Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Haya mambo ys nitaendelea ningejua ningefanya kama ile hadithi ya msitu wa nairoto. Niliacha uzi utiririke week kadhaa. Nilipokuja kusoma nikasoma yote.
 
MKASA WA KWANZA - Sehemu ya 7


Inaendelea.............



Ulipokatika mwezi mmoja toka mama mdogo kaja pale nyumbani kuna hali fulani za kutisha na kusikitisha zilianza kujitokeza,nakumbuka siku moja nilichelewa kufua nguo zangu za shule kwasababu ya michezo maana tulivyotawanyika shuleni mimi nikaelekea kucheza mpira na marafiki zangu ,nimerudi nyumbani usiku sana hivyo ilinibidi nifue nguo za shule usiku huo,nilichofua ilikuwa shati na tai maana bukta ilikuwepo nyingine,mashati nilikuwa nayo mawili,moja lilikuwa na muhuri wa shule na lingine lilikuwa halina muhuri,kwahiyo nilifua lenye muhuri maana kesho yake ilikuwa ni siku ya ukaguzi,siku ya ukaguzi ulikuwa ukivaa shati lisilokuwa na muhuri viboko vilikuwa vinakuhusu,lile lisilokuwa na muhuri nilikuwa nalivaa siku za kawaida,hivyo ilibidi nifue kwa maana shati lenye muhuri ndilo lilikuwa chafu.Hivyo nilivyomaliza kufua ilibidi usiku huohuo nilipige pasi ili liweze kukauka!,mama mdogo aliniambia siku nyingine nisiwe nafua usiku kwa maana huwa si vizuri.

Basi shughuli zote zilipoisha tuliingia kula kisha kila mtu kuendelea na shughuli zake,mimi sikutaka kukaa sebuleni,niliingia chumbani kuendelea na ishu zangu za matayarisho ya shule,baada ya hapo niliingia kulala,nilikuja kushitushwa usiku wa saa 9 na sauti za watu,kumbe walikuwa ni kina mama mdogo na dada zangu wameamka wakiongea,ndipo dada yangu mkubwa alikuwa akinigongea mlango wa chumbani kwangu.Nilipoamka kitandani ile nimekanyaga chini nikakutana na maji yenye kimo cha magotini,nilishituka sana,nilipoufungua mlango swali la kwanza kwa dada yangu lilikuwa ni " Haya maji yametoka wapi?".

Nilimtazama dada yangu alipokuwa kasimama nikaona maji yapo magotini,Kumbe nyumba nzima ilijaa maji na bado mabomba yalikuwa yakitoa maji nyumba nzima,ndipo mama mdogo alipoingia bafuni na chooni kufunga mabomba,alimwambia pia dada aingie kule jikoni kufunga mabomba ya maji,baada ya hapo mama mdogo alituita na kutuuliza "ni nani jana hakufunga mabomba alipo maliza shughuli zake?".

Kila mtu alisema alipomaliza kutumia maji alifunga bomba,mimi kwa upande wangu nilisema nilipomaliza kufua nilifunga bomba na bahati nzuri niliingia chumbani kwangu nikawaacha wao sebuleni,hivyo kama sikufunga bomba ingeonekana.Kila mtu humo ndani alikuwa akishangaa hilo suala la maji kujaa ndani ya nyumba,kile chumba cha wazazi wangu kilipofunguliwa ndipo nako tukakuta mabomba ya bafuni yanamwaga maji!,ndipo sasa akili zilianza kuruka kwa kasi na kila mtu kuingiwa na uoga!.

Mama mdogo alisema "Hiki chumba hakina mtu na kilikuwa kimefungwa,kama kweli tungekuwa tumeacha mabomba bila kufunga ilipaswa yawe ya huku kwetu tu,sasa na huku je nani kafungua haya mambomba?".


