Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Mikasa ya ajabu niliyoishuhudia kwa macho yangu

Leo wakati natoka Arusha naelekea moshi kuna eneo kuna daraja afu ni bondeni nime kuta ajari abiria wa kwenye haic wame kufa wotee..ina semekana apo ajari za kuuwa watu wengi ni kawaida sana kila mwaka afu zina husisha magari matatu
 
Leo wakati natoka Arusha naelekea moshi kuna eneo kuna daraja afu ni bondeni nime kuta ajari abiria wa kwenye haic wame kufa wotee..ina semekana apo ajari za kuuwa watu wengi ni kawaida sana kila mwaka afu zina husisha magari matatu
watu wanaongeza utajiri
 
Haya telegram mmeshindwa
IMG_1952.png

Kisa hiko hapo youtube ingia kwenye channel ya davista mata media.


Lwanda magere anaendelea kushusha vitu huko youtube
 
Ila kwakweli mnaongozwa kama MAPUNDA ...ajali zinatokea kwa UZEMBE wa MADEREVA na kuendesha kwa kasi pasipo na sababu ya kuendesha kwa kasi, kibao kinasema tembea na 50 wewe unaenda 80 hadi 100 unategemea nini, unaendesha ukiwa umelewa, unaaendesha ukiwa unaongea na simu, unategemea nini, acheni mawazo ya kipumbavu namna hii, ndivyo mnavyodanganywa na hawa wasimulia hadithi

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu za masiku? Ushakua bilionea Mkuu naona kwenye avatar umetupia ndinga lako hongera Mkuu. Vp ule utajir ulifanikiwa? Tupe mrejesho Mkuu?
 
MKASA WA PILI - Sehemu ya 18.


Inaendelea...............




Asubuhi kulipokucha na nilimuaga mzee Nchibaronda nikaianza safari ya kurejea Mwanza.Mzee Nchibaronda nilimwachia shilingi laki moja ile ya kitanzania pamoja na kiasi kidogo nilichokuwa nacho cha faranga.Mzee alikuwa ameniambia kwamba siku nitakayofanikiwa inabidi nirudi kumpa shukurani maana shukurani huwa ni lazima.Kwakuwa wakati huo nilikuwa nina uwezo wa ajabu kutokana na ile irizi niliyowekewa mkononi nilitamka ya kwamba "Ninataka muda huu niwe ziwa Tanganyika".

Nilijikuta nipo ziwani upande wa Kongo,kiukweli nilijiona nina bahati kuliko binadamu wote waliyoko kwenye hii sayari ya dunia!.Nilitembea hapo ufukweni kuelekea kaskazini mwa Kongo,muda si mrefu nilifika pale kwenye bandari ya Kalemii!,bado nilikuwa sielewi ule uwezo wa kutembea kwa haraka ulitoka wapi,yawezekana ilikuwa ile irizi ya Malikia,maana kutoka hapo ufukweni nilipokuwepo mpaka hapo bandari ya Kalemii kulikuwa na umbali wa kufa mtu,lakini cha ajabu nilitembea muda mfupi nikawa nimefika.Nilipofika pale bandarini nilikuta boti nyingi za kisasa,niliuliza boti zilizokuwa zinaelekea kigoma nikaonyeshwa,nilipofika kwenye hiyo boti nilipanda na kuingia ndani,hakuna aliyeweza kuniuliza kuhusu nauli nilitamka ya kwamba nisisumbuliwe kuhusu nauli na ikawa hivyo!.Huu mtindo wa kusafiri bila nauli baadae ndiyo yalikuwa maisha yangu siku zote tangu nilipotoka huko chini ya maji!.Ile boti haikuchukua muda sana ilianza safari kuelekea Kigoma,ndani ya saa kadhaa tukawa tumetia nanga bandari ya Kigoma!.Nilipofika kigoma nilijaribu kumpigia simu yule jamaa tuliyeachania Kasulu kwa yule mama lakini alikuwa hapatikani,baada ya kumkosa jamaa nilijaribu kumtafuta mama yangu,alipopatikana tulisalimiana akaniambia wao wanaendelea vizuri,Mama aliniuliza "Kwani ukowapi wewe?,mbona hujaja nyumbani takribani wiki mbili?".

