Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Au mkuu boss wa tegeta na mbez beach wameingilia kati ?
 
Ahsante kwa ushauri na mimi nimesema lazima NIENDELEE NA KISA HIKI ILI WATU WENYE TAMAA YA UTAJIRI WA KISHIRIKINA WAELEWE MADHIRA YALIYO HUKO KWA IBILISI


NITAENDELEA KAMA KAWAIDA
Kati ya watu ambao tumeguswa na hichi kisa chako na mimi nimo mkuu.
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 17.



Inaendelea.............



Zamu yangu hatimaye ilifika na nilisimama mbele ya mungu ambaye alikuwa mnene ajabu.Nilimsalimia wakati huo nilikuwa nikitetemeka sana kwa uoga!.

Aliniambia "usiogope!"

Akaniuliza "Unaitwa nani?".

Nilipomtajia jina langu akaendelea kuniuliza "Umefata nini huku?".

Nilimwambia "ninataka kuwa tajiri!".

Akaniambia "Bila shaka utakuwa umeelezwa kila kitu".

Nilimwambia "hapana sijaambiwa chochote!".

Basi alimuita yule dada aliyetupeleka hapo akamwambia" huyu bado,hebu mpeleke akapate maelekezo kwanza ndiyo umrudishe hapa!".

Yule dada alinichukua tukaingia chumba kilichokuwa mkono wa kushoto wa kile kiti cha mungu,nilipofika humo ndani nilimkuta mwanamke mmoja aliyekuwa mzuri ajabu halafu alikuwa amekaa kwenye dimbwi(swimming pool) iliyokuwa imejaa damu akiwa anaoga humo,Yule mwanamke mikononi alijaa vito vya thamani tupu,vidole vyote alikuwa amevaa pete zilizokuwa ziking'aa sana,shingoni napo alikuwa amevaa mikufu iliyokuwa iking'aa ajabu!.Nilimsalimia lakini hakuitikia!,alikuwa bize na mambo yake kana kwamba hajatuona.Yule dada niliyeingia naye mle ndani aliniambia kwa sauti ya juu iliyojaa ukali "Sujudu mbele ya Malikia!".

Bila kupoteza muda nilisujudu,ndipo sasa nilimsalimia akaitikia!.Alianza kuniambia kwamba,safari yangu yote ya maisha anaifahamu na ametokea kunipenda sana kwakuwa mimi nilikuwa jasiri.Aliendelea kuniambia kwamba kuna utajiri wa aina mbili ambao inapaswa nichague mmoja wapo.

Moja,ilikuwa kumtoa mama yangu kafara na nikishamtoa kafara kama msukule niwe ninashiriki naye ngono kila inapohitajika ambapo ningepata utajiri mkubwa wa kutisha duniani.

Pili,aliniambia ilikuwa kutoa kafara za watu mbalimbali kila mwisho wa mwezi na ilipaswa nipewe nguvu za ziada ili kutekeleza adhma yangu hiyo na endapo nisingefanikiwa kutoa kafara kwa mwezi hata mmoja basi ningefanywa kafara mimi!.

Huyo Malikia aliniambia nichague moja,kiukweli sikuwa na muda hata wa kupoteza maana ilitakiwa nitoe majibu bila kufikiria,basi mimi nilichagua huo utajiri namba mbili ambao nilipaswa kutoa kafara kila ifikapo mwisho wa mwezi,niliona nisingeweza kumtoa mama yangu kafara kwa maana huo utajiri nilienda kuutafuta kwa ajili yake kutokana na kudharauriwa na yule shemeji na baadhi ya watu wengine mtaani.Baada ya ule uchaguzi niliyoufanya Yule Malikia aliniambia "Nimekupenda sana kijana jasiri!".

Aliinuka kutoka kwenye lile dimbwi lililokuwa limejaa damu na alinisogelea,kiukweli alikuwa mzuri ajabu,muda huo alikuwa uchi kama alivyozaliwa,sijawahi kukutana na mwanamke mzuri kama yule duniani,uenda labda kwakuwa sijatembea nchi za watu lakini kwa Tanzania hii sijapata kuona!.Alikuwa na nywele ndefu sana ambazo zilikuwa zinaburuzika chini kama mwanamke aliyevaa shela ya harusi.Alinishika mkono wangu wa kushoto akaniambia ananiwekea irizi ambayo ingenipatia nguvu ya kufanya chochote nitakachokitaka duniani, aliniambia hiyo irizi ingenipatia uwezo wa kulala na mwanamke yeyote ambaye ningemtaka duniani,aliniambia pia ningeweza kuingia popote ambapo ningetaka bila kuhojiwa wala kusumbuliwa na yeyote duniani,aliniambia pia kwakutumia ile irizi na dawa zile nilizofundishwa kuchanganya kule msituni nitaweza kutoa kafara mahala popote nitakapo na kwa wakati wowote!.

