Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA KWANZA - Sehemu ya 10


Inaendelea.............




Nakumbuka ilipita miezi 2 na nusu mimi sijakanyaga shuleni maana niliumwa sana na mgongo!,kiukweli ndani ya muda huo mauzauza yakapungua ila uoga wa hapa na pale haukuisha!,baba alirejea ndani ya zile siku alizokuwa amesema na tukaendelea na maisha kama kawaida,kuna siku baba alimwambia mama kwamba anataka kurudi Dar es salaam kazini lakini kabla hajarudi kazini anataka kwenda kwa rafiki yake akaonane naye sehemu moja inaitwa Utegi,huko Utegi kwa wale ambao hamjafika Tarime nadhani leo ndiyo inaitwa Rorya,tayari ishakuwa wilaya inayojitegemea,zamani ilikuwa sehemu ya vijiji vya Tarime.

Mama pia alimwambia na yeye hatakuwa na siku nyingi pale nyumbani maana anamsubiri mama mdogo amalize mambo yake huko nyumbani kwake atakaporudi naye ataondoka kurudi huko Babati kazini kwake,Kiukweli mimi kadri ulivyofika mwezi wa tatu katikati baada ya lile tukio la kuanguka bafuni hali ilianza kuwa nzuri,nilianza sasa kutembea nikawa naweza hata kuinama na nikaanza kujifulia hata nguo zangu mwenyewe.Baba alipoondoka nakumbuka miaka hiyo si mama wala baba hawakuwa na simu za mkononi,mawasiliano yalikuwa ya simu ya mezani tu!,baada ya mzee kuondoka zilipita siku tatu hakuna mawasiliano,mama alikuwa na mashaka sana maana hakuzoea baba kwenda mbali bila kumpigia simu,na hakujua huko alikokwenda baba ni nini kilikuwa kinaendelea!,mama akaendelea kujipa moyo,baada ya wiki kupita,wasiwasi ulianza kumjaa mama maana alisema "Huyu baba yenu alipaswa arudi kazini,kaondoka hakuna mawasiliano,na ameendelea kukaa kimya wakati anaelewa kabisa hapa nyumbani katuacha na hali gani".


Nakumbuka baada ya wiki hiyo kupita mimi nikaanza sasa kufanya shughuli zangu kwa ukakamavu!,baada ya siku kadhaa ya hiyo wiki ya pili baba akawa amerejea,siku hiyo nakumbuka mama alimsimanga sana baba na kumsema sana,baba alikaa kimya na alikuwa mtulivu maana kelele za mama yawezekana alikuwa alishazizoea,hakuna aliyefahamu huko Utegi alienda kufanya nini,labda yawezekana alimwambia mama lakini sisi watoto hatukujua lolote!.Baada ya kutoka huko Utegi,alikaa siku mbili pale nyumbani na safari ya kuondoka kurudi Dar es salaam iliwadia,akatuaga akasema anaenda kukatia tiketi Musoma kwa ajili ya kuondoka,kwa wakati huo kuna gari lililokuwa linaenda Dar es salaam lilijulika kama SCANDINAVIA na lilikuwa linapitia Nairobi, ili upate tikiti ilikulazimu uende Musoma kukata tikiti maana enzi hizo hakukuwa na wakala wa hayo magari pale Tarime mjini,baada ya kukata tikiti wewe ndiye ungeamua upandie kulekule Musoma au urudi uje upandie Tarime,baba aliamua akapandie Musoma.

Mungu mkubwa nikawa sasa nimepona na nikaanza kurejea shule kama kawaida,mauzauza yakawa yameenda likizo kwa muda usiojulikana!,Kiukweli tulikaa sasa kwa amani na furaha ilianza kurejea kama kawaida maana hakukuwa na vitisho tena hapo nyumbani,Kumbuka nimesema mauza uza yalienda likizo kwa muda.Baada ya siku kadhaa mama alituaga akaondoka kurudi kazini kwake huko Babati,Manyara!,mama mdogo naye akawa amerudi na maisha yakaendelea kama kawaida.

Basi siku moja baba alirudi kutoka Dar es salaam alipokuwa amehamishiwa kikazi na hatukujua ni nini kirimrudisha hapo nyumbani ghfla hivyo.Nadhani niliiwaambia kuna siku aliaga akasema anaelekea kwa rafiki yake mmoja Utegi,kumbe kule Utegi hakwenda kwa rafiki yake wala nini bali alikuwa kaenda kwa mganga wa kienyeji,kwa taarifa tulizozipata pale nyumbani ni kwamba,kipindi kile alipo enda kwa huyo mganga hakumkuta, ikabidi amsubiri pale nyumbani kwa mganga ambako muda huo kulikuwa na wasaidizi wake tu,Kwahivyo baba ilibidi amsubiri yule mganga kwa muda wa wiki nzima,alipoona harudi kwa wakati ndipo ilibidi arudi nyumbani kujiandaa na safari ya Dar es salaam.

