Mikasa ya kweli (kufurahisha na kukera)

Mikasa ya kweli (kufurahisha na kukera)

Hahaha nimekusema wapi tena mwana??????
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ unajua siamini nilichokiandika πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimetoka boko πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Embu rudia kusoma tena maana nimesha edit. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ unajua siamini nilichokiandika πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimetoka boko πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Embu rudia kusoma tena maana nimesha edit. πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚

Hahaha na mie ni me edit, mwanzo ulisema "mwana unanisema sana" kumbe ulimaanisha "mwana una sinema". Boko wamekufanya nini huko umevurugwa mbaya au umepiga vyombooooo?

Ngoja nikupe mkanda wa mpiga vyombo mwenzako:

Kuna baba yangu mdogo alipita glossary akakuta wanakunywa mkoa huko. Sasa akawa anasema "wape kama walivyo wape kama walivyo". Yeye kaka kisha kaagiza bia zake mbili kanywa taratibu, na wale wazee na wana waliokuwa wamekaa pale kwa gloassary wakaagiza kama walivyo mbili wengine tatu kwa kujinafasi.

Baba mdogo alipomaliza bia zake mbili akaingiza mkono mfukoni akatoa buku mbili (bia moja buku buku) kisha akampa mwenye duka. Wale wana na wazee wakiwa kwenye mshangao wakiwa wameduwaa wengine wanauliza "vipi bwana imekuaje mbona umetoa buku mbili??" Akawajibu "Kwani nilikuja na nyie? Mie niliwaambia nitawalipia??". Nao wakamkumbusha "mbona ulisema tuchukue kama tulivyo???" Ahahaha akawambia "Mie sikuwaagizia bia wala sikuja na nyie wala sikuwa nasemesha mtu"


Wale wana na wazee ilibidi watoe hela mfukoni mwao kwani hawakuwa na jinsi ila walimlaani kinyama. Mzee mmoja alisikika akisema "cheki lilivyokuwa jeupe jeupe likilala kifua wazi kwenye banda la nguruwe lazima vitoto vya nguruwe vikamnyonye chuchu vikifikiri ni mama yao". .
 
Hahaha na mie ni me edit, mwanzo ulisema "mwana unanisema sana" kumbe ulimaanisha "mwana una sinema". Boko wamekufanya nini huko umevurugwa mbaya au umepiga vyombooooo?
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kuna fala mmoja alikuwa ananisemesha ndio maana nikatoa boko kama moro wa yanga.
 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kuna fala mmoja alikuwa ananisemesha ndio maana nikatoa boko kama moro wa yanga.

Hahaha boko lazima litoke:Ngoja nikupe kisa cha marehemu chura


Kuna jamaa mmoja ameshakufa kipindi hicho alikuwa anaishi kinondoni B na maarufu kwa jina la chura. Huyu jamaa alikuwa anachimba makaburi, makaburi ya Kinondoni. Kuna kipindi katika mabaunsa walioenda kulinda shamba huko Tegeta alikuwepo na alichezea sana panga nadhani ndicho kilichomuua:

Nikiwa form five hivi aliwekeana dau na wana wa kitaa kwamba hawezi tembea uchi, jamaa wakadhani utani, chura akavua nguo akawa uchi wa mnyama anatembea mitaa ya Kino "mtaa wa kazima" huku akiimba "Chura kapita uchi" watoto wanaitikia "kapita uchi". Sasa polisi kupata taarifa si wakamfatilia bana, mpaka nyumbani wanataka kumkamata. Jamaa akaingia chooni akachota mavi 'vyoo vya shimo vya kizamani' akajipaka mwili mzima mpaka kwenye kende. Alafu akatoka na kopo la kuogoea limejaa mavi. Polisi wanawa wanamkimbia sasa akawa anawafukuza wale polisi na kopo lake la mavi mkononi huku akiimba "Chura kapita uchi" watoto wanamfukuzia nyuma nao wanaitikia "chura kapita uchi"

Kweli polisi wa bongo bwana yani hawaogopi risasi ila wanaogopa mavi, kila mtu alikimbilia kwake anapopajua wanaogopa kukumbatiwa na chura au kuogeshwa na mavi. Kifupi jamaa alishinda lile dau sema sasa hatuko nae duniani ni marehemu. Jina lake halisi Amri Abdallah

 
πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ huyo chura ni bangi sana.

Hiyo blog ni yako?

