Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Hahahah watu na macrush wenu
Mbona story zipo nzuri tatizo unapata notification za tag

Halafu uko kwingine kuna arosto sana utazivumilia
Watu na macrush wetu[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Wametukatili, ilikuwa leo jioni tuwataje hao macrush.. ndiyo basi tena[emoji134]

Nitag,nitaona

Mimi hapa ni mgumu mno kuikubali story na kuisoma hadi mwisho.
Yaani hadi stori inivutie basi iwe imeenda shule sana.
 
Nimeshakutag kama tatu
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Mwenyewe nilikuwa nataka kumtaja wangu leo
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 46.

Inaendelea.............

Lile vumbi lilipotulia niliwaona wale wachawi wakiwa wameganda juu ya anga kama mwewe nikazidi kuwasogelea pale walipokuwa,wakati huo sikuwa na uwezo wa kupaa angani,kama nilivyosema hapo awali mimi sikuwa mchawi bali nilikuwa mshirikina!.

Sasa labda hapa nieleze vizuri,kuna tofauti kati ya kuwa mchawi na kuwa mshirikina!,mchawi anaweza kuwa navyo vyote viwili yaani ushirikina na uchawi ila mshirikina anaweza kuwa anafanya ushirikina na asiwe mchawi.
Kwa mfano- Kama wewe unatumia dawa ili mambo yako ya kimaisha au biashara yasonge mbele huo ni ushirikina lakini si Uchawi!.

Sasa kwa wakati huo mimi sikuwa mchawi ndiyo maana uwezo kama kupaa na kuning'inia angani sikuwa nao ila nilikuwa na uwezo mwingine tu mkubwa wa kuweza kupambana na wachawi wa kiwango cha kawaida ila wale mangunguli nilikuwa siwawezi,sasa utofauti wa mchawi wa kawaida na yule konkodi ulikuwa ni katika vitendo.Mchawi ngunguli mara nyingi hawakuwa na maneno mengi bali vitendo na vitendo vyao vilikuwa vinatisha,kwa wakati ule endapo ningekutana na ngunguli na ikajulikana nimevamia anga lake nilikuwa ninakwenda na maji,ila kwasababu hawa walikuwa wachawi wa kawaida tu ndiyo maana tulisumbuana.

Mpaka muda huo nilikuwa nina hasira sana yaani nilikuwa nimekasirika mpaka macho yalikuwa mekundu kama damu,ndipo sasa nilinyoosha ile pembe kuelekea juu walipokuwa wamening'inia wale wachawi,uwezo wa ile pembe iliwashusha chini kwa spidi kali kama umeme,kwakuwa walikuwa umbali mrefu kwenda juu,walipofika chini walivunjika viuno na hawakuweza tena kusimama,niliwasogelea na kuanza kuwasemesha pale "Nyie ndiyo mliyoniaharibia mipango yangu?".

Wakati huo nilikuwa ninaongea mpaka natetemeka kwa hasira maana nilifahamu kwamba,Malikia asingenielewa maana uwezo wote alikuwa amenipatia na aliniambia kabisa nisije nikarudia kosa nililokuwa nimelifanya Bungu,sasa kwasababu nilikuwa nimeikosa ile kafara niliyokuwa nimeitega pale barabarani kulikosababishwa na wale wachawi,nilidhamiria niwakarabati wale wachawi mpaka wanitambue.

Niliwauliza "Nyinyi ni akina nani na mnatoka wapi?".

Niliendelea kuwauliza kwa jazba niliyokuwa kuwa nayo,wale kina mama walikuwa watu wazima,kiumri nadhani walikuwa wakipelekana na marehemu mama yangu,sikuwa na huruma hata chembe wakati huo,niliendelea kuwahoji lakini walionekana kuwa na viburi,kwakuwa hawakuweza kunyanyuka niliona niwakaushe palepale kama nyama iliyokaushwa,kuna dawa niliwamwagia iwaozeshe ili hata kama kuna wenzao wangetaka kuja kuwachukua kwa ajili ya kuwala nyama washindwe kutokana na harufu kali!.