Sasa kumbe ule ujio wa mzee inaonekana aliwasiliana na huyo mganga akamwambia safari hii aende atamkuta,basi baada ya siku tatu akaondoka na kauli yake ileile ya kwenda kuonana na rafiki yake kule Utegi!,kweli,tulikaa pale nyumbani siku hiyo ikapita na siku iliyofuata nakumbuka ilikuwa mida ya saa 10 jioni,wakati narudi nyumbani kutoka shule,ile naingia ndani nikakutana na kikao sebuleni,alikuwepo mama mdogo pamoja na dada zangu wakizungumza!,ndipo nilipoambiwa muda si mrefu,yule kiumbe wa ajabu(Ashura) alikuwa hapo na katoka kuwaambia kila kitu alichokuwa anakifanya baba,sasa kabla ya Ashura kuondoka aliwaambia wajiandae kufanya msiba maana baba angerudi asingemaliza siku pale nyumbani,angekufa!.Mimi nilidhani ni kama maigizo lakini ndivyo ilivyokuwa,maana Ashura aliwahi kusema yeyote atakayejifanya kwenda kwa mganga kwa ajili yake ina maana alikuwa anataka kumuua yeye au kumsababishia matatizo kutoka kwa ndugu zake ikiwemo kuuliwa!,alikuwa kasema kabla ya yeye hayo hayajamkuta inapaswa huyo anayetekeleza huo ujinga afe yeye kwanza!,Pia aliwahi kusema ni marufuku kuomba au kusoma vitabu vitakatifu,hili agizo walitoa wale waliokuwa wanafahamika kama wazazi wake!.

Basi baada ya siku kadhaa baba alirejea nyumbani,dada zangu walimsimulia yote yaliyosemwa na Ashura,baba akawaambia"nilienda huko kwa ajili yenu wanangu,na kwa ajili ya kazini kwangu!".

Baba hakumaliza siku damu zilianza kumtoka puani kama maji,dada mkubwa ilibidi ampigie simu mama kumuleza hali namna ilivyokuwa,mpaka mama anafika pale nyumbani alikuta tayari kuna msiba wa baba (R.I.P).Baba yangu alifariki tarehe 21.5.2001 na alizikwa makaburi ya Ronsoti(Wenyeji wa Tarime watakuwa wanayafamu).
Baada ya baba yangu kufa,kiukweli hali ilikuwa mbaya sana,ukizingatia tena ndiye alikuwa nguzo ya familia,baba yangu kidogo alikuwa na vipesa vya hapa na pale maana kwa wakati huo kukaa maeneo hayo ya bomani haikuwa kazi nyepesi sana,wakazi wa Tarime nadhani watakuwa wanaelewa vizuri hayo maeneo.

Baada ya msiba wa baba ni kama familia nzima ilikumbwa ni mikosi maana mama naye aliacha kazi kwasababu ile kampuni yao ya ujenzi aliyokuwa akiifanyia kazi ilifilisika,sikujua ilikumbwa na nini maana kipindi kile sikuwa na ufahamu sana wa haya mambo ya kufilisika,mama alisimama kwenda kazini!.Maisha yalivyozidi kuwa magumu yule Shangazi yetu aliyekuwa akikaa Mwanza alimshauri mama atafute pesa akafanye biashara huko Mwanza!,mama alipata wazo la kuuiuza ile nyumba yetu,ndipo alipotuita wanae wote akatushirikisha na sote tulikubaliana,ukizingatia nyumba yenyewe ilikuwa na mauzauza,mpaka wakati huo hakuna jirani yeyote ambaye alielewa mauzauza ya ile nyumba ila ilibaki kuwa ni siri ya familia.Baada ya ile nyumba kuuzwa sote tulihamia Mwanza,wenzangu waliondoka wakaniacha pale Tarime kwa mama mdogo,nilipomaliza darasa la saba niliondoka kuelekea mwanza huo mwaka 2003.



Itaendelea..........................
 
Hii episode mkuu umetung'ong'a kiukweli ........
Ila angalau Leo ntalala Kwa Amani....
mambo ya dada Ashura Leo yameenda likizo kwa muda...😊
Kesho nitakua hapa asubuhi na mapema .....
Chai na episode 11 tafadhali..
Ujitahidi.
 
phonex a.k.a fupa. ngoja nisubiri muendelezo
Hapana mkuu, Fupa ni Baiskeli kuu kuu, yaani unakuta baiskeli ipo kama namba nane vile yaani unakuta baiskeli imebaki vyuma tupu hata zile gadi za kuzuia uchafu usimpate mwendeshaji haina wala vile vipila vya pedeli hakuna, breki unaikuta ipo ya nyuma au isiwepo kabisa

Mfano hiyo iliyopo pichani toa hizo bati zinazofunika tairi kisha kwenye pedeli toa vipira ibaki vyuma tupu
 

Attachments

  • DSCF4261.JPG
    DSCF4261.JPG
    170.1 KB · Views: 125
Hapana mkuu, Fupa ni Baiskeli kuu kuu, yaani unakuta baiskeli ipo kama namba nane vile yaani unakuta baiskeli imebaki vyuma tupu hata zile gadi za kuzuia uchafu usimpate mwendeshaji haina wala vile vipila vya pedeli hakuna, breki unaikuta ipo ya nyuma au isiwepo kabisa

Mfano hiyo iliyopo pichani toa hizo bati zinazofunika tairi kisha kwenye pedeli toa vipira ibaki vyuma tupu
Umenikumbusha mbali sana hii chombo ilikuwepo home alaf breki hakuna kwaiyo huwa nikiendesha nikitaka kufunga breki naweka mguu wangu wenye ambao nimevaa ndala kwenye tairi la nyuma hapo kumbuka baiskeli ni fupa
 
Hapana mkuu, Fupa ni Baiskeli kuu kuu, yaani unakuta baiskeli ipo kama namba nane vile yaani unakuta baiskeli imebaki vyuma tupu hata zile gadi za kuzuia uchafu usimpate mwendeshaji haina wala vile vipila vya pedeli hakuna, breki unaikuta ipo ya nyuma au isiwepo kabisa

Mfano hiyo iliyopo pichani toa hizo bati zinazofunika tairi kisha kwenye pedeli toa vipira ibaki vyuma tupu
Aisee hii picha kali sanaa. picha ya kufungia mwaka hii
 
Back
Top Bottom