MKASA WA PILI -Sehemu ya 43.
Inaendelea.............
Asubuhi kulipokucha siku hiyo nilielekea kwa Shanghazi msibani maana ule msiba bado ulikuwa wa mbichi sana,Kwakuwa nilishiriki kuanzia hatua ya mwanzo mpaka hatua ya mwisho kwenye ule msiba,haikuwa rahisi mtu kujua kwamba mimi ndiye niliye husika kwa namna moja ama nyingine!.Nilipokuwa hapo msibani,niliona sasa ulikuwa muda muafaka wa kumpiga bakora za kim-kakati Scolastica,nilimpigia simu nikamwambia ninapotoka msibani nitampitia twende zetu nyumbani kwangu,aliniambia kuna mahala ningemkuta mida hiyo ambayo ningetoka msibani.Kweli,nilipofika hayo maeneo nilimkuta akinisubiri,kwa kweli yule mwanamke alikuwa mzuri sana.Kama nilivyosema hapo awali ni kwamba nilitembea na wanawake wachache lakini walikuwa na kiwango cha kimataifa!,wanawake wazuri ndiyo ilikuwa starehe yangu wakati huo maana pombe nilikuwa sinywi hata kidogo,ilikuwa mimi na wanawake tu na kila mwanamke mzuri niliyemtaka kwa wakati huo nilimpata bila wasiwasi!.
Basi tulifika nyumbani ilikuwa mida ya saa 10 jioni ndipo nilielekea bafuni kuoga,kwakuwa Scolastica yeye alikuwa mnywaji,nilimchukulia wine akaendelea kutwanga kama kawaida,nilipomaliza kukoga nilielekea jikoni kwa ajili ya kutengeneza ile dawa ambayo ilipaswa niinywe kwenye chai kwa ajili ya kumshughulikia kikamilifu.Ilipofika mida ya saa 12 jioni nilimchukua na kumpeleka chumbani ambako ndipo nilipomkung'utia yule mwenzie,nnilianza kumcharaza bakora za kim-kakati mpaka ilipofika mida ya saa 3 usiku ndipo nikamwachia ili akaandae chakula tule na baada ya chakula shughuli iendelee kama kawaida!.
Baada ya kumtembezea bakora za kutosha,nilimwachia mida ya saa 5 usiku akiwa hoi,alikuwa amelala kama mtu aliyekufa kwasababu ya kuchoka zile purukushani,ndipo sasa nilitoka kwenye hicho chumba kuelekea kujiandaa maana kwa ajili ya kwenda kule kwenye apartments zangu,Malikia usiku wa siku iliyokuwa imepita alikuwa kanimbia ifikapo saa 6 usiku wa siku ambayo ingefuatia,ilipaswa nielekee kule site kwenye apartment zangu ili nikafukie ile dawa aliyokuwa amenipatia ambayo ilifanana na goroli kimuonekano.Nilipoingia kwenye kile chumba cha siri nilijiandaa kikamilifu na nilipomaliza kujiandaa niliukamata mkono wangu uliyokuwa na irizi,nikatamka kwamba inapswa niwe maeneo ya site kwa wakati ule,ilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua nilijikuta nipo pale site.Nilianza kuchimba pale katikati ya nyumba kama nilivyoelekezwa na Malikia,nilipomaliza kuchimba nilichukua ile dawa nikaifukia pale,nilihakikisha nimepafukia vizuri kiasi kwamba isingekuwa rahisi mtu yeyote kufahamu kilichokuwa kinaendelea.
