Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 20

Inaendelea.............

Niliondoka hapo geto kwangu nikiwa nimejianda kikamilifu kwa ajili ya kuelekea Shinyanga,Nilifika maeneo fulani hv panaitwa Tinde,pale Tinde kuna njia moja ilikuwa ikielekea Kahama.
Sasa kabla hujafika kahama hapo katikati huwa kuna ka mji kanaitwa Isaka,Tukio nililoenda kupiga siku hiyo ilikuwa katikati ya Tinde na Isaka!

Nilipofila pale nilianza kuangalia magari yanayopita pale!,Nilikuwa nina uwezo wa kuliona gari lote na uwezo wa abiria waliokuwemo!,Kama hilo gari lilikuwa limebeba watu waliokuwa wamejizindika nilikuwa nina achana nalo!

Sasa hapa labda nieleze kidogo!,Iko hivi,Mara nyingi mshirikina yeyote au mchawi akimuona mtu hata kama analindwa na Mungu yeye kwa akili yake anajua huyo mtu atakuwa na dawa kali kuliko zake!
Hiyo hali na mimi nilikutana nayo kwenye baadhi ya magari na kiukweli nilikuwa ninaachana nao maana nilijua naweza kupata majanga!
Nilipokaa kwa muda mrefu kidogo yale maeneo niliona kuna Gari aina ya Noah lilikuwa linakuja kwa kasi sana!,nilipopiga darubini yangu niliona waliokuwa ndani ya hilo gari walikuwa emptiness(Hawakuwa na chochote ambacho kingenizuia mimi kufanya tukio).

Basi kuna tego nililiweka pale Barabarani na gari ilipofika yale maeneo ilikula mzinga wa maana na palepale walikufa watu 3,Ndani ya lile gari kulikuwa na Mwanaume na mwanamke wamekaa mbele na nyuma kulikuwa na abiria kama 5 hivi,kwa muonekano wa lile gari nadhani wale wa Mbele walikuwa ni mke na mume ambao walionekana kabisa ndiyo wamiliki wa lile gari wale wengine nadhani walikuwa tu abiria ambao walikuwa wamewachukua njiani ili kupata hela kidogo!
Nililisogelea lile gari na nikachukua kibuyu kile na kuanza kuweka damu!,Nilihakikisha siachi hata tone la damu na wale ambao niliwakuta hai nilihakikisha nawanyonya damu yote kiasi kwamba hata wangepelekwa hospitali wasingefika kabla hawajafa!,Na hivyo ndivyo ilivyokuwa!

Nilipomaliza zangu kufanya kilichonipeleka niliondoka yale maeneo pasipo kuonekana na yeyote!
Nilipofika geto kama kawaida nilichukua kile kibuyu nikakiweka chini ya uvungu na mimi nikaondoka zangu kupiga mishemishe zangu za ualimu!
Kwa wakati huo nilikuwa ninapiga pamba kali na nilikuwa nina pendeza sana na isingekuwa rahisi kwa mtu yeyote kujua ninachokifanya!

Sasa pale shuleni nilipokuwa nikifundisha kama kuzuga ili nionekane nina kazi,kuna demu mmoja alikuwa Mwalimu ameajiriwa,kumbuka mimi nilikuwa mwalimu temporary mpaka wakati huo!
Yule Maalimu alikuwa mzuri sana na alikuwa na maringo sana,kuna wakati unaweza kumsalimia na asikuitikie kisa tu alikuwa mzuri na wengine tulionekana vibaka tu,Kwa wakati huo alikuwa na gari ambayo inasemekana alinunuliwa na jamaa yake ambaye tuliambiwa alikuwa na mshiko!
Alikuwa na kigari fulani hivi kinaitwa Duet,nadhani kalikuwa kametengeneza na kampuni ya Toyota kama sikosei!

Nilijiapiza ya kwamba wikiendi itakayofuata,yaani ndani ya wiki hiyo lazima atanitambua maana nilisema lazima nimkung'ute shipa la maana!
Basi baada ya vipindi nilirudi zangu nyumbani na nilipofika nilikuta kama kawaida begi lile limejaa pesa na nkaanza kuzihesabu mara hii zilikuwa kama milioni 15,Nilizitoa kwenye Begi na nikaziweka kwenye sanduku moja ambalo ndo nilikuwa natunzia hela na lile begi nikalirudisha uvunguni!
Wakati huo kwakuwa ndo kwanza mwezi ulikuwa umeanza nilikuwa nimelipwa vi-hela vya kazi yangu hiyo niliyokuwa naifanya!

