Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Wakuu habarini za mchana?,bila shaka Mungu amewajaalia afya njema.Poleni pia kwa majukumu ya haya masumbufu ya maisha,Mungu ni mwema atafungua njia kwa wote wasumbukao na wenye kulemewa na haya maisha.

Kitabu kimetoka na kiko tayari kabisa,ila kutokana na maboresho kukifanya kuwa bora,gharama za uchapaji ziliongezeka kidogo na hivi sasa kinapatikana kwa gharama ya Tsh 10000/=tu,hivi sasa nipo Morogoro kuna jambo lilinileta huku linalohusu vijana namna ya kujitambua ambapo msimamizi mkuu ni ELIMIKA TANZANIA,hivyo niwaombe mlioko Morogoro na mnahitaji kitabu cha UTAJIRI WA NGUVU ZA GIZA ULIVYOHARIBU MAISHA - Sehemu ya 1,tafadhali nifahamisheni ndugu zangu. Watu wa Dar es salaam na mikoa mingine ambako nilikuwa nimepewa oda,kuanzia Jumatatu nitawafikia.

Watu wa Morogoro nipo kuanzia leo Ijumaa tarehe 5 mpaka tarehe 7 siku ya jumapili.

Kwa mawasiliano zaidi nipigie hapa +255683588226
Mkuu hiko kitabu nataka kwa Dodoma nitakipata wap ,
 
Mkuu hivi kweli uko serious?,aliyekwambia mtu aliyetubu dhambi alizofanya hapendi pesa ni nani?,hujui pesa ndiyo inayoendesha maisha ya mahitaji yetu ya kila siku?,na aliyekwambia kwamba nimesitisha masimulizi ni nani?,Mimi nimetoa tangazo la namna ya watu kupata vitabu,wewe unaleta ujuaji mwingi usiyokuwa na faida,Quran na Biblia ni vitabu vitakafu lakini bado vinauzwa,hata hao wanaovigawa bure unakuta wamevinunua mahali.
Hiki kisa hapa nitaendelea kukisimulia lakini lazima na watu wanaotaka kopi za vitabu wajipatie maana kwanza kuna kisa humu sikukimalizia lakini kwenye kitabu kitakuwepo,pia kuna mambo ya kikatili niliyafanya ambayo hapa sitaweza kuyazungumza lakini kwenye kitabu yapo,pia wengine huwa wanataka kitabu kama kumbukumbu,hivyo mkuu msiwe mnapenda kupotosha.

Mimi mwenyewe ndiye niliamua kusimulia historia ya maisha yangu,hukunituma wewe,hivyo muda mwingine ni vema ukatulia wanaoweza watanunua.
Kwa Sasa Mimi nitapigwa ban ,nitakula sahani moja na wakosoaji humu Kama huwezi kufatililia story utoke humu sio kumkwamisha magere asisimulie story wengi tunajifunza hapa
 
Kwakweli hii story inafundisha na inaelimisha.
Yaaani ulimwengu una mambo mengi sana Lwanda Magere umetoa Elimu kubwa Sana kwa jamii na kupitia story hii nitaakikisha watu wa karibu yangu wanasoma hiki kitabu,
Please kitabu Cha sehemu ya pili naomba nijulishwe lini kitakuwa tayari.
 
Attachments

  • IMG_20210306_083013_055.jpg
    IMG_20210306_083013_055.jpg
    199.9 KB · Views: 86
Mkuu hivi kweli uko serious?,aliyekwambia mtu aliyetubu dhambi alizofanya hapendi pesa ni nani?,hujui pesa ndiyo inayoendesha maisha ya mahitaji yetu ya kila siku?,na aliyekwambia kwamba nimesitisha masimulizi ni nani?,Mimi nimetoa tangazo la namna ya watu kupata vitabu,wewe unaleta ujuaji mwingi usiyokuwa na faida,Quran na Biblia ni vitabu vitakafu lakini bado vinauzwa,hata hao wanaovigawa bure unakuta wamevinunua mahali.
Hiki kisa hapa nitaendelea kukisimulia lakini lazima na watu wanaotaka kopi za vitabu wajipatie maana kwanza kuna kisa humu sikukimalizia lakini kwenye kitabu kitakuwepo,pia kuna mambo ya kikatili niliyafanya ambayo hapa sitaweza kuyazungumza lakini kwenye kitabu yapo,pia wengine huwa wanataka kitabu kama kumbukumbu,hivyo mkuu msiwe mnapenda kupotosha.

