Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

MKASA WA PILI - Sehemu ya 8


Inaendelea.............


Tulitembea kwa muda wa saa moja na nusu hivi tukawa tumefika hayo maeneo ya Butiama,Kumbuka tulitoka Kiabakari kama saa 4,Hivyo ukijumlisha hayo masaa tuliyotumia mpaka hapo Butiama ni kama masa 5 :30,Kwakuwa kipindi tupo Kiabakari yule mama muuza ndizi alituambia kwamba tukifika hayo maeneo ya hapo Butiama tuulize mtu yeyote atuelekeze njia ya kwenda Ikizu!

Basi kuna jamaa tulikutana nae pale na tulimuuliza atuelekeze njia ya kwenda Ikizu,Yule jamaa kuna njia alituonyesha ambayo ilikuwa inapitia porini,Hakukuwa na mapori makubwa sana bali ilikuwa ni vichaka tu na mashamba ya watu!,Nilimuuliza kutoka hapo Butiama mpaka Ikizu kuna umbali gani?
Jamaa alituambia wala si mbali maana wao walishazoea kwenda na Baiskeli na kwakutembea ingetuchukua kama masaa 3 na nusu au 4!,Basi yule jamaa kuna njia alituonyesha akatuambia nyie fuateni hii njia na mkifika huko mbele mtakuwa mnauliza watu watawaelekeza!

Kabla ya kuanza safari ya kutoka hapo Butiama nilimpigia yule Mganga nkamwambia ndo tumefika Butiama na yeye akasema kumbe hatukuwa mbali sana!,Alituambia tujitahidi taratibu tutafika!
Nilimpgia mama Bi mkubwa pia na tukasalimiana na nkamweleza namna ilivyokuwa na Nkamwambia na mahala tulipo,Kauli ya bi mkubwa mara zote ilikuwa ni kunisisitiza niwe makini!,Basi tulianza mdogo mdogo kuitafuta njia ya Ikizu!

Zile ndizi ambazo dogo alikuwa kazibeba kwenye mfuko ilibidi sasa na mimi nimsaidie maana niliona kama kaanza kuchoka!
Wakati tukiwa tunatembea yule Jamaa Mkenya aliyetupatia hiyo dili alinipigia simu na akawa anataka kujua ni nini kinaendelea,Nilimwambia bado tunaendelea kutafuta na endapo ikipatikana basi tutamjulisha haraka iwezekanvyo!
Jamaa alinambia kwa wakati huo naongea naye alikuwa Mwanza na kuna bosi wake ameenda kumpokea maana kuna dili nyingine pia walikuwa wanafuatilia!,Nilimwambia asiwe na shaka!

Safari ilisonga sana tukipita milimani na mashambani ambako tulikuwa tukielekezwa na kila tuliyekutana nae!,Kuna mahali tulifika kulikuwa kuna mti wa Mkwaju ikabidi dogo aniambie tupumzike kidogo!,Basi tulipumzika pale na tukaanza tena kula zile ndizi mpaka zikaisha!,Kiukweli zile ndizi zilikuwa kubwa na tamu hivyo tulishiba!
Ishu sasa ilikuwa ni kupata maji ya kunywa!

Nilimwambia dogo tumepumzika vya kutosha hivyo hatuna budi kusonga mbele!,Tulifika maeneo fulani kulikuwa kumechangamka kidogo na kulikuwa wanapiga muziki fulani hivi wa kilugha!,Kumbe maeneo hayo kulikuwa na harusi!,Bila shaka harusi za vijijini wengi wetu tunazifahamu maana kulikuwa kumefungwa spika zile za vipaza sauti na mziki ukipigwa kama kawaida!

Basi dogo akanambia tutafute mji au nyumba yeyote hapo tuombe maji ya kunywa!,Tulitafuta nyumba zilizokuwa pale jirani kuna mama mmoja hivi tulimsalimia na tukamwomba maji ya kunywa!,Yule mama alituuliza "Nyinyi ni wageni haya maeneo"?,Nkamwambia "Ndiyo mama",Yule mama akasema ametuuliza kwasababu ameona sura si za hapo kijijini,Yule mama alituletea maji na baada ya kunywa nilimuuliza Kutoka hapo mpaka Ikizu bado kuna Umbali gani?,Mama alituambia kwamba si mbali bado kidogo tufike na alituambia tuifuate ile ile njia!