Kiukweli nilikuwa sioni faida yeyote ya ile hela kwa wakati huo maana nilijiona kama ni pesa ninayo ya kutosha hivyo kule nilienda tu kufanya kazi kama geresha tu!
Sasa niliamua kulivalia njuga suala la yule Maalimu aliyekuwa na maringo,Kuna dawa nilitengeneza hapo ndani na nikaiweka mfukoni nikaondoka zangu!

Ndugu zangu kwa ile dawa hakukuwa na kiumbe yeyote anayeitwa mwanamke ambaye alikuwa anachomoa,sema mimi na wanawake ilikuwa ni mbalimbali ila nilikuwa na dili na wale tu waliokuwa na nyodo na dharau!
Nilipofika shuleni niliendelea na shughuli zangu kama kawaida na nilipopata wasaa wa mapumziko nilimfata yule demu aliyekuwa kaumbika kila idara,nikamsalimia na aliitikia siku hiyo kwa uchangamfu kama wote!
Nilimuomba baadae atakapotoka taka kuondoka anipe lift na akakubali akasema "Ondoa shaka".
Sikuwa na wasiwasi maana nilijua huyu tayari ni wa kwangu!
Baadae nilipomaliza kufundisha kama kawa ilibidi nimsubiri na alipomaliza tuliondoka zetu akanibeba kwenye hicho kigari chake!

Tukiwa ndani ya gari sikutaka kupoteza muda nilimgusa mkono na palepale alisema "leo naenda kulala kwako", Nilimuuliza "Kwanini"?,Akaendelea kusema "Huwa nakupendaga muda mrefu sema hujuagi tu",nilitambua tayari kitu kimeshatiki! Kwa maana alikuwaga hanaga muda na mtu hasa ukizingatia kipindi kile nilikuwa nimechoka na isingekuwa rahisi kupendwa na mtoto mzuri kama yule!
Kwakuwa hapo kwenye hiyo nyumba niliyopanga kulikuwa na geti hivyo kuliwezesha lile gari lake kupata nafasi ya kupaki!
Ilikuwa mida ya jioni na wapangaji wenzangu walikuwa wakishangaa namna nilivyokuja na yule demu mkali,wengi walishangaa maana hawakuwahi kuniona pale nyumbani na demu yeyote!
Tulipofika nyumbani nilimwacha mi nikaelekea zangu kununua nyama ya kuchoma na viazi vilivyokaangwa(chips)nikamletea!
Mle ndani kwangu nilikuwa najitahidi kupaweka safi maana sikutaka yeyote afahamu kilichokuwa kinaendelea na nilihakikisha kile kibuyu nimekificha kimazingara hakuna yeyote aliyekiona ila mimi tu!

Kiukweli usiku huo yule mwanamke hatokuja kuusahau maana nilimkung'uta shipa la ki-mkakati na namna alivyokuwa mzuri nilihakikisha hatonisahau!
Asubuhi kulivyokucha alikataa kuamka kabisa na akasema kama nikufukuzwa kazi basi afukuzwe ila pale aondoki maana hajawahi kukutana na mwanaume kama mimi!,Nilimsihi sana tuende kazini lakini aligoma katakata!
Basi siku hiyo nzima tulichapana mle ndani bakora za hali ya juu na kiukweli nilikuwa sichoki maana nilikuwa nina uwezo huo!,Nilimchapa bakora sana na alishindwa kuamka kabisa akawa kama mgonjwa siku nzima hiyo!

Kuanzia hapo nilimtengenezea dawa yaani amsahau yule jamaa yake na aniwaze mimi tu lakini baadae nilikuja kuona anaweza kuwa mwendawazimu maana alikuwa kama kachanganyikiwa kwa ajili yangu!,Nililegeza kidogo na akawa anaenda kwake kama kawaida ila nilipomuhitaji nilimpata kwa wakati niliotaka mimi!