Mimi mwenyewe ndiye niliamua kusimulia historia ya maisha yangu,hukunituma wewe,hivyo muda mwingine ni vema ukatulia wanaoweza watanunua.

Lwanda tuendelee mkuu ,kitabu kitanunulika tu shaka ondoa
Vikifika mwanza tangaza mimi nachukua[emoji736]
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 42.

Inaendelea.............

Usiku huo nilikuwa nina na mawazo mengi sana lakini nilijipa moyo maana sikuwa na namna nyingine ya kufanya!.Kwakuwa yule Malikia alinipa ndani ya wiki niwe nimetekeleza lile agizo nilituliza kwanza akili ili nione cha kufanya.Niliendelea na ujenzi wa apartment zangu na sikuwa na presha kabisa maana kama ni kuua nilikuwa nishazoea.Basi nakumbuka siku moja yule shemeji alinipigia simu akaniambia kwamba alienda kupima akagundulika ni mjamzito,kiukweli yeye kwa upande wake alifurahi sana akawa anasema nimemrudishia furaha ambayo siku kadhaa nyuma ilikuwa imetoweka,wakati huo ilikuwa ni mwezi wa 11 mwaka wa 2014.

Nilimwambia "Sawa mke wangu mzuri nami pia nimefurahi maana ndiye atakuwa mtoto wangu wa kwanza na vile nilikuwa napenda kuzaa na wewe nimefurahi sana".

Nilikuwa najifanya kumwambia yule shemu ili asijisikie vibaya maana ukweli nilikuwa naufahamu mimi kwamba hata hao watoto ambao wangezaliwa walikuwa si mali yetu bali walikuwa mali ya wenye mali!,pia huyo hakuwa mtoto wangu wa kwanza kama nilivyomdanganya,maana mwanamke ambaye nilikuwa nimempatia mimba tayari alikuwa Zainati.

Aliniambia "Sawa baby mimi sitoweza kukaa peke yangu nataka nije huko tuishi wote ".

Nilimuuliza "Hapo nyumbani utamuacha nani?".

Aliendelea kuniambia "Yupo mdogo wangu na wanaye wawili walikuja kutoka Arusha sema sikukwambia mapema".

Niliendelea kumuuliza "Kwahiyo watakaa hapo siku zote?".

Aliniambia "Nilimwambia aje akae huku maana jamaa waliyekuwa wakiishi naye alimpata mwanamke mwingine akaoa akamtelekezea watoto,hivyo yupo yupo tu nataka nimtafutie kazi awe anafanya".

Nikamuuliza "Kwahiyo mke wangu unakuja lini?".

Nilimuuliza anakuja lini niweze kujiandaa maana kule chumbani kwangu sikuruhusiwa kumuingiza mwanamke yeyote,na yeye asingekubali nimlaze vile vyumba vingine alale mwenyewe halafu mimi nikalale chumbani kwangu mwenyewe.

Aliniambia "Nitakujulisha baby uje unichukie ngoja kwanza kuna mambo niyaweke sawa hapa nyumbani nadhani next week nitakujulisha".

Basi siku moja usiku chumbani kwangu nikiwa nawaza hapa na pale,nikapata wazo la namna ya kumuua yule binti ili isiwe rahisi mimi kufahamika na nilihakikisha nawapiga misumari ya ushirikina ndugu zake akiwemo mama yake ili wasiwe na akili ya kwenda kwa waganga kuangalia chanzo cha kifo cha binti yao.Asubuhi kulivyokucha niliingia chumba cha siri,kuna dawa ambayo nilianza kuitengeneza ile dawa ilipaswa ifanyike kwa umakini mkubwa sana maana ningekosea kidogo tu,yule binti anageitumia alikuwa anakufa na kukauka palepale kama mkaa!.Sikutaka afe kawaida bali nilitaka nisababishe chanzo cha kifo chake.Nilipomaliza kuitengeneza nilienda nikaiweka kwenye majani ya chai nikaichanganya vizuri nikiwa na lengo kwamba akiisha amka cha kwanza kushughulika nacho ilikuwa ni chai halafu ndiyo mambo mengine yanaendelea,nilisema akiisha itumia ile dawa ningeitupa maana haikupaswa mtu mwingine aitumie!.Ile dawa niliyoitengeneza ilikuwa na sifa ifuatayo,nilitaka nimuwekee mimba ya uongo tumboni mwake na akienda kupima hospitali ionekane ana mimba,nilitaka ile impelekeshe hatimaye apoteze maisha!.Wakati huo nilikuwa nina roho chafu sana,kiukweli kuna muda huwa nikikaa najiona nilifanya dhambi nyingi sana kuliko hata Ibilisi alizozifanya ila kwakuwa hivi sasa nilishajisalimisha kwa Yesu hiyo ndiyo inayonipa tumaini jipya kwenye maisha yangu.