Nilipomaliza ile kazi niliukamata tena mkono wangu wa kushoto uliyokuwa irizi na kutamka kama kawaida,ghafla nikawa ndani ya kile chumba changu cha siri,nikavua zana za kazi na kuelekea chumba alichokuwa amelala Scolastica,nikamkuta bado amelala fofofo,niliondoka kuelekea chumbani kwangu kwanza!,sasa ile nimefika ndiyo nagusa kitasa ili nifungue mlango niingie chumbani kwangu nikasikia sauti ya Malikia ikiniita kule kwenye chumba cha siri,hivyo sikuweza kuingia chumbani kwangu ilibidi nigeuze kurudi kule chumbani sauti ilipotokea.Safari hii Malikia alikuja akiwa na binti mmoja ambaye sikumfahamu,bila shaka walikuwa miongoni mwa wale mabinti ambao niliwakuta ziwa Tanganyika maana alikuwa uchi kama alivyozaliwa na alikuwa mzuri sana,mkononi alikuwa kabeba kitu kilichokuwa kimefunikwa kwa ustadi wa hali ya juu,kwa wakati ule sikukifahamu kilikuwa ni kitu gani!.
Malikia aliniambia "Naona unaendelea kufanya kazi nzuri inayonifurahisha,sasa sikiliza kwa makini maana sina muda wa kukaa hapa kuna mahali naelekea".
Aliniambia "Kwakuwa ulitaka ufanye Maendeleo kwa pesa ninazokupatia basi na mimi nakuomba unisaidie jambo moja".
Nilimwambia "nipo tayari Malikia".
Akaanza kuniambia "Hapo kwenye hiyo apartment yako watu wataanza kuhamia hivi karibuni,nakutaka kila mwanamke atakayehamia hapo awe kaolewa au hajaolewa hakikisha unamwingilia,watoto watakao patikana itakuwa ni mali ya wenye mali,umenielewa?".
Nilimjibu "Ndiyo Malikia nimekuelewa".
Basi baada ya kunipatia hayo maelekezo,alimwambia yule dada aliyekuja naye mwamba "Mkabidhi".
Basi yule dada alitembea mpaka pale nilipokuwa nimesujudu huku akiwa kainamisha uso wake kwa unyenyekevu,alinikabidhi kile kitu kilichokuwa kimefunikwa.
Malikia aliniambia "simama".
Niliposimama aliniambia "fungua".
Nilipofungua kile kitu kilichokuwa kimefunikwa kwa ustadi kumbe ilikuwa ni upembe ambao ulikuwa umevishwa irizi moja kubwa,nilipoukamata vizuri ule upembe Malikia aliniambia "Unaona huo upembe?".
Nilimjibu "Ndiyo Malikia nimeuona".
Aliniambia "Huo ni kwa ajili ya kuwashulikia wale wote wakorofi,kwa kutumia upembe huo utafanya kila tukio la kutisha na kukupendezesha nafsi wakati wowote ,kwa kutumia huo upembe utaingia nyumba yeyote hata ikiwa na zindiko la namna gani!,kwa kutumia huo upembe utaweza kwenda anga ambazo zinamilikiwa na wenye nguvu na hakuna ambaye atakugusa".
Ndugu zangu ule upembe kwa kifupi ni kwamba nilikuwa sasa nimepandishwa cheo cha kufanya makubwa zaidi ya yale niliyoyafanya.Basi baada ya yale maelekezo aliendelea kuniambia "Nimekupenda sana kijana wangu na kakamilishe ndoto zako".
Baada ya hayo mazungumzo na kukabidhiwa rasmi ule upembe walitoweka mle chumbani,niliuhifadhi ule upembe kimazingara ili ikitokea mtu akiingia kwenye kile chumba kama alivyokuwa amefanya mtoto wa shangazi,basi isiwe rahisi kuonekana.Basi nilitoka ndani ya kile chumba nikaelekea chumba alichokuwa amelala Scolastica,nilliangalia muda ilikuwa saa 8 usiku,ilibidi nimuamshe na bakora zikaanza tena kumtembelea mpaka ilipofika saa 10 ndipo tulialala mpaka asubuhi.Asubuhi alipokuwa aanaondoka nilimpatia pesa ambayo ingemsaidia katika matumizi yake ya kawaida.Nilimwambia dereva wangu amsindikize mpaka nyumbani kwake.