Yule jamaa wa Igoma mwenye nyumba alinipigia simu na akawa ananikumbushia kuhusu kile kiasi kilichokuwa kimebaki na nilimwambia ndani ya siku mbili hizo nitampa!
Kwenye begi nilikuwa nina milioni 15 hivyo pungufu ya kumpa mzee ilibaki milioni kumi na tano nyingine!,Na kwa wakati huo haukuwa mwisho wa Mwezi ambapo niingeenda kufanya tukio!
Basi nilimshawishi yule demu ticha amwambie mumewe ampe milioni kumi na tano,Kuna kitu nilitamka pale kwenye mkono wangu wa kushoto uliokuwa na ile Irizi ya kwamba amuombe yule bwana yake hiyo milioni kumi na tano aniletee na asihoji chochote!
Hivyo ndivyo ilivyokuwa!,Yule mwanamke alionekana sana kuchizika na mimi laki sikutaka iwe hivyo sana maana niliona ntampoteza!
Baada ya siku hizo nilizomuahidi mzee kweli nilimpelekea ile hela na kutakaandikishiana pale na nkakabidhiwa ile nyumba rasmi!

Kiukweli lilikuwa bonge la nyumba la kisasa na nikaona litanifaa sana kwenye shughuli zangu!
Hivyo nilijisema kwamba ikifika mwisho wa mwezi nikienda kupiga tukio pesa nitakayo ipata nitanunua kila kitu cha ndani na kuhamia huko Igoma.



Itaendelea...................
Shipa la kimkakati[emoji23]
 
Asee hii kitu kuna jamaa pia aliniambia
Mara nyingi mshirikina yeyote au mchawi akimuona mtu hata kama analindwa na Mungu yeye kwa akili yake anajua huyo mtu atakuwa na dawa kali kuliko zake!
Hakuna mshirikina anaeamini Mungu yupo,ila ataamini kuna mkali kuliko yeye tu, asante mkuu LwandaMagere leo nimepata ushahidi wa ulichosema hapo
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 21.


Inaendelea.............



Wakati nikiwa geto kwangu nilisikia sauti ikiniambia niende mkoa wa Mbeya,nikifika Mbeya nitapewa ishara ya nini cha kufanya!.Kwakuwa tayari nilikuwa nimeshaizoea ile hali ya kutoa kafara,kiukweli nilikuwaga siogopi hata kidogo wala sikuwa na wasiwasi.Wakati ule sikuwa kabisa na akili nyingine zaidi ya kuona nilikuwa nina faidi maisha,kila nilichokitaka nilikipata kwa wakati sahihi.

Basi nilijiandaa nikaweka mambo yangu sawa,nilipohakikisha kila kitu kipo sawa,niliushika mkono wangu wa kushoto uliyokuwa na irizi nikatamka "Ninataka niwe Mbeya eneo lililokusudiwa muda huu",ilikuwa ni kitendo cha kufumbua na kufumbua nikajikuta nipo Uyole,mkoa wa Mbeya!.Kiukweli ile irizi ambayo iliwekwa mkononi mwangu na yule Malikia ilikuwa na nguvu za ajabu,kipindi hicho ilikuwa ikinipa kiburi sana mpaka nikawa nawaoana binadamu wenzangu kama takataka.Namshukuru sana Mungu kwa kunitoa huko,Mungu wetu ni mwema sana,uwezo,upendo,rehema na fadhili zake hazina mwisho.Basi nilipofika hayo maeneo ya Uyole,kuna gari niliiona ilikuwa costa,hiyo costa ndiyo niliyoambiwa kwamba,waliomo ndani hapaswi kupona mtu,ndiyo gari ambayo ilipaswa nikaiangushe ili nitoe kafara,hiyo gari ilipofika maeneo nilipokuwa nimesimama,konda akawa anasema "Kyela hiyooooo,twenzetu Tukuyu mpaka Kyela hiyoooooo!".

Nilipanda ndani ya ile costa na kama kawaida sikulipa nauli,yule konda hata hakuniuliza kuhusu nauli.Sasa ile gari ilifika kwenye mji mmoja ulikuwa unaitwa Kimo,huo mji wa Kimo ulikuwa kabla ya kufika Tukuyu!,ile sauti iliniambia nishuke kwenye gari halafu niendee mbele ya Tukuyu kuelekea Kyela nikaisubiri.Nilifanya kama ile sauti ilivyonitaka nifanye,niliposhuka tu kwenye ile gari nilipotea ghafla yale maeneo na hapo Kimo nikajikuta nipo eneo la tukio,Kiukweli hilo eneo ambalo ilipaswa nitoe kafara kulikuwa na mteremko mkali sana,sikumbuki yalikuwa maeneo gani maana kulikuwa na miti mingi sana ya mbao hilo eneo,nadhani ilikuwa ni hapohapo Tukuyu,sikuweza kupafahamu kwasababu ya ule msitu.Ila mkoa ulikuwa ni Mbeya,wilaya ya Rungwe,mji wa Tukuyu.

