Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mimi ni mtumiaji wa telegram mzuri tu shida kwanini asingezichangisha hapa hapa?? Sababu telegram ameweka kwenye private group au channel angefanya hivyo hapa pia ukituma iyo buku unatupiwa episode pm. Mambo ni yale yale sema ana agenda ya siri
Alikuwa na lengo la kimkakati,kwan angesema tuchange si tungempa
 
Sikieni ambae anaona telegram miyeyusho anaweza kununua vocha ya jero aipige picha anitumie PM na mie nitazicopy kule episodes zote alizopost kule halafu nazipaste kwenye pm yake maana sasa hivi kaishampa shipa la kimkakati Zainati shombe shombe na Yusra pisi kali sana na kaishamuweka kwenye rada shemeji kingine kizuri zaidi katutajia ule mti wa kunywea na chai kiufasaha
Acha utoto wa kuharb mipango ya mwenzeo sijui mshamba wa wap ww
 
Inaendelea.............MWISHO


Wakuu habarini za Asubuhi,Bila shaka mko vyema mkiendelea na majuku kama kawaida!

Nimepitia comment nyingi na wengi wanalaumu mimi kurefusha uzi na kuandika kwenye stori yasiyotakiwa,Labda niseme niliamua kuandika hivi ili nieleweke wapi nilipotoka na mikasa niliyokutana nayo kwenye maisha!,Lengo la kuandika kila nilililokutana nalo kwenye huu mkasa wa kwanza ni kutoa picha na uelekeo wa mkasa wa pili ambao ni Maisha ya Yangu ya kutafuta Utajiri ambao ndani yake kuna safari ya kutisha na kugopesha!,hivyo niliona nifanye hivi ili huko mbele kwenye mkasa wa pili maswali yapungue!

Sasa kwakuwa watu wanaona kama narefusha stori ngoja niikatishe ili ikiwezekana leo leo au kesho niianze kusimulia mkasa wa pili wa Maisha yangu dhidi ya utafutaji wa maisha mazuri uliogeuka shubiri!(HAKUNA SHOTI KATI YA MAISHA,MAISHA NI KUPAMBANA KIUHALISIA)

Inaendelea...........

Japo hamkutaka nimalizie story yote lakini humo katikati niliwahi kuitwa mwizi na ilikuwa ni vurumai!


Basi bana nadhani mnakumbuka niliwaambia kwamba mauza uza pale nyumbani "YALIKUWA LIKIZO KWA MUDA",Siku moja Mzee alirudi kutoka Dar es salaam alipokuwa amehamishiwa kikazi na hatukujua ni nini kirimrudisha hapo homu ghfla hivyo!
Nadhani niliiwaambia kuna siku aliaga akasema anaelekea kwa rafiki yake mmoja Utegi!,Kumbe kule UTegi hakwenda kwa rafiki yake wala nini bali alikuwa kaenda kwa Mganga wa kienyeji,Kwa taarifa tulizozipata pale nyumbani ni kwamba,kipindi kile alipo enda kwa huyo mganga hakumkuta na ikabidi amsubiri pale nyumbani kwa mganga ambako muda huo kulikuwa na wasaidizi wake tu!

Kwahivyo Mzee ilibidi Amsubiri yule Mganga kwa muda kama wiki nzima lakini halikuwa hakurudi maana alikuwa kaenda kuagua mahala pengine, ndipo Mzee ilibidi arudi nyumbani kujiandaa na Safari ya Dar es salaam!
Sasa kumbe ule ujio wa mzee inaonekana aliwasiliana na huyo Mganga na akamwambia safari hii aende atamkuta!,Basi Mzee baada kama ya siku tatu akaondoka na kauli yake ile ile ya anaenda kuonana na rafiki yake kule Utegi!,Kweli tumekaa pale nyumbani siku hiyo ikapita na siku iliyofuata nakumbuka ilikuwa kama mida ya 10 jioni mi narudi zangu maskani kutoka Shule naingia Ndani nakutana na kikao hapo sebuleni,Alikuwepo Yule mama mdogo pamoja na Masista wakizungumza!,Ndipo nilipoambiwa Muda si mrefu Yule kiumbe wa Ajabu Ashura alikuwa hapo na katoka kuwaambia kila kitu alichokuwa anakifanya Mzee na safari ya yeye kwenda Utegi,sasa kabla ya Ashura kuondoka aliwaambia wajiandae kufanya msiba maana Mzee Atarudi na hatomaliza siku pale nyumbani!

