mke wangu aliniambia "Mume,huyu ni binti wa kazi nilimwambia mama mmoja pale kazini ambaye tunafanya naye kazi anitafutie binti wa kazi,uliponipigia simu muda ule ndiyo tulikuwa tunaelekea kwake kumchukua huyu binti".
Usiku baada ya kupata chakula nilimwambia mke wangu akamwonyeshe yule binti chumba atakachokuwa akiishi!.Sasa ilipofika usiku wa saa 6 nilisikia sauti ya Malikia ikiniita kule chumbani,nilipoamka nilimtazama mke kama amelala ili niweze kuelekea kule chumbani,bahati nzuri mke wangu alikuwa amelala kwa kuchoka ndipo niliamka kuelekea kule kwa Malikia.
Itaendelea......................
Swala la kukukubalia mkuu halitawezekana mimi ni babe wa mtu
Mwee[emoji134]Nimeshakutag kama tatu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mwenyewe nilikuwa nataka kumtaja wangu leo
Sawa mkuu kila la herimi mwenyewe nba mwingine anaitwa @Khamtwe
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Mwee[emoji134]
Njoo basi selfika tuendeleze kuwataja[emoji23][emoji23]
Inabidi tuendeleze kule[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kwahiyo selfika bado mnaendelea kuwataja sijajaj hiko kipande mda sana
Utasoma ukipata mda kidogo kidogoInabidi tuendeleze kule[emoji23]
Story zote ulizonitag nimeshindwa kuendelea nazo..labda nitajaribu tena kesho kusoma.
NdiyoUtasoma ukipata mda kidogo kidogo
[emoji536][emoji536][emoji536]UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA YANGU- Hiki ndicho kisa cha pili cha maisha yangu,hapo mwanzo nilisema nina visa viwili,cha kwanza nimeshakisimulia,hivyo hiki ni kisa cha pili.KARIBUNI MJIFUNZE.
MKASA WA PILI- Sehemu ya 1.
MWAKA 2012.
Baada ya kuwa nimemaliza shule ya sekondari nilirudi nyumbani Mwanza,baada ya mama kuwa ameuza ile nyumba ya Tarime ilibidi ajenge nyumba nyingine Mwanza,japo haikuwa kubwa kama ile ya Tarime lakini kwa kiasi fulani ilikuwa nzuri naya wastani!,nilirudi nyumbani nikawa nafundisha wanafunzi tuisheni ili angalau niweze kupata hela za kununua sabuni na mahitaji madogo madogo,sikuweza tena kumuomba mama pesa maana tayari nishakuwa mtu zima,pia kwa wakati huo hali ya mama haikuwa nzuri kifedha,kuna shuke moja ambayo haikuwa ya serikali huko maeneo ya buhongwa,waliniajiri kama mwalimu wa muda na wakawa wananilipa kutoka na vipindi ambavyo nilikuwa nikihudhuria,hivyo nilikuwa nikitoka hapo shuleni naelekea ilipokuwa kituo cha tuisheni kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi masomo ya ziada,nilikuwa nalipwa na wale wanafunzi Tsh elfu 3000 kila nilipokuwa nikimaliza topic.
Basi kuna siku katika pitapita zangu mtaani wakati natoka huko shuleni,kwa mbali kidogo nikamuona jamaa mmoja tuliyekuwa tumesoma wote shule ya msingi Turwa kule Tarime,kiukweli sikuweza kufahamu kama ndiye au nilimfananisha,jamaa alikuwa pembeni anaongea na simu,hivyo nilijaribu kusogea karibu nione kama ndiye!.Kweli!,baada ya kusogea karibu nikamwita jina lake,jamaa aliitika na aliponiona alinifanyia ishara kwamba nisubiri kwanza amalize kuongea na simu,basi jamaa alipomaliza kuongea na simu alifurahi sana kukutana na mimi,mimi pia nilifurahi sana maana jamaa alikuwa kabadilika sana na kanenepa ile kishenzi,watoto wa mjini wanasema "Shavu dodo",kiukweli jamaa alikuwa kanawili,nilivyomuona tu nilifahamu lazima alikuwa na maisha mazuri.
Jamaa aliniuliza "Aisee za miaka mingi?".
Nikamjibu "Nzuri".
Jamaa akaniambia "Hebu nikumbushe wewe ni nani na nilikuona wapi vile!".
Kimoyo moyo nilijisemea "Ina maana jamaa mara hii kanisahau au ndiyo mambo ya mjini?".
