Mikasa ya Dunia: Mtu asiye na Kivuli, anayeweza kuwa sehemu mbili kwa wakati Mmoja

Mikasa ya Dunia: Mtu asiye na Kivuli, anayeweza kuwa sehemu mbili kwa wakati Mmoja

Chizi Maarifa

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2013
Posts
10,931
Reaction score
24,816
Ni siku ya Pili sasa nipo Tanga na hapa leo nimekutana na jambo la kushangaza sana. Nikiwa nmepark gari wanaosha nikaona ni vyema nikae sehemu nipate Dafu pia na kubadilishana mawili matatu na wenyeki kwenye Bench wakicheza Draft.

Hii dunia imejaa visa,mikasa,vioja na maajabau yake.kuna mambo ya kutisha,sikitisha,furahisha na kustaajabisha.

Tulikuwa tumekaa watu 6 wawili wakicheza. Hivyo nlinunua madafu 6 tuendelee na Jumatatu yetu huku jamaa wakiosha gari.

Tukiwa tunaongea alikuja kijana mmoja akasalimia na hakukaa sana akaondoka. Hakuna ambaye alipenda sana ku jihusisha naye ni kama watu walikuwa wanamjibu tu ili aondoke.

Alipoondoka ndo bwana mmoja akaanza kunambia.

"Bro wewe unatokea wapi?" Nlimjibu akaanza elezea.
"Yule Bwana xxx aliyekuja hapa ukaona tuna mjibu kifupi sana bila stories naye.ulimwangalia vizuri?" Kiukweli sikuwa na sababu ya kumwangalia vizuri so sikuwa nmemwangalia vizuri. Nikamjibu "hapana" akaanza kunielezea.

" Yule jamaa ungemwangalia ungegundua kuwa hana kivuli" personally sikuwahi kuwa na wazo la kukagua kama kuna mtu ana au hana kivuli.

"Yule jamaa alikuja hapa toka Zanzibar ilitokea tu jamaa kijiwe flani wanaamka asubuhi wanamkuta jamaa pale kijiweni. Alipoulizwa aliwajibu kuwa katokea Zanzibar.jamaa waliendelea kupiga naye kazi mbalimbali hasa za kuuza ujenzi n.k moja ya mambo ambayo yalikuwa yanawashangaza jamaa ni kuwa alikuwa anakaa hata siku nne tano hali.

Wakawa wanajiuliza huwa anakula wapi na muda mwingi wanakuwa naye kazini then wanaenda lala ghetto.ndo siku moja jamaa akawasimulia kuwa yeye huwa anakunywa damu za binadamu na akinywa anaweza kaa hata wiki bila kula.

Akaendelea kuwaambia kuwa hata kivuli hana sababu ana nafsi mbili.anaweza kuwa hapa Tanga halafu watu wengine muda huo huo wakamwona Dar es salaam.

Katika kuthibitisha hilo kweli kesho yake wakiwa juani watu walifanya uchunguzi mdogo na kugundua hana kivuli. Wakati wao wanaonekana kuwa na vivuli yeye alikuwa hana.

Lakini pia wanasema mara kadhaa amekuwa akionekana kabisa wapo naye sehemu A lakini jamaa yao mwingine anasema alikuwa na naye sehemu B. Jamaa amekuwa hivyo na aliwasimulia chanzo mpaka cha yeye kuwa hivyo.

Na kuwa alifika hapo Tanga baada ya kudondoka akiwa safarini kuelekea sehemu nyingine.

Jamaa alikuwa anaweza wasimulia wao mambo ya ndani kwao na sometimes akilala na wanawake wa pale mtaani usiku bila wao kujitambua."

Hali hiyo ilisimuliwa na wenzake jamaa pale maskani wakiunga mkono kuwa kama atarudi niangalie kama ana kivuli.

Hapo ikabidi nianze kuwakagua jamaa pale kama wana vivuli.nami nikajiangalia na kukuta ninacho.nimashusha pumzi. Mambo mengi yalizungumzwa ila nikasema

Nije wauliza wana JF je inawezekana kabisa mtu akakosa kivuli? Akawa two places at the same time? Inakuwaje kuwaje?

Nawasilisha.
 
Ishu ya mtu kutokiwa ni kivuli nilisoma miaka ya elfu 20 mwanzoni. Ilikuwa stry ya bwana mmoja hivi WA KENYA. Yeye aliingia kwenye Haya mambo ya cult alizama mazima huko kiasi Kwamba ikafikia akawa hana kivuli akitembea. Yaani usipokua na kivuli ni kama NUSU mfu. Maana binadamu aliye hai ni lazima awe na Kivuli
 
Mkuu ungemuona wewe na kuthibitisha Kuwa hana kimvuli kidogo ningekuelewa lkn kwa jua hili nalolijua Mimi ukiwa huna hela linakuonyesha kimvuli chako mpk chunusi na jipu litashindwaje kuonyesha kimvuli cha huyo binadamu anaeweza shikika na akafanya kazi..😅
Mwili wake utakuwa umevunja sheria za kifizikia..
 
Ishu ya mtu kutokiwa ni kivuli nilisoma miaka ya elfu 20 mwanzoni. Ilikuwa stry ya bwana mmoja hivi WA KENYA. Yeye aliingia kwenye Haya mambo ya cult alizama mazima huko kiasi Kwamba ikafikia akawa hana kivuli akitembea. Yaani usipokua na kivuli ni kama NUSU mfu. Maana binadamu aliye hai ni lazima awe na Kivuli
Miaka ya elfu 20,ndo lini hiyo mkuu?
 
IMG_5067.jpg
 
Back
Top Bottom