Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

It's time for reasoning, ngoja tuwashe taa kidogo!

Hii ni hoja rahisi sana ambayo mpaka leo sijapata mtu wa kuikosoa.

Ipo hivi,hakuna tofauti yoyote ile kati ya kisa cha kweli cha kichawi/ushirikina/maajabu(kama kimewahi kuwepo) na kisa cha kutunga(work of fiction) kinachohusu uchawi/ushirikina/maajabu

Hata kama katika kisa cha kutunga kumetajwa maeneo ya kweli ambayo wenyeji wamekili kuyafahamu
Filamu ya Titanic ime base katika tukio la kweli lakini sote tunajua Jack na Rose hawakua Real

Mwandishi yoyote makini anaweza Fanya extensive research ya maeneo mbalimbali,Lugha,na key people katika maeneo hayo kisha akaja na kisa cha kutunga ambacho kipo consistent na research aliyofanya

Point hapa ni hivi,ni vigumu kutofautisha kisa cha kweli cha kichawi/kishirikina/maajabu na kile kilichobuniwa

Hata kama una amini uchawi au imani za kishirikina ni mambo ya kweli bado ni vigumu kutofautisha kati ya kisa cha kweli na kile kilichotungwa unless upo tayari kuamini kila aina ya taka taka utakayosimuliwa na mgeni yoyote utakayekutana nae mtandaoni

Pia tukipiga mahesabu,probability ya simulizi hii kuwa ya tukio la kweli ni ndogo sana kuliko probability ya simulizi hii kuwa kisa cha kutunga

Kwa maneno mengine,kuna 99.9% kuwa kisa hiki ni cha kutunga kuliko 0.1% kuwa kisa hiki ni cha kweli.....

Kivipi,tukio moja tu katika kisa hiki,kama ni cha kweli kina uwezo wa ku "disprove" misingi yote ya Sayansi kwanzia kipindi cha Aristotle,Copernicus,Leibniz, Newton, Dirac,Einstein, Bohr,Gödel,Feyman,Hawking na wengine wengi

Mfano kama kweli mtu anaweza fumba macho na kufumbua(almost sekunde moja) akatoka Mwanza mpaka mbeya,hakuna Energy yoyote iliyotumika,na wala hakuonekana kuchoka
Then ni Obvious, Principle of conservation of Energy ambayo imekua msingi Wa sayansi kwa karne,na kutupa majibu sahihi mda wote ni ya "UONGO"

Kama kweli ziwa linaweza gawanyika,na ndani kukawa na mji mkubwa,Sayansi nzima kama tunavyoijua inakua ni "Takataka" kwasababu haiwezi tupa maelezo ya tukio hilo na matukio mengine yote ya kushangaza katika simulizi hii

Sasa kati ya maelezo haya mawili,yapi yanaweza kuwa sahihi?

1.Simulizi hii,ambayo ushahidi pekee tulio nao kuihusu,unatoka kwa msimulizi aliyetuletea simulizi hii na baadhi wanao support kuwepo kwa maeneo tajwa(means setting ya story ni ya kweli japo hii haiwezi count kama evidence) ni ya kweli,na Aristotle,Copernicus, Leibniz, Newton,Darwin,Einstein, Dirac,Bohr,Plank,Maxwell wote hawakua sahihi pamoja na scientific papers zote zilizowahi kuandikwa pamoja na tafiti zote za kisayansi zilizofanyika na zilizowahi kufanyika

Au
2.kisa hiki ni cha kutunga

Maelezo yapi yanaweza kuwa sahihi? 1 au 2?

Tuwe tunatumia akili zote kuhoji vitu,
The reason why nakua mgumu kuamini visa kama hivi ni jinsi gani haviweka "more details" haswa hapo kwenye matukio muhimu

Mfano,ni kwa jinsi gani alikua ananyonya damu za abiria kwenye kibuyu na kuwakausha kabisa,ili hali hakujawahi ripotiwa ajari yoyote ambayo maiti zote zilikutwa bila damu?

Huo ungo ulikua mkubwa kiasi gani kutosha watu watatu,uliundwa kwa material gani? Au ni zoom tu huu ungo wa kawaida?

Pia kwanini ungo?, hii imeshakuwa common trope kwenye simulizi za aina hii,

Achilia mbali characters waliokosa uhalisia kabisa kama "Mungu bonge mwenye sauti ya mtoto"
 
Eti achilia mbali "mungu bonge mwenye sauti ya mtoto"😂😂 bro sema umeelezea more scientifically kitu ambacho no opposite na hayo mambo ya magic ambayo yako against laws of physics.
 