Nilimwambia mama "Nitakuja kesho maana nilikuwa bize kuna kazi nilikuwa naifanya".

Baadae nilitafuta hoteli maeneo ya hapo kwa ajili ya kupumzika ili kesho nianze safari ya kuelekea Mwanza.Usiku huo nilikuwa nawaza namna nitakavyokuwa tajiri na namna ya kufanya watu wasigundue utajiri wangu kuwa niwa kishirikina!.Kulipokucha asubuhi nilielekea kupanda basi lililokuwa linaelekea Mwanza,kama kawaida nilipanda bure sikuweza kulipa nauli na hakuna aliyeniuliza.Wakati huo nilikuwa nina jeuri na kiburi kisichokuwa na mfano,maana niliona mimi ndiye mimi na kwamba hakukuwa mbwa yeyote wa kunibabaisha!.Baada ya safari ndefu tuliingia Mwanza mida ya usiku.Nilipofika hapo stendi ya Nyegezi nilipanda bodaboda mpaka Geto kwangu,Kwakuwa ile nyumba tuliyokuwa tumepanga ilikuwa na geti,nilianza kugonga,kuna jamaa mmoja alikuja kunifungulia.

Jamaa aliniambia "Mwanangu mambo vipi?".

Nikamwambia "Poa kaka".

Aliniuliza "Ulikuwa wapi kaka maana nilijaribu kukuulizia lakini kila mtu hakuwa na jibu".

Nilimwambia "Nilisafiri kidogo kaka,siunajua tena utafutaji?".

Aliniambia "Ok sawa,karibu siye tupo".

Basi nilielekea chumbani kwa yule jamaa yangu ambaye tulienda naye Kasulu,nilikuwa nimempatia funguo za chumbani kwangu anitunzie,niligonga mlango ukafunguliwa lakini ilikuwa sura ngeni machoni kwangu!.Alikuwa mwanamke ambaye nilidhani uenda angekuwa mke wa jamaa lakini kumbe kile chumba kilikuwa na mpangaji!.

Nilimuuliza "Vipi,jamaa amelala?".

Yule dada aliniuliza "jamaa yupi?".

Ndipo aliniambia yeye alikuwa kahamia kwenye hicho chumba kama wiki moja iliyopita na huyo jamaa niliyekuwa nikimuulizia yeye hakuwa akimfahamu.Nilimuomba samahani mimi nilifahamu tangia mwanzo uenda angekuwa mwanamke wa jamaa,nilimwambia kwamba kwenye hicho chumba alichohamia yeye kulikuwa na mpangaji ambaye nilimwachia funguo za chumbani kwangu maana nilikuwa nimesafiri.Yule dada aliniambia nijaribu kuwauliza wapangaji wengine maana yeye hakufahamu kitu chochote!.

Nilienda kumgongea yule jamaa aliyenifungulia geti nikajaribu kumuulizia uenda jamaa alikuwa kamuachia funguo.

Jamaa akasema "Hapana sikuachiwa funguo kaka".

Niliona isiwe taabu sana,nilielekea chumbani kwangu nikagusa kile kitasa kwa mkono wa kushoto uliyokuwa na ile irizi ndipo mlango ukafunguka nikaingia ndani!.Kiukweli sikutaka mtu yeyote aone lile tukio ndiyo maana kwanza nilijaribu kuutafuta ufunguo wangu,kwakuwa ilishakuwa usiku sikuwa na namna ingawa hakuna aliyeona nafanya nini!.Kuna jamaa mmoja alikuwa jirani na chumba changu,ambaye usiku niliporudi hakuwepo,alikuwa ameenda kwenye shughuli zake za viwandani huko Igoma;Sasa asubuhi jamaa alipokuja kutoka shift huko kiwandani alishangaa kunikuta nafanya usafi ndani kwangu!.

Jamaa aliniambia "Aisee mambo vipi,umerudi lini?".

Nilimjibu "nimefika jana usiku".

Aliendelea kuniuliza "Ulikuwa na funguo nyingine nini!,maana jamaa aliniachia funguo zako".

Nilimwambia "Ndiyo nilikuwa na funguo moja,hiyo niliyompa jamaa huwa naiacha kama dharula".

Nilimuuliza "jamaa kahamia wapi?".