Kiukweli mimi nilidhani ni kama maigizo lakini ndivyo ilivyokuwa,Maana Ashura aliwahi kusema yeyote atakayejifanya kwenda kwa mganga kwa ajili yake ina maana alikuwa anataka kumuua yeye au kumsababishia matatizo kutoka kwa ndugu zake ikiwemo kuuliwa!,Akasema sasa kabla ya yeye hayo hayajamkuta inapaswa huyo anayetekeleza huo ujinga afe yeye kwanza!,Pia aliwahi kusema ni marufuku kuomba au kusoma vitabu Vitakatifu,Hili agizo walitoa wale waliokuwa wanafahamika kama wazazi wake!

Basi bhana baada ya siku kadhaa mzee alireje a pale nyumbani na Masista walimsimulia yote yaliyosema na Ashura na Mzee akawaambia" nilienda huko kwa ajili yenu wanangu,na kwa ajili ya kazini kwangu"!
Mzee akimaliza siku hiyo bali damu zilianza kumtoka puani kama maji,Sista mkubwa ilibidi ampigie simu Mama na kumuleza hali namna ilivyokuwa!
Lakini ndugu zangu mpaka Bi mkubwa anarudi nyumbani ndipo alikuta tayari kuna Msiba wa Mzee (R.I.P),Mzee alizikwa kwenye makaburi ya Ronsoti(Wenyeji wa Tarime watakuwa wanayafamu),Kiukweli hali ilikuwa mbaya sana na ukizingatia mzee tena ndo alikuwa nguzo ya familia na Mzee wetu kidogo alikuwa na vipesa vya hapa na pale maana kwa wakati huo kukaa maeneo hayo ya Bomani haikuwa kazi nyepesi sana!,wakazi wa Tarime nadhani watakuwa wanaelewa vizuri hayo maeneo!

Basi baada ya Msiba wa mzee ni kama familia nzima ilikumbwa ni mikosi maana Maza nae ile kampuni yao ya ujenzi aliyokuwa akifanyia kazi ni kama ilifilisika,sikujua ilikumbwa na nini maana kipindi kile sina ufahamu sana wa haya mambo ya kufilisika,Lakini Bi mkubwa alisimama kwenda kazini!

Maisha yalivyozidi kuwa magumu kuna yule Shangazi yetu aliyekuwa akikaa mwanza alimshauri Bi Mkubwa atafute pesa na akafanye biashara huko Mwanza!,Bi mkubwa wazo la kuuiuza ile nyumba yetu lilimjia na ndipo alipotuita wanae wote pamoja na yule aliyekuwa kwa Shangazi Mwanza na akatushirikisha na sote tulikubaliana ukizingatia Nyumba yenyewe ilikuwa na Mauza uza,mpaka wakati huo hakuna ambaye alielewa mauza uza ya pale nyumbani ila ilikuwa ni siri ya familia!

Ndani ya siku kadhaa mwaka huohuo ilibidi mimi sasa nitafutiwe uamisho wa kuelekea kusoma Mwanza na kiukweli sote tulihamia Mwanza,sikutaka kufahamu ile nyumba aliuziwa nani na ilikuwaje,mi nilichojua ni kwamba Tumehamia Mwanza na maisha ya Mwanza yakaanza kama kawaida!

Ninapoandika hiki kisa Bi mkubwa Tayari pia ni Marehemu,Mimi ninaishi Dar es salaam now,Dada yangu Mkubwa yupo hapo Mwanza kaolewa na Yule Sista Mdogo nae yupo Arusha kaolewa!


............................................................


Sasa kabla ya kuuanza Mkasa wa pili wa mimi kwenda kuusaka utajiri na chanzo chake kikiwa ni dharau na maisha magumu,naomba niruhusu maswali kama yapo ili nikianza kisa cha pili ni kupepea tu!

Karibuni kama kuna maswali
Pole sana mkuu kwa kuondokewa na wazazi.
Vipi mauzauza yalikoma baada ya kuamia Mwanza?
 
