Leo nimekumbuka mbali kidogo kumbe naweza itwa muhenga mtarajiwa eti, nimekumbuka mita za TANESCO za zamani nikiwa kwenye nyumba ya kupanga Kinondoni B. Kipindi kile tulikuwa tunanunua kadi za umeme kwenye vituo maalumu vilivyotengwa na TANESCO. Kuna kituo kilichokuwepo karibu na sheli ya mwanamboka kinondoni, nyingine ilikuwepo Moroco na mpaka leo kuna nyingine iko sheli ambayo iko kituo cha Fire Dar es Salaam kwa wanaoelekea Posta au Kariakoo wanatambua hapo. .
Mkasa wa leo:
Kipindi kadi inaponunuliwa basi kadi ilikuwa inawekwa kwenye mita kisha umeme unaingia. Ile kadi bhana ikishikwa vibaya ikapinda ilikuwa inaleta sana tabu umeme kusoma. Nimekumbuka jinsi nyumba nzima ilivyokuwa inaniamini katika kuingiza umeme, basi bhana ile nikija na mikogo mingi naingiza kadi, mara ya kwanza hola, najaribu mara ya pili hola, mara ya tatu mara unasikia KTAAAAAAA umeme huooooooo. Wapangaji wenzangu walikuwa wanapiga makofi na kushangilia na siku hiyo hata waliopika pilau basi nilikuwa naletewa sahani teh teh teh. .
Wahenga wenzangu mpooooo mnakumbuka umeme wa kadi, ukisia KTAAAAAA ujue umeme huoooooo teh teh teh. .