Baada kama ya masaa 4 tulifanikiwa kufika hapo Ikizu!,Ulikuwa ni mji au kijiji kilicho changamka kidogo!,Dogo aliamua kukaa chini maana alikuwa kachoka,Basi nilimpigia simu yule Mganga na tukamweleza tulipokuwa na akasema bado hatujafika kwani hayo maeneo tulipokuwa panaitwa Nyamuswa,alituambia tutembee tena kidogo kama nusu saa hivi tukifuata barabara tutafika Ikizu!

Nilimwambia dogo safari bado inaendelea!,Dogo alinyanyuka lakini alionekana kuchoka na ikabidi tuendelee na safari!

Kweli Baada kama ya dakika 45 hv tukafika hapo Ikizu na tulipofika nilimpigia tena simu huyo Mganga akatuelekeza kuna maeneo tusimame na akaja hapo kutuchukua!

Tulifika hapo Ikizu mida ya saa 11 jioni n kiukweli yule dogo alikuwa kachoka sana,yule Mzee alituchukua kuelekea kwake ambako nako kulikuwa nje kidogo ya mji wa Ikizu!

Tulipofika hapo kwake kulikuwa na watu wengi kidogo inaelekea wale watu walienda kufata tiba pale!,Basi baada ya muda mzee alituambia alishindwa kutuambia wakati tupo barabarani tunaenda maana ingetukatisha tamaa!,Mzee anasema hiyo hela alikuwa nayo ila kuna kipindi alikuja pale Mdogo wake inavyoonekana aliondoka na hayo ma-hela ya zamani maana yeye alikuwa na muda hajakagua kwenye masanduku yaliyokuwa na hizo hela maana hakuwa na kazi nayo!

Basi ilibidi nimuulize huyo Mdogo wake anapatikana wapi?,Mganga alituambia Mdogo wake huyo sasa hivi anaishi Ukerewe ila akasema kwakuwa simu yake haikuwa na salio nikamnunulie vocha ampigie!,Kwakuwa simu yangu ilikuwa na dakika za kutosha ilibidi nimpe ampigie huyo mdogo wake!,kweli Mungu saidia huyo mdogo mtu akapatikana na wakaanza kuzungumza,walizungumza kwa muda kidogo na baada ya Mazungumzo mzee alirudi tulipokuwa tumekaa!

Yule Mzee alituambia yule Mdogo wake anasema hiyo hela tunayoitafuta sisi ipo ila yeye katoka yupo Ukerewe ila inabidi twende Bunda jiarani na Chuo cha ualimu kuna mwanamke wake yupo hapo nyumbani tutamkuta na atampa maelekezo yote na tukifika hapo akishatuonyesha hiyo hela inapaswa tuache hiyo hela tuliyokubaliana 300000/=ndipo tuchukue hicho ki-hela!

Kiukweli nilifurahi sana na nkapata nguvu mpya japo hatukujua kutoka hapo kwenda Bunda tunafikaje maana tulikuwa tumechoka sana na giza tayari lilishaanza kuingia maana ilikuwa saa 12 kuelekea saa 1 usiku!

Nilimwambia Dogo usiku ule tungelala wapi na kula wapi maana tukiangalia pale kwa mganga kulikuwa hakuna uelekeo wa kulala na kula maana kulikuwa hakueleweki!,Dogo alinishauri tuondoke hapo kwa mganga ili tukajadiliane mbele!

Tulimuaga yule mganga pale na kuondoka na wala hakuonyesha mashaka ya sisi kuondoka pale usiku!,Tulivyofika maeneo ya Hapo senta nilimwambia dogo kwakuwa nina buku mfukoni twende tutafute hayo maeneo wanapouza uji tunywe halafu tutajua la kufanya!


Itaendelea.................

Piga namba hii kwa ajili ya maswali na maulizo yoyote 0757453320
[emoji120][emoji120][emoji120]
 
Mimi siamini tena kama ni kisa cha kweli, angalia mwandiko wake kwenye hadithi (Nadra sana kukosea, lakini akiwa anajibu comments za wadau makosa mengi sana). Wakati huo huo anasema anatumia simu kuandika. Story ya kweli huwezi kukumbuka mambo yote yale anayo yaandika kwani kwa binadamu wa kawaida ukiambiwa hata uandike maisha yako ya week moja nyuma tu ni ishu sana.
Story inavyoonekana ni ya kweli sema mdau analia lia sana maisha magumu
 
Story inavyoonekana ni ya kweli sema mdau analia lia sana maisha magumu
Sawa yaweza kuwa ni story ya kweli lakini kuna chumvi pia, je wewe huja notice tofauti ya mwandiko wake kwenye story na comments zake? Kwenye story makosa ya kimaandishi ni kidogo sana au hakuna kabisa(Kumbuka anatumia simu kwa mujibu wake) lakini kwenye comments zake makosa ni mengi sana ili hali comment ni fupi kuliko story. Anyway all in all story yake iko poa na ina mafunzo.
 