Siyo blog yangu ila nimemtauta online nimempata, huyo jamaa wakati niko darasa la pili alikuwa na mwenzake anaitwa Chopa mchopanga, nae ni marehemu, Huyo chopa vidole vyole vya miguu alikuwa hana mana vililiwa na fangasi. Hawa jamaa walikuwa hawashikiki yani noma

Chopa mchopanga alishawahi mkaba mtu, bonde la mkwajuni, jamaa alitoa bomba la sindano likiwa ndani lina damu. Akamkamata jamaa mmoja roba kali, akamwambia "Ndani ya hii sindano kuna damu ina ngoma, najua unaweza pambana ila lazima nikuambukize ukimwi, kama unataka usalama toa kila kitu". Lile jamaa wakati anakabwa mbona alitoa kila kitu kuogopa kuambukizwa ukimwi na chopa mchopanga

Hawa jamaa walikuwa ni noma, kpindi hicho ila sasa wote marehemu
 
Leo nimekumbuka mbali kidogo kumbe naweza itwa muhenga mtarajiwa eti, nimekumbuka mita za TANESCO za zamani nikiwa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni B. Kipindi kile tulikuwa tunanunua kadi za umeme kwenye vituo maalumu vilivyotengwa na TANESCO. Kuna kituo kilichokuwepo karibu na sheli ya mwanamboka kinondoni, nyingine ilikuwepo Moroco na mpaka leo kuna nyingine iko sheli ambayo iko kituo cha Fire Dar es Salaam kwa wanaoelekea Posta au Kariakoo wanatambua hapo. .

Mkasa wa leo:

Kipindi kadi inaponunuliwa basi kadi ilikuwa inawekwa kwenye mita kisha umeme unaingia. Ile kadi bhana ikishikwa vibaya ikapinda ilikuwa inaleta sana tabu umeme kusoma. Nimekumbuka jinsi nyumba nzima ilivyokuwa inaniamini katika kuingiza umeme, basi bhana ile nikija na mikogo mingi naingiza kadi, mara ya kwanza hola, najaribu mara ya pili hola, mara ya tatu mara unasikia KTAAAAAAA umeme huooooooo. Wapangaji wenzangu walikuwa wanapiga makofi na kushangilia na siku hiyo hata waliopika pilau basi nilikuwa naletewa sahani teh teh teh. .


Wahenga wenzangu mpooooo mnakumbuka umeme wa kadi, ukisia KTAAAAAA ujue umeme huoooooo teh teh teh. .
 

Attachments

  • mita za luku.jpg
    mita za luku.jpg
    20.7 KB · Views: 6
Hii kutoka Mtwara bado ya moto moto ngoja niwape:


Leo nikiwa na mzee mmoja kutoka Mtwara wakiwa wanatetea dawa za miti shamba akasema "Kipindi hicho wakiwa mtwara kuna dawa inaitwa CHIDUDU ilikuwa inawekwa kwenye mchonyo '0713, 0714, 0715, 0716, 0717, 0718, 0719' lengo hasa ni kutibu MALARIA"

Wana Mtwara hii kitu kweli? Ila nachotaka kujua kwa nini inaitwa CHIDUDU????. .
 
Ngoja niwape mkasa mwingine kutoka mtandaoni: Msamilo Mastermind akimchokoza Mo Dewji
 

Attachments

  • Tweet.jpeg
    Tweet.jpeg
    35 KB · Views: 6
Bange mbaya sana usisikie:


KONDA:
Oya mie MENDE unanijua mie? nakwambia mie MENDE, baba yangu MENDE, mama yangu MENDE na hata mie mwenyewe MENDE. .

ABIRIA: Sawa utapuliziwa dawa kama wewe MENDE, wewe unadai ni MENDE utapuliziwa dawa, baba yako ni MENDE naye atapuliziwa dawa, mama yako naye ni MENDE utapuliziwa dawa. Nakwambia wote mtapuliziwa dawa nakwambia. .
 
Kiswahili kazi sana:

Jamaa anazungumza na simu; "Niko hapa BARABARA ya Morogoro ROAD; utanikuta hapa pembeni ya NGUZO ya MSTIMU ya umeme". .
 
Onyo: usimsindikize mkeo dada au mama yako anapoenda keepununua vitu karume, kariakoo mtaa wa Kongo au manzese maana kushikwa tako, kushikwa matiti, kuvutwa vutwa Jambo la kawaida...na ukitaka kugombana kwa Jambo ilo utapoteza kila ulichonacho Kama simu na pesa...dada zetu wanajua.
 
Onyo: usimsindikize mkeo dada au mama yako anapoenda keepununua vitu karume, kariakoo mtaa wa Kongo au manzese maana kushikwa tako, kushikwa matiti, kuvutwa vutwa Jambo la kawaida...na ukitaka kugombana kwa Jambo ilo utapoteza kila ulichonacho Kama simu na pesa...dada zetu wanajua.

Wanawake wanapitia mambo mengi na kudhalilika; ni jambo la kusikitika sana. Hapo zamani kidogo ukisikia mtu jambazi au kabakwa lazima ushangae sana si taarifa unazo sikia kila wakati. Ila sasa watoto wanabakwa kila kona hata katika wanawake ndoa wanabakwa na wame zao, ni jambo la kawaida kusikia mtu kadhalilishwa. Mie binafsi kama mtoto wa kiume, nasikitika sana kwa hili jambo. .

Kuna jamaa anaitwa madumu manzese, alikaa baa anakunywa pombe sasa siku hiyo sijui dharau za kushika pesa, akamwita yule bahamedi akamtia dole. Dada yule aliwaka sana mwisho wa siku maaskari waliitwa jamaa alichezea miezi sita jela. Ni jambo la kusikisha sana na la kufadhaisha. Wanaume wenzangu tubadilike, ukimfanyia kibaya mwanamke kinamuathiri yeye na jamii nzima. .
 