Mimi ni mtumiaji wa telegram mzuri tu shida kwanini asingezichangisha hapa hapa?? Sababu telegram ameweka kwenye private group au channel angefanya hivyo hapa pia ukituma iyo buku unatupiwa episode pm. Mambo ni yale yale sema ana agenda ya siri
Mkuu naomba kuuliza.. mi sipo bongo vp nikitumia iyo telegram iyo buku anayotaka nitamtumia vp?
 
Ushauri kwa LwandaMagere we si upo mwanza mzee mtafute basi zabroni mwita akusaidie mtoe kitabu bila shaka wengi wana mjua ana kitabu cha sitoisahau gamboshi Maana ye alishachukuliwa na wachawi na kupelekwa ukogamboshi ila mungu mwema alifanikiwa kurudi duniani mzee kitabu hiki utapga pesa ndefu zabron alishapata mpaka m 100 na machenchi kupitia ushuhuda wake. kwa hicho kitabu chake alafu hapa usiache kusimulia, maliza na ukitoa kitabu utapiga pesa mim nimesoma kitabu chake zabron alinitumia kwa wasap through hard copy lakini pia kuna Chanel ipo YouTube ya davistar mata media story take ipo furu mpka zabron mwenyewe unamuona akisimulia na ameshawai simulia redio free Africa hii sitosahau gamboshi wengi humu wanamjua juzi kati ndio kamalizia story yake. Kwaiyo zabron alisimulia story yake ya maisha na akatoa na kitabu so asikuzie mtu kusimulia eti kisa autauza kitabu waongo, izo pesa sasa ndio utapata kwenye hiki kitabu. NB sija tangaza biashara ya mtu nimetoa ushauri kwa mshkaji maana naweza pokea mapovu kibao kwa watu ambao sio waelewa, ZABRON anafahamika na wengi wana mjua na hii story ya sitosahau GAMBOSHI mpaka boss wa publish jina kapuni ambae anajulikana kwa hadithi nyingi gazetini alitaka kumtapeli ambae saiz ni muheshimiwa mkubwa tu mjiongezee na bila shaka msha elewa ndio ivyo mzee ushauri wangu kwako.
Nilisoma Part One ya "Sintosahau Gamboshi" sijabahatika kukipata Part Two....

Hakika Zabton alipiga hela ndefu kwani wengi tulokisoma hapa JF, ilibidi tutafute na hardcopy...
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 5


Inaendelea.............


Asubuhi kulipokucha ilitubidi tuamke Asubuhi ya saa 12 maana tuliambiwa kupata magari ya huko Bukima ni mpaka tupitie Musoma,Tulifanikiwa kuondoka mimi na Huyo dogo Mtoto wa Ma mdogo!,ilibidi tukae barabarani kusubiri Hiace zinazoenda Musoma,Kiukweli mimi mpaka wakati huo nilibaki na 48000/= tu,Nauli ya kutoka Bunda kwenda Musoma kwa wakati huo ilikuwa 3000 hivyo nilivyolipia naulia ya watu wawili nilibakiwa na 42000/=,Basi safari ikaanza na ilituchukua kama lisaa kufika Musoma,Hiyo ilikuwa yapata kama saa 2 kasoro dakika kadhaa!
Tulipofika pale stendi ya Musoma hatukutaka kupoteza Muda maana tuliambiwa hapo huwa kuna gari moja la kuelekea Huko Bukima na endapo tungelikosa ingetubidi tulale!,Kweli!,kuna basi moja tulikukuta pale stendi likiwa limechoka sana!,ilikuwa ni aina fulani ya magari ya zamani!,ilibidi niulizie nauli!,Konda akasema nauli ya kutoka Musoma Mpaka huko tunakoenda ni 5000 maana barabara si nzuri!,Ila akatuambia ili gari lenyewe linaitishia njiani na akasema kuna kijiji kinaitwa MRANGI ndo wao wataishia hapo!,Ilibidi nimuulize kwani kutoka hapo nyinyi mnapoishia na huko Bukima kuna umbali gani?,Jamaa alisema si mbali ila tungefika hapo angefanya namna ili sisi tuendelee na safari!,Jamaa alisisitiza sana kwamba kwa wakati huo pale stendi hakukuwa na gari lingine la kuelekea huko!