Mimi siamini tena kama ni kisa cha kweli, angalia mwandiko wake kwenye hadithi (Nadra sana kukosea, lakini akiwa anajibu comments za wadau makosa mengi sana). Wakati huo huo anasema anatumia simu kuandika. Story ya kweli huwezi kukumbuka mambo yote yale anayo yaandika kwani kwa binadamu wa kawaida ukiambiwa hata uandike maisha yako ya week moja nyuma tu ni ishu sana.
Tulia wewe....saa hivi tupo kipindi cha maswali na majibu!
Jamaa anajibu maswali yote kwa ufasaha
 
Tulia wewe....saa hivi tupo kipindi cha maswali na majibu!
Jamaa anajibu maswali yote kwa ufasaha
Sijasema kuwa hajibu kwa ufasaha, nazungumzia uandishi wake wa story ni tofauti na uandishi wake kwenye comments zake. Kwenye comments kuna makosa kibao kama yangu na yako lakini kwenye story makosa ya kiuhandishi ni kama hayapo kabisa. Kumbuka anadai anatuma simu kuandika.... [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
 
LWANDA MAGERE
umeacha watu wanashikana mashati, blauz na vitopu humu.

Ila uzi huu unaenda tu
Ha ha nimecheka sana eti uzi unaenda tu. Kimsingi sikua nimeingia huku toka uzi ulipohamishiwa telegram, Ila wabongo tunapenda sana slope povu lote kisa uzi umehamishwa, kuna raia mmoja humu (Ke) kila nikisoma comment zake ni kama kachafukwa mbaya
 
Huko michango imepamba moto huku story zinapungua mtakuja kujikuta mmebaki wenyewe nastory zikaishia hewani
 
Sijasema kuwa hajibu kwa ufasaha, nazungumzia uhandishi wake wa story ni tofauti na uhandishi wake kwenye comments zake. Kwenye comments kuna makosa kibao kama yangu na yako lakini kwenye story makosa ya kiuhandishi ni kama hayapo kabisa. Kumbuka anadai anatuma simu kuandika.... [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Kwahiyo unatakaje kwa mfano mbona mna wivu Sana nyie tunga basi yakwako na wewe tutakuchangia
 
Sawa yaweza kuwa ni story ya kweli lakini kuna chumvi pia, je wewe huja notice tofauti ya mwandiko wake kwenye story na comments zake? Kwenye story makosa ya kimaandishi ni kidogo sana au hakuna kabisa(Kumbuka anatumia simu kwa mujibu wake) lakini kwenye comments zake makosa ni mengi sana ili hali comment ni fupi kuliko story. Anyway all in all story yake iko poa na ina mafunzo.
Unagubu
 
Mimi siamini tena kama ni kisa cha kweli, angalia mwandiko wake kwenye hadithi (Nadra sana kukosea, lakini akiwa anajibu comments za wadau makosa mengi sana). Wakati huo huo anasema anatumia simu kuandika. Story ya kweli huwezi kukumbuka mambo yote yale anayo yaandika kwani kwa binadamu wa kawaida ukiambiwa hata uandike maisha yako ya week moja nyuma tu ni ishu sana.
Mkuu wakikusikia[emoji23]utaoga povu
 
Acha wivu usituletee umaskini wako kwani hizo hela tunazo changa umewahi kutupa??
Acha kupaniki kijana au wewe na yeye lenu moja kama wacheza kamali, au ndio shipa la kimkakati limekuingia kiasi kwamba chochote anachowafanyia huko mmekuwa mbumbu
 
Acha kupaniki kijana au wewe na yeye lenu moja kama wacheza kamali, au ndio shipa la kimkakati limekuingia kiasi kwamba chochote anachowafanyia huko mmekuwa mbumbu
Kuna aliye walazimisha kusoma uzi wake? Yani buku linawatoa jasho kiasi hicho? Ngoja nikakulipie
 
Mkuu mbona umepanic kwa kitu kidogo sana hicho? Pia unapata wapi ujasiri wa kumwambia beberu kuwa ana gubu? Seriously!
Beberu hana akili za kushikiwa Kama hizi hivi ni lazima msome huo uzi? Kwanini msisimulie story zenu na nyie
 
Wewd umeamua kulikuza jambo bure, ishu ni uandishi wake katika kujibu comments ukilinganisha na uandishi wake katika kusimulia, sasa mambo ya yeye kushindwa kujibu maswali wapi na wapi na nani kasema hayo?
 
Back
Top Bottom