Habarini za kutwa wanajamvi ,Bila shaka wote mko bìèn!
Kwanza kabisa nianzè kwa kusema ninayo mìkasa miwili ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho yangu na hii mikasa inanihusu mimi moja kwa moja! Kuna nyuzi kadhaa humu nimekuwa nikizisoma za watu mbalimbali kusimulia visa na mikasa ya maisha yao au jamaa zao ambayo waliwahi pitia. Hivyo nami nkaona sasa ni muda muafaka kuleta simulizi nilizo-experience katika maisha!
MKASA WA KWANZA
Mnamo mwaka 2000 nikiwa mkoani Mara, wilaya ya Tarime mimi, ndugu zangu pamoja na wazazi wangu tukiishi mitaa ya Bomani(wenyeji wa Tarime wanaielewa vizuri hii mitaa) Sisi hatukuwa wenyeji wa Tarime ila Mama na Mzee walikuwa kule kikazi hivyo nasi pia elimu yetu tuliipata huko.
Mzee alikuwa ni mtu wa kusafiri kikazi na mama alikuwa yeye kazi anazifanyia pale japo walikuwa wakitoka anaweza kukaa hata miezi 6 hajarudi nyumbani, Bi mkubwa alikuwa akifanya kazi kwenye kampuni ya Ujenzi so nadhani zile pilika pilika za ujenzi pia zilimfanya kuwa bize kidogo!
Mzee alipata safari ya kwenda kikazi mkoani Singida ambako alikaa kama miezi miwili na aliporudi alirudi na mwanadada mmoja mwenye asili ya kiarabu akiwa kama mfanyakazi,Nakumbuka bi mkubwa alim-maindi sana mzee akimtuhumu kwamba uenda yule anaweza akawa mchepuko wa Mzee ila mzee anazuga kwamba ni mfanyakazi(siunajua tena mambo ya wivu),Baadae mambo yalikaa sawa na kweli yule bi dada akawa mfanyakazi pale maskani
Kiukweli alikuwa mzuri na sisi kwa sababu tulifundishwa nidhamu na heshima hivyo tulimheshimu kama dada na tukampenda!
Miezi ikakata,hatimaye mwaka pia ukakata tukiishi kwa furaha,amani na upendo!
Mzee alihamishwa kikazi kupelekwa Dar esa salaam hivyo pale tukabaki na Bi mkubwa ambaye pia alianza kusafiri kikazi na kukaa hata miezi 5 au 6 hajarudi nyumbani, kilichokuwa kinafanyika yeye ni kutuma pesa tu ya matumizi na kutupigia simu kutujulia hali!
Baada ya siku kadhaa kukatika yule dada (Binti wa kazi), alituita sebuleni wote mimi pamoja na ma-sister zangu na akatueleza kwamba yeye anawageni wake ambao ni ndugu zake watakuwa wanakuja kumtembelea kila mwisho wa mwezi! Kwa kuwa tulifundishwa ukarimu na wazee hivyo hatukuona taabu, ila alitueleza ya kwamba hao ndugu zake wanamashariti makali na inapaswa tuyaelewe ili watakapokuja tusipate taabu. Kwa hiyo kutuita pale ilikuwa ni kutupa namna iliyo bora ya kuwapokea hao ndugu zake!
Kiukweli mimi nilipata mshituko kidogo, nijiuliza maswaĺi kadhaa lakini sikupata majibu, tulikuwa tumezoea kuwapokea wageni mbalimbali siku zote na walikuwa wakija bila masharti! sasa nkawa najiuliza hao ni wageni wa namna gani waliokuwa na masharti tena akasema ni makali na kila mtu anapaswa ayafuate si ombi bali ni lazima!
Watu wote pale sebuleni tulikaa kimya na nilikuwa nkiziangalia sura za ma-sista zangu zilibadilika ghafla na kuonyesha huzuni!
Basi masharti yenyewe yakawekwa bayana kama ifuatavyo:-
1. Siku hiyo wote tutavaa nguo za kulalia(pajama)nyeupe
2. Siku hiyo vyumba vya kulala vihakikishwe vinakuwa safi isionekane hata nukta ya uchafu
3. Siku kama ukienda kuoga basi hakikisha unaenda kuoga na sabuni ambayo alikuwa akiitumia yeye,siikumbuki ile sabuni lakini ilikuwa na marashi sana!
4. Akawaambia ma-sista kwamba kama siku hiyo ambayo wageni walikuwa wanakuja kuna mtu atakuwa kwenye siku zake basi hakutakiwa aonekane pale nyumbani maana angejuta!,It means ilipaswa aende akalale kwa majirani au ndugu!
Kumbuka hayo maeneo ya Bomani yalikuwa maeneo fulani ya wazito na miji ilikuwa iko mbalimbali na ilikuwa geti kali,sijajua nowadays maana sijakwenda Tarime kitambo sana!
Hayo ndo yalikuwa masharti tuliyopewa siku hiyo!
Fuatana nami kujua nini kitaendelea................................
Muendelezo 1
Habarini za kutwa wanajamvi ,bila shaka wote mko bìèn!. Kwanza kabisa nianze kwa kusema ninayo mikasa miwili ambayo nimewahi kuishuhudia kwa macho yangu na kuifanya kwa mikono yangu mwenyewe,mkasa wa kwanza ulituhusu mimi na ndugu zangu ambapo wakati huo nikiwa nina miaka 14 - 15 mwaka 2000 -...
Muendelezo 2
Muendelezo 3