Basi ilibidi nimkumbushie jina langu na tulisoma wote Tarime,jamaa alicheka sana,ndipo tukaanza kukumbushiana matukio,vimbwanga na vitimbi vya shule!,tulipiga michapo sana na nikamueleza mimi niliendelea na shule na nikamwambia Tarime tulihama muda sana.Jamaa alinichukua tukasogea mbele kidogo kumbe alikuwa kapaki gari!.Tulipanda kwenye gari kuelekea maeneo ya Igoma ambako alikuwa kachukua hoteli huko.Wakati tukiwa kwenye gari alikuwa ananiambia kwamba yeye baada ya kumaliza shule ya msingi matokeo yake hayakuwa mazuri,hivyo ilibidi aende kutafuta maisha,akaniambia yupo huko mkoani Geita sehemu moja inaitwa Katoro,kajenga huko na maisha yake yapo huko,ila siku hiyo alikuwa kaja hapo Mwanza kwa ajili ya biashara zake nyingine.Huyu jamaa kipindi tunasoma alikuwa hajiwezi kimasomo(kilaza),kiukweli ningeshangaa sana kusikia aliendelea na Shule!.
Baada ya kufika hapo hotelini alipofikia mimi nilikaa nje yeye akaingia huko ndani,muhudumu alikuja kuniuliza natumia nini lakini nilisita kumwambia maana sikuwa na kitu, mtu ambaye ndiye mwenye pesa alikuwa kaingia ndani,hivyo nisingeweza kuagiza bila ruhusa ya mtoa pesa!,baada ya dakika kadhaa jamaa alikuja kwa mbwembwe huku akiniambia "Mwanangu agiza chochote uletewe ule".
Kabla sijamuita muhudumu jamaa alipaza sauti "Wewe muhudumu njoo umsikilize jamaa hapa".Mrume ndago niliagiza wali samaki pamoja na Soda.
Jamaa aliniuliza "Vipi mwanangu upigi mambo yetu?".
Nikamwambia "Hapana kaka sipigi".
Jamaa akaniambia "inaonekana kijana ushakuwa mlokole,yaani ukorofi na utundu wote ule wa shule ya msingi hupigi huang'unywa?".
Neno "Huang'unywa" alimaanisha pombe,ndizo lugha tulizokuwa tunazitumia kipindi hicho tukiwa wadogo.Basi stori za hapa na pale ziliendelea tukiendelea kukumbushana jamaa na marafiki tuliosoma nao,baada ya kumaliza kula ilibidi nimuulize jamaa alikuwa anapiga ishu gani!,maana alikuwa kanawili sana na ukiangalia mimi wakati huo nilikuwa nimechoka ile kishenzi.Jamaa aliniambia yeye anajihusisha na mambo ya madini ila akasema isingekuwa vyema tuongee pale hilo jambo ila aliniambia nijitahidi nitafute siku niende Geita,ndani ya siku chache ili nika-experience maisha ya kule namna yalivyo.Basi baada ya hapo jamaa akanipa elfu 30 ,mimi nikamuaga ila nilimwambia sina hata simu,aliniambia nisiwaze nijatahidi nitafute siku niende huko Geita kwani angesababisha hayo yote!,Baada ya maongezi nilimuaga jamaa ili kuondoka,alinipakia kwenye gari yake mpaka mabatini kisha nikachukua daladala za kuelekea Nyegezi nyumbani!.
Kiukweli ile elfu 30 niliona kama kanipa milioni,ukizingatia nilikuwa nimepigika na maisha ile sana!,Pia nilikuwa nawaza sana,inawezekanaje mtu niliyemzidi kila kitu kuanzia akili,elimu mpaka maisha enzi hizo leo anizidi maisha?,niliumia sana lakini sikuwa nala kufanya!,sasa pale nyumbani kuna hela nilikuwa nimesevu,hivyo nikachukua na hii jamaa ambayo alinipa nikajumlisha ikawa ya kutosha japo si haba!,kesho yake ilibidi niingie kwenye mitumba kusaka nguo za kushindia hapo mtaani.Nilipata suruali mbili nikanunua na makobazi pamoja na sweta.
Baada ya wiki nilianza kuwaza namna ya kwenda Geita ili nikaonane na jamaa uenda angenipataia kazi yoyote nifanye maana niliona kama nimechelewa sana katika maisha!,jamaa kipindi tupo hotelini kule Igoma, alinipa direction ya kwamba nikifika Katoro kuna jina alilokuwa analitumia huko lilikuwa maarufu sana,hivyo alinitajia hilo jina akasema endapo nitafika hapo nikimuuliza hata watoto wangenipeleka kwake!,lile jina lake la shule ya msingi aliniambia kule hakuna aliyekuwa analifahamu bali lilikuwa limebaki kwenye vyeti vya kuzaliwa tu.
Itaendelea......................
Mimi namuwazia dada yake mkubwa [emoji26][emoji26]Huu ni ukatili ukiwaua hao mabinti
Sawa mkuu kila la heri
Nimeshakutag kama tatu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mwenyewe nilikuwa nataka kumtaja wangu leo