Ndugu zangu labda tu niseme sijawahi kushuhudia mauzauza kama niliyoyashuhudia kipindi hicho,maji yalikuwa yamejaa nyumba nzima,ndipo kazi ya kuyachota ikaanza,tulichota yale maji kuanzia mida ya saa 9 usiku mpaka asubuhi,mimi ilibidi nijiandae kuelekea shule asubuhi hiyo maana sikuwa na namna,viatu vyangu vililowana na maji lakini nilijitahidi kuvikamua na kuvikung'uta,vilipoonyesha hali ya kukauka,nilivaa nikasepa zangu shule nikawaacha wao wakiendelea kuyatoa maji ndani ya nyumba.,Baadae niliporudi nyumbani niliwakuta vijana wawili walikuwa ni vijana wa majirani wakisaidia kuyatoa yale maji,sasa hebu fikiria toka asubuhi mpaka ile saa 9 mchana, mimi nafika nyumbani maji hayajaisha ndani!.Kiukweli tulipambana sana mpaka yakaisha na tulimshukuru Mungu sana.

Baada ya siku kupita ambayo sasa ilikuwa ni jumamosi siku hiyo,tulipo kuwa nje kila mtu akiwa na shughuli zake ndipo ndani tukasikia yule dada yangu niliyekuwa namfuatia mimi kwa uzao akipiga kelele sana!,tulitimua mbio kuelekea ndani na kumkuta kajifungia chumbani,baada ya kugonga sana akafungua mlango akiwa bado ana maji mwilini,kwa maana kwamba alikuwa bafuni akioga,ndipo akaanza kusema kwamba alipokuwa bafuni alikuwa anahisi kuoshwa na mtu asiyeonekana na kumshikashika mwilini,ndipo alipopiga kelele na kukimbilia chumbani!.Tukiwa bado tumekaa tukishangaa humo chumbani,ghafla tukaanza kusikia watu wakitembea wakiwa wanakuja mle chumbani tulimokuwamo.

Hapa naomba nielezee kidogo,ulishaonaga mwanamke amevaa viatu virefu akiwa anaingia eidha kanisani au sehemu zilizotulia kwa ukimya?,huwa kuna mlio fulani ambao viatu alivyovaa huwa vinatoa,huwa ni kama kwaaaa.....kwaaaa.....kwaaaa,basi huo mlio ndiyo tuliyokuwa tunausikia,kwa sauti zile za viatu yaelekea walikuwa wengi wanatembea maana milio ya hizo skuna ilikuwa mingi ikija mahali ambapo tupo.Ghafla kila mtu alitafuta mahali pa kujificha,si mama mdogo wala dada zangu, kwani kila mtu aliogopa,mimi nakumbuka niliingia kabatini(makabi yale ya ukutani),hao wengine sikutaka kufahamu wao walijificha wapi maana hali ilikuwa ni mtafutano!,baada ya kuwa tumejificha na kuwa kimya zile sauti zilikoma,ndipo kila mtu alitoka kwenye maficho,nakumbuka nilipotoka kabatini niliwakuta wenzangu wakiwa uvunguni.

Basi mama mdogo ile hali ilimpatia wasiwasi sana,alisema "Sidhani hapa kama pana nifaa,hii hali mlikuwa mnakaa nayo siku zote?".

Dada mkubwa alimjibu "Hapana,hii imeanza baada ya Ashura kuondoka na imeanza hivi majuzi tukiwa wote sisi na wewe!".

Tulikaa kwa wasiwasi sana siku hiyo,ilipofika usiku kila mtu aliingia kulala,siku hiyo hakuna ambaye alitaka kubaki sebuleni mwenyewe!.Nilipoingia chumbani kwangu kabla ya kulala nilichukua madaftari na kuanza kujisomea kama kawaida yangu,nakumbuka nilijisomea mpaka mida ya saa 4 usiku ndipo nikazima taa na kuingia kulala.Mara ghafla baada ya dakika 10 nikasikia taa imewashwa!.



Itaendelea.....................
 
Nachomkubali mwamba pamoja na "Itaendelea" nyingi lakini hakawii sana

Wengine ukiambiwa itaendelea ni wiki hiyo
ila kuna viashiria vingi kuwa hii ni zile hadithi za hekaya za Abunuwasi iliyoimarishwa!
 
Back
Top Bottom