Hivyo ndivyo nilivyofanya,baada ya kupika chai na kuinywa,nilichukua yale majani nikaenda chumbani kwangu nikayamwaga chooni kisha nika-flash na maji mengi.Ilpofika jioni alianza kutapika kama mtu mwenye mimba,alikuwa hajui kilichokuwa kinaendelea masikini ya Mungu!.

Nilijifanya namuuliza"Wewe leo unatatizo gani maana nakuona kila mara unakimbia chumbani".

Aliniambia "Hapana kaka niko vizuri tu".

Nadhani pia na yeye alishajua zile ni dalili za mimba maana alikuwa mtu mzima ila akawa kama ananificha nisijue kitu wakati kumbe mimi ndiye nilikuwa chanzo.Ile hali iliendelea kumsumbua sana,siku iliyofuata nilimpigia dada yangu mkubwa nikamwambia amueleze Shangazi kuhusu huyo binti yake hali aliyokuwa anaipitia,nilijiwahisha mapema ili kuanza kujiondoa kwenye lawama.

Nilimwambia "Sista hebu mwambie mama yake aje kama vipi ampeleke hospitali maana huyu dogo kuna mambo siyaelewi,yawezekana akawa na mimba maana kwa dalili hizi,mmh sijui!".
Dada aliniambia "Eeeh jamani mbona mapema sana,hivi huyo mtoto kakutwa na nini?,mbona alikuwa mstaarabu sana?".

Nilimwambia "Wewe unasema alikuwa mstaarabu kwani ulikuwa ukiongozana naye kwenda shule?,hivi wewe watoto wa siku hizi unawajua vizuri kweli?".

Dada aliniambia"Ila hilo nalo neno mwenzangu,ngoja basi nimwambie mama yake".

Haukupita muda mrefu mama yake alinipigia simu nikamweleza kila kitu akasema nimwambie binti yake aende!.Baada ya siku mbili yule mdogo wangu kuwa ameenda kwa mama yake ambaye alikuwa Shangazi yangu sikutaka kabisa kucheza mbali maana nilitaka nifuatilie kila hatua.Nilienda mpaka kwa Shangazi nikamkuta ila binti alikuwa ndani!.

Nilimuuliza Shangazi "Mlimpeleka hospitali?".

Shangazi aliniambia "Ndiyo mwanangu nilimpeleka afanyiwe vipimo".

Niliendelea kujifanya namuuliza "Ni nini kilichokuwa kinamsibu".

Shangazi akaniambia "Itakuwa nini zaidi ya mimba mwanangu,nilimkanya sana huyu mtoto kuhusu wanaume akiwa bado anasoma lakini alikuwa anielewi".

Nilimuuliza Shangazi "Kwani mpaka sasa kesha waambia hiyo mimba kampa nani Shangazi?".

Nilimuuliza shangazi nikiamini atakuwa alimwambia mtu aliyempa mimba maana kwa binti mzuri kama yule aikuwa rahisi kukosa mtu ambaye niliamini ndiye angebebeshwa zigo la lawama.

Shangazi aliniambia "Aseme wapi?,nimejaribu kumuuliza hasemi,toto limechukua akili ya baba yake lina kiburi kama nini!".

Nilimwambia shangazi "wakati alipomaliza shule nilitaka kuna mahali nimpeleke akafanye kazi lakini sasa kwa hali hii itabidi kwanza ajifungue ndiyo tuangalie utaratibu mwingine".

Nilimuuliza Shangazi "Kwani yuko wapi?".

Shangazi aliniambia "Yuko ndani huko".

Shangazi akaanza kumuita "wewee........njoo huku unaitwa".