Hivi ndugu zangu umewahi kupita mahali iwe porini au kando ya barabara au mazingira yeyote yale ukakutana na harufu kali inayoumiza mapua na kila ukiangalia labda kuna mzoga wowote wa mnyama aliyekufa hayo maeneo humuoni?,bila shaka baadhi yetu hiyo hali tumewahi kukutana nayo,sasa ukikutana na hiyo hali ya harufu kali na ukitazama kila pembe ya eneo ulilosimama usione mzoga,tambua kabisa wachawi unakuta wamefanya kama nilichokuwa nimekifanya kwa wale wachawi.

Muda huo nilikuwa nina hasira sana na nilijiona kila mara nilikuwa nina bahati mbaya kwa Malikia,baada ya kuwaua wale wachawi na kuwaozesha,niliondoka zangu eneo la tukio kuelekea nyumbani,niliukamata mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na ile irizi kisha nikatamka ya kwamba inapaswa niwe nyumbani kwangu kwenye chumba cha siri,kilikuwa ni kitendo kufumba na kufumbua nikawa mle ndani ya nyumba,niliweka zana za kazi mahali ambapo huwa zinakaa siku zote,safari hii kibuyu kilirudi bila hata tone la damu,baada ya kuhakikisha kila kitu kimekaa mahali pake nikakifunga kile chumba nikaelekea zangu chumbani kupumzika.Nilipotoka huko Mulowo ilikuwa saa 10 jioni na kafara ya mwisho wa mwezi huo niliyokuwa nimeagizwa kuitekeleza ikawa imeshindikana,wakati huo mke wangu alikuwa hajarudi nyumbani.Sasa nilipokuwa nimepitiwa na usingizi,nilishitushwa na mlio wa simu,kuangalia vizuri kumbe alikuwa yule mwanamke ambaye ni mke wa bosi wake wa zamani dereva wangu aliyenifata pale nyumbani kwangu wakiwa na Scolastica kwa ajili ya kutaka mkopo.Baada ya kuopokea ile simu alianza kuniambia "Kumbe ulikuwa unatuzunguka ili utulale mimi na Scola?".

Muda huo alikuwa akiongea kwa jazba sana.

Nilimuuliza "Unasemaje mama mbona sikuelewi?".

Akaniambia "Kwanza acha kuniita mama,mimi si mama yako,pili ambacho huelewi ni nini,wewe siumetembea na Scola wewe!".

Akaendelea kuniambia "Mimi nilikwambia kabisa Scola anakupenda,wewe ukadai unanipenda mimi na nilitaka tu umuonyeshe kwamba una girlfriend ili asiendelee kukusumbua,kumbe nilipokupa namba yake wewe ulimtongoza na ukashiriki naye wakati unafahamu kabisa mimi na wewe ni wapenzi,sasa siku Scola akijua huoni kama utahatarisha urafiki wetu?".

Nilimwambia "Hawezi kujua kitu mama labda wewe tu uamue kumwambia".

Aliniambia "Mimi siwezi kumwambia ila naomba uhusiano wetu uwe mwisho,sitaki tena kuendelea na wewe".

Nilijaribu kumkumbushia ile hela niliyompatia ili kama anaweza kunirudishia basi anirudishie,hapo mwanzo sikuwaga kabisa na wazo na ile hela maana niliamua kuwapatia tu,nilitaka iwe kama chambo ya kuwapata wote wawili na kuwashughulikia,sikuwahi kuwaambia kama niliamua tu kuwapa.Sasa hii yote nilitumia tu kama fimbo kwa ile kauli yake ya kuanzia leo mimi na wewe iwe baasi!.

Aliniambia "Nilikuambia tangu mwanzo kwamba nipatie muda nitakurudishia pesa yako maana kila kitu nilikueleza".