Alichukua kidole chake ambacho kilikuwa na kucha ndefu akanitoboa pembeni ya mkono akaniwekea kitu kidogo mithili ya mbegu la haragwe halafu akapalamba mahali pale palipokuwa na damu pakaziba,Kiukweli niliona kama miujiza lakini lilikuwa tukio halisi lililonishangaza mpaka leo.Aliniambia itanipasa kutenga chumba mahali cha siri kwenye nyumba nitakapoishi,hicho chumba haikupaswa aingie mtu yeyote ila mimi peke yangu,pia aliniambia itakapokuwa inafika tarehe 15 ya kila mwezi nitakuwa ninaingia kwenye hicho chumba kuchukua pesa itakayokuwa inaletwa na kiumbe asiyefahamika baada ya mimi kutoa kafara!.Pia aliniambia kila mwisho wa mwezi baada ya kuwa nimetoa kafara itanibidi zile damu ambazo nitakuwa nimeziweka kwenye kibuyu kidogo ambacho aliniambia mzee Nchabironda angenipatia niwe naziweka kwenye hicho chumba cha siri ambapo zingekuwa zinachukuliwa humo.Aliendelea kuniambia kwamba,nitakapofika duniani nihakikishe natafuta mwanamke ambaye nitakuwa nikimpa ujauzito halafu watoto baada ya kuzaliwa wagekuwa wanachukuliwa kwa ajili ya kafara!.

Baada ya hayo maelekezo nilimuuliza kuhusu nyota yangu maana nilimweleza kwamba niliambiwa nyota yangu ya utajiri alikuwa nayo marehemu baba.

Alinijibu kwamba "Tangu siku umefika hapa kila kitu kilirudishwa kwako,ondoa mashaka kuhusu nyota".

Aliendelea kuniambia "Haya maagizo ninayokupatia hapa ni zaidi ya kuwa na nyota na utafanikiwa kila engo ya duniani cha msingi ukienda kafanye niliyokuagiza".

Baada ya yale maelekezo ilibidi arudi ndani ya lile dimbwi lililokuwa limejaa damu!,Yule dada alinichukua tena kunirudisha kwa yule mungu!.

Nilipofika yule mungu aliuliza "umepata maelekezo?".

Nikamjibu "Ndiyo".

Akaniambia "kafanye kama ulivyoelekezwa,usipofanya kama ulivyoelekezwa,wewe ndiye utakuwa kafara".

Huyo mungu alikuwa akiongea sauti ndogo sana kama ya mtoto mdogo,kiukweli nilikuwa nikimshangaa sana namna alivyokuwa.Yule dada alinichukua na kunirudisha kule kwenye lile jumba la mara ya kwanza tulikofikia,nikavalishwa kile kinguo changu cha ngozi kilichokuwa kinafunika sehemu zangu za siri.Wale jamaa niliyoenda nao kule chini ya ziwa sikufahamu mpaka wakati huo walikuwa maeneo gani kwasababu baada ya kutenganishwa ile siku ya kwanza sikuwaona tena.Nilimuuliza yule dada namna ya kutoka huko chini ya maji.

Akaniambia "hiyo irizi uliyowekewa mkononi ndiyo kila kitu".

Akaniambia "tamka ya kwamba unahitaji kurudi ulikotoka".

Kweli,nilitamka ya kwamba "nataka nirudi nilikotoka".

Kufumba na kufumbua nilishitukia nipo ufukweni mwa ziwa Tanganyika lilelile eneo ambalo mwanzo tulipandia ule ungo!.Baada ya muda kidogo alifika mzee Nchibaronda na akainipongeza sana,Nilimuuliza siku hiyo ilikuwa lini akanimbia ilikuwa jumatatu!,niliguandua kwamba kule chini nilikaa siku zipatazo tatu tu,maana tuliondoka kwenda huko chini ya ziwa ilikuwa siku ya Ijumaa.Basi mzee aliniambia nimshikirie,baada ya sekunde alitoweka hilo eneo la ufukweni kwa mwendo mkali sana ambapo haikuchukua muda tukawa tumefika pale nyumbani kwake.

Siku zote utajiri na uchawi/ushirikina haviachani!,ni kama watoto mapacha!,Mimi pamoja na kwenda kuusaka utajiri lakini nikajikuta naufahamu na ushirikina ambao ulinisaidia kwenye mambo yangu ya kafara!.Basi tulivyofika hapo Kirungu kwa mzee nilipumzika kwa uchovu niliyokuwa nao,kwakuwa kule hakukuwa na usiku wala kulala,nilipotoka huko nilijikuta nina usingizi wa ajabu,nililala pale kwa mzee siku hiyo nzima,nilimwambia mzee kwamba kesho yake mimi ningeondoka zangu kurudi Mwanza,Tanzania.


Itaendelea.....................
 
Hizo ni hila za yule mwovu mkuu, anataka tusifahamu mungu wa ulimwengu anavodanganya na kunasa watu kupitia utajiri, usikubali kusujudia pesa kama ulishayashinda vipi unataka kurubuniwa kirahisi hivi?

Vv
 
Duh noma sana, endelea kushusha vitu mzee baba pia usisahau kutuma hiyo picha yamkono
 

Kuna watu wanatamani wapate nafasi ya kufika huko walipo hao wadada wazuri unaowaelezea.

Shida sio wapate utajiri ila wale matunda kimasihara masihara.
 
Umeanza tena tamaa,
Tumalizie kisha ndio mfanye biashara na huyo jamaa,
Kwani jf ina watu wangapi hata stori isiuzwe kama tukiisoma??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…