Daaah! kiukweli nilipo muona nilitamani kulia maana tumbo lilikuwa kubwa kama mimba ya miezi 5,nilianza kumuhurumia nikijua kabisa mimi ndiye niliyesababisha!.

Nilijifanya namuuliza "Hebu nieleze mdogo wangu nani ni muhusika wa hii mimba,mimi nitakusaidia ,wewe niambie ukweli usinifiche".

Alianza kuniambia "Hii mimba itakuwa ya ......... maana nilitembea naye kabla hata ya kuanza mitihani,mara ya mwisho kufanya naye mapenzi ilikuwa kabla ya mitihani,nakumbuka tulipimwa shuleni kabla ya mitihani lakini sikuwa na mimba sasa na mimi nashangaa kaka".

Alikuwa akieleza yule binti huku machozi yaki mlenga lenga machoni,nilimuhurumia sana na nilijiona nimefanya kitendo cha kikatili sana,sikuwa na namna nyingine ya kufanya ilipaswa iwe hivyo.

Nilimwambia "basi sawa kwakuwa umeniambia ukweli wewe kaa nyumbani ukishaa jifungua mimi nitakupeleka shule za kulipia ukasome A - level".

Aliniambia "Sawa kaka nimekuelewa".

Basi nilimuaga Shanghazi nikaondoka zangu,kuna kiasi cha pesa nilimpatia ili kiwasaidie hapo nyumbani kwa ajili ya matumizi.Siku iliyofuata kama saa 8 mchana alinipigia simu dada yangu akanimbia yule binti kafariki,sababu za kufariki kwake ilikuwa tumbo limemuuma sana,sasa wakati wakiwa njiani kumpeleka hospitali akawa amekufa kabla hata ya kufika hospitalini,nilihuzunika sana lakini sikuwa na njia nyingine ya mimi kuepuka adhabu zaidi ya kufanya kile nilicho ambiwa nikifanye na Malikia.Ule msiba niliugharamikia siku zote,baada ya siku hiyo kumaliza kuzika kama kawaida usiku nilisikia sauti ya Malikia ikiniita kwenye kile chumba cha siri,niliamka kitandani nikaelekea huko,nilipoingia desturi ilikuwa ni ileile ya kusujudu na kuanza kusikiliza maelekezo nitakayoambiwa!.

Malikia aliniambia "Umenifurahisha sana kijana wangu mtiifu".

Aliendelea kuniambia"Wewe ni mtiifu sana na ndiyo maana nakupenda sana,hebu omba chochote utakacho nitakupatia".

Nilimwambia "Yule mwanamke ambaye anataka tuishi wote amesema anataka kuhamia hapa,sasa itakuwaje Malikia?".

Malikia aliniambia "Usiwe na wasiwasi kijana wangu,atakuja na utaweza kumdhibiti".

Nilimuuliza "Sasa si atataka tuwe tunalala wote chumbani kwangu na moja ya maelekezo niliyopewa ziwani ni kwamba mwanamke yeyote asiingie chumbani kwangu?".

Ndipo Malikia aliniambia "Huyo mwanamke ni mali yetu si yako hivyo wewe lala naye popote utakapo".

Baada ya kusikia hivyo nilishituka kidogo sikuelewa ile kauli alikuwa akimaaniaha nini aliposema ya kwamba yule shemeji alikuwa Mali yao.Baada ya yale maelekezo yule Malikia aliniambia "Shika hii".

Alinipa kadude fulani kalikokuwa kadogo kama goroli,kisha akaniambia "Kesho saa 6 usiku nenda mpaka pale kwenye apartments yako unayojenga uchimbe katikati ya uwanja na uweke hiko kitu nilichokupatia na nitakupatia maelekezo baada ya wewe kufanya hivyo".

Nikamjibu "Sawa Malikia".

Baada ya maelekezo hayo alitoweka mle chumbani kama upepo.Kiukweli mara ya kwanza mimi nilikuwa nikiogopa sana lakini kadri siku zilivyokuwa zikisonga hofu ilikuwa ikiinisha,nilipokuwa najua nimekosea ndiyo mkojo ulikuwa unakaribia kutoka maana nilijua fika nitakavyo muona Malikia sivyo nilivyomzoea,nilipofanya vizuri alichokuwa akiniambia nilikuwa naingia chumbani bila hofu kabisa!.Basi nilifunga zangu mlango wa kile chunba cha siri na kuelekea chumbani kwangu kulala.