Gily, wabongo kupaza sauti juu ya udhalilishaji kwa kina dada bado kabisa, ukipita ubungo stand ya mkoa tazama kina dada wanavyobughudhiwa na wapiga debe

dada adi anapiga kelele "niacheni" watu wanapita tu na Mambo yao Kama hawaoni kinacho tendeka...pita masokoni Kama Kongo au stand ya mkoa huwezi kuta mwanaume anavutwavutwa kijinga..

.matukio mengi yanatokea ubungo darajani kina dada wanavuliwa nguo wanapigwa madole kisa wamevaa nguo fupi wengine maumbile yao ya nyuma yanakua ya matamanio Basi kundi la bodaboda na masela wengine wanamzonga adi kumvua nguo

lakini sijawahi sikia mwanaume kavuliwa nguo kisa kavaa mlegezo wengine sio chupi tu kuonekana adi makalio huonekana achilia mbali wanaume wanaokojoa hadharani kila anaepita huona maumbile yake.
 
kalipeni,

Hilo neno kuna wanawake wanawadhalilisha sana wanawake wenzao kutokana na mazingira wanayojiwekea wenyewe. Hata kama ni kuvaa nguo fupi zina maeneo yake, hata huko ulaya mtu hawezi vaa nguo za beach kutokea. Sasa bongo bhana unakuta mtu kavaa nguo za kuogelea na yuko anakata mitaa tu. Mwanamke kuvaa nguo za kujiheshimu haimpunguzii uzuri wake ila ukiwaeleza hawa wasiojielewa yani kama una mpigia mbuzi kengele. .


Mie binafsi sipendi hata kidogo, watu wavae mavazi kulingana na sehemu usika. Kuwekea watu matamanio yasiyo ya msingi na kujidhalilisha utu wanahitajin kubadilika sana. .
 
Hivi bongo kuna nini? wakati naingia kazini nimemkuta mlinzi nje ya jengo la ofisi amekaa kwenye kiti chake huku akitoa uchafu kwenye masikio yake na NJITI YA KIBERITI, yani nimemsalimia "shikamoo mzee" hana habari yani kalegea macho huku kama anasikilizia utamuu wa kujikuna na njiti kwenye sikio hana habare kabisa yuko ulimwengu wa roho sijui duh nouma anapumulia juu juu...
 

Attachments

  • maxresdefault.jpg
    maxresdefault.jpg
    29.6 KB · Views: 5
Nimepitia sokoni ninunue nazi nipeleke nyumbani wakapike kisamvu cha nazi maana nina hamu nacho sana. Ile kila nashika nazi inatia huruma, sijui machi yangu au wenzangu mnaonaje, hizi nazi hapa tu zinatia huruma, nahisi hazitaki kukunwa. .
 

Attachments

  • IMG_20191212_170111_6.jpg
    IMG_20191212_170111_6.jpg
    148.8 KB · Views: 3
  • IMG_20191212_170154_4.jpg
    IMG_20191212_170154_4.jpg
    127.6 KB · Views: 5
Izo sio nazi mkuu ni Vitoto vta Wrong Turn
Hahahaah hizo nazi nilivyozishika nikamwambia arudishe maana hata kama zingewekwa kwenye wali nisingeweza kula nikikumbuka. Huwezi amini najua tuko kwenye uzi wa jokes na nini ila nimezipiga picha kwa simu nikazirudisha. Zinatia sana huruma aiseee. .
 
Kuna mda mwingine bhana watu kwenye halmashauri ya ubongo wangu wananifurahisha sana.


Hahahaha Tanzania kwa vituko bhana hata uko duniani hawaoni ndani. Sijui wanasiasa wa bongo huwa wanatoaga maneno wapi eti viongozi wa serikali za mitaa wamepita bila KUPINGWA hahaha. .
 
Aisee nikiwa natokea Kariakoo ile daladala ilipofika bonde la mkwajuni tu pale si mtu kaachia ushuzi ule wa kimya kimya, tena inaonekana aliubana akasubiria tufike mkwajuni kwenye dampo, lile tunamaliza dampo tu yule mtu akauachia ushuzi. Ile kumaliza dampo tu ule ushuzi ukaanza kunuka huku harufu ya dampo inaishia. Ile harufu ilikaa kila mtu kwenye gari akageuka bubu, gari imeenda kufika kituo cha studio bado ipo tu watu wakashuka. Ile harufu ya mavi kabisa yani ilifika kwa dereva mpaka akazima redio maana sauti ilikuwa inasikika kwa juu kulingana na ukimya ule. Gari ilienda kufika kituo cha manyanya tukashuka aisee niliposhuka na ostadhi mmoja alivyoshuka tu akaropoka "Alhamdulillah"

What was weird everyone was looking at a fat people giving them looks like "its you who farted". And fart people were giving innocent looks like "I havent eaten much today". Hahah you should have been there...

Hahaha watu wote kwenye gari wakajikuta wanacheka aisee that was so funny. .
 
Back
Top Bottom