Glenn
JF-Expert Member
- May 23, 2015
- 69,329
- 164,730
Wakuu sana pokeeni salamu zangu.
Naomba leo nisimulie visa viwili vya kusikitisha ambavyo niliwahi kushirikishwa na rafiki zangu kwa nyakati tofauti.
KISA CHA KWANZA:
Huyu ni rafiki yangu kipenzi sana, na naomba nimpe jina Tonia (jina sio halisi)
Tonia nilikutana naye katika mazingira yangu ya kazi. Ni msichana mrembo sana na aliyebarikiwa karibu kila kitu ambacho binti/ke angetamani kuwa nacho na mwenye mvuto ambao ulisababisha kila mahali apitapo kazi zisimame kwa muda ili kumtazama.
Nakumbuka siku ambayo alikuja ofisni kwangu na alipotoka alipishana na vijana kama watano hivi wa kazini kwangu...walimsindikiza kwa macho hadi anatoka getini cha ajabu kila mmoja aliguna kwa sauti na wengine wakasema ee Mungu unajua kuuumba😅
Kwa kadiri siku zilivyokwenda tulijikuta kila mtu akivutiwa na mwenzake, mvuto ambao mwisho wa siku tulijikuta
tukiwa marafiki wakubwa.
Kutokana na safari yetu mpya ya urafiki, ziliingia zama zile za kila wakati kutamani kujua mwenzie yuko wapi na
anafanya nini kwa wakati husika.
Ulifika wakati Tonia akawa na wivu mkubwa na kutaka kuwa nami kila wakati. Hili halikuwa gumu kwangu kutokana na nature ya kazi yangu kuwa mimi ndiye alpha na omega kazini kwangu.Kila wakati aliponimiss ilikuwa ni kunyanyua simu na kutoa taarifa kuwa D..najiandaa kuja...uko ofisni au...nije?
Kutokana na muonekano, ukarimu wake hakika nami Glenn nilihisi kuwa sasa Mungu nami amenikumbuka na kunipa paradiso na pumziko la moyoduniani japo niseme kweli uhuru wangu ulifia pale kwasababu kila tulipokwenda si hotelini' shopping au popote tulipopita tuligeuka kivutio' hii ilininyima kutembea kwa miguu tukiwa pamoja.
Niwe mkweli Tonia alibadili upepo wote ndani ya moyo wangu kwa jinsi alivyoonyeshs kunikubali, kunipenda
na alivyonisemesha kwa upendo ambao haukuwa na chembe ya unafiki.
Alichokosea Tonia ni kitendo cha kuonyeshs kunipenda kwa moyo wake wote bila kujua linapokujasuala la kupenda Glenn huwa hujui kutania kwa hiyo ikawa ni sawa petrol na kiberiti kilichowashwa vimewekwa
pamoja. Naomba nihame hapa naona nashindwa kuhimili kusimulia..
Zilipita siku, miezi hatimaye miaka, kuna siku Tonia alipata msiba wa mtu ambaye kwa wakati huo alimfahamu kama SHANGAZI YAKE nimeandika kwa herufi kubwa kwasababu ndiko mkasa wake wa kusikitisha uliko.
Wakati Tonia anapata huo msiba mimi nilipata safari ya ng'ambo hivyo sikuweza kumsindikiza. Baada ya majuma matatu nilirejea kutoka safarini.
Baada ya kurejea nilimpasha habari na hakukawia kuondoka huko alilokwenda msibani alinifuate town.
Aliporejea alinyoosha moja kwa moja kazini.
Mara alipowasili na kuniona alikuwa ana uso wa simanzi kupita kawaida na kama kawaida alikimbilia kifuani na kunikumbatia kwa muda mrefu na akalia sana hadi nilikuta nakosa uvumilivu nami simanzi ilinijaa sana japo nilijikaza kiume na kuanza kumbembeleza na kumsihi ajikaze na ajipe moyo aache kulia maana hiyo ni kazi ya Mungu.
Pamoja na kumtulliza sana sikuona dalili ya kufarijika kwa Tonia na ilikuwa kama nimetonesha kidonda kibichi moyoni mwake. Katika kuendelea kumfariji ghafla Tonia alisema kwa sauti ya ya chini na yenye simanzi:
(Glenn, tangu nikufahamu umekuwa rafiki wa kweli, mpenzi ambaye sijawahi kujuta kupendwa nawe na kama baba kwangu kwani hujawahi kuniangusha kwa lolote na umeyabadilisha maisha yangu kwa kiwango cha juu sana hivyo kutokana na heshima hiyo naomba nikushirikishe SIRI ya familia yangu iliyofichwa kwa muda wa miaka 25 na ambayo leo hii inaniliza kwa uchungu) note: Tonia alikuwa na umri wa miaka 25.
Baada ya Tonia kusema maneno haya nilipata mshtuko mkubwa kwani pamoja na hayo alinisisitiza kuwa nisiwajulishe dada zake kwani hii siri kwani wao bado hawaifahamu isipokuwa kaka yake mkubwa tu
na baba na mama yake tu.
Baada ya kumhakikishia kuwa kamwe sitawaambia hii siri ndipo alipoanza kunisimua. Naomba niseme kidogo kuhusu dada zake na familia yake. Katika familia yao walizaliwa wasichana wanne na upande wa kiume wakowawili, na yeye amezaliwa wa tatu akifuatiwa na mabinti mapacha wawili warembo sana sana japo hawamfikii dada yao Tonia na wote niliwfahamu kwa ukaribu sana kwani mahusiano yetu yalianza kuvuka mipaka. Tonia ndiye binti anapendwa upendo usiokuwa wa kawaida na familia yake hasa baba kiasi cha kuwa kero kwake kwani kila kitu kidogo tu baba yake anamwita nyumbani
Turudi kwenye jambo la linalomuumiza Tonia alilloliita ni SIRI ya familia na alianza kama hivi:
TONIA: Glenn unakumbuka yule shangazi yangu ambaye nilikuonyeshs picha kuwa anafanana nami sura hadi umbo?
GLENN: Ndio namkumbue si ndiye aliyefariki sio?
TONIA: Glenn kumbe huyo ndiye mama yangu mzazi..(akali machozii)
GLENN: Tonia unasema???? kwani mama yake si .....? nilimtaja mama aliyemlea tangu udogoni.
TONIA: Ndio maana nilitangulia kukwambia ni siri ya familia, hili jambo baada ya msiba baba aliniita na kuniambia kuwa huyo aliyefariki ndiye mama yangu mzazi. Nilimuuliza baba ilikuwaje anifiche hii siri siku zote? Lakini alinijibu kuwa hakutaka nijue hili jambo alinificha kwasababu baba yangu alimtelekeza mama na mama alipitia hali ngumu hivyo hakutaka niyajua haya kwani yangeniumiza. Glenn mpenzi wangu hili jambo lina utata mkubwa nashindwa nisemeje lakini hii ndio hali halisi.
Baada ya kusimuliwa hili jambo ambalo mimi kama mtu mzima niliunganisha dots na kugundua kuwa Tonia alizaliwa kwa mtu na mdogo wake. Yaani baba yake ni mjomba na mama ni shangazi yake. Naomba hili niishia hapa nitarudi wakuu kwa mkasa wa pili
Mkasa wa pili soma post #15