Itaendelea....................
 
Watu wa JF Wengi Tunapenda Vya bure, Kazi kukosoa Na Kulalama Kama Vile Mtoa Simulizi Hana Majukumu Na Watu Wanaomtegemea

Kama Kuna soft Copy Tupe utaratibu wa kununua, Mambae Hawezi kujichanga Tutamalizana Sisi Wenyewe
 
Shusha vitu mkuu
 
Mikasa hii inasikitisha sana,mpaka mwili wangu unasisimka kwa hofu.
 
We jamaa utakua na homoni za kike wewe ,mwanaume unakua Kama demu ,umetukera sana
we sasa ulichokereka nn mtoto wa kiume? kitabu tutanunua,kule alikoenda tulikipia...na hapa aflow tu...

Ameombwa kama ana nafasi aflow tu....kama ana softcopy tutanunua tu faster...tusimpotezee muda kwa kumsumbua...hakujakua na nia mbaya...ila uko huru kutukana uwezavyo.
 
MKASA WA PILI -Sehemu ya 43.

Inaendelea.............

Asubuhi kulipokucha siku hiyo nilielekea kwa Shanghazi msibani maana ule msiba bado ulikuwa wa mbichi sana,Kwakuwa nilishiriki kuanzia hatua ya mwanzo mpaka hatua ya mwisho kwenye ule msiba,haikuwa rahisi mtu kujua kwamba mimi ndiye niliye husika kwa namna moja ama nyingine!.Nilipokuwa hapo msibani,niliona sasa ulikuwa muda muafaka wa kumpiga bakora za kim-kakati Scolastica,nilimpigia simu nikamwambia ninapotoka msibani nitampitia twende zetu nyumbani kwangu,aliniambia kuna mahala ningemkuta mida hiyo ambayo ningetoka msibani.Kweli,nilipofika hayo maeneo nilimkuta akinisubiri,kwa kweli yule mwanamke alikuwa mzuri sana.Kama nilivyosema hapo awali ni kwamba nilitembea na wanawake wachache lakini walikuwa na kiwango cha kimataifa!,wanawake wazuri ndiyo ilikuwa starehe yangu wakati huo maana pombe nilikuwa sinywi hata kidogo,ilikuwa mimi na wanawake tu na kila mwanamke mzuri niliyemtaka kwa wakati huo nilimpata bila wasiwasi!.

Basi tulifika nyumbani ilikuwa mida ya saa 10 jioni ndipo nilielekea bafuni kuoga,kwakuwa Scolastica yeye alikuwa mnywaji,nilimchukulia wine akaendelea kutwanga kama kawaida,nilipomaliza kukoga nilielekea jikoni kwa ajili ya kutengeneza ile dawa ambayo ilipaswa niinywe kwenye chai kwa ajili ya kumshughulikia kikamilifu.Ilipofika mida ya saa 12 jioni nilimchukua na kumpeleka chumbani ambako ndipo nilipomkung'utia yule mwenzie,nnilianza kumcharaza bakora za kim-kakati mpaka ilipofika mida ya saa 3 usiku ndipo nikamwachia ili akaandae chakula tule na baada ya chakula shughuli iendelee kama kawaida!.

Baada ya kumtembezea bakora za kutosha,nilimwachia mida ya saa 5 usiku akiwa hoi,alikuwa amelala kama mtu aliyekufa kwasababu ya kuchoka zile purukushani,ndipo sasa nilitoka kwenye hicho chumba kuelekea kujiandaa maana kwa ajili ya kwenda kule kwenye apartments zangu,Malikia usiku wa siku iliyokuwa imepita alikuwa kanimbia ifikapo saa 6 usiku wa siku ambayo ingefuatia,ilipaswa nielekee kule site kwenye apartment zangu ili nikafukie ile dawa aliyokuwa amenipatia ambayo ilifanana na goroli kimuonekano.Nilipoingia kwenye kile chumba cha siri nilijiandaa kikamilifu na nilipomaliza kujiandaa niliukamata mkono wangu uliyokuwa na irizi,nikatamka kwamba inapswa niwe maeneo ya site kwa wakati ule,ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua nilijikuta nipo pale site.Nilianza kuchimba pale katikati ya nyumba kama nilivyoelekezwa na Malikia,nilipomaliza kuchimba nilichukua ile dawa nikaifukia pale,nilihakikisha nimepafukia vizuri kiasi kwamba isingekuwa rahisi mtu yeyote kufahamu kilichokuwa kinaendelea.

