LwandaMagere
JF-Expert Member
- Mar 15, 2020
- 264
- 2,484
- Thread starter
- #2,321
MKASA WA PILI - Sehemu ya 48.
Inaendelea.............
Baada ya kuwa tumefika nyumbani nilimwita dereva ndani nikawa namuuliza maswali kadhaa ili nipate kufahamu pa kuanzia.
Nilimuuliza "Hivi Scolastica anakaa wapi?,huyo mwingine yeye aliniambia kwake ni Nyakato,je ni kweli?".
Dereva aliniambia "Ndiyo,bosi yule anakaa pale National ila Scola sijajua huwa anakaa wapi maana mimi wakati nafanya kazi pale kwa yule bosi nilikuwa nadhani ni ndugu maana walikuwa hawachani,muda wote walikuwa wanakuwa pamoja,nilipojua ni marafiki nilishangaa sana".
Dereva aliniuliza "Mbona umeuliza bosi kuna nini?".
Nilimwambia "Nilikuwa nataka nikawashitaki polisi ili wakawachukue".
Niilimdanganya dereva ili asinishitukie yale niliyotaka kuyafanya.
Dereva aliniambia "Bosi mimi nadhani kama uliamua tu kuwapa ile hela ungeachana nao tu,japo ni pesa nyingi lakini achana nao".
Nilimwambia "Wazo ni zuri sana,kiukweli nimeachna nao wajinga wale ipo siku watapata shida naamini watakuja tu".
Nilimwambia dereva lakini wakati huo moyo wangu ulishaamua siku nyingi kwamba niwashughulikie!.
Nilimwambia dereva "Basi sawa wewe kaendelee na shughuli zako".
Basi siku iliyofuata niliamka mapema nikajianda na mambo yangu kisha nikaondoka kuelekea site,sasa kwakuwa ilikuwa wikiendi,mke wangu alikuwa hakwenda kazini alikuwepo tu nyumbani,Kile chumba cha siri hakuwahi kabisa kukitilia mashaka kwasababu nilikuwa nikikiwekea zindiko,isingekuwa rahisi yeye kukumbuka.Yule Dalali alikuwa kanitaarifu kwamba kuna jamaa kaongea nao na alisema wangekuja kuzitazama zile nyumba hivyo nilipaswa niwepo pale site,nilipofika sikumkuta mtu zaidi yangu mimi na dereva,baada ya muda kidogo jamaa walifika pale wakiwa kwenye land cruiser nyeupe ikiwa na namba za DFP,tukasalimiana nao pale,yule dalali akawatambulisha kwangu kwamba mimi ndiye mmiliki wa zile nyumba.Jamaa mmoja aliniambia walikuwa wanataka zile nyumba mbili maana kuna familia ya bosi wao walitaka moja na mmoja wapo wa waliokuja naye pia alihitaji moja.Basi baada ya kukubaliana na hao jamaa nilimwambia dereva anirudishe nyumbani yeye aendelee na shughuli zake.
Nilipofika nyumbani kwakuwa ilikuwa mida ya saa 6 mchana nilikula na nilipomaliza nilielelekea chumbani kupumzika mpaka ilipofika mida ya saa 10 jioni ndipo nilipoamka.Nilimtafuta mke wangu hapo nyumbani sikumuona,nikamuuliza yule binti akasema alitoka kwenda kufanya mazoezi ya kutembea,ndipo nilichukua simu nikampigia Scolastica lakini haikupokelewa,nilijaribu kumpigia tena na tena lakini hakupokea simu,niliamua kumpigia yule mwanamke jeuri ambaye alikuwa mke wa bosi wa zamani wa dereva wangu nikamwambia "Samahani sana nakuomba umpigie simu Scolastica umwambie apokee simu yangu tafadhari".
Yule mwanamke aliniambia "Wewe sema shida yako bhana,Scola niko naye hapa na anakusikia".
Kiukweli toka awali sikuwa kabisa na niya ya kuwafanyia kitu kibaya ila kwasababu ya dharau za yule mwanamke ndizo zilikuwa zikichochea hasira yangu maradufu.Nilikuwa nimejaa hasira sana na sikutaka kumaliza kuongea naye nilikata simu.Nilichukua funguo za kile chumba cha siri nikaenda sasa kujiandaa ili nikawaadhibu kikamilifu.Nilipofika ndani nilichukua ile pembe nikailekezea ukutani ndipo ikaja sinema pale ukutani nikawaona wote wawili wakiwa wamekaa kwenye nyumba ambayo sikuifahamu,hawakuwa peke yao bali walikuwa na mwanamke mmoja wa makamo pamoja na mtoto ambaye umri wake ulikuwa kama miaka 3.Nilipomaliza kuwamulika niliondoa ile pembe ueleko wa ukuta nikarudi tayari kwa ajili ya kuondoka mpaka walipokuwa.
