Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

porojo tupu, majini hawana masharti hayo katika hali halisi ila kwa tungo kama hizi ama kwenye video ndo unasikia jini anakuja kwa kishindo, ama ile cheka yake ya makelele

jini kupanda hahitaji bwebwe anapanda kistarabu na anaeleza yake

mapepo /misukule ndo wanazingua ivo.
Zipompa, wewe nawe ni jini?

Vv
mkuu humu tunaleteana story za bongo movie kuona jini kuja anakuja kwa kelele mara kucheka kwa sauti porojo tupu

jini anakuja kawaida sana tena kwa amani zote.a

ujaona jamaa anakuletea stori za magazetini mara uogee sabuni ya geisha mara uvae pajama

alafu jini anakuja vp kukusalamia wakati jini ulipo yupo ni ww kuchoma udi na ubani kumwomba atatue shida zako.

alafu pombe za mlinzi zinawakera vp majini wakati wao wana mishe zao. (wao wakute chumba cha mgeni wao kisafi, sasa waangike na mlinzi wa nini

bongo movie imeathiri bongo za vijana na kuleta stori za kijinga jinga
 
MKASA WA KWANZA - Sehemu ya 6


Inaendelea.............




Baada ya siku mbili mama alirudi kutoka huko kazini kwake alikokuwa amesafiri,kiukweli kwa upande wangu nilifurahi sana maana mara zote mama alipokuwa akienda safari na akirudi,lazima aniletee viatu vipya,hivyo kila alipokuwa akija mimi nilikuwa nafurahia,alifika mida ya saa 7 mchana.Basi jioni baada ya kula chakula,mama alituita wote sebuleni,ndipo maongezi yakaanza.Mama akasema yote yaliyokuwa yakiendelea hapo nyumbani anayafahamu kwani dada yetu mkubwa alimwambia kila kitu,alichokuwa anataka ni kwamba, dada Ashura aeleze ni nini kilichokuwa kinamsibu na asifiche chochote.Baada ya dada Ashura kuwa ameeleza kila kitu kilichotokea,alilisitiza kwamba hatupaswi kuwa na hofu maana wale ni wazazi wake na wangekuwa wanakuja pale nyumbani kila ifikapo mwisho wa mwezi.

Mama niliona anahuzunika sana na akamhoji Ashura "Ina maana wazazi wako kuja hapa kwangu mpaka masharti?".

Yule dada kwa kiburi akajibu "Ndiyo".


Mama alikasirika sana, palepale alitamka ya kwamba "Kapange nguo zako kesho asubuhi nahitaji nisikuone hapa kwangu".

Mama akaendelea kumuuliza "Unanidai shilingi ngapi?".

Yule dada wa kazi kuna kiasi alikitaja ambacho nilishakisahau lakini ilikuwa zaidi ya laki moja kwa maana mama aliwahi kusema kwamba kuna siku alimwambia hela yake awe anamtunzia na endapo angehitaji ndiyo angempatia.Kweli,dada Ashura aliondoka hapo sebuleni kwa hasira kuelekea chumbani ambako alienda kupanga nguo zake.Mama alituambia angempigia simu mdogo wake ambaye alikuwa mama yetu mdogo aje pale nyumbani tukae naye kwa wakati huo maana yeye alihitajika kuwahi kazini.Siku hiyo tulilala kwa amani kabisa bila bugudha ya aina yeyote,Yale mauzauza kiukweli ilifika mahala nikaanza kuyazoea na kuona ni mambo ya kawaida,sasa sijajua uenda ilikuwa ni akili za utoto!.

Asubuhi kulipokucha mama ndiye aliwahi kuamka na kusalimia kwenye kila chumba,alimwamsha dada yetu mkubwa akamwambia "Mimi leo naondoka namrudisha huyu Ashura kwao,niliwasiliana na baba yenu toka ile majuzi nikamwelezea hali halisi na yeye pia akasema nikamlipie tiketi arudi kwao".

Kwa wakati huo mama yangu walikuwa wanafanya kazi zao hizo za ujenzi huko Babati,hivyo ili yule dada wa kazi afike kwao Singida ilipaswa wapitie Nairobi kisha Arusha ndiyo iwe rahisi kufika kwao, maana enzi hizo njia za huku kwetu zilikuwa hazipitiki,hivyo mama akamwambia dada yangu kwamba,watakapofika Arusha atampandisha kwenye magari ya Singida na yeye ataelekea Babati kwenye shughuli zake.Hivyo ndivyo ilivyokuwa,mama alituambia mama mdogo angekuja jioni ile,pia aliahidi kulitafutia ufumbuzi suala la mlinzi siku si nyingi,kuna hela ya matumizi akampa dada,dada Ashura alituaga hapo nyumbani mimi na dada zangu,kwa vile tulishamzoea tulihuzunika ijapokuwa tulipitia mambo mengi ya kutisha!.Kabla hajaondoka alisema "Nitarudi",sasa kwa vile mimi bado nilikuwa mdogo,ile kauli sikuitilia maanani sana maana nilijua uenda atarudi siku moja kutusalimia!.

Basi mama na Ashura waliondoka na tukabaki wenyewe pale nyumbani mpaka ilipofika jioni mama mdogo alikuja na maisha yakaendelea kama kawaida,zilipita siku tatu mama alipiga simu,aliongea na mama mdogo akamweleza yeye keshafika huko kazini kwake na Ashura walipofika Arusha alimpakia kwenye magari ya kuelekea kwao Singida hivyo hajui kama alifika ama la!,lakini mama anasema alimuuliza akamhakikishia angefika salama pasipo shaka yeyote!.Tulikaa hapo nyumbani na shughuli zikawa za kawaida mpaka shule zilipofunguliwa ile mwezi januari nikaanza kwenda shule kama kawaida!.



Itaendelea........................
 
porojo tupu, majini hawana masharti hayo katika hali halisi ila kwa tungo kama hizi ama kwenye video ndo unasikia jini anakuja kwa kishindo, ama ile cheka yake ya makelele

jini kupanda hahitaji bwebwe anapanda kistarabu na anaeleza yake

mapepo /misukule ndo wanazingua ivo.
ko wewe ndo unayajua sana majini sio
 
Back
Top Bottom