Nilipomaliza ile kazi niliukamata tena mkono wangu wa kushoto uliyokuwa irizi na kutamka kama kawaida,ghafla nikawa ndani ya kile chumba changu cha siri,nikavua zana za kazi na kuelekea chumba alichokuwa amelala Scolastica,nikamkuta bado amelala fofofo,niliondoka kuelekea chumbani kwangu kwanza!,sasa ile nimefika ndiyo nagusa kitasa ili nifungue mlango niingie chumbani kwangu nikasikia sauti ya Malikia ikiniita kule kwenye chumba cha siri,hivyo sikuweza kuingia chumbani kwangu ilibidi nigeuze kurudi kule chumbani sauti ilipotokea.Safari hii Malikia alikuja akiwa na binti mmoja ambaye sikumfahamu,bila shaka walikuwa miongoni mwa wale mabinti ambao niliwakuta ziwa Tanganyika maana alikuwa uchi kama alivyozaliwa na alikuwa mzuri sana,mkononi alikuwa kabeba kitu kilichokuwa kimefunikwa kwa ustadi wa hali ya juu,kwa wakati ule sikukifahamu kilikuwa ni kitu gani!.

Malikia aliniambia "Naona unaendelea kufanya kazi nzuri inayonifurahisha,sasa sikiliza kwa makini maana sina muda wa kukaa hapa kuna mahali naelekea".

Aliniambia "Kwakuwa ulitaka ufanye Maendeleo kwa pesa ninazokupatia basi na mimi nakuomba unisaidie jambo moja".

Nilimwambia "nipo tayari Malikia".

Akaanza kuniambia "Hapo kwenye hiyo apartment yako watu wataanza kuhamia hivi karibuni,nakutaka kila mwanamke atakayehamia hapo awe kaolewa au hajaolewa hakikisha unamwingilia,watoto watakao patikana itakuwa ni mali ya wenye mali,umenielewa?".

Nilimjibu "Ndiyo Malikia nimekuelewa".

Basi baada ya kunipatia hayo maelekezo,alimwambia yule dada aliyekuja naye mwamba "Mkabidhi".

Basi yule dada alitembea mpaka pale nilipokuwa nimesujudu huku akiwa kainamisha uso wake kwa unyenyekevu,alinikabidhi kile kitu kilichokuwa kimefunikwa.

Malikia aliniambia "simama".

Niliposimama aliniambia "fungua".

Nilipofungua kile kitu kilichokuwa kimefunikwa kwa ustadi kumbe ilikuwa ni upembe ambao ulikuwa umevishwa irizi moja kubwa,nilipoukamata vizuri ule upembe Malikia aliniambia "Unaona huo upembe?".

Nilimjibu "Ndiyo Malikia nimeuona".

Aliniambia "Huo ni kwa ajili ya kuwashulikia wale wote wakorofi,kwa kutumia upembe huo utafanya kila tukio la kutisha na kukupendezesha nafsi wakati wowote ,kwa kutumia huo upembe utaingia nyumba yeyote hata ikiwa na zindiko la namna gani!,kwa kutumia huo upembe utaweza kwenda anga ambazo zinamilikiwa na wenye nguvu na hakuna ambaye atakugusa".

Ndugu zangu ule upembe kwa kifupi ni kwamba nilikuwa sasa nimepandishwa cheo cha kufanya makubwa zaidi ya yale niliyoyafanya.Basi baada ya yale maelekezo aliendelea kuniambia "Nimekupenda sana kijana wangu na kakamilishe ndoto zako".

Baada ya hayo mazungumzo na kukabidhiwa rasmi ule upembe walitoweka mle chumbani,niliuhifadhi ule upembe kimazingara ili ikitokea mtu akiingia kwenye kile chumba kama alivyokuwa amefanya mtoto wa shangazi,basi isiwe rahisi kuonekana.Basi nilitoka ndani ya kile chumba nikaelekea chumba alichokuwa amelala Scolastica,nilliangalia muda ilikuwa saa 8 usiku,ilibidi nimuamshe na bakora zikaanza tena kumtembelea mpaka ilipofika saa 10 ndipo tulialala mpaka asubuhi.Asubuhi alipokuwa aanaondoka nilimpatia pesa ambayo ingemsaidia katika matumizi yake ya kawaida.Nilimwambia dereva wangu amsindikize mpaka nyumbani kwake.