Basi nilipofika hilo eneo niliweka tego kama kawaida,mkononi wakati huo nikiwa nimeshika kibuyu kwa ajili ya damu,baada ya kusubiri kwa muda niliiona ile costa ikiwa inakuja kwa mwendo wa kasi sana,ilipofika lile eneo nililoweka ile dawa ya tego,ile gari ilihama njia ikaelekea kwenye lile shamba la miti ndipo ilipopata ajali mbaya sana.Nilisogea taratibu kwenda kuanza kuchukua kilichonipeleka huko,lakini nilipotaka tu kuanza kuchukua damu za watu waliyokuwa wamekufa,ghafla niliwaona akina mama wawili ndani ya ile gari wakiwa wananiangalia sana,kisha wakaanza kuniambia "Wewe mtoto unafanya nini?".

Wale kina mama walikuwa wachawi na watu wengine walipokuwa wamelaliwa na viti wao walikuwa wamekaa wakinikodolea macho,na yaelekea huko walipokuwa wakienda walikuwa wanaenda kwenye mikutano ya kichawi,waliniita mimi mtoto si kwamba umri wangu bado ulikuwa wa kitoto,la hasha! bali walionyesha dharau kwamba mimi sikuwa na chochote cha kuwafanya,kwa maana nyingine ni kwamba uwezo wangu ulikuwa mdogo.Niliwaambia kwakuwa waliniita mimi mtoto,wao ndiyo ningekuwa wa kwanza kuchukua damu zao na kuweka kwenye kibuyu,walidhani natania lakini nilikuwa siwatanii hata kidogoo,nilitaka niwaonyeshe ya kwamba sikuwa mtoto kwenye ile kazi,Kama nilivyosema hapo awali kwamba nilikuwa nina uwezo wa ajabu na kiburi kilikuwa kimenijaa sana kipindi hicho.Niliwasogelea na kuanza kushindana nao kichawi,nilipoona wanataka kunipotezea muda,nilitamka ya kwamba "Naomba mkauke muwe kama mkaa",haikuchukua muda walikuwa wamekauka kama mkaa,Wao ndiyo niliyoanza nao,baada ya hapo nilianza kukusanya damu za abiria wengine na kuzitia kwenye kibuyu,nilipomaliza kufanya lile zoezi nilipotea yale maeneo,nikatokezea lile eneo nililokuwepo mwanzo la Uyole!.

Basi kwakuwa nilikuwa nina njaa,niliingia kupata chakula kwenye mgahawa mmoja ambao ulikuwa mkubwa kama hoteli,sasa ile nimeingia ndani ya huo mgahawa niliona kuna mama na binti walikuwa wakitoa huduma hapo hotelini wakiwa uchi kama walivyozaliwa,alikuwa mwanamke mmoja mnene na binti yake ambaye pia alikuwa uchi.Sasa kitu kibaya zaidi ni kwamba,huyo binti yake yeye alikuwa akivuja damu kwenye sehemu yake ya siri (uke),zile damu alikuwa akizichukua na kuzipakaza kwenye vile vyakula vya wateja walivyokuwa wamemwagiza!.Aisee ile hali sikuwahi kuiona mahali popite pale,ndiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza kushuhudia ule uchafu,kwa bahati mbaya sana hakuna mteja ambaye alikuwa akiona yale matukio yote isipokuwa mimi niliyekuwa na uwezo huo.

Huo mgahawa ulikuwa umechangamka sana maana hadi madereva wa magari makubwa niliona walikuwa wakiingia kula pale!,ukimuondoa yule mama na yule binti niliyewakuta uchi,pia kulikuwa na wahudumu wengine wawili,mmoja alikuwa mpishi na mwingine pia alikuwa akihudumia lakini hawa wao walikuwa wamevaa nguo zao za kawaida,na walikuwa hawaelewi chochote,wateja wengi walikuwa wakiingia kwenye ule mgahawa wao walikuwa wakiwaona wamevaa nguo,kumbe haikuwa hivyo.Sikupata shida kuelewa kwamba yule mama ndiye alikuwa mmiliki wa ule mgahawa na yule aliyekuwa akivuja damu ukeni alikuwa binti yake wa kumzaa!.Yule mama aliponiona alinifanyia ishara ya kidole mdomoni,kwamba nikae kimya!Yule binti aliyekuwa akivuja damu alikuwa akinitolea macho sana,nilimuona anakuwa na wasiwasi mkubwa!,uenda alidhani nilikuwa nimeenda pale kuwafichua.Basi nilimuita yule mwanamke nikamwambia aniletee chakula ila kiwe kisafi,tofauti na hapo ningemuumbua!,alimuita yule binti aliyekuwa kavaa nguo akamwambia "Mpe yule kaka chakula".