Ila amini mkuu watu wanamiliki utajiri wa kichawi it means uchawi upo ninaushuhuda na huo utajiri wa kichawi place majini
 
WAPENDWA NAPENDA KU SHARE NANYI UCHAMBUZI WA MTUMISHI MMOJA JUU YA STORY HII 👇🏾👇🏾👇🏾

Jamani! Kuna vitu vingi moyo wangu unanishuhudia kuvisemea kutokana na ile mikasa!
Tuliisoma bila kujifunza au kufafanua

Kwanza kuanzia mkasa wa baba kuja na binti wa kazi hadi kifo chake!

Nilijifunza kuwa ktk kutafta wasaidizi wa nyumbani Mungu atuongoze siyo kupokea tu kutoka kwa mtu kisa tunafahamiana! Rafiki alileta majuto ktk familia ya jamaa

Lkn pia kuna Tabia ambayo Dada mkubwa alizuiliwa ni Tabia za maombi! Kumbe kwa njia ya maombi kulikuwa na mateso yanawapata na kusoma neno!
Leo hii kuna wapendwa wamepoteza ladha ya kusoma neno na hata maombi! "" IKO NGUVU KTK MAOMBI ""

Hatua ya familia ktk kutafta msaada!
Baba anaondoka kwenda kwa mgaga Utegi. Mimi huko ndiko maeneo ya kijijin kwetu na ndo sasa Wilayan kwetu.
Mganga hakuwa msaada KWA ile familia, lkn ikumbukwe yule mtu alimkosa mganga anaondoka kurud Dar kazin kwake ndo baadae akapata appointment mpya, na alipokwende this time HAKURUDI SALAMA! Japo nyumbani kwake alifika.

Yesu! Unapobisha hodi kwake, ni wakati huo huo ukizama huleta msaada wa kukutoa ktk dhiki! Lkn mgaga ilibidi asubiriwe! Hata hivyo mganga alipojileta kwenye ule mji Hakurudi kwake bali yule Dada aliondoka nae!
Mungu wetu halogeki wala wasingeondoka na Yesu bali wao wangeondoka!
Amen
 
Mkasa wa pili kuna mambo mengi mnooo ya kujifunza!👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾

Kuna mtu anaitwa "" RAFIKI " tuwe makini nao, ktk mkasa wa kwanza Rafiki alileta shida kwenye familia kwa kumkabidhi binti aliyesababisha mateso ktk ile familia na ni kama vile alikuwa Jini! Ktk mkasa wa pili pia tunamwona huyu Rafiki waliyesoma naye, alikuwa ni Jambazi jamaa aliamua kuondoka, lkn bado Rafiki mwingine akampeleka Kasulu Kigoma !!
"Tuwe makini na Marafiki"
Hasara! Hasara ya kwanza na nitataja zingine ni ile ya ADUI kuandaa mlango wa kumaliza pesa alizokusanya mgodini! Tsh 180,000/= zinayeyuka ktk kutafta shilingi 100 ya mwaka 1993 ktk vijiji mbali mbali ktk mkoa wa mara, Wawili hawa, jamaa na mtoto wa mamdogo wake, walitembea ndani ya mkoa wa Mara mwendo wenye mzunguko mfano na siyo uhalisia wa mwendo wa wana wa Israel jangwani! Wametoka Bunda kwenda kuitafta shilingi 100 Musoma vijiji, Wakakosa, akiba ya ikanunua tena Pombe, bila msaada, wakarudi Ikizu huko wakiwa wameishiwa, wakaikosa lkn wakaondoka na ramani Bwana aliwaandalia mfadhili wakanywa uji wakalala kesho yake ! Sh 100 ilipatikana Bunda walikotoka! Je! Kwanini hawakuipata mlemle?! Bila mzunguko?! Hii ni kwasabu ya Hasara iliyokuwa imeandaliwa mbele yao
Bado waliponea chupu chupu kutapeliwa au kufunguliwa shtaka la uongo!