Siku ziliendelea kukatika,kama kawaida mwisho wa mwezi ukawa umekaribia na hivyo nilipaswa kutoa kafara,hiyo sasa ilikuwa mwezi 12 mwaka 2014.Sasa kuna dada mmoja wakati nilipokuwa nikienda pale dukani kwao Zainati,alikuwaga na dharau sana,kuna kipindi Zainati alikuwa ananiambia kwamba alikuwa akiniponda sana,alikuwa akimwambiaga Zainati aachane na mimi kwani sikuwa na hadhi ya kutembea naye,sasa yeye kumbe alikuwa mtoto wa mama yake mdogo Zainati,yaani yule dada na Zainati walikuwa ndugu,yaani mtoto wa mama mdogo na mtoto wa mama mkubwa,kwasababu ya zile dharau na nyodo zake,yeye ndiye nilipanga mwisho wa mwezi huo wa 12 mwaka huo wa 2014 nimtoe kafara,kilichofanya nimtoe kafara yule dada ni namna alivyokuwa akijisikia,kuna kipindi nilikuwa nikifika hapo dukani kwao ananitazama kwa kunipandisha na kunishusha kwa nyodo zote,pia nilikuwaga nikimsalimia aitikii salamu yangu,kitendo kile kiukweli kilikuwa kinaniudhi sana,kilichokuwa kinanikasirisha zaidi,ni yeye kumwambia Zainati aachane na mimi kwasababu eti tulikuwa hatuendani naye kisa yeye alikuwa mwarabu,hasira zangu zilijaa kikombe na nikaona alikuwa ameigusa mboni ya jicho langu.Sasa kabla ya tarehe ya mwisho wa mwezi 12 mwaka huo 2014 nilienda dukani kwao Zainati,bahati nzuri yule dada nilimkuta,nilipomsalimia aliniitikia kwa dharau huku akinipandisha na kunishusha kama kawaida yake,lile duka lilikuwa kubwa na lililokuwa limejaa vito(jewels),hivyo hata kama wateja wangekuwa wengi kiasi gani kulikuwa na nafasi ya kuhudumiwa bila usumbufu!.Nikimsalimia Zainati wangu yeye akaitikia kwa furaha na alifurahi kuniona,mimba yake ilikuwa ishaanza kuwa kubwa,lengo la kunipeleka pale,nilitaka Zainati anitajie jina lake tu huyo ndugu yake ili nimshugulikie!.

Nilimuuliza "Hivi huyu ndugu yako anaitwaga nani mama maana mbona ananyodo sana".

Zainati aliniambia "Hana lolote anajishaua tu,mbona yeye anatembea na vibwana vyake vimechoka na hakuna anayemsema".

Sasa wakati nikiwa nazungumza na Zainati sikutaka kumchota sana ili asije kuhisi kitu,Kwa bahati nzuri kuna mteja aliingia mle dukani nikasikia Zainati anamwambia "wewe........njoo umsikilize mteja huku".

Ndipo nikajisemea kimoyomoyo "Kumbe ndilo jina lako hilo,tutaonana".

Kwa wakati huo nilikuwa nikipata jina la mtu ambaye nilimkusudia,basi alikuwa anaisoma namba.Kwakuwa sasa nilishalifahamu jina lake,nilimuaga Zainati ili niondoke kuelekea nyumbani nikajiandae kwa ajili ya kurudi kumshughulikia yule dada.

Zainati aliniambia "Unaenda wapi baby jamani!,situkae tuongee".

Nilimwambia "naenda kuendelea na shughuli zangu mama niruhusu niende".

Kama kuna wanawake ambao hawakula pesa yangu basi Zainati alikuwa miongoni mwao maana nilikuwa nikimpa pesa hachukui ananiambia yeye hakunipendea pesa bali alinipenda mimi kama mimi,alikuwa akiniambia kama ni pesa basi kwao ilikuwepo.Niliondoka zangu kurudi nyumbani ili sasa kujiandaa kwa ajili ya kumshughulikia huyo ndugu yake.

Itaendelea....................
 
Back
Top Bottom