Yule mwanamke baada ya kusikia nakumbushia ile hela alianza kuzungumza kama kapunguza jazba akidhani kwamba nitalegeza kamba.

Nilimuuliza "Utanilipa lini maana muda nao unazidi kusonga na mimi nina shida nayo".

Aliniambia kwa dharau "Kwani hata hivyo nisipokupa utanifanya nini,je ulikuwa na mashahidi walishuhudia umenipa pesa?,hata hivyo si umeshanitumia!,kwani ulinitumia bure?".

Nilimwambia "Lakini hayo hayakuwa makubaliano yetu".

Akaendelea kuniambia "Kwahiyo kama hayakuwa makubaliano mimi nifanyeje,hiyo hela mimi sina wewe fanya unalotaka".

Nilimwambia"Ok haina shida".

Toka nilipotoka Mbeya na kishindwa kutoa kafara sababu ya wale wachawi,yeye alikuwa ni kiumbe mwingine aliyepigilia msumari kwenye kidonda cha hasira nilizokuwa nazo wakati huo.

Nilikuwa najisema "Wewe utanitambua vizuri mimi ni nani mbwa wewe".

Niliapa ndani ya siku chache ningemshughulikia kikamilifu,sasa kwakuwa wakati huo hakuwa kwenye mipango yangu nilimuweka kwanza kiporo!.Ilipofika mida ya saa 12 jioni mke wangu alirudi akiwa na binti mmoja ambaye nilikuwa simfahamu.

Mke wangu aliniambia "Mume,huyu ni binti wa kazi nilimwambia mama mmoja pale kazini ambaye tunafanya naye kazi anitafutie binti wa kazi,uliponipigia simu muda ule ndiyo tulikuwa tunaelekea kwake kumchukua huyu binti".

Usiku baada ya kupata chakula nilimwambia mke wangu akamwonyeshe yule binti chumba atakachokuwa akiishi!.Sasa ilipofika usiku wa saa 6 nilisikia sauti ya Malikia ikiniita kule chumbani,nilipoamka nilimtazama mke kama amelala ili niweze kuelekea kule chumbani,bahati nzuri mke wangu alikuwa amelala kwa kuchoka ndipo niliamka kuelekea kule kwa Malikia.

Itaendelea......................
 
Haya matukio ya nyungu uliyafanya lini? Hii episode inanijulisha kuna baadhi ya episodes zingine sijasoma 😢

Ngoja nikaanze mwanzo
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 47.

Inaendelea.............

Nilikifungua kile chumba taratibu na kuingia ndani,nilipomtazama Malikia safari hii alikuwa kainamisha sura ambayo sikuweza kuiona vizuri!,nikaanguka chini na kusujudu kama kawaida,kichwa chake kilikuwa kimefunikwa na nywele zake ndefu,aliponyanyua kichwa nilitaka kukimbia kwa namna nilivyomuona!,alikuwa akilia machozi ya damu!.Ninaposema machozi ya damu naamanisha ya kwamba alikuwa akilia na machozi yalikuwa yakitoka si kama haya ya kwetu ya kawaida bali yeye alikuwa akimwaga damu!,niliogopa sana nikawa nijikisemea kimoyomoyo kwamba "leo ndiyo mwisho wangu".

Malikia aliniuliza "Kwanini unanitesa mwanangu?".

Nilimjibu "Malikia tafadhali nisamehe sana,kuna mbwa nilikutana nao wakanizuia mimi kutoa ile kafara".

Akaniambia "Mbona nilikupatia uwezo wote mwanangu kwanini uliniangusha?".

Nikamwambia "Sikujua kama ingetokea hivyo Malikia ninaomba unisamehe na unipatie tena nafasi nyingine".

Nilimwambia Malikia huku nikiwa ninalia mle chumbani ili anionee huruma maana nilijua kwa hasira alizokuwa nazo mpaka kutoa machozi ya damu basi nisingebaki salama!.