Sasa kwasababu sisi hatukuwa wenyeji nilimwambia dogo ngoja nilipe nauli twende zetu maana tunachoenda kukifata ni kikubwa sana kuliko kitu chochote!,Basi nilitoa elfu 10000/= nkampa yule konda,Baa ya kumpa akasema gari itaanza safari mida ya saa 5 Asubuhi hivyo kama mnazunguka nyie zungukeni ila msiende mbali sana!
Kwakuwa tulitoka homu Bunda Bila kupata chochote kitu nilimwambia dogo twende tukatafute sehemu wanauza chai tunywe!

Kwa bahati nzuri tulipozunguka tu nyuma kidogo ya stendi kuna mama tulimkuta akichoma vitumbua,hivyo tulikaa hapo tukaagiza na chai tukaanza kunywa!,mpaka hapo mfukoni nilibaki kama 30000/= maana hapo kwenye chai tulitumia kama 2000/=,Basi baada ya kupata chai na vitumbua nikamwambia dogo tusikae sana mbali maana hatukuwa wenyeji hapo Musoma,Hiyo ilikuwa mida ya saa 3 Asubuhi hivyo tulikuwa kama na masaa 2 mbele!,Masaa yaliposogea ilibidi na sisi tusogee kwenye gari na baada ya muda ule alotuambia konda kufika!,kweli! gari lilianza kuondoka,watu walikuwa wengi kwenye gari na wengine walisimama na kiukweli nilisema yawezekana gari lilikuwa lile tu maana yangekuwepo mengi basi watu wasingesimama!

Ilikuwa ni safari ya muda mrefu kidogo,Kuna jamaa nilimuuliza hiyo safari huwa inachukua muda gani hadi kufika,Jamaa alisema kutokana na gari kusimama simama njiani ni Takribani kama Masaa 2 : 30,Baada kama ya masaa 3 na ushee gari lilifika mwisho na baada ya kuuliza tuliambiwa hapo ni sehemu moja ambayo bado naikumbuka jina ilikuwa inaitwa Mrangi!,Basi tulitelemka pale na nkamfata dereva nkamueleza kwamba sisi tulikuwa tunaenda Bukima na yule jamaa aliyekuwa anakata tiketi alituambia tukifika hapa angetufanyia namna ya kufika huko Bukima!
Yule dereva alisikitika sana "Yule jamaa ni mpumbavu,kwanini hakuwaambia kwamba kuna Hiace ya Bukima?",Jamaa akaendelea kusema kwamba "Maana kutoka hapa mpaka Bukima bado kuna umbali,lakini subirini kuna watu hapa niongee nao huwa wanakodisha baiskeli kama vipi wawapeleke,japo itachukua muda maana ni mbali"
Ilibidi tuwe wapole maana tayari tulishaingizwa cha kike na yule Mpiga debe tuliyemkuta akikata tiketi,Kumbe nia yake ni sisi tulipe ili yeye apate posho!,Tufike au tusifike hilo lilikuwa halimihusu tena!

Jamaa alituitia vijana wawili pale na akaanza kuongea nao kwa Lugha ya kwao,nadhani ilikuwa ni Wajita,Basi wale jamaa wakamwambia jamaa kwa ki-lugha kwamba tuwalipe 5000 wote wawili!,Hatukuwa na namna ilibidi niwape ile hela na wakatuchukua mimi na dogo kila mmoja kwenye baiskeli yake na safari ikaanza,Hiyo ilikuwa yapata kama saa 9 Alasiri!,Basi safari ilikuwa ndefu kidogo na tuliingia Hapo Bukima mnamo saa 10 kasoro kuelekea 11!

Tulivyofika hapo Bukima hatukupoteza Muda ilibidi sasa tuanze kumuulizia yule Mganga tuliyeelekezwa na yule Dingi wa Bunda!,Kwa bahati nzuri hakuwa mgeni sana pale Bukima maana ule mji haukuwa mkubwa bali ilikuwa kama ki-center fulani hivi!,Basi tukianza safari ya kuelekea kwake tukiongozwa na dogo mmoja tuliyemkuta pale center ya Bukima!,Kwa kuwa tulikuwa wageni watu walikuwa wakitushangaa,nadhani kwakuwa ilikuwa center ndogo hivyo watu au wenyeji wengi wanafahamiana!Hivyo ukiwa mgeni ilikuwa ni rahisi sana kufahamika!,yule Mzee(Mganga),Tulifika kwake na alikuwa akiishi nje kidogo ya center na ilikuwa karibu na ziwani,maana ulikuwa ukikaa nje ya nyumba ya Huyo mzee ziwa lilikuwa kama mita 300 hivi!
Tulimsalimia Mzee na tukajitambulisha kwake!,tulimweleza ya Kwamba tuliagizwa kwake na Mzee yule wa Bunda,kiukweli alionyesha kumfahamu yule mzee na alikuwa akituuliza hali yake vipi!