Jamaa aliniambia "Mshikaji aliniaga akaniambia anaelekea Kahama mkoani shinyanga,anasema kuna chimbo la dhahabu kalipata hivyo aliona aachane na ile kampuni ya ujenzi aelekee mgodini kutafuta mali!".

Nilimwambia "Ok ,sawa".

Tuliendelea kupiga stori pale na jamaa na akanipatia ule ufunguo wa chumba changu,Nilipomaliza kufanya usafi,nilijilaza ndani nikiwa nawaza namna ya kuianza ile kazi maana niliambiwa nijitahidi ndani ya mwezi huo mwishoni damu iwe imepatikana!.Niliamkana kuelekea nyumbani kwa mama,nilipitia sokoni nikanunua matunda na vyakula baadhi nikawapelekea.

Siku zilipozidi kuyoyoma,nilipata wazo sasa la kuianza kazi rasmi!.Kumbuka niliambiwa nihakikishe kuna chumba maalumu nilichokitenga kwa ajili ya kukiweka kile kibuyu alichonipa mzee Nchibaronda baada ya kufanya tukio.Kile kibuyu kilikuwa ni kidogo sana kwa muonekano wa kawaida lakini kilikuwa na uwezo wa kubeba damu lita 200 kwa wakati mmoja!,endapo ungepewa ukinyanyue kwa uwezo wa kawaida ulikuwa huwezi mpaka uwe na nguvu za ziada kama nilizokuwa nazo mimi!.Sasa kuna siku nakumbuka ilikuwa mida ya saa 3 usiku nilielekea mitaa ya Bugando kufanya tukio,kuna ajali niliisababisha ya bodaboda kugongwa na lori mpaka vichwa vikasagika kabisa,ile bodaboda ilikuwa imebeba abiria mwanamke,Nilisogea na kibuyu changu nikaweka damu yao wote wawili,sikubakiza hata tone la damu maana kuna dawa nilichanganya ambayo ilivuta damu zote kwenye ile miili hakikubaki kitu.Tukio hilo nililifanya pasipo kuonekana na mtu yeyote yule usiku huo.Basi baada ya kuwa nimeiweka ile damu kwenye kibuyu nilielekea geto kwangu,nilipofika nilikiweka kile kibuyu chini ya uvungu!.Asubuhi nilipoamka nilikiangalia kile kibuyu sikukuta damu yoyote,nikajua tayari wazee wa kazi walikuwa wamekuja wamechukua chakula chao!.

Siku iliyofuatia nilisikia sauti ikiniambia kwamba nielekee maeneo ya Nyegezi,eneo ambalo lilikuwa jirani na stendi ya Bus,hayo maeneo niliambiwa kulikuwa na kituo cha mafuta au alimaarufu sheli(sitokitaja jina).Ile sauti iliniambia kwamba nikifika hayo maeneo kuna dada mmoja nitamuona hapo sheli atakuwa ameshika hela,nisiwe na wasiwasi nimsalimie kisha atanipa hizo hela bila kupenda!,niliambiwa yeye atakuwa anaona ameshika hela kumbe kashikilia gunzi la muhindi!.Nilifanya nilivyoagizwa,nilipofika nilimsalimia yule dada maana nilipomuona tu nilimfahamu ndiye.Baada ya kumshika mkono na kumsalimia alinipa pesa zote alizokuwa nazo,ndipo ghafla nikaona ameshikilia gunzi la muhindi pasipo kufahamu akidhani ni pesa!.Nilipozihesabu zile hela zilikuwa laki tatu na elfu hamsini.Ndipo nikarudi zangu geto kwangu!,nilipofika ndani kwangu pia kuna hela nilizikuta kitandani zilikuwa burungutu zimefungwa na raba bendi.

Kiukweli nilifurahi sana,nilianza kuzihesabu zilikuwa milioni 2.



Itaendelea.....................
Watu uliowakuta huko chini ya bahari walikua waafrika au walikua na rangi ya kizungu?
 
Dah, braza mimi sio kwamba nashindwa kulipa hyo buku. Ila tatzo nikishaipakua hyo app ya telegram lazma nianze kutafta link za magroup ya malaya na mim ctaki kurudi tena huko. Yani hyo app ctak kuiona kabisa kwny cmu yangu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Back
Top Bottom