Malikia aliniambia "Hili unapaswa ulipe kwa gharama kubwa zaidi".

Baada ya ukimya kupita, Malikia aliniambia "ninamtaka huyu mtu akawe mbadala wa ulichoshindwa kukifanya".

Nilimuuliza "Ni mtu gani huyo Malikia?".

Nilimuuliza kutaka kufahamu mtu ambaye angekuwa mbadala wa wale watu niliopaswa kuwatoa kafara kule Mulowo lakini nikashindwa.

Malikia aliniambia "Inua kichwa chako na utazame hapa ukutani".

Daah!,nilipoinua kichwa na kutazama pale ukutani alikuwa ni dada yangu mkubwa!,Kiukweli niliingiwa na hofu sana na kuanza kutetemeka,moyo ulianza kuniuma ila sikutaka kuonyesha mbele ya Malikia japo yeye alikuwa akifahamu.

Aliendelea kuniambia "Mwezi huu unaonza leo ukifika mwisho ninamtaka huyu mtu na utakaposhindwa kunipatia wewe ndiye utakuwa mbadala wake".

Malikia aliendelea kuniambia "Na kuanzia leo sitokupa tena pesa maana naona unashindwa kuyatekeleza ninayokuagiza,naona unatamani kurudi ulikotoka!".

Baada ya kuniambia hiyo kauli nilimsogelea Malikia huku nikitembea kwa magoti,nilipomkaribia niliangua kilio kikuu kwamba anihurumie na asinirudishe kwenye umasikini maana bado nilikuwa ninaupenda utajiri,nikamuomba asiniondolee fedha maana ningedharaulika sana na watu ambao tayari nishaanza kuijenga heshima yangu kwao.

Malikia aliniambia "Nimesikia kilio chako kijana wangu,nimekuhurumia jipe moyo utashinda".

Aliendelea kuniambia "Nimekupenda toka zamani kwa utii wako ila hakikisha unaendelea kunifurahisha zaidi,nakuomba huyu mtu ni mpate mwisho wa mwezi".

Nilimjibu "Sawa Malikia nimekuelewa nitafanya ulichoniambia?".

Baada ya hayo maelekezo ya Malikia,ghafla alitoweka mle chumbani,Malikia alipoondoka kiukweli nililia sana,sikuwa na namna ya kufanya nilipaswa kumtoa kafara dada yangu,wakati nilikuwa nikiupenda sana utajiri,pia sikutaka kabisa mimi kufa ila wenzangu nilikuwa napenda kuwaua!,nilifahamu fika nisipomtoa dada yangu kafara kama nilivyoambiwa na Malikia,basi ndiyo ungekuwa mwisho wa maisha yangu,wakati huo mimi sikutaka kabisa kufa.Basi nilikifunga kile chumba nikarudi chumbani kulala huku nikiwa ninawaza sana,nilimkuta mke wangu bado amelala hivyo hakuweza kuelewa chochote.

Asubuhi ya siku iliyofuata yule jamaa injinia niliyompa kazi ya kusimamia zile nyumba zangu alinipigia simu na akataka tukaonane kule site.

Jamaa aliniambia "Bosi nyumba zako ziko tayari nadhani waweza kuja kuzi kakagua".

Baada ya kuwa nimeziona zile Apartments,nilimwambia dereva wangu atafute dalali ambaye atakuwa akisimamia hizo nyumba,aliniambia kulikuwa na dalali mmoja ambaye alikuwa akimfahamu,alijaribu kutafuta namba yake kwa watu wake wa karibu na alipompata alimwambia aje mpaka pale site ili nielewane naye.Tulielewana na yule dalali ya kwamba yeye nitamlipa asilimia 10% kwa kila nyumba endapo mteja angepatikana!,hivyo ndivyo tulivyokubaliana,yule dalali tukaachana naye na alituhakikishia kwasababu nyumba zilikuwa nzuri basi zisingechukua muda mrefu kuwapata wateja!,nilimwambia dereva wangu tuelekee maeneo yale ya Kirumba ambapo siku zote tulikuwa tukienda kuenjoy.