Basi baada ya mazungumzo kadhaa hapo ilibidi tumueleze kilichotupeleka hapo kwake!

Baada ya kutusikiliza kwa muda mrefu alituambia ya kwamba kuna watu fulani waliwahi kwenda hapo kama miaka 2 iliyopita na wao walikuwa wakitafuta zile pesa zilizokuwa na tundu katikati,kwakuwa kwa wakati huo alikuwa nazo ilibidi awape na walimpa pesa!,Sasa sisi alituuliza endapo hiyo shilingi 100 ya Mwaka 1993 ingepatikana tungempa kiasi gani?,Kiukweli Moyo ulipiga Paaah!mawazoni nilikuwa naamini ya kwamba sasa naenda kuuaga Umasikini na utajiri ulikuwa ushafika mlangoni,kazi iliyokuwepo ni kufungua tu mlango uingie ndani!
Nilimwambia mzee endapo tungekipata hicho ki hela basi tungempa laki 200000/=,Yeye alituuliza "Nyinyi mkikipata mnaenda kupata bei gani"?,Ilibidi nimdanganye Yule Mzee ya kwamba sisi tumeambiwa tukikipeleka tunalipwa milioni moja hivyo endapo tungekuwa wewe hiyo laki 200000/=,sisi tungebaki na laki 800000/=ambayo tutagawana na mwenzangu maana kuna gharama pia zimetumika mpaka kufika hapo!

Basi yule mzee alisema funguo za Sanduku ambamo zime hela mbalimbali za miaka ya nyuma anazo mke wake ambaye kwa wakati ule hakuwepo,Alituambia tumsubiri na akatusihi ya kwamba kwakuwa jioni ilishaingia hatuna budi tulale pale!,Basi mimi na dogo ilibidi twende ziwani tukashangae shangae huku tukibadilisha mawazo!,Ilipofika saa 12 jioni tulirudi hapo nyumbani kwa huyo mzee na siku hiyo yule mzee alichinja Bata kwa ajili ya kitoweo!
Yule mzee kiukweli sikuona uganga wowote alokuwa nao maana hata pale kwake hatukukuta watu bali walikuwa watu wa familia yake!,Nadhani kama alikuwa mganga basi ni wale wasiyokuwa na mbwembwe nyingi!

Jioni ile Mkewe alirudi akiwa na baiskeli kafunga mzigo nyuma na alipokewa na kijana wake mmoja tulimkuta pale!,Kwakuwa sasa usiku ulishaingia Mzee alituambia zoezi litafanyika kesho Asubuhi!,Basi usiku ule tulipata zetu ugali wa muhogo na Bata,kiukweli Msosi ule ulikuwa umeenda skuli kwa namna ulivyokuwa na kiwango!,Baada ya chakula ilibidi kile chumba alichokuwa kuwa analala yule kijana wa yule mzee tulale sisi na yeye nadhani alienda kulala kwa jirani au rafiki!,Siunajua tena mambo ya vijijini suala la wapi pa kulala huwaga halisumbui!Siyo kama mjini!

Itaendelea...................
story inogile
 
Stori hatari wakuu nawasii mjiunge na group la VIP Kuna Mambo muhimu mnayakosa amabayo yangewafaa ktk maisha haya ya kawaida.

Ushuhuda wa kiwango Cha lami aisee.
 
Stori hatari wakuu nawasii mjiunge na group la VIP Kuna Mambo muhimu mnayakosa amabayo yangewafaa ktk maisha haya ya kawaida.

Ushuhuda wa kiwango Cha lami aisee.
Mkuu mi natamani kweli niendelee kuisoma story sema nipo nje ya Bongo Sijui nitumie njia gani kuituma iyo buku
 
Back
Top Bottom