UZUSHI: ADUI shetani anapenda kutumia uszushi kwa lengo la kutudak ktk mtego wake! Hili linathibitka pale jamaa alipoletewa maneno aiyoyaongea Shemeji yake juu ya Familia ya "Familia yenu ni Masikini, sijui kwanini kaka yangu alimwoa Dada yenu"!
Ujinga wa huyu jamaa, eti hii kauli ilimjaza sumu akaamua kutafta Utajiri ili tu aje amwoneshee kuwa sasa kapata! Hapa inachomoza roho ya kisasi na kweli alifaulu ktk visasi wakati Kisasi ni juu ya Bwana!

UAMINIFU na UTII: Nimejifunza kuwa hata huko kwenye ufalme wa Giza ili wafanikiwe ni sharti wayazingatie hivi vitu viwili!
Leo hii baadhi ya wapendwa wetu, Hatuna Utii na Uaminifu kwa Mungu wetu na hii imemfanya Mungu nae kubaki akitutizama aone mwisho wetu japo hachoki kuendelea kutusihi tubaki ktk UTII na Uaminifu lkn mwanadamu ni Mkaidi!
Nimeona kama vile kuna Rufaa ktk ulimwengu wa Giza, mganga wa kike Kasulu alitoa kinga ila Utajiri akampa Rufaaa tena kwa ujumbe maalumu wa kichawi kwenda kwa Mzee Nchibaronda! Mzee alifanya yake kwa siku kadhaa Naye akampa rufaa ya kwenda mbele zaidi ndani ya Ziwa Tanganyika, yamkini ni lango la Kuingia Kuzimuni! Hii ni mfano wa kumtoa mgonjwa hospitali ya WILAYA, kwenda Mkoa na baada hospitali ya Taifa!!


UTII niliouona ni kwa Nchibaronda porini alipoachwa akatokewa na sura ya binti mzuri akiwa akiwa anaoga akamwomba amsogelee !! Aliikumbuka sauti ya mzee! Ina maana kwa kutokutii asingeweza kukipata kilivhompeleka, Alitambua alichokifuata !! Wa Kristo tumeokolewa na mpango mkuu ni kuwa siku moja tukayaishi maisha ya raha na Bwana Yesu kwa Baba yake Mbinguni. Lkn tuwahubiri wenzetu waipokee injili ya Kristo Yesu kama tulivyoagizwa ktk Mathayo 28:19-20. Tukitambua Kusudi la kuokolewa, Hatutoacha kutii sauti ya ki Mungu!

Chini ya Ziwa kulikuweko na majaribu mengi lkn ni alishinda kutokana na alichokuwa anakipata!
Alipotoka Wapendwa nilijifunza kuwa kuna Wanadamu wanaishi bila shughuli yyte ya maana lkn wana vipato vya kushtusha jamii zetu! ONYO! Hatupashwi kushabikia Utajiri wa mtu! Wengine wana siri nzito sana ktk utaftaji wao! Siufurahii Umasikini, NINAUCHUKIA mnoo, lkn kama njia ndiyo hii ya watu baadhi ninaowafahamu, bora Mungu anipe uwezo wa kuihudumia familia yangu na jamii inayonizunguka na kwaajili yake Mungu mwenyewe yataosha!

Huyu ndg. Alianza kutoa Kafara za watu wengine siyo hata wa nyumbani kwao lkn mdogo mdogo Familia ilianza kuingia gharama kwa kuanza na kibinti cha Dada kilichokuwa kimetoka shule kikaumwa kichwa na damu kutoka puani kukimbizwa hospital ! Mwisho wake! Tatizo likaendelea kwa wengine lkn Shetani ameshaingiza mguu wake ndani ya Familia!
Alikuja kufa mamake kiulainiiiiii!!! Na hii ndo ilikuwa the big deal kwa shetani na yamkin walijua wangemwomba kirahisi asingekubali inabidi kwa taarfa za kuwa ameanza kutembea na yule shemeji yake ambae ni mdogo wa kijana aliyemwoa Dada wa jamaa! Eti mama alizimia 🙆🏿‍♂🙆🏿‍♂🙆🏿‍♂🙆🏿‍♂ inawezkana lkn lile lilikuwa ni daraja ya ufalme ule kumchukua Ampendae!!
 
hii ni google translate ama?
 
Daah mkuu light angeimalizia story then ungeshusha huu uchambuzi ingekuwa poa sana ila hapo mwisho kwa mama yake kufa jinsi ulivyochambua nadhani hata alikuwa hajui kama niwao walimchukua

Nimeinjoi uchambuzi wako mkuu
 
Hii ajali naikumbuka bado tangu nipo advance maeneo hayo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…