Niliukamata mkono wangu uliyokuwa na ile irizi Kuna maneno nilitamka pale ya kwamba kwa wakati huo ninapswa niwe ndani ya nyumba walimokiwemo wale viumbe niliowaona kwenye skrini pale ukutani!.Kilikuwa ni kitendo cha kufumba na kufumbua nilikuwa pale sebuleni!,nilihakikisha hakuna anayeniona nikajisogeza mpaka kwenye kochi alilokuwa amekaa Yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu aliyekuwa na dharau nyingi.Yule mama mtu mzima niliyemuona kwenye skrini pale ukutani nilimkuta na niligundua alikuwa mama mkwe wake na huyo mwanamke mwenye nyodo na dharau.Nilikaa pale mpaka saa 12 jioni maana walikuwa wakiangalia tamthilia kwenye luninga,giza lilipoanza kuingia nilisikia Scolastica anamwambia yule mwanamke kwa kumnong'oneza kwamba "Mimi naenda zangu nyumbani,leo mambo yameharibika".
Nilitaka kufahamu walichokuwa wakiteta maana nilikuwa nao sahani moja.
Yule mwanamke alimwambia "Hakuna kuondoka Scola maana yeye atalala na mwanangu kule chumbani halafu sisi tutalala zetu kama kawaida hivyo si rahisi kugundua".
Basi baada ya yale mazungumzo niliona yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu anaingia jikoni kupika,nilibaki pale kwenye kochi na Scolastica nikiwa namtazama bila ya yeye kufahamu chochote kilichokuwa kinaendelea.Ile nyumba ilikuwa kubwa na inavyoonekana yule jamaa yake alikuwa na pesa maana haikuwa mchezo hata kidogo!,chakula kilipoiva walitenga dining room na kila mmoja alielekea kupakua,walipo pakua walirudi kukaa sebuleni kuangalia luninga huku wakiendelea kula,yule mama mke wake na huyo mwanamke yeye alikaa dinning room akiwa anamlisha yule mtoto mdogo.
Sasa nilisogea karibu na chakula cha yule mwanamke mwenye aliyekuwa na dharau nikaanza kula chakula chake!,alipokuwa akila na mimi nakula,mpaka chakula kilipoisha akawa anasema "mmh mbona leo nakula si shibi?".
Alinyanyuka tena kwenda kupakua chakula kingine,nakumbuka ilikuwa ndizi iliyochanganywa na nyama,nilimfanyia vitimbi yule mwanamke alimradi tu kumkomoa.
Kama nilivyosema hapo awali ya kwamba ukiamua kumuabudu Mungu basi muabudu Mungu na kama ukiamua kuwa wa Ibilisi basi wewe kuwa wa Ibilisi,wale watu wangekuwa wa maombi wakaombea chakula kile kwa uaminifu basi hata nisingewasogelea ila kwasababu walikuwa watu wa maombi ya kuunga unga nilikula nao pamoja chakula bila wao kufahamu!.
Baada ya kula ilipofika mida ya saa 3 usiku yule mama aliaga akawaambia yeye anaelekea kulala,wao waliendelea kubaki pale sebuleni.Ilipofika mida ya saa 4 usiku,niliona yule mwanamke ambaye ni mke wa bosi wake wa zamani dereva wangu anamsogelea Scolastica wakaanza kunyonyana ndimi(denda),kiukweli nilishituka sana nikawa naendelea kuwatazama kwa mshangao!,madenda yalipokuwa yamekolea aliamka yule mwanamke akazima ile televisheni pamoja na taa za sebuleni wakaelekea chumbani.Baada ya kufika chumbani wakavua nguo vizuri huku nikiwatazama kisha wakaelekea wote bafuni kuoga,walipomaliza nusu saa wakawa wametoka,walianza kushikana na kuchezeana kama mke na mume!,ndipo nikagundua kwamba walikuwa wanafanya mapenzi ya jinsia moja(wanasagana),kumbe hata ule urafiki wao wa karibu uliyokuwa kama undugu ambao yule dereva aliniambia bila shaka uliletwa na hiyo hali!.
Basi wakati wakiwa kwenye lindi la mahaba mazito kuna namna niliifanya pale hata kama wangeniona na wakapiga kelele basi hakuna ambaye angesikia!.Niliamua sasa kujitokeza hadharani ili wanione,aliyekuwa wa kwanza kuniona ni yule mwanamke wa bosi wake wa zamani dereva wangu,kwasababu yeye alikuwa chini akiangalia juu.
Itaendelea................