Zilikuja ndizi na nyama zikiwa zimejaa sahani,kabla ya kula nilianza kukiangalia kile chakula kama kilikuwa kisafi ama la!,baada ya kujiridhisha kwamba kilikuwa kisafi kwa maana kwamba hawakuweka mambo yao ya kishirikina nilianza kula!.Wakati nakula watu wengi walikuwa wakiingia kupata msosi wakiamini ni msosi mtamu kumbe yule binti alikuwa akichanganya na damu zake zilizokuwa zinatoka ukeni!.Sasa Wakati nikiwa bado naendelea kupata msosi aliingia jamaa mmoja akiwa na mwanamke,bila shaka alikuwa mtu na mke wake,walipotengewa chakula kabla ya kula walifanya ishara ya msalaba,nadhani walikuwa wakiombea kile chakula,ile ishara ya msalaba haikusaidia kitu kwani walilishwa uchafu kama wenzao!.Ule mgahawa ulikuwa na wateja wengi sana,yule mama kama ni pesa basi alikuwa akizipata ki kwelikweli!.

Ndugu zangu ukiamua kuwa mfuasi wa Kristo basi achana na mambo mengine ya duniani vinginevyo unaweza ukadhani Yesu anakulinda kumbe hakuna,yule jamaa aliyeingia kwenye ule mgahawa na mkewe,ilionekana walikuwa wakimpenda sana Yesu kwa maneno ila matendo hakuna!,Kiukweli wangekuwa watu wa maombi wasingelishwa ule uchafu,lakini kwasababu wengi wetu dini tumezifanya kama fasheni ilikuwa haijawasaidia kitu,ukiamua kuwa mtu wa dini,ni vema ukawa mtu wa dini,lakini ukiamua kuwa mtu wa kidunia,ni vema ukawa mtu wa kidunia.Inapaswa uchague moja ambalo utasimama nalo,mimi mwenyewe kuna wakati nilishindwa kufanya tukio lolote la ushirikina kwasababu kuna watu niliyokutana nao wakiwa na nguvu ya Mungu,nilishindwa pamoja na ujanja wangu wote!.Hivyo watu wengi waliyolishwa kile chakula chenye uchafu,hawakuwa na ulinzi wa Mungu hata kidogo.

Baada ya kumaliza kula niliondoka zangu bila kulipa,yule mama aliniita kabla ya kuondoka akaanza kuniuliza "Vipi mwenzetu wewe niwa nchi gani?".

Nilimwambia "mimi natokea Kigoma na hapa nilipo nipo safarini kurudi kigoma?".

Yule mwanamke alikuwa akinishangaa sana namna nilivyokuwa jasiri,wakati huo naongea naye alikuwa uchi kama alivyozaliwa ila watu wengine walikuwa wakimuona amevaa nguo!.Nipomaliza kuzungumza naye nilimwambia mimi naondoka zangu.Basi niliukamata mkono wangu uliyokuwa na irizi nikatamka kama ambavyo nimekuwa nikifanya,ndani ya sekunde nilijikuta nipo geto kama kawaida,ndipo nilikiweka kile kibuyu chini ya uvungu,nilijipumzisha kidogo kisha baada ya kuamka nilielekea nyumbani kwa mama kupata chakula.



Itaendelea......................
 
Wakuu habarini za kazi

Kuna jamaa kanifata inbox kaniambia nisimalizie kusimulia hiki kisa kwani anataka kunipatia hela halafu yeye akinunue akiandike kwenye kitabu hivyo nikisimulia chote anaweza akakosa wateja!,Bado hajanambia anataka kunipa bei gani ndo namsubiri anieleze vizuri!

Nyie ndugu zangu mnaonaje?
Au ndio yule tajiri wa tegeta ameanza kuminya uhuru wa habari mkuu😂
 
Back
Top Bottom