Siku ziliendelea kukatika,kama kawaida mwisho wa mwezi ukawa umekaribia na hivyo nilipaswa kutoa kafara,hiyo sasa ilikuwa mwezi 12 mwaka 2014.Sasa kuna dada mmoja wakati nilipokuwa nikienda pale dukani kwao Zainati,alikuwaga na dharau sana,kuna kipindi Zainati alikuwa ananiambia kwamba alikuwa akiniponda sana,alikuwa akimwambiaga Zainati aachane na mimi kwani sikuwa na hadhi ya kutembea naye,sasa yeye kumbe alikuwa mtoto wa mama yake mdogo Zainati,yaani yule dada na Zainati walikuwa ndugu,yaani mtoto wa mama mdogo na mtoto wa mama mkubwa,kwasababu ya zile dharau na nyodo zake,yeye ndiye nilipanga mwisho wa mwezi huo wa 12 mwaka huo wa 2014 nimtoe kafara,kilichofanya nimtoe kafara yule dada ni namna alivyokuwa akijisikia,kuna kipindi nilikuwa nikifika hapo dukani kwao ananitazama kwa kunipandisha na kunishusha kwa nyodo zote,pia nilikuwaga nikimsalimia aitikii salamu yangu,kitendo kile kiukweli kilikuwa kinaniudhi sana,kilichokuwa kinanikasirisha zaidi,ni yeye kumwambia Zainati aachane na mimi kwasababu eti tulikuwa hatuendani naye kisa yeye alikuwa mwarabu,hasira zangu zilijaa kikombe na nikaona alikuwa ameigusa mboni ya jicho langu.Sasa kabla ya tarehe ya mwisho wa mwezi 12 mwaka huo 2014 nilienda dukani kwao Zainati,bahati nzuri yule dada nilimkuta,nilipomsalimia aliniitikia kwa dharau huku akinipandisha na kunishusha kama kawaida yake,lile duka lilikuwa kubwa na lililokuwa limejaa vito(jewels),hivyo hata kama wateja wangekuwa wengi kiasi gani kulikuwa na nafasi ya kuhudumiwa bila usumbufu!.Nikimsalimia Zainati wangu yeye akaitikia kwa furaha na alifurahi kuniona,mimba yake ilikuwa ishaanza kuwa kubwa,lengo la kunipeleka pale,nilitaka Zainati anitajie jina lake tu huyo ndugu yake ili nimshugulikie!.
Nilimuuliza "Hivi huyu ndugu yako anaitwaga nani mama maana mbona ananyodo sana".
Zainati aliniambia "Hana lolote anajishaua tu,mbona yeye anatembea na vibwana vyake vimechoka na hakuna anayemsema".
Sasa wakati nikiwa nazungumza na Zainati sikutaka kumchota sana ili asije kuhisi kitu,Kwa bahati nzuri kuna mteja aliingia mle dukani nikasikia Zainati anamwambia "wewe........njoo umsikilize mteja huku".
Ndipo nikajisemea kimoyomoyo "Kumbe ndilo jina lako hilo,tutaonana".
Kwa wakati huo nilikuwa nikipata jina la mtu ambaye nilimkusudia,basi alikuwa anaisoma namba.Kwakuwa sasa nilishalifahamu jina lake,nilimuaga Zainati ili niondoke kuelekea nyumbani nikajiandae kwa ajili ya kurudi kumshughulikia yule dada.
Zainati aliniambia "Unaenda wapi baby jamani!,situkae tuongee".
Nilimwambia "naenda kuendelea na shughuli zangu mama niruhusu niende".
Kama kuna wanawake ambao hawakula pesa yangu basi Zainati alikuwa miongoni mwao maana nilikuwa nikimpa pesa hachukui ananiambia yeye hakunipendea pesa bali alinipenda mimi kama mimi,alikuwa akiniambia kama ni pesa basi kwao ilikuwepo.Niliondoka zangu kurudi nyumbani ili sasa kujiandaa kwa ajili ya kumshughulikia huyo ndugu yake.
Itaendelea....................