Sasa wakati nikiwa pale niliona simu ya Scolastica ikiita nikaipokea!.

Aliniuliza "Mambo baby".

Nikamjibu "Poa mama,vipi?".

Aliniambia "Nikuulize kitu baby?.

Nilimjibu "Niulize mama".

Akaniambia "Wewe unatembea na ..........?,tafadhali niambie ukweli baby maana yeye kaniambia kila kitu".

Nilimwambia "Kakudanganya mama maana yeye siku moja alinipigia simu akaniambia ananipenda nitoke naye kimapenzi na nisikwambie wewe ila kwasababu nilikuwa nakupenda nilimkatalia".

Ilinibidi nimdanganye Scolastica maana nilifahamu fika yule mwendawazimu atakuwa alimwambia kila kitu.

Scolastica aliniambia "Sikia baby nikuambie kitu,mimi kiukweli ninavyoheshimiana na ..............sitoweza kuendelea na wewe maana tunaheshimiana sana na nimetoka naye mbali hivyo sitaki tugombane kwasababu ya mwanaume!".

Moja kwa moja niliwaza yawezekana ni janja yao wameongea ili wajitenge na mimi nisiweze kuwadai ile hela ambayo hata hivyo haikuwa kwenye akili yangu.Kiukweli Scolastica aliamsha tena hasira zangu zilizokuwa zimepotea kwa muda mfupi uliopita,niliwaza namna yule mpumbavu alivyokuwa kanijibu kwa nyodo na dharau siku si nyingi zilizokuwa zimepita nikaona kabisa tayari alikuwa ameshaharibu na kwa Scolastica tena.Sasa kwakuwa walikuwa wamejifanya wajanja niliapa kuwashughulikia muda mfupi ujao na nilisema lazima wote niwashikishe adabu kisawasawa.Sasa kumbe wakati Scolastica anaongea na mimi alikuwa yupo na huyo mwenzake maana muda mfupi baadae walimpigia simu dereva wangu nikiwa naye pale.

Nikamwambia dereva "Huyo mwendawazimu akikuuliza mwambie bosi yupo nyumbani".

Baada ya kumpigia simu dereva wangu,yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu alimuuliza dereva wangu"Vipi..........uko wapi?".

Dereva alimjibu "Nipo zangu mjini,vipi?".

Yule mwanamke alimuuliza "Haupo na huyo bosi wako mjinga mjinga?".

Dereva alimjibu "Hapana siko naye kwa sasa hapa".

Nilimfanyia dereva ishara ya kwamba awaache wafunguke kila kitu ili nielewe mchezo mzima waliyokuwa wameupanga.

Aliendelea kumwambia dereva kwamba "Yaani yule mjinga ile hela simrudishii ng'oo,anajifanya mtoto wa mjini wakati hajui sisi ndiyo tumezaliwa mjini".

Dereva wangu alitulia kimya akawa anamsikiliza anavyoongea kwa mbwembwe na nyodo bila kufahamu nilikuwa niko na dereva.

Aliendelea kusema "Na bahati nzuri nipo na Scola naye kampa makavu yake mpaka sura imemshuka shuu!".

Basi baada ya kuongea na dereva kwa kejeli za kutosha,nilimwambia dereva aachane nao kwani hiyo hela ni ndogo sana na mimi ilìkuwa hainiumizi akili,wakati huo nilikuwa nimejaa sana hasira na sikutaka dereva wangu atambue kitu chochote!.Basi tulipomaliza tulirudi nyumbani,nilivyokuwa nikiwaza yale maneno waliyoniambia wale viumbe nilikuwa nataka niwafuate muda huo huo lakini nilijisemea ngoja kwanza niwaache wafurahie maisha ila watanitambua mimi ni nani katika siku chache zilizokuwa zikifuatia.

Itaendelea...............
 
UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA YANGU- Hiki ndicho kisa cha pili cha maisha yangu,hapo mwanzo nilisema nina visa viwili,cha kwanza nimeshakisimulia,hivyo hiki ni kisa cha pili.KARIBUNI MJIFUNZE.

MKASA WA PILI- Sehemu ya 1.

MWAKA 2012.

Baada ya kuwa nimemaliza shule ya sekondari nilirudi nyumbani Mwanza,baada ya mama kuwa ameuza ile nyumba ya Tarime ilibidi ajenge nyumba nyingine Mwanza,japo haikuwa kubwa kama ile ya Tarime lakini kwa kiasi fulani ilikuwa nzuri naya wastani!,nilirudi nyumbani nikawa nafundisha wanafunzi tuisheni ili angalau niweze kupata hela za kununua sabuni na mahitaji madogo madogo,sikuweza tena kumuomba mama pesa maana tayari nishakuwa mtu zima,pia kwa wakati huo hali ya mama haikuwa nzuri kifedha,kuna shuke moja ambayo haikuwa ya serikali huko maeneo ya buhongwa,waliniajiri kama mwalimu wa muda na wakawa wananilipa kutoka na vipindi ambavyo nilikuwa nikihudhuria,hivyo nilikuwa nikitoka hapo shuleni naelekea ilipokuwa kituo cha tuisheni kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi masomo ya ziada,nilikuwa nalipwa na wale wanafunzi Tsh elfu 3000 kila nilipokuwa nikimaliza topic.

Basi kuna siku katika pitapita zangu mtaani wakati natoka huko shuleni,kwa mbali kidogo nikamuona jamaa mmoja tuliyekuwa tumesoma wote shule ya msingi Turwa kule Tarime,kiukweli sikuweza kufahamu kama ndiye au nilimfananisha,jamaa alikuwa pembeni anaongea na simu,hivyo nilijaribu kusogea karibu nione kama ndiye!.Kweli!,baada ya kusogea karibu nikamwita jina lake,jamaa aliitika na aliponiona alinifanyia ishara kwamba nisubiri kwanza amalize kuongea na simu,basi jamaa alipomaliza kuongea na simu alifurahi sana kukutana na mimi,mimi pia nilifurahi sana maana jamaa alikuwa kabadilika sana na kanenepa ile kishenzi,watoto wa mjini wanasema "Shavu dodo",kiukweli jamaa alikuwa kanawili,nilivyomuona tu nilifahamu lazima alikuwa na maisha mazuri.

Jamaa aliniuliza "Aisee za miaka mingi?".

Nikamjibu "Nzuri".

Jamaa akaniambia "Hebu nikumbushe wewe ni nani na nilikuona wapi vile!".

Kimoyo moyo nilijisemea "Ina maana jamaa mara hii kanisahau au ndiyo mambo ya mjini?".

Basi ilibidi nimkumbushie jina langu na tulisoma wote Tarime,jamaa alicheka sana,ndipo tukaanza kukumbushiana matukio,vimbwanga na vitimbi vya shule!,tulipiga michapo sana na nikamueleza mimi niliendelea na shule na nikamwambia Tarime tulihama muda sana.Jamaa alinichukua tukasogea mbele kidogo kumbe alikuwa kapaki gari!.Tulipanda kwenye gari kuelekea maeneo ya Igoma ambako alikuwa kachukua hoteli huko.Wakati tukiwa kwenye gari alikuwa ananiambia kwamba yeye baada ya kumaliza shule ya msingi matokeo yake hayakuwa mazuri,hivyo ilibidi aende kutafuta maisha,akaniambia yupo huko mkoani Geita sehemu moja inaitwa Katoro,kajenga huko na maisha yake yapo huko,ila siku hiyo alikuwa kaja hapo Mwanza kwa ajili ya biashara zake nyingine.Huyu jamaa kipindi tunasoma alikuwa hajiwezi kimasomo(kilaza),kiukweli ningeshangaa sana kusikia aliendelea na Shule!.

Baada ya kufika hapo hotelini alipofikia mimi nilikaa nje yeye akaingia huko ndani,muhudumu alikuja kuniuliza natumia nini lakini nilisita kumwambia maana sikuwa na kitu, mtu ambaye ndiye mwenye pesa alikuwa kaingia ndani,hivyo nisingeweza kuagiza bila ruhusa ya mtoa pesa!,baada ya dakika kadhaa jamaa alikuja kwa mbwembwe huku akiniambia "Mwanangu agiza chochote uletewe ule".

Kabla sijamuita muhudumu jamaa alipaza sauti "Wewe muhudumu njoo umsikilize jamaa hapa".Mrume ndago niliagiza wali samaki pamoja na Soda.

Jamaa aliniuliza "Vipi mwanangu upigi mambo yetu?".

Nikamwambia "Hapana kaka sipigi".

Jamaa akaniambia "inaonekana kijana ushakuwa mlokole,yaani ukorofi na utundu wote ule wa shule ya msingi hupigi huang'unywa?".

Neno "Huang'unywa" alimaanisha pombe,ndizo lugha tulizokuwa tunazitumia kipindi hicho tukiwa wadogo.Basi stori za hapa na pale ziliendelea tukiendelea kukumbushana jamaa na marafiki tuliosoma nao,baada ya kumaliza kula ilibidi nimuulize jamaa alikuwa anapiga ishu gani!,maana alikuwa kanawili sana na ukiangalia mimi wakati huo nilikuwa nimechoka ile kishenzi.Jamaa aliniambia yeye anajihusisha na mambo ya madini ila akasema isingekuwa vyema tuongee pale hilo jambo ila aliniambia nijitahidi nitafute siku niende Geita,ndani ya siku chache ili nika-experience maisha ya kule namna yalivyo.Basi baada ya hapo jamaa akanipa elfu 30 ,mimi nikamuaga ila nilimwambia sina hata simu,aliniambia nisiwaze nijatahidi nitafute siku niende huko Geita kwani angesababisha hayo yote!,Baada ya maongezi nilimuaga jamaa ili kuondoka,alinipakia kwenye gari yake mpaka mabatini kisha nikachukua daladala za kuelekea Nyegezi nyumbani!.

Kiukweli ile elfu 30 niliona kama kanipa milioni,ukizingatia nilikuwa nimepigika na maisha ile sana!,Pia nilikuwa nawaza sana,inawezekanaje mtu niliyemzidi kila kitu kuanzia akili,elimu mpaka maisha enzi hizo leo anizidi maisha?,niliumia sana lakini sikuwa nala kufanya!,sasa pale nyumbani kuna hela nilikuwa nimesevu,hivyo nikachukua na hii jamaa ambayo alinipa nikajumlisha ikawa ya kutosha japo si haba!,kesho yake ilibidi niingie kwenye mitumba kusaka nguo za kushindia hapo mtaani.Nilipata suruali mbili nikanunua na makobazi pamoja na sweta.

Baada ya wiki nilianza kuwaza namna ya kwenda Geita ili nikaonane na jamaa uenda angenipataia kazi yoyote nifanye maana niliona kama nimechelewa sana katika maisha!,jamaa kipindi tupo hotelini kule Igoma, alinipa direction ya kwamba nikifika Katoro kuna jina alilokuwa analitumia huko lilikuwa maarufu sana,hivyo alinitajia hilo jina akasema endapo nitafika hapo nikimuuliza hata watoto wangenipeleka kwake!,lile jina lake la shule ya msingi aliniambia kule hakuna aliyekuwa analifahamu bali lilikuwa limebaki kwenye vyeti vya kuzaliwa tu.

Itaendelea......................
[emoji536][emoji536][emoji